8:43 AM
Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima-Sura ya 30

Mwenyezi Mungu anasema, Kati ya binadamu, wakati mmoja Nilifanya muhtasari wa ukaidi na udhaifu wa mwanadamu, na hivyo Nilielewa udhaifu wa binadamu na Nikafahamu vema ukaidi wake. Kabla ya kuwasili kati ya binadamu, Nilikuwa nimekuja kuelewa kitambo furaha na huzuni kati ya binadamu—na kwa sababu ya hili, Ninaweza kufanya kile ambacho binadamu hawezi, na kusema kile ambacho binadamu hawezi, na Mimi hufanya hivyo kwa urahisi sana. Je, hii siyo tofauti kati ya Mimi na binadamu? Na hii siyo tofauti dhahiri? Yaweza kuwa kwamba kazi Yangu hutimizwa na watu wa mwili na damu? Inawezekana kwamba Mimi ni wa aina moja na viumbe vilivyoumbwa? Watu wameniweka katika tabaka la aina ya kufanana—na hii siyo kwa sababu hawanijui Mimi? Kwa nini, badala ya kuinuka juu zaidi kati ya binadamu, lazima Nijinyenyekeze? Kwa nini wanadamu huendelea kunikataa Mimi, kwa nini wanadamu hawawezi kulitangaza jina Langu? Kuna huzuni kubwa moyoni Mwangu, lakini watu wangewezaje kujua? Wangewezaje kuona? Kutochukulia kile kinachonisikitisha Mimi kama muhimu sana katika maisha yao kimewaacha watu wakiwa wametiwa bumbuwazi na kuchanganyikiwa, kama kwamba wamemeza tu dawa ya usingizi; Ninapowaita, wao huendelea tu kuota, na hiyo hakuna ambaye amewahi kufahamu matendo Yangu. Leo, watu wengi sana bado wamelala fofofo. Ni wakati tu ambapo wimbo wa ufalme husikika ndipo wao hufumbua macho yao yenye usingizi na kuhisi huzuni kidogo ndani ya mioyo yao. Wakati ambapo fimbo Yangu hugonga kati ya binadamu, wao bado tu[a] husikiliza kidogo sana, kana kwamba majaliwa yao hayana thamani kama mchanga wa baharini. Ingawa wengi sana kati yao wana ufahamu fulani, bado hawajui umbali ambao hatua Zangu zimefika—kwani hawajaribu kuuelewa moyo Wangu, na hivyo hawajawahi kamwe kuweza kujinasua kutoka kwa utumwa wa Shetani. Mimi hutembea juu ya vitu vyote, na Huishi kati ya vitu vyote, na wakati huo huo, Mimi huchukua nafasi ya kati ndani ya mioyo ya watu wote. Kwa sababu hii, watu huniona Mimi kuwa tofauti, wakiamini kwamba Mimi ni wa ajabu, ama sivyo kwamba Mimi na kutokana na hilo, imani yao Kwangu huimarika kila siku. Wakati mmoja Nilijinyoosha katika mbingu ya tatu, Nikiwatazama watu wote na vitu vyote ulimwenguni. Wakati ambapo Mimi hulala, watu hutulia, wakiwa na hofu kabisa ya kusumbua pumziko Langu. Wakati ambapo Mimi huamka, wao huchangamshwa mara moja, kana kwamba wanafanya kazi ya kunipa Mimi furaha kabisa. Je, huu sio mtazamo wa watu walio duniani Kwangu? Nani kati ya watu wa leo huniona Mimi mbinguni na duniani kama mmoja? Nani asiyeniheshimu Mimi katika mbingu? Na nani hanidharau Mimi duniani? Kwa nini mwanadamu hunitenganisha Mimi kila mara? Kwa nini mwanadamu kila mara huwa na mitazamo miwili tofauti kunihusu Mimi? Je, Mungu aliyepata mwili aliye duniani si Mungu anayeamrisha vyote mbinguni? Je, Mimi Niliye mbinguni Siko duniani sasa? Kwa nini watu huniona Mimi lakini hawanijui Mimi? Kwa nini kuna umbali mkubwa hivyo kati ya mbingu na dunia? Je, mambo haya hayastahili kuchunguzwa kwa kina sana na mwanadamu?

Wakati ambapo Mimi hufanya kazi yangu, na katika nyakati ambazo Mimi hutamka sauti Yangu, watu kila mara hutamani kuongeza "ladha" kwayo, kana kwamba kunusa kwao ni kukali zaidi kuliko Kwangu, kana kwamba wao hupendelea ladha yenye nguvu, na kana kwamba Mimi Sifahamu kile ambacho mwanadamu huhitaji, na hivyo lazima "Nimsumbue" mwanadamu "kujaliza" kazi Yangu. Mimi Sififizi nguvu za uhalisi wa watu kwa makusudi, lakini Huwauliza wajitakase kutegemea msingi wa kunijua Mimi. Kwa sababu wao hukosa mengi sana, Napendekeza kwamba watumie juhudi zaidi kufidia upungufu wao ili kuuridhisha moyo Wangu. Watu walinijua Mimi wakati fulani katika dhana zao, lakini hawakufahamu hili kabisa, na hivyo utunzaji wao ulikuwa sawa na kuuchukulia mchanga kama dhahabu. Wakati ambapo Niliwakumbusha, waliachilia tu kwa sehemu ya hili, lakini badala ya kubadlisha sehemu iliyokuwa imeenda na vitu vya fedha na dhahabu, wameendelea kufurahia sehemu iliyo mikononi mwao ambayo bado inasalia—na kutokana na hili, wao kila mara huwa wanyenyekevu na wavumilivu mbele Yangu; hawana uwezo wa kutangamana na Mimi, kwani wana dhana nyingi sana. Hivyo, Niliamua kukamata chote ambacho mwanadamu anacho na alicho na kukivurumisha mbali sana, ili wote waweze kuishi na Mimi na wasiweze tena kuwa mbali na Mimi. Ni kwa sababu ya kazi Yangu ndio mwanadamu haelewei mapenzi Yangu. Wengine huamini kwamba Nitahitimisha kazi Yangu kwa mara ya pili na kuwatupa jehanamu. Wengine huamini Nitaanza mbinu mpya ya kunena, na wengi wao hutetemeka kwa woga: Wao huogopa kwamba Nitakamilisha kazi Yangu na kuwaacha bila mahali pa kwenda, na wao huogopa kabisa kwamba Nitawaacha mara nyingine. Kila mara watu hutumia dhana za zamani kutathmini kazi Yangu mpya. Nilisema kwamba watu hawakuwa wameelewa kamwe mbinu ambayo Mimi hufanyia kazi—je, wangejieleza vizuri wakati huu? Je, dhana za zamani za watu si silaha ambazo huharibu kazi Yangu? Ninaponena na watu, wao huhepa kukaza macho Kwangu kila mara, wakiogopa sana kwamba macho Yangu yatatua juu yao. Hivyo, wao huinamisha vichwa vyao, kana kwamba wanakubali ukaguzi kutoka Kwangu—na hili halisababishwi na dhana zao? Kwa nini Nimejinyenyekeza mpaka leo, lakini hakuna aliyewahi kufahamu? Ni lazima Nimwinamie mwanadamu? Nilikuja kutoka mbinguni hadi duniani, Nilishuka kutoka juu hadi mahali pa siri, na kuja kati ya binadamu na kufichua kila Nilicho nacho na Nilicho kwake. Maneno Yangu ni ya kweli na yenye ari, mavumilivu na yenye huruma—lakini nani amewahi kuona kile Nilicho na Nilicho nacho? Bado Nimefichwa kwa mwanadamu? Kwa nini ni vigumu sana Kwangu kukutana na mwanadamu? Ni kwa sababu watu wana shughuli nyingi sana katika kazi zao? Je, ni kwa sababu Ninapuuza wajibu Wangu, na watu wote wana kusudia kufuatilia ufanisi?

Katika mawazo ya watu, Mungu ni Mungu, na Hawezi kushughulishwa kwa urahisi, ihali mwanadamu ni mwanadamu, na hapaswi kuwa mpotovu kwa urahisi—lakini matendo ya watu bado hayawezi kuletwa mbele Yangu. Yawezekana kuwa matakwa Yangu ni ya juu sana? Yawezekana kuwa mwanadamu ni mdhaifu sana? Kwa nini kila mara watu huviangalia viwango ambavyo Mimi huhitaji kutoka mbali? Je, kweli haviwezi kufikiwa na mwanadamu? Matakwa Yangu yanapangwa kutegemea "katiba" ya watu, na kwa hiyo hayajawahi kuzidi kimo cha mwanadamu—lakini hata hivyo, watu husalia wasioweza kutimiza viwango ambavyo Mimi huhitaji. Mara nyingi mno Nimetorokwa kati ya binadamu, mara nyingi mno watu wamenitazama Mimi na macho ya kudhihaki, kana kwamba mwili Wangu umefunikwa kwa miiba na ni wa kuchukiza sana kwao, na hivyo watu hunichukia Mimi sana, na huamini kwamba Sina thamani. Kwa njia hii, Mimi husukumwa mbele na nyuma na mwanadamu. Mara nyingi mno watu wamenileta nyumbani kwa bei ya chini, na mara nyingi mno wameniuza Mimi kwa bei ya juu, na ni kwa sababu ya hili ndio Najikuta katika hali Niliyo ndani leo. Ni kana kwamba watu bado wananipangia Mimi njama; wengi wao bado wanataka kuniuza Mimi kwa faida ya mamia ya mamilioni ya dola, kwani mwanadamu hajawahi kunitunza Mimi. Ni kana kwamba Nimekuwa suluhishi kati ya watu, au silaha ya nyuklia ambayo wao hutumia kupigana kati ya wenyewe kwa wenyewe, au mapatano yaliyowekwa sahihi kati yao—na kutokana na hili, Mimi, kwa kifupi, Sina thamani kabisa moyoni mwa mwanadamu, Mimi ni chombo cha nyumbani kisicho cha muhimu. Lakini Simshutumu mwanadamu kwa sababu ya hili; Sifanyi chochote ila kumwokoa mwanadamu, na kila mara Nimekuwa mwenye huruma kwa mwanadamu.

Watu huamini kwamba Nitahisi starehe wakati ambapo Nitawatupa watu jehanamu, kana kwamba Nafanya maafikiano hasa na jehanamu, na kana kwamba Mimi ni aina fulani ya idara ambayo ina utaalamu wa kuwauza watu, kana kwamba Mimi ni mtaalamu katika kuwatapeli watu na Nitawauza kwa bei ya juu mara tu Nikiwa nao mikononi Mwangu. Vinywa vya watu havilisemi, lakini ndani ya mioyo yao hili ndilo wao huamini. Ingawa wote wananipenda Mimi, wao hufanya hivyo kisiri. Je, Nimelipa gharama kubwa hivyo na kutumia nyingi hivyo kupata kiasi kidogo hiki cha upendo kutoka kwao kama malipo? Watu ni walaghai, na Mimi kila mara huchukua nafasi ya anayelaghaiwa. Ni kama kwamba Mimi ni mkosa hila kabisa. Mara tu wakishaona udhaifu huu, wao huendelea kunilaghai. Maneno kutoka kinywani Mwangu hayakusudii kuwafisha watu au kubandika vitambulisho juu yao bila mpango maalum—hayo ni uhalisi wa mwanadamu. Labda baadhi ya maneno Yangu "hupita kiasi," kwa hivyo basi Naweza tu "kuomba" msamaha wa watu; kwa sababu Mimi sina "ustadi" katika lugha ya mwanadamu, mengi ya yale ambayo Mimi husema hayawezi kuridhisha matakwa ya watu. Labda baadhi ya maneno Yangu huipenya mioyo ya watu, kwa hiyo Naweza tu "kuomba" kwamba wawe wastahimilivu; kwa sababu Mimi si stadi wa falsafa ya maisha ya mwanadamu na si hodari katika njia ya kuzungumza, mengi ya maneno Yangu huleta uchungu ndani ya watu. Labda baadhi ya maneno Yangu hukemea kiini cha ugonjwa wa watu na kufichua ugonjwa wao, na hivyo Mimi hushauri kutumia baadhi ya dawa Niliyokutayarishia, kwani Sina kusudi la kukuumiza na dawa hii haina athari. Labda baadhi ya maneno Yangu hayaonekani kuwa "yenye uhalisi," lakini "Nawaomba" watu wasiwe na wasiwasi—Mimi si "hodari" wa mkono na mguu, kwa hiyo maneno Yangu hayajatekelezwa. Naomba kwamba watu "wanivumilie" Mimi. Je, maneno haya yanamsaidia mwanadamu? Natumaini kwamba watu watapata kitu kutoka kwa maneno haya, ili maneno Yangu yasiwe bure kila mara!

Aprili 9, 1992

 

Chanzo: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima-Sura ya 30

Maneno Husika ya Mungu: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima-Sura ya 35

 

Views: 139 | Added by: flickrpinquorettfb | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar