6:26 PM
Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetan

 

Unaelewa vipi umaalum katika roho? Roho Mtakatifu hufanya vipi kazi ndani ya mwanadamu? Shetani hufanya vipi kazi ndani ya mwanadamu? Roho waovu hufanya vipi kazi ndani ya mwanadamu? Na maonyesho ya kazi hii ni yapi? Wakati kitu kinakufanyikia, je, kinakuja kutoka kwa Roho Mtakatifu, na je, unapaswa kukiheshimu, au kukikataa? Utendaji halisi wa watu huibua mengi ambayo ni ya mapenzi ya kibinadamu ilhali ambayo watu daima huamini kutoka kwa Roho Mtakatifu. Mengine hutoka kwa roho waovu, ilhali watu bado hudhani yanatoka kwa Roho Mtakatifu, na wakati mwingine Roho Mtakatifu huwaongoza watu kutoka ndani, ilhali watu wanaogopa kwamba mwongozo kama huo hutoka kwa Shetani, na hawathubutu kutii, wakati kwa kweli ni nuru ya Roho Mtakatifu. Hivyo, bila utofautishaji hakuna njia ya kupitia wakati uzoefu kama huo kwa hakika unakufanyikia, na bila utofautishaji, hakuna njia ya kupata maisha. Roho Mtakatifu hufanya kazi vipi? Roho waovu hufanya kazi vipi? Nini hutoka kwa mapenzi ya mwanadamu? Na ni nini hutoka kwa mwongozo na nuru ya Roho Mtakatifu? Kama unaelewa amri za kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya mwanadamu, basi utaweza kukuza maarifa yako na kutofautisha katika maisha yako ya kila siku na wakati wa uzoefu wako halisi; utakuja kumjua Mungu, utaweza kumwelewa Shetani, hutachanganyikiwa katika kutii ama kufuatilia kwako, na utakuwa mtu ambaye fikira zake zi wazi, na ambaye hutii kazi ya Roho Mtakatifu.

Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu. Wakati watu wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndani yao ni watakatifu hasa. Wale ambao wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu huishi kwa kudhihirisha upendo wa Mungu, upendo wa kaka na dada zao, na kufurahia vitu ambavyo Mungu hufurahia na kuchukia vitu ambavyo Mungu huchukia. Watu ambao wanaguswa na kazi ya Roho Mtakatifu wana ubinadamu wa kawaida, na wanamiliki ubinadamu na daima hufuatilia ukweli. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani ya watu, hali zao huwa nzuri zaidi na zaidi, na ubinadamu wao unakuwa wa kawaida zaidi na zaidi, na ingawa ushirikiano wao mwingine unaweza kuwa mpumbavu, motisha zao ziko sahihi, kuingia kwao ni kwa hali nzuri, hawajaribu kukatiza, na hakuna nia mbaya ndani yao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida na ya kweli, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa mwanadamu kulingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na Yeye huwapa nuru na kuongoza watu kulingana na ufuatiliaji halisi wa watu wa kawaida. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa watu, Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, Anawakimu kwa msingi wa mahitaji yao, na Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kwa hali nzuri kwa msingi wa kile ambacho wanakosa, na kwa upungufu wao; wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, kazi hii inalingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na ni katika maisha halisi pekee ndio watu wanaweza kuona kazi ya Roho Mtakatifu. Iwapo, katika maisha yao ya kila siku, watu wako katika hali nzuri na wana maisha ya kawaida ya kiroho, basi wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali kama hiyo, wakati wanakula na kunywa maneno ya Mungu wana imani, wakati wanaomba wanatiwa moyo, wakati kitu kinawafanyikia wao si baridi, na wakati kinawafanyikia wanaweza kuona masomo ambayo Mungu anawahitaji kujifunza, na hawako baridi, ama dhaifu, na ingawa wana ugumu wa kweli, wako tayari kukubali mipango yote ya Mungu.

Ni matokeo yapi yanayotimizwa na kazi ya Roho Mtakatifu? Unaweza kuwa mpumbavu, na kunaweza kuwa hakuna utofautishaji wowote ndani yako, lakini Roho Mtakatifu anapaswa tu kufanya kazi ili kuwe na imani ndani yako, ili wewe daima uhisi kwamba huwezi kumpenda Mungu vya kutosha, ili uwe tayari kushiriki, uwe tayari kushiriki bila kujali ugumu mkuu ulio mbele. Mambo yatakufanyikia na haitakuwa wazi kwako iwapo yanatoka kwa Mungu ama kwa Shetani, lakini utaweza kungoja, na hutakuwa baridi wala mzembe. Hii ndiyo kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao, watu bado hukabiliwa na ugumu wa kweli, wakati mwingine wanalia, na wakati mwingine kuna mambo ambayo hawawezi kuyashinda, lakini hii yote ni hatua ya kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Ingawa hawashindi mambo hayo, na ingawa, wakati huo, wao ni dhaifu na hulalamika, baadaye bado wanaweza kumpenda Mungu na imani dhabiti. Ubaridi wao hauwezi kuwazuia kuwa na uzoefu wa kawaida, na bila kujali kile watu wengine husema, na jinsi wanavyowashambulia, bado wanaweza kumpenda Mungu. Wakati wa maombi, daima wanahisi kwamba walikuwa wadeni wa Mungu sana, na wanaamua kumridhisha Mungu na kuukataa mwili wakati wanakabiliwa na mambo kama hayo tena. Nguvu hii inaonyesha kuna kazi ya Roho Mtakatifu ndani yao, na hii ndiyo hali ya kawaida ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia katindani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuwa na hali za kawaida mbele ya Mungu. Ambayo ni kusema, punde tu kuna kazi ya Shetani ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba. Kazi ya roho waovu huharibu uhusiano wa kawaida kati ya mwanadamu na Mungu, na huvuruga maono ya awali ya watu na njia ambayo maisha yao yameingia, katika mioyo yao hawawezi kamwe kumkaribia Mungu, daima mambo hufanyika ambayo huwasababishia vurugu na kuwatia pingu, na mioyo yao haiwezi kupata amani, kuacha upendo wao wa Mungu bila nguvu, na kuwafanya kusononeka. Hayo ndiyo maonyesho ya kazi ya Shetani. Kazi ya Shetani inadhihirishwa katika yafuatayo: kutoweza kushikilia msimamo na kuwa na ushuhuda, kukusababisha kuwa mtu ambaye ana makosa mbele ya Mungu, na ambaye hana uaminifu kwa Mungu. Kwa kuingilia kwa Shetani, unapoteza upendo na uaminifu kwa Mungu ndani yako, unaondolewa uhusiano wa kawaida na Mungu, hufuatilii ukweli, ama kujiendeleza, unarudi nyuma, na kuwa baridi, unajipendeza, unaachia uenezaji wa dhambi, na huchukii dhambi; zaidi ya hayo, kuingilia kwa Shetani kunakufanya mpotovu, kunasababisha mguso wa Mungu kutoweka ndani yako, na kunakufanya kulalamika kuhusu Mungu na kumpinga Yeye, kukufanya uwe na shaka na Mungu, na hata kuna hatari ya wewe kumwacha Mungu. Hii yote ni kazi ya Shetani.

Wakati kitu kinakufanyikia katika maisha yako ya kila siku, unapaswa kutofautishaje kati ya iwapo kinatoka kwa kazi ya Roho Mtakatifu ama kwa kazi ya Shetani? Wakati hali za watu ni za kawaida, maisha yao ya kiroho na maisha yao katika mwili ni ya kawaida, na mantiki yao ni ya kawaida na ya mpangilio; kwa jumla kile wanachokipitia na kuja kujua ndani yao wakati huu kinaweza kusemwa kutoka kwa kuguswa na Roho Mtakatifu (kuwa na umaizi au kumiliki maarifa ya juu juu unapokula na kunywa maneno ya Mungu, au kuwa mwaminifu wakati mambo yanakufanyikia, au kuwa na nguvu ya kumpenda Mungu wakati mambo yanafanyika—haya yote ni ya Roho Mtakatifu). Kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya mwanadamu hasa ni ya kawaida: mwanadamu hana uwezo wa kuihisi, na inaonekana kuwa ni kupitia kwa mwanadamu mwenyewe—lakini kwa kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu. Katika maisha ya kila siku, Roho Mtakatifu hufanya kazi ndogo na kubwa kwa kila mtu, na ni tu kwamba kiwango cha kazi hii hubadilika. Watu wengine ni wa ubora mzuri wa tabia, wanaelewa mambo haraka, na nuru ya Roho Mtakatifu hasa ni kubwa ndani yao; watu wengine ni wa ubora duni wa tabia, na inachukua muda mrefu zaidi kwao kuelewa mambo, lakini Roho Mtakatifu huwagusa ndani, na wao, pia, wanaweza kutimiza uaminifu kwa Mungu—Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa wale wote wanaomfuatilia Mungu. Wakati, katika maisha ya kila siku, watu hawampingi Mungu, au kuasi dhidi ya Mungu, hawafanyi mambo ambayo yanazozana na usimamizi wa Mungu, na hawakatizi kazi ya Mungu, ndani ya kila mmoja wao Roho wa Mungu hufanya kazi kwa kiwango kikubwa au kidogo, na kuwagusa, kuwapa nuru, kuwapa nguvu, na kuwasisimua kuingia kimatendo, sio kuwa wazembe au kutamani raha za mwili, kuwa tayari kutenda ukweli, na kutamani maneno ya Mungu—hii yote ni kazi ambayo hutoka kwa Roho Mtakatifu.

Wakati hali ya watu si ya kawaida, wanatelekezwa na Roho Mtakatifu, kuna malalamishi ndani yao, motisha zao si sahihi, wao ni wazembe, wanajiingiza katika tamaa za kimwili, na mioyo yao huasi dhidi ya ukweli, na haya yote hutoka kwa Shetani. Wakati hali za watu si za kawaida, wakati wana uovu ndani yao na wamepoteza mantiki yao ya kawaida, wametelekezwa na Roho Mtakatifu, na hawawezi kuelewa Mungu ndani yao, huu ndiyo wakati Shetani anafanya kazi ndani yao. Ikiwa watu daima wana nguvu ndani yao na daima humpenda Mungu, basi kwa jumla wakati mambo yanawafanyikia yanatoka kwa Roho Mtakatifu, na yeyote wanayekutana naye ni tokeo la mipango ya Mungu. Ambayo ni kusema, wakati hali zako ni za kawaida, wakati upo katika kazi kubwa ya Roho Mtakatifu, basi haiwezekani Shetani kukufanya uyumbayumbe; juu ya msingi huu inaweza kusemwa kwamba kila kitu hutoka kwa Roho Mtakatifu, na ingawa unaweza kuwa na mawazo yasiyo sahihi, unaweza kuyakataa, na usiyafuate. Hii yote hutoka kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Shetani huingilia katika hali zipi? Wakati hali zako si za kawaida, wakati hujaguswa na Mungu, na uko bila kazi ya Mungu, na wewe ni mkavu na bure ndani, wakati unasali kwa Mungu lakini huelewi chochote, na kula na kunywa maneno ya Mungu lakini hujapewa nuru au mwangaza—wakati kama huo ni rahisi kwa Shetani kufanya kazi ndani yako. Kwa maneno mengine, wakati umeachwa na Roho Mtakatifu na huwezi kumwelewa Mungu, basi mambo mengi hukufanyikia ambayo hutoka kwa majaribu ya Shetani. Shetani hufanya kazi wakati sawa na ule Roho Mtakatifu hufanya kazi, na huingilia kwa mwanadamu wakati sawa na ule Roho Mtakatifu hugusa ndani ya mwanadamu; wakati kama huo, hata hivyo, kazi ya Roho Mtakatifu huchukua nafasi ya kwanza, na watu ambao hali zao ni za kawaida wanaweza kushinda, ambao ni ushindi wa kazi ya Roho Mtakatifu juu ya kazi ya Shetani. Lakini wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, kuna kazi kidogo sana ya Shetani; wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi bado kuna tabia ya kutotii ndani ya watu, na yote ambayo kiasili yalikuwa ndani yao bado yamo hapo, lakini na kazi ya Roho Mtakatifu ni rahisi kwa watu kujua mambo muhimu kuwahusu na tabia yao asi kwa Mungu—ingawa wanaweza tu kujiondolea hayo wakati wa kazi ya polepole. Kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni ya kawaida, na Anapofanya kazi kwa watu bado wana shida, bado wanalia, bado wanateseka, bado ni dhaifu, na bado kuna mengi ambayo si dhahiri kwao, ilhali katika hali kama hiyo wanaweza kujisitisha kurudia mazoea mabaya, na wanaweza kumpenda Mungu, na ingawa wanalia na wana dhiki ndani, bado wanaweza kumsifu Mungu; kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni ya kawaida, na si ya mwujiza hata kidogo. Watu wengi sana huamini kwamba, punde tu Roho Mtakatifu huanza kufanya kazi, mabadiliko hutokea katika hali ya watu na mambo muhimu kuwahusu yanaondolewa. Imani kama hizo ni za uwongo. Roho Mtakatifu afanyapo kazi ndani ya mwanadamu, mambo baridi ya mwanadamu bado yako hapo na kimo chake kinabaki sawa na awali, lakini ana mwangaza na nuru ya Roho Mtakatifu, hali yake ni ya kimatendo zaidi, hali ndani yake ni za kawaida, na anabadilika kwa haraka. Katika uzoefu wa kweli wa watu, kimsingi wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu au Shetani, na iwapo hawawezi kuwa na madaraka juu ya hali hizi, na hawatofautishi, basi uzoefu wa kweli hauwezekani, sembuse mabadiliko katika tabia. Hivyo, ufunguo wa kuwa na uzoefu wa Mungu ni kuweza kubaini mambo kama haya; kwa njia hii, itakuwa rahisi zaidi kwao kupitia.

Kazi ya Roho Mtakatifu ni maendeleo ya kimatendo, ilhali kazi ya Shetani ni kurudi nyuma na hali ya ubaridi, kutotii Mungu, kumpinga Mungu, kupoteza imani kwa Mungu, na kutotaka hata kuimba nyimbo ama kuinuka na kucheza ngoma. Kile ambacho hutoka kwa nuru ya Roho Mtakatifu hakilazimishwi kwako, lakini hasa ni cha asili. Ukikifuata, utakuwa na ukweli, na usipo, basi baadaye kutakuwa na shutuma. Kama ni nuru ya Roho Mtakatifu, basi hakuna ufanyacho kitakachoingiliwa au kuzuiliwa, utawekwa huru, kutakuwa na njia ya kutenda katika vitendo vyako, na hutapatwa na vizuizi vyovyote, na kuweza kutekeleza mapenzi ya Mungu. Kazi ya Shetani huleta mambo mengi ambayo husababisha kukatiza kwako, inakufanya kutotaka kusali, kuwa mzembe sana kula na kunywa maneno ya Mungu, na kutotaka kuishi maisha ya kanisa, na inakutenganisha na maisha ya kiroho. Kazi ya Roho Mtakatifu haiingilii maisha yako ya kila siku, na haiingilii kuingia kwako katika maisha ya kawaida ya kiroho. Katika mambo mengi yanayokufanyikia, huwezi kutofautisha wakati huo. Hata hivyo, baada ya siku chache, unaishi kwa kudhihirisha kiasi, na kuonyesha kiasi, na kuna mijibizo fulani ndani yako, na kupitia maonyesho haya unaweza kujua iwapo mawazo ndani yako yanatoka kwa Mungu au kwa Shetani. Mambo mengine kwa dhahiri yanakufanya umpinge Mungu na kuasi Mungu, au kukusitisha kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo, na mambo haya yote hutoka kwa Shetani. Mambo mengine si dhahiri, na huwezi kujua ni nini wakati huo; baadaye, wakati umeona maonyesho yao, unaweza kujua yapi yanatoka kwa Shetani na yapi yanaelekezwa na Roho Mtakatifu. Baada ya kufahamu mambo kama hayo kwa dhahiri, hutapotoshwa kwa urahisi katika uzoefu wako. Wakati mwingine, hali zako zisipokuwa nzuri, una mawazo fulani yanayokutoa katika hali yako baridi—ambalo huonyesha kwamba wakati hali zako ni zisizofaa, mawazo yako mengine yanaweza pia kutoka kwa Roho Mtakatifu. Sio ukweli kwamba wakati wewe ni baridi, mawazo yako yote yanatumwa na Shetani; huo ungekuwa ukweli, basi ni lini ungeweza kugeukia hali ile nzuri? Baada ya kuwa baridi kwa kipindi cha muda, Roho Mtakatifu anakupa fursa kukamilishwa, Anakugusa, na kukutoa katika hali yako baridi.

Baada ya kujua kazi ya Roho Mtakatifu ni ipi, na kazi ya Shetani ni ipi, unaweza kulinganisha haya na hali yako mwenyewe wakati wa uzoefu wako, na uzoefu wako mwenyewe, na kwa njia hii kutakuwa na ukweli mwingi zaidi unaohusiana na kanuni katika uzoefu wako. Baada ya kuelewa mambo haya, utaweza kudhibiti hali yako halisi, na utaweza kuwa na utambuzi kwa watu na mambo yanayokufanyikia[a], na hutahitajika kutumia nguvu nyingi sana katika kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Bila shaka, hiyo ni ilimradi motisha zako ziko sahihi, na ilimradi uko tayari kutafuta, na kutenda. Lugha kama hii—lugha inayohusiana na kanuni—inapaswa kuonyeshwa katika uzoefu wako. Bila hiyo, uzoefu wako utakuwa umejaa kukatizwa na Shetani, na umejaa maarifa ya upuuzi. Ikiwa huelewi jinsi Roho Mtakatifu hufanya kazi, basi huelewi jinsi unapaswa kuingia, na ikiwa huelewi jinsi Shetani hufanya kazi, basi huelewi jinsi unapaswa kuwa mwangalifu katika nyayo zako. Watu wanapaswa kuelewa jinsi Roho Mtakatifu hufanya kazi na jinsi Shetani hufanya kazi; ni sehemu ya lazima ya uzoefu wa watu.

Ingawa unamwamini Mungu pekee, je, una uhusiano wa kawaida na Mungu? Watu wengine husema la muhimu tu ni kuwa wana uhusiano wa kawaida na Mungu, na hawajishughulishi na uhusiano na wengine. Lakini uhusiano wa kawaida na Mungu unadhihirishwa vipi? Je, watu kama hao sio wasio na maarifa halisi hata kidogo? Mbona inasemwa kwamba kiwango cha uamuzi wako kumpenda Mungu, na iwapo kweli umeukataa mwili, kinategemea iwapo una chuki bila sababu kwa ndugu zako, na iwapo, kama una chuki bila sababu, unaweza kuweka kando chuki bila sababu kama hiyo. Ambayo ni kusema, wakati uhusiano wako na ndugu zako ni wa kawaida, basi hali zako mbele ya Mungu pia ni za kawaida. Wakati mmoja wa ndugu zako ni dhaifu, hutamchukia, kumdharau, kumtania, ama kutomthamini. Ikiwa unaweza kumsaidia, utawasiliana naye na kusema, “Nilikuwa baridi na dhaifu. Kwa kweli sikutaka kuhudhuria mkutano, lakini kitu kilifanyika ambacho kupitia kwacho Mungu alinipa nuru ndani na kunifundisha nidhamu; nilishutumiwa ndani, nilikuwa na aibu sana, na daima nilimhurumia Mungu. Baadaye, nilijitolea kwa maisha ya kanisa, na kadiri nilivyojishughulisha na ndugu, ndivyo nilihisi zaidi singeweza kumudu bila Mungu, Nilipokuwa na wao sikuhisi mpweke; nilipokuwa chumbani peke yangu nilihisi mpweke na asiye na rafiki, Nilihisi kuwa maisha yangu yalikuwa matupu, na mawazo yangu yaligeukia kifo. Sasa kwa kuwa nilikuwa na ndugu zangu, Shetani hakuthubutu kufanya kazi yake, na sikuhisi mpweke. Nilipoona jinsi upendo wa ndugu zangu kwa Mungu ulikuwa wa nguvu, nilitiwa moyo, na hivyo daima nilikuwa na ndugu zangu, na hali yangu ya baridi ikatoweka kwa kawaida.” Baada ya kusikia hili, anahisi kwamba ni bure kusali nyumbani, bado anahisi kwamba hakuna upendo kati ya ndugu zake, kwamba maisha yake ni matupu, kwamba hana mtu wa kutegemea na kwamba haitoshi kusali tu. Ukiwasiliana na yeye kwa njia hii, basi atakuwa na njia ya kutumia kutenda. Ukihisi huwezi kumkimu, basi unaweza kumtembelea. Si lazima hili lifanywe na kiongozi wa kanisa—ni jukumu la kila ndugu kufanya kazi hii. Ukiona kwamba kaka au dada yuko katika hali mbaya, unapaswa kumtembelea. Hili ni jukumu la kila mmoja wenu.

Tanbihi:

a. Maandiko asilia yameacha “yanayokufanyikia.”

Chanzo: Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetan

Views: 112 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: kazi ya Roho Mtakatifu, kumjua mungu, neno la Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar