1:13 PM
Utendaji (7)

Ubinadamu wenu ni wenye upungufu mno, hali yenu ya maisha ni ya chini na kushusha hadhi mno, hamna ubinadamu, na hamna utambuzi. Hiyo ndiyo maana mnahitaji kujiandaa na mambo ya ubinadamu. Kuwa na dhamiri , urazini, na utambuzi, kujua jinsi ya kuzungumza na kutazama vitu, kuwa makini kwa usafi, kutenda kama binadamu wa kawaida—vyote hivi ni ufundi ustadi wa ubinadamu wa kawaida. Mnapofanya hivi vizuri, ubinadamu wenu ni wa kiwango kinachohitajika. Kipengele kingine ni kujihami kwa ajili ya maisha yenu ya kiroho. Lazima mjue kazi yote ya Mungu duniani na muwe na uzoefu wa maneno Yake. Unapaswa kujua jinsi ya kutii mipangilio Yake, na jinsi ya kutimiza majukumu ya kiumbe aliyeumbwa. Hivi ndivyo vipengele viwili unavyopaswa kuingia ndani yake leo. Kipengele kimoja ni kujiandaa kwa ajili ya maisha ya ubinadamu, na kipengele kingine ni kutenda kuhusu maisha ya kiroho—na vyote viwili ni vya lazima. Watu wengine ni wapumbavu, na wanajua tu kujiandaa na yale ambayo yanahusu ubinadamu Wanavaa mavazi ya kupendeza na nywele zao huwa safi kila mara; hakuna dosari inayoweza kupatikana katika sura zao. Vitu wasemavyo na mwenendo wao wa kuzungumza ni wa kufaa, na nguo zao ni zenye heshima mno na sahihi. Lakini hawana chochote ndani yao; ubinadamu wao wa kawaida ni wa nje tu. Wanalenga tu kile cha kula, kile cha kuvaa, na kile cha kusema. Kuna hata wale ambao wanalenga mahsusi kufagia sakafu, kurundika vitani vya vitanda, na kusafisha Wamefanya mazoezi mazuri katika mambo haya, lakini unapowauliza wazungumze kuhusu ufahamu wao wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na kuhusu kuadibu, usafishaji, majaribu, na hukumu, basi hawana hata tajriba kidogo ya mambo kama haya. Unawauliza: “Je, unaelewa kazi ya msingi ambayo Mungu hufanya duniani?” Ni nini kazi iliyofanywa na Mungu aliyepata mwili? Iko tofauti vipi na kazi ya Yesu? Na inatofautiana vipi na kazi ya Yehova? Wao ni Mungu mmoja? Amekuja kuleta kuhitimisha enzi, ama kumwokoa mwanadamu? Kazi ambayo Yeye hufanya ni ipi? Hawatakuwa na lolote la kusema kuhusu hili. Kijuujuu, wamepambwa vizuri: Akina dada wamejitayarisha kupendeza kama maua, na kaka wanaonekana kama wana wafalme, ama kama vijana tajiri fulani walio safi sana. Wao wanajali tu kuhusu vitu wanavyokula na kuvaa kwa nje; ndani, wao ni fukara, na hawana hata kiwango kidogo cha ufahamu wa Mungu. Kuna haja? Wengine wamevalia kikoo, kama waombaji, na wanakaa kama watumwa wa pande za mashariki! Je, kwa kweli hamwelewi yale Ninauliza kutoka kwenu? Wasilianeni miongoni mwenu: Mmefaidi nini? Mmekuwa mkitafuta kwa miaka hii yote, na haya ndiyo yote mliyovuna—hamhisi fedheha? Hamna aibu? Mmetafuta njia ya ukweli kwa miaka hii yote, na leo kimo chenu ni hata kidogo kuliko cha jurawa. Tazamaneni wanawake vijana miongoni mwenu, wamejitayarisha kupendeza kama maua, mwajilinganisha ninyi. Ni kipi mnachotumia kujilinganisha? Je, sio raha? Na madai mnayoweka? Je, mnadhani Nimekuja kusajili waonyeshaji mitindo? Nyinyi hamna aibu! Maisha yenu yako wapi? Je, nyinyi hamtafuti tamaa badhirifu? Unafikiri kuwa wewe ni mrembo sana. Unaweza kuwa mrembo sana, lakini wewe sio buu anayefurukuta aliyezaliwa ndani ya rundo la samadi? Leo, kwamba una bahati kufurahia hizi baraka za mbinguni ni kwa sababu Mungu anafanya jambo la kipekee kwa kukuinua wewe juu, na sio kwa sababu ya uso wako mzuri; bado wewe huko wazi kuhusu kule ulikotoka? Kwa kutajwa kwa uzima unafunga mdomo wako na husemi lolote, wewe ni kama vifaranga vya mbao, ilhali bado una ujasiri wa kujipaka vipodozi? Bado unafikiri kuweka poda usoni mwako? Na tazameni wapenda sana starehe kati yenu—ni wapotovu zaidi, wao wanashinda siku nzima wakielea huku na kule, wakiwa na sura isiyoonyesha kupenda nyusoni mwao. Wana tabia mbaya popote waendako, kuna chochote cha kibinadamu kuwahusu? Ni nini ambacho kila mmoja kati yenu, awe mwanamme ama mwanamke, hutolea uangalifu wake kila siku? Je mnajua yule mnayemtegemea ili kula? Tazama mavazi yako, tazama kile umevuna mikononi mwako, sugua tumbo lako—ni nini matunda ya gharama ya damu na jasho ambayo umelipa? Wewe bado unafikiri kuenda kutalii sehemu maarufu, wewe bado unafikiri kupamba mwili wako wenye uvundo—ni nini thamani ya haya? Unaulizwa kuwa wa kawaida, lakini leo wewe si tu wa kawaida, uko kinyume. Ni vipi mtu wa namna hii anaweza kuthubutu kuja mbele Yangu? Na ubinadamu kama huu, kujionyesha na kufichua mwili wako, kila mara kuishi kati ya tamaa ya mwili, wewe sio mzawa wa mapepo wachafu na roho wabaya? Sitaruhusu pepo mchafu kama huyo kusalia kwa muda mrefu! Na usifikiri kwamba sijui ni nini unachofikiria moyoni mwako. Unaweza kudhibiti vikali tamaa na mwili wako, lakini Singeweza kujua fikira iliyo ndani ya moyo wako na yote ambayo macho yako yatamani? Je, nyinyi wanawake wadogo hamjitayarishi kupendeza kama maua ili kuonyesha miili yenu? Wanaume ni wa faida gani kwenu? Wanaweza kweli kuwaokoa nyinyi kutoka ziwa la mateso? Na nyinyi wanaume wapenda sana starehe nyote mnavaa kujifanya muonekane waungwana na wenye heshima—sio ili kuonyesha sura zenu? Na ni nani mnayemfanyia haya? Wanawake ni wa manufaa gani kwenu? Wao sio chanzo cha dhambi zenu? Nyinyi wake na waume, Nimenena maneno mengi kwenu, ilihali mmetekeleza machache kwa hayo. Masikio yenu ni mazito, macho yenu yameingia giza, na nyoyo zenu ni ngumu, kiasi kwamba hakuna chochote ila tamaa katika miili yenu; mmetegwa ndani yake, hamuwezi kutoroka. Nani anayetaka kwenda mahali popote karibu na nyinyi mabuu, wanaofurukuta kwa taka na uchafu? Msisahau kwamba nyinyi sio kitu zaidi ya wale ambao Nimewainua kutoka kwenye rundo la samadi, kwamba mwanzoni, hamkuwa na ubinadamu wa kawaida. Ninachoomba kwenu ni ubinadamu wa kawaida ambao hamkuwa nao awali; Siulizi kwamba muonyeshe tamaa yenu, au kwamba muipe uhuru miili yenu iliyooza, ambayo imefundishwa na ibilisi kwa miaka mingi. Mnapojivisha nguo hivi, hamwogopi kuwa mtategwa zaidi milele? Je, hamjui kwamba kiasili mlikuwa wa dhambi? Je, hamjui kwamba miili yenu imejazwa na tamaa? Ni kiasi kwamba tamaa zenu hata zimepenya kutoka kwenye mavazi yenu, zikifichua hali yenu kama pepo mchafu, mbaya asiyevumilika. Je, si hii ndiyo iliyo wazi kabisa kwenu nyote? Mioyo yenu, macho yenu, midomo yenu—je, si yote yamechafuliwa na pepo wachafu? Je, hayo si machafu? Unadhani kwamba mradi tu usipofanya chochote kilicho kiovu,[a] wewe ni mtakatifu zaidi; unadhani kuvaa vizuri kunaweza kufunika nafsi zenu duni—hakuna uwezekano wa hilo! Ninawashauri kuwa wa kweli zaidi: msiwe wadanganyifu na bandia, wala msijitembeze. Mnaringiana tamaa yenu, lakini yote mtakayopata ni mateso ya milele na adabu katili! Je, una haja gani kuonyeshana mapenzi na kuwa katika mapenzi? Je! Huu ni uadilifu wenu? Je, hii inawafanya wenye nguvu? Ninawachukia wale miongoni mwenu wanaotenda tiba ya uchawi na kushiriki katika usihiri, Nawachukia vijana kati yenu wanaopenda miili yao wenyewe. Itakuwa vyema mkijizuia, kwa kuwa leo Ninaomba umiliki ubinadamu wa kawaida, sio kwamba uringe kwa sababu ya tamaa yako. Daima mnachukua fursa yoyote mnayoweza, kwa kuwa miili yenu ni maridhawa sana, na tamaa yenu ni kubwa sana!

Kwa nje, umepanga maisha yako ya ubinadamu vizuri sana, lakini unapoulizwa kuzungumza juu ya ujuzi wa maisha, huna chochote cha kusema—na katika hili wewe ni dhaifu. Lazima ujitayarishe na ukweli! Maisha yako ya ubinadamu yamebadilika kuwa bora, na maisha ndani yako yatabadilika pia—kubadilisha mawazo yako na kubadilisha maoni yako juu ya imani katika Mungu, kubadilisha ufahamu na fikira ndani yako, na kubadilisha ufahamu wa Mungu ndani ya mawazo yako. Kupitia ushughulikiaji, ufunuo, na utoaji, hatua kwa hatua unabadilisha ujuzi wako mwenyewe, kuwepo kwako, na imani katika Mungu, kuruhusu ujuzi wako kuwa safi. Kwa njia hii, mawazo ndani ya mwanadamu yatabadilika, jinsi wanavyoona vitu itabadilika, na mtazamo wao wa akili utabadilika. Hapo tu ndipo tabia ya maisha yao itakuwa imebadilika. Huulizwi kushinda siku nzima ukisoma vitabu, au kupanga vizuri chumba chako au kuosha nguo na kusafisha. Kwa kawaida, hakupaswi kuwa na masuala na ubinadamu wako wa kawaida—hiki ni kiwango cha chini sana kinachohitajika. Unapoenda nje, bado unapaswa kuwa na ufahamu na urazini, lakini muhimu zaidi ni kwamba umejitayarisha na ukweli wa maisha. Wakati mambo kuhusu roho yanasemwa, wewe unapaswa kupuuza hoja ya ubinadamu; hiyo si sahihi. Wakati unajitayarisha kuhusiana na maisha, lazima uweze kuzungumza juu ya ufahamu wa Mungu, ya maoni yako juu ya kuwepo, na, hasa, ufahamu wako kuhusu kazi iliyofanywa na Mungu wakati wa siku za mwisho. Kwa kuwa unafuatilia maisha, lazima ujiweke tayari na mambo haya. Unapokula na kunywa maneno ya Mungu, lazima uyapime dhidi ya hali yako halisi. Hiyo ni, baada ya kugundua upungufu ndani yako mwenyewe wakati wa uzoefu wako wa kweli, lazima uwe na uwezo wa kupata njia ya kutenda, na kukwepa motisha na mawazo yako ambayo si sahihi. Ikiwa daima utajitahidi sana katika hili, na moyo wako daima unazingatia mambo haya, utakuwa na njia ya kufuata, hutahisi mtupu, na hivyo utakuwa na uwezo wa kudumisha hali ya kawaida. Hapo tu ndipo utakuwa mtu ambaye ametwishwa mzigo na maisha yako mwenyewe, na hapo tu ndipo utakuwa mtu mwenye imani. Kwa nini, baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu hawawezi kuyaweka katika vitendo? Je, si ni kwa sababu hawawezi kufahamu ni nini muhimu? Je, si ni kwa sababu wao wanacheza na maisha? Kwamba hawawezi kufahamu ni nini muhimu, na hawana njia ya kutenda, ni kwa sababu hawawezi kutathmini hayo dhidi ya hali yao wenyewe, na hawawezi kuwa na ujuzi wa hali yao wenyewe. Watu wengine husema: Nimeyatathmini dhidi ya hali yangu, najua kwamba mimi ni mpotovu na mwenye ubora wa tabia ya chini, lakini siwezi kukidhi mapenzi ya Mungu. Katika hili, umeona tu juu; jinsi ya kuweka kando raha ya mwili, jinsi ya kuweka kando kujidai, jinsi ya kujibadilisha mwenyewe, jinsi ya kuingia mambo haya, jinsi ya kuboresha ubora wa tabia yako, kuanzia kipengele kipi—haya yote ni yale yaliyo kweli. Unafahamu tu mambo machache ya nje, unajua tu kwamba wewe ni mbaya kabisa. Unapokutana na kaka zako na dada zako, unazungumza juu ya jinsi ulivyo mpotovu, na inaonekana kuwa unajua jambo hili, na kwamba unasumbuliwa na maisha yako. Kwa kweli, hujabadilika, ambayo inathibitisha kuwa haujapata njia ya kutenda. Ikiwa unaongoza kanisa, unapoonyesha hali ya kaka na dada katika kanisa, unaweza kusema: "Hakuna mahali penye maendeleo kidogo mno zaidi kuliko hapa; ninyi watu ni wasio watiifu!" Kuhusu ni kwa nini wao ni wasiotii na wenye maendeleo kidogo mno, unapaswa kuzungumza juu ya maonyesho yao—ya hali yao ya kutotii na tabia ya kutotii—na kuwafanya wasadikike kabisa. Lazima uzungumze juu ya ukweli na kutoa mifano ya kuelezea suala hilo, na lazima pia uweze kuzungumza juu ya jinsi ya kujitenga na tabia hii ya uasi kwa kweli, na lazima uonyeshe njia ya kutenda. Ni hapo tu ndipo utawashinda! Ikiwa unasema tu, "Sitaki kutembelea mahali hapa; hakuna aliye mwenye maendeleo kidogo zaidi kukuliko nyinyi, nyinyi ni waasi mno, “basi, unaposema kwa njia hii, baada ya kusikiliza hakuna hata mmoja wao atakuwa na njia—na hivyo je, utawaongozaje watu? Lazima uongee kuhusu hali yao halisi na maonyesho halisi; ni hapo tu ndipo utakuwa na njia ya kutenda, na ni hapo tu ndipo utakuwa na ukweli.

Kufikia leo, ukweli mwingi umetolewa. Lakini lazima uone uhusiano kati ya mambo haya: Unapaswa kuwa na uwezo wa kuhitimisha ni ukweli ngapi uliopo. Ni vipengele vipi vya ubinadamu wa kawaida ambavyo mtu anapaswa kumiliki, vipengele vikuu vya mabadiliko kwa tabia ya maisha ya mtu, maono kuwa ya kina, ni njia zipi zisizo sahihi za kujua na kupitia kwa watu katika enzi zote ambazo umepata kuelewa—utaingia tu katika njia sahihi wakati una uwezo wa kutofautisha na kujua mambo haya. Watu wa dini wanaabudu Biblia kana kwamba ni Mungu. Hasa, wanatazama Injili Nne za Agano Jipya kama nyuso nne za Yesu. Vilevile, pia, kuna majadiliano ya Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Haya ni ya upumbavu zaidi ya yote. Lazima nyote myabaini, na zaidi ya hayo, lazima mjue dutu ya Mungu kuwa mwili na kazi ya siku za mwisho. Pia kuna mbinu za zamani za kutenda: kuishi katika roho, kujazwa na Roho Mtakatifu, kukubali bila malalamiko katika hali ya shida, kutii mamlaka—lazima pia ujue uongo huu na mkengeuko unaohusiana na kutenda; unapaswa kujua[b] jinsi watu walivyotenda awali, na jinsi watu wanapaswa kutenda leo. Jinsi wafanyakazi wanapaswa kushirikiana katika makanisa, jinsi ya kuweka kando kujidai na kutotegemea hali, jinsi kaka na dada wanapaswa kuhusiana, jinsi ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na watu wengine na Mungu, jinsi ya kufanikisha ukawaida katika maisha ya kibinadamu, kile ambacho watu wanapaswa kuimiliki katika maisha yao ya kiroho, jinsi wanapaswa kula na kunywa maneno ya Mungu, yanayohusiana na ujuzi, na nini kinachohusika na maono, ni njia gani ya kutenda—vitu hivi vyote havijazungumziwa ? Maneno haya ni wazi kwa wale wanaofuatilia, na hakuna mtu anayetendewa kwa upendeleo. Leo, mnapaswa kuendeleza uwezo wa kuishi kwa kujitegemea. Ikiwa daima mna fikira ya utegemezi, basi baadaye, wakati hakuna mtu wa kukuongoza, utafikiria maneno haya Yangu. Wakati wa dhiki, haiwezekani kuishi maisha ya kanisa: Ndugu hawawezi kukutana, wengi wao wako peke yao na wanaweza tu kuwasiliana na watu wa sehemu moja, na hivyo kimo chako cha sasa hakitoshi. Katika dhiki, wengi wataona vigumu kusimama imara. Ni wale tu ambao wanajua njia ya uzima na waliojiandaa na ukweli ndio wanaweza kuzidi kuendelea na kutimiza utakatifu. Sio rahisi kwako kupitia matata; ikiwa unafikiri inachukua siku chache tu kustahimili dhiki, basi wewe ni wa kawaida sana katika kufikiri kwako! Unafikiri kwamba kwa kula na kunywa maneno ya Mungu kwa upofu, wakati unapokuja utakuwa na uwezo wa kusimama imara—hiyo sivyo! Ikiwa hujui mambo haya ya msingi, huwezi kuelewa ni nini muhimu, na huna njia ya kutenda, basi wakati unapokuja na kitu kikufanyikie, utafadhaishwa, hutaweza kustahimili jaribio la Shetani, wala mwanzo wa usafishaji. Ikiwa hakuna ukweli ndani yako na unakosa maono, basi wakati unapokuja hutaweza kujizuia kuanguka; wakati huo utaacha tumaini lote na kusema, "Naam, ninaenda kufa hata hivyo, afadhali niadibiwe mpaka mwisho kabisa! Haijalishi kwangu, iwe kuadibiwa au kwenda katika ziwa la moto, navikubali vyote viwili—nitayachukua mambo vile yanavyokuja!” Ni kama wakati wa watenda huduma: Watu walidhani kwamba[c] kwa sababu walikuwa watenda huduma, haikuwabidi kufuata maisha, na kwamba ilikuwa ni sawa kuvuta sigara na kunywa. Kutazama televisheni, kutazama filamu—walifanya yote. Wakati mazingira ni makali, ikiwa huwezi kuyashinda, utaacha tumaini lote mara tu utakapojiachilia kidogo. Kwa njia hii, bila wewe kutambua, utachukuliwa mateka na Shetani. Ikiwa huwezi kushinda ushawishi wa Shetani, utachukuliwa mateka na Shetani, na utapelekwa kwa maangamizi tena. Na hivyo, leo unapaswa kujitayarisha, lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kujitegemea, na unaposoma maneno ya Mungu lazima uweze kutafuta njia ya kutenda. Ikiwa hakuna mtu anayekuja kanisani kufanya kazi, unapaswa bado kuwa na njia ya kufuata, unapaswa kupata upungufu wako, na kupata ukweli unaopaswa kuweka katika vitendo na kujitayarisha nao. Baada ya kuja duniani, je, Mungu atafuatana milele na mwanadamu? Katika mawazo yao, baadhi ya watu wanaamini hili: Usipotufinyanga kwa kiwango fulani, kazi Yako haiwezi kuchukuliwa kama iliyomalizika, kwa maana Shetani anakushutumu. Nakwambia, Nitakapomaliza kuzungumza maneno Yangu hapo ndio wakati Nimekamilisha kazi Yangu kwa mafanikio. Mradi tu maneno Yangu yameisha, kazi Yangu itakuwa imekamilika. Mwisho wa Kazi Yangu ni ushahidi wa kushindwa kwa Shetani, na hivyo inaweza kusema kuwa imekamilika kwa ufanisi, bila ya mashtaka ya Shetani. Lakini wakati kazi Yangu imeisha, ikiwa bado hakujakuwa na mabadiliko yoyote kwenu, basi watu kama nyinyi ni wasiookoleka na mtaondolewa; Sifanyi kazi yoyote zaidi kuliko inayohitajika. Sio kweli kwamba Nitamaliza kazi Yangu duniani wakati umeshindwa kwa kiwango fulani—wakati nyote mna ufahamu ulio wazi, ubora wa tabia yako umeendelezwa, na unakuwa na ushuhuda ndani na nje. Hiyo ingekuwa haiwezekani! Leo, kazi Ninayofanya ndani yenu ni ili kuwaongoza katika maisha ya kawaida, na ili kuikaribisha enzi mpya na kuongoza kazi mpya. Kazi hii, inayofanywa hatua kwa hatua, hufanyika kati yenu moja kwa moja: Mnafundishwa uso kwa uso, mkono kwa mkono; Nawaambia kitu chochote msichokielewa, Nikiwapa yote mliyokosa. Inaweza kusemwa kuwa, kwa ajili yenu, kazi hii yote ni utoaji wa maisha kwenu, na inawaongoza katika maisha ya ubinadamu wa kawaida; ni ya kutoa maisha ya kundi la watu wakati wa siku za mwisho pekee. Kwangu, kazi hii yote ni ili kukamilisha enzi na kuikaribisha enzi mpya; ikija kwa Shetani, Mungu alipata mwili ili Amshinde. Kazi Ninayofanya kati yenu sasa ni utoaji wa leo na wokovu wa wakati wa kufaa, lakini wakati wa miaka michache hii, Nitawaambia ukweli wote, njia ya uzima, na hata kazi ya siku zijazo, na itakuwa ya kutosha kwenu kupata uzoefu kwa kawaida katika siku zijazo. Maneno yote Ninayosema ndiyo ushawishi Wangu pekee kwenu. Mimi Sifanyi ushawishi mwingine; leo, maneno yote Nawaambieni ni ushawishi Wangu kwenu, kwa kuwa leo hamna uzoefu wa mengi ya maneno ambayo Ninayosema, wala hamwelewi maana ya ndani ya maneno haya. Siku moja, uzoefu wenu utapata mafanikio kama tu ambavyo Nimezungumzia leo. Maneno haya ni maono yenu ya leo, na ndiyo mtakayotegemea katika siku zijazo, ndiyo utoaji wa maisha leo, na ushawishi wa wakati ujao, na hakuna ushawishi ulio bora zaidi. Hiyo ni kwa sababu wakati Nilio nao wa kufanya kazi duniani sio muda mrefu kama wakati mlio nao wa kupitia maneno Yangu; Mimi Ninakamilisha tu kazi Yangu, wakati nyinyi mnafuatilia maisha, ambayo inahusisha safari ndefu ya maisha. Ni baada tu ya kupitia mambo mengi ndiyo mtaweza kupata njia ya uzima kabisa, hapo tu ndipo mtaweza kubaini maana ya ndani ya maneno Ninayosema leo. Katika mikono yenu, mna maneno Yangu, mmepata maagizo Yangu yote, mmeagizwa kwa yote mnayopaswa kuagizwa. Bila kujali athari inayopatikana ni kubwa kiasi gani, wakati kazi ya neno imefikia mwisho, mapenzi ya Mungu yametekelezwa. Sio kama unavyofikiri kwamba lazima ubadilishwe kwa kiwango fulani; Mungu hafanyi kulingana na mawazo yako.

Maisha ya watu hayakui katika siku chache tu. Wanaweza kuwa na vitu vingi vya kula na kunywa kila siku, lakini hivyo havitoshi—wanapaswa kupitie kipindi cha kukua katika maisha yao, huu ni mchakato muhimu. Na ubora wa tabia ambao watu wanao leo, maisha yao yanaweza kukua kwa kiasi gani? Mungu hufanya kazi kwa mujibu wa mahitaji ya watu, Akitoa madai yanayofaa kulingana na ubora wa tabia yao ya asili. Tuseme kwamba kazi hii ingetekelezwa kati ya kikundi cha watu wenye ubora wa tabia ya juu: Maneno Yake yangekuwa ya juu kuliko yale kati yenu, maono yangekuwa ya juu, na ukweli hata juu zaidi. Maneno ya Mungu yangepaswa kuwa kali zaidi, na yenye uwezo zaidi wa kutoa kwa mtu na kufichua siri. Akizungumza kati yao, Mungu angewakimu kulingana na mahitaji yao. Leo, madai yaliyotolewa kwenu yanaweza kusemwa kuwa ni madai ya juu kabisa iwezekanavyo kwenu; kama kazi hii ingetekelezwa katika wale w ubora wa tabia ya juu, basi madai ingekuwa ya juu bado. Kazi yote ya Mungu inafanywa kulingana na ubora wa tabia ya watu ya asili. Leo, hakuna kitu cha juu zaidi kuliko kiwango ambacho Mungu amewabadilisha na kuwashinda watu. Msitumie mawazo yenu wenyewe kupima matokeo ya hatua hii ya kazi. Mnapaswa kuwa wazi juu ya kile ambacho mnamiliki kiasili, na hampaswi kuwaangalia ninyi watu kama juu sana; kwa asili, hakuna mmoja wenu aliyefuatilia uhai, ninyi mlikuwa waombaji ambao walizurura mitaani. Kwa Mungu kukufinyanga kwa kiwango unachofikiria ambapo unasujudu kwenye ardhi, ukiwa umeshawishika kabisa, ni kama ulikuwa umeona maono mazuri—hiyo haingewezekana! Hiyo ni kwa sababu hakuna mtu ambaye hajaona ishara anaweza kuamini kikamilifu maneno Ninayosema. Mnaweza kuyachunguza kwa karibu, lakini bado hamngeyaamini kabisa; hii ni asili ya mwanadamu! Kwa wale wanaofuatilia, kutakuwa na mabadiliko fulani, wakati imani ya wale wasiofuatilia itapungua, na hata huenda ikatoweka. Tatizo kubwa na nyinyi ni kwamba hamwezi kuamini kabisa bila kuona kutimizwa kwa maneno ya Mungu, na hamjapatanishwa bila kuona ishara. Kabla ya mambo hayo, ni nani ambaye angeweza kuwa mwaminifu kwa Mungu bila kukosa? Na hivyo Nasema kwamba hammwamini Mungu, bali ishara. Kufikia leo, Nimesema kwa uwazi juu ya vipengele mbalimbali vya ukweli, Nikiandaa vipengele vyote vya ukweli, na ukweli huu pia huweza kutumikiana. Kwa hivyo, sasa lazima uuweke katika vitendo: Leo Ninakuonyesha njia, na katika siku zijazo, unapaswa kuuweka katika matendo mwenyewe. Leo, maneno Ninayosema yanatoa madai kwa watu kulingana na mazingira yao halisi, na Ninafanya kazi kulingana na mahitaji yao na mambo ndani yao. Mungu wa vitendo Amekuja duniani kufanya kazi ya vitendo, kufanya kazi kulingana na hali halisi ya watu na mahitaji yao; Yeye sio asiye na busara. Na wakati Mungu hutenda, Hawalazimishi watu. Kwa mfano, kama utaolewa inapaswa kuwa kulingana na hali yako halisi; ukweli umezungumzwa kwa dhahiri kwako, na Mimi sikuzuilii. Familia zingine zinanyanyasa watu kwa kiwango ambacho hawawezi kumwamini Mungu isipokuwa wakiolewa—hivyo ndoa, kinyume chake, ni kwa manufaa yao. Kwa watu wengine, ndoa haikosi tu kuleta faida, lakini huwapotezea yale waliyokuwa nayo awali. Hii lazima itegemee hali yako halisi na azimio lako mwenyewe. Sibuni sheria ambazo kwazo Natoa madai kwako. Watu wengi daima wanasema, "Mungu ni wa kweli, kazi Yake imetegemezwa kwa ukweli na kutekelezwa kulingana na mazingira yetu halisi"—lakini unajua ni nini kinachofanya iwe kweli? Usiseme maneno matupu siku nzima! Kazi ya Mungu ni ya kweli, na imewekwa kwa msingi wa kweli, haihusishi mafundisho, inatolewa katika ukamilifu wake, na yote ni wazi na isiyofichwa. Je, kanuni hizi zinajumuisha nini? Je, unaweza kusema ni kazi gani ya Mungu ambayo inahusika na hii? Lazima uzungumze juu ya mambo maalum, na lazima uwe umepitia na kuwa na ushuhuda katika vipengele kadhaa. Ni wakati tu kipengele hiki kiko wazi hasa kwako na unakijua ndio utakuwa na sifa zinazostahili kuzungumza maneno haya. Mtu akikuuliza: Ni kazi gani ambayo Mungu aliyepata mwili wa vitendo duniani Anapaswa kufanya? Kwa nini mnamwita Mungu wa vitendo? Je, "utendaji" unahusisha nini? Je! Unaweza kuzungumza juu ya kazi Yake ya vitendo, juu ya inajumuisha nini hasa? Yesu alikuwa Mungu aliyepata mwili, na Mungu wa vitendo ndiye pia Mungu aliyepata mwili—ni tofauti gani iliyopo kati Yao? Na usawa ni upi? Wamefanya kazi gani? Je, unaweza kusema? Yote haya ni kutoa ushuhuda! Usichanganyikiwe kuhusu mambo haya. Kuna wengine ambao husema: "Kazi ya Mungu wa vitendo ni halisi, kamwe Haonyeshi ishara na maajabu." Je, kweli Haonyeshi ishara na maajabu? Je, unajua jambo hili? Je, unajua kazi Yangu ni ipi? Ilisemwa kuwa ishara na maajabu hazingeonyeshwa, lakini kazi Anayofanya na maneno Anayosema sio ishara? Ilisemwa kuwa ishara na maajabu hazingeonyeshwa, lakini hiyo inategemea, inategemea maneno hayo yalizungumzwa kwa nani. Bila kwenda kanisani, Ameweka wazi hali za watu, na bila kutekeleza kazi nyingine yoyote, kwa kuzungumza tu, Amewahimiza watu kuendelea mbele—je, hizi si ishara? Kwa kusema maneno tu, Amewashinda watu, na bila matarajio au matumaini, watu bado wanafuata kwa furaha—hizi si ishara? Anapozungumza, maneno Yake huwaweka watu kwa hali fulani, moja ambayo wanaweza kujisikia kuwa wenye furaha au wenye uzito wa moyo, au waliosafishwa au kuadibiwa. Kwa maneno machache tu kali, Yeye huleta kuadibu kwa watu—je, hii sio ya mwujiza? Mtu anaweza kufanya jambo kama hilo? Ulisoma Biblia kwa miaka yote hiyo, lakini hukuelewa chochote, hukuona chochote, na wewe hukuweza kujitenga na njia hizo za amani zilizopitwa na wakati, za zamani, na hukuweza kuelewa Biblia. Ilhali Anaweza kubaini Biblia—je, hiki si kitu kisicho cha kawaida? Ikiwa hakungekuwa na kitu kisicho cha kawaida kuhusu Mungu wakati Alikuja duniani, Angeweza kuwashinda? Bila ya kazi Yake isiyo ya kawaida, ya kiungu, ni nani kati yenu ambaye angeshawishika? Kwa macho yako, inaonekana kama mtu wa kawaida anafanya kazi na anaishi nanyi—Anaonekana kuwa na sura ya mtu wa kawaida. Unachoona ni sura ya ubinadamu wa kawaida, lakini kwa kweli, Yeye anayefanya kazi ni wa kiungu. Yeye anayefanya kazi sio wa ubinadamu wa kawaida, bali ni wa kiungu; Huyu ni Mungu Mwenyewe, ni kwamba tu Yeye hutumia ubinadamu wa kawaida kufanya kazi—na matokeo yake ni kwamba kazi Yake ni ya kawaida na isiyo ya kawaida. Kazi Anayofanya haiwezi kufanywa na mwanadamu. Kazi ambayo haiwezekani kwa watu wa kawaida hufanywa na mtu asiye wa kawaida. Na bado, umiujiza huu ni takatifu; sio kwamba binadamu ni wa ajabu, lakini kwamba uungu ni tofauti na binadamu. Yule anayetumiwa na Roho Mtakatifu pia ni wa ubinadamu wa kawaida, lakini hawezi kufanya kazi hii. Hapa ndipo kuna tofauti. Unaweza kusema: "Mungu si Mungu asiye wa kawaida, Hafanyi chochote kisicho cha kawaida. Mungu wetu huzungumza maneno ambayo ni ya matendo na ya kweli, kwa kweli Ameenda kanisani kufanya kazi, kila siku Anazungumza nasi uso na uso, na, uso kwa uso, Anaonyesha hali zetu—Mungu hakika ni wa kweli! Anaishi pamoja nasi, kila kitu ni cha kawaida sana, hakuna, kwa urahisi hasa kitu cha kuonyesha kwamba Yeye ni Mungu. Kuna nyakati ambazo Yeye huwa na hasira, na tunaona uadhama wa hasira Yake, na wakati Anapotabasamu, tunaona mwenendo Wake wa kutabasamu. Yeye ndiye Mungu Mwenyewe ambaye ana umbo linalogusika, Ambaye ni wa mwili na damu, Ambaye ni wa kweli na halisi. "Unaposhuhudia kwa njia hii, ushuhuda wako haujakamilika. Je, utakuwa ni msaada gani kwa wengine? Ikiwa huwezi kushuhudia hadithi ya ndani na kiini cha kazi ya Mungu Mwenyewe, basi hushuhudii! Zaidi ya yote, kushuhudia kunahitaji kwamba ueleze juu ya ujuzi wako wa kazi ya Mungu, wa jinsi Mungu anavyowashinda watu, wa jinsi Yeye huwaokoa watu, wa jinsi Yeye huwabadilisha watu, na wa jinsi Yeye huwaongoza watu kuingia ndani, Akiwawezesha kushindwa, kufanywa wakamilifu, na kuokolewa. Kushuhudia kuna maana ya kuzungumza kuhusu kazi Yake na yote ambayo umeyapitia. Kazi Yake pekee ndiyo inayomwakilisha Yeye, na ni kazi Yake tu ndiyo inayoweza kufichua ukamilifu Wake hadharani; kazi Yake hutoa ushahidi Kwake. Kazi Yake na maneno Yake moja kwa moja yanamwakilisha Roho, kazi Anayofanya inatekelezwa na Roho, na maneno ambayo Anasema yanazungumzwa na Roho. Mambo haya yanaelezewa tu kupitia mwili wa Mungu; kwa kweli, hayo ni maneno ya Roho. Kazi Anayofanya na maneno Anayosema yanawakilisha dutu Yake. Ikiwa, baada ya kujivika Mwenyewe katika mwili kati ya mwanadamu, Mungu hakusema au kufanya kazi, na kisha Akawaomba mjue ukweli Wake, ukawaida Wake, na uweza Wake wote, je, ungeweza? Ungeweza kujua kiini cha Roho ni nini? Ungeweza kujua sifa Yake ni nini? Ni kwa sababu tu mmepitia kila hatua ya kazi Yake kwamba Anawaomba muweze kuwa na ushuhuda Kwake, na kama hamkuwa mmepata uzoefu huu, basi Hangetoa madai kama hayo kwenu. Kwa hivyo, unapomshuhudia Mungu, sio kuwa na ushuhuda wa umbo Lake la nje la ubinadamu wa kawaida, lakini kwa kazi ambayo Yeye hufanya, na njia Anayoongoza, ni kushuhudia jinsi ambavyo umeshindwa na Yeye, na katika vipengele gani umefanywa kuwa mkamilifu. Hii ndiyo aina ya ushuhuda unayostahili kuwa nao. Ikiwa, popote unapoenda, unatangaza: Mungu wetu Amekuja kufanya kazi, Yeye ni wa vitendo kweli! Ametupata bila kitu chochote kisicho cha kawaida au ishara na maajabu yoyote! Wengine watauliza: Unamaanisha nini unaposema Yeye haonyeshi ishara na maajabu? Je, Anaweza kukushinda bila kuonyesha ishara na maajabu? Na unasema: Kile Anachofanya ni kuzungumza. Ametushinda bila kutuonyesha ishara na maajabu yoyote—kazi Yake imetushinda. Hatimaye, ikiwa huwezi kusema chochote cha maana, na huwezi kuzungumza kuhusu mambo maalum, basi utakuwa unashuhudia? Wakati Mungu wa vitendo Anawashinda watu, ni maneno Yake takatifu ambayo yanashinda watu. Binadamu hawawezi kukamilisha hili, sio kitu ambacho mwanadamu yeyote anaweza kufanikisha, na hata wale walio kati ya watu wa kawaida wenye ubora wa tabia ya juu zaidi hawawezi hili, kwa kuwa uungu Wake ni mkuu zaidi kuliko kiumbe yeyote aliyeumbwa. Kwa watu, hii ni ya ajabu; Muumba, hata hivyo, ni mkuu zaidi kuliko kiumbe yeyote aliyeumbwa Imesemwa kuwa wanafunzi hawawezi kuwa wakubwa zaidi kuliko walimu wao. Viumbe walioumbwa hawawezi kuwa wa juu kuliko Muumba; ikiwa ungekuwa mkuu zaidi kuliko Yeye, Hangeweza kukushinda—Anaweza kukushinda kwa sababu Yeye ni mkuu zaidi kuliko wewe. Yeye Anayeweza kushinda wanadamu wote ni Muumba, na isipokuwa Kwake, hakuna mwingine anayeweza kufanya kazi hii. Huu ni ushuhuda; Hii ni aina ya ushuhuda ambao unapaswa kuwa nao. Umepitia kila hatua ya kuadibu, hukumu, utakaso, majaribio, vipingamizi, na taabu, na umepata ushindi, na kuweka kando matarajio ya mwili, motisha yako ya kibinafsi, na maslahi ya kibinafsi ya mwili—kwa maneno mengine, mioyo ya watu wote imeshindwa na maneno ya Mungu. Ingawa maisha yako hayajakua kufikia kiwango ambacho Aliuliza, unajua mambo haya, na unaridhishwa kabisa na kile Anachofanya—basi huu ni ushuhuda, na ushuhuda huu ni wa kweli! Kazi ambayo Mungu amekuja kufanya—hukumu na kuadibu—ni kwa ajili ya kumshinda mwanadamu, lakini pia Huhitimisha kazi Yake, Hukamilisha enzi, kutekeleza sura ya mwisho ya kazi Yake. Anakamilisha enzi nzima, Anaokoa binadamu wote, Anaokoa kabisa binadamu kutoka kwa dhambi, na kuwapata kikamilifu binadamu, ambao Yeye Aliwaumba. Hii ndiyo yote unayopaswa kutolea ushuhuda.

Umepitia kazi nyingi sana ya Mungu, umeiona kwa macho yako mwenyewe na ukaipitia mwenyewe, na hivyo ingesikitisha sana ikiwa, mwishowe, huwezi hata kutekeleza kazi unayopaswa. Katika siku zijazo, wakati injili inaenezwa, unapaswa kuweza kuzungumza juu ya ujuzi wako mwenyewe, utoe ushuhuda wa yote uliyopata ndani ya moyo wako, na kutumia jitihada yote. Hii ndiyo inapaswa kufikiwa na kiumbe aliyeumbwa. Ni nini umuhimu wa hatua hii ya kazi ya Mungu? Je, matokeo yake ni nini? Na ni kiasi gani chake kinachotekelezwa kwa mwanadamu? Watu wanapaswa kufanya nini? Wakati mnaweza kuzungumza wazi juu ya kazi yote iliyofanywa na Mungu mwenye mwili baada ya kuja duniani, basi ushuhuda wenu utakuwa kamili. Wakati unaweza kuzungumza wazi juu ya mambo haya matano—umuhimu, maudhui, kiini cha kazi Yake, tabia Yake inayowakilishwa nayo, na kanuni Zake za kazi—basi hii itathibitisha kuwa una uwezo wa ushuhuda, na kwamba kweli una ujuzi. Ninayouliza kutoka kwenu sio mengi, na inaweza kufikiwa na wale wote wanaofuatilia kweli. Ikiwa umeamua kuwa mmoja wa mashahidi wa Mungu, lazima uelewe kile ambacho Mungu huchukia, na kile ambacho Mungu hupenda. Umepitia mengi ya kazi Yake, na kwa njia ya kazi hii, lazima ujue tabia Yake, na kile Yeye huchukia na kupenda, na kuelewa mapenzi Yake na mahitaji Yake kwa wanadamu, na kutumia hili kushuhudia kwake na kufanya kazi yako. Unaweza kusema tu hili: "Tunamjua Mungu, hukumu Yake na kuadibu Kwake ni kali sana, maneno Yake ni makali sana, ni yenye haki na ya uadhama, na yasiyokiukwa na mtu yeyote." Lakini, hatimaye, yanamtolea mwanadamu? Je, matokeo yao kwa watu ni yapi? Unajua kweli kwamba kazi hii ni nzuri? Je, hukumu na kuadibu kwa Mungu kunaweza kufichua tabia yako? Je, vinaweza kufichua uasi wako? Je, vinaweza kufukuza mambo hayo ndani yako? Ungekuwaje bila hukumu na kuadibu kwa Mungu? Je, kweli unajua jinsi ulivyopotoshwa na Shetani? Yote haya ndiyo mnayopaswa kujitayarisha nayo na kujua leo.

Sasa si wakati wa aina ya imani katika Mungu iliyopo katika mawazo yenu: Sio ukweli kwamba mnahitaji tu kusoma maneno ya Mungu, kuomba, kuimba, kucheza, kufanya kazi yenu, na kuishi maisha ya kawaida ya binadamu ... Je, mambo yanaweza kuwa rahisi hivyo? Kilicho muhimu ni matokeo—si mambo mangapi unayofanya, lakini ni jinsi gani kwa kweli unaweza kutimiza matokeo bora kabisa? Unaweza kuzungumza juu ya ufahamu mdogo wakati unashikilia kitabu, lakini unapokiweka chini, huna ujuzi wowote; wewe una uwezo tu wa kuzungumza maneno na mafundisho, na huna ujuzi wa uzoefu. Leo, lazima ujue ni nini muhimu—hii ni sehemu muhimu ya kuingia katika ukweli! Kabla ya chochote kingine, fanya mazoezi yafuatayo: Kwanza soma maneno ya Mungu—jitahidi kuelewa maneno ya kiroho ndani yao, pata maono muhimu ndani yao, tambua sehemu za njia ya kutenda, na kuyaweka yote pamoja. Tafuta kila moja yao, na uingie ndani yao wakati wa uzoefu wako. Haya ni mambo muhimu ambayo unapaswa kufahamu. Moja ya mazoezi muhimu zaidi wakati wa kula na kunywa maneno ya Mungu ni baada ya kusoma moja ya matamshi ya Mungu, kuwa na uwezo wa kupata sehemu muhimu kuhusu maono, na pia kuwa na uwezo wa kutambua sehemu muhimu kuhusu kutenda, kutumia maono kama msingi na mazoezi kama mwongozo katika maisha yako. Haya ndiyo yote mnayokosa zaidi ya yote, na pia ni tatizo kubwa na ninyi—mioyoni mwenu hulitilia maanani kwa nadra sana. Nyote mna hali ifuatayo: wavivu, msio na ari, msiotaka kulipa gharama, au kusubiri kwa kukaa tu. Watu wengine hata hutoa malalamiko; hawaelewi malengo na umuhimu wa kazi ya Mungu, na ni vigumu kwao kufuata ukweli. Watu kama hao huchukia ukweli, na hatimaye wataondolewa. Hakuna kati yao anayeweza kufanywa mkamilifu, na hakuna atakayeokolewa. Ikiwa watu hawana uamuzi kidogo kupinga ushawishi wa Shetani, hakuna kitu ambacho kinaweza kufanyika kwao!

Ikiwa ufuatiliaji wenu umekuwa wenye ufanisi hupimwa kulingana na ufuatiliaji wenu leo, na kwa nini mlicho nacho sasa. Hizi ndizo zinazotumiwa kuamua mwisho wenu, ambayo ni kusema, mwisho wenu unaonyeshwa kwa gharama ambayo mmelipa na mambo ambayo mmefanya. Mwisho wenu utafichuliwa kwa ufuatiliaji wenu, imani yenu, na kile ambacho mmefanya. Miongoni mwenu, kuna wengi ambao tayari hawawezi kuokolewa—kwani leo ni wakati wa kufichua mwisho wa watu, na Sitafanya kazi kwa upumbavu, Nikiwaongoza wale ambao hawawezi kuokolewa katika enzi ijayo. Kutakuwa na wakati ambapo kazi Yangu itaisha. Sitafanya kazi kwa mizoga hiyo inukayo, isiyo na roho ambayo haiwezi kuokolewa; leo ni wakati wa siku za mwisho za wokovu wa mwanadamu, na Sitafanya kazi ambayo haina maana. Usiweke upinzani dhidi ya Mbingu na dunia—mwisho wa ulimwengu unakuja, na hauwezi kuepukika; vitu vimefikia hatua hii, na hakuna kitu ambacho wewe kama mwanadamu unaweza kufanya ili kuvizuia, huwezi kuvibadilisha kwa kupenda. Jana, hamkulipa gharama kufuatilia, na hamkuwa waaminifu. Leo, wakati umefika, wewe huwezi kuokolewa, na kesho utaondolewa. Hakuna njia ya kupenyeza ya wewe kuokolewa. Ingawa moyo Wangu ni mpole na Ninajitahidi niwezavyo kukuokoa, usipopambana ama kuwa na fikira yoyote ya wewe, hii inahusiana vipi na mimi? Wale ambao wanafikiri tu juu ya miili yao na wanapenda starehe, wale ambao imani yao ni tata, wale wanaoshiriki katika tiba ya uchawi na usihiri, wale ambao ni wazinzi, na waliovaa matambara na wasio sawa, wale wanaoiba dhabihu kwa Yehova na mali Yake, wale ambao wanapenda rushwa, wale wanaoota kwa uzembe kwenda mbinguni, wale ambao wana kiburi na wenye majivuno, na wanajitahidi tu kwa ajili ya umaarufu wa kibinafsi na utajiri, wale ambao hueneza maneno yasiyofaa, wale wanaomkufuru Mungu Mwenyewe, wale ambao hawafanyi lolote ila kumhukumu na kumkashifu Mungu Mwenyewe, wale wanaokusanyika na wengine na kujaribu kujitegemea, wale wanaojitukuza juu zaidi kuliko Mungu, wale wanaume na wanawake wapuuzi, na wanaume na wanawake wenye umri wa kati na wazee ambao wametegwa katika uovu, wanaume na wanawake wanaofurahia umaarufu wa kibinafsi na utajiri na kufuata hadhi ya kibinafsi kati ya watu wengine, wale watu wasio na toba ambao wamenaswa katika dhambi—je, si wao wote hawawezi kuokolewa? Ufisadi, hali ya kuwa mwenye dhambi, tiba ya uchawi, usihiri, mwenendo chafu, na maneno mafidhuli hufanya fujo kati yenu, maneno ya kweli na uhai hukanyagwa kati yenu, na lugha takatifu inanajisiwa kati yenu. Ninyi Mataifa, mliojawa na uchafu na kutotii! Mtaishia wapi? Je, wale wanaopenda mwili, ambao wanafanya matendo maovu ya mwili, na ambao wametegwa katika uasherati wanawezaje kuthubutu kuendelea kuishi? Je, hujui kwamba watu kama nyinyi ni mabuu ambao hawawezi kuokolewa? Ni nini kinachowapa sifa inayostahili ya kudai hili na lile? Hadi leo, hakujakuwa na mabadiliko hata kidogo kwa wale ambao hawapendi ukweli na wanapenda tu mwili—hivyo watu hawa wanaweza kuokolewaje? Hata leo, wale ambao hawapendi njia ya uzima, ambao hawamtukuzi Mungu na kumshuhudia Yeye, ambao hupanga njama kwa ajili ya hali yao wenyewe, ambao wanajisifu wenyewe sana—je, wao bado si sawa? Iko wapi thamani ya kuwaokoa? Kama mnaweza kuokolewa hakutegemei jinsi ulivyo na sifa za kustahili, au ni umefanya kazi kwa miaka ngapi, sembuse idadi ya sifa ambazo unazo. Kunategemea na ikiwa kumekuwa na matokeo yoyote katika kufuatilia kwako. Unapaswa kujua kwamba wale ambao wameokolewa ni miti ambayo huzaa matunda, si miti ambayo ina majani ya kustawi sana na maua mengi lakini haizai matunda. Hata kama umetumia miaka mingi kuzurura mitaani, ina maana gani? Ushahidi wako uko wapi? Uchaji wako kwa Mungu ni mdogo sana kuliko upendo wako wa wewe na hamu zako za tamaa—mtu kama huyu si mpotovu? Ungewezaje kuwa mfano na kielelezo cha wokovu? Asili yako haibadiliki, wewe ni muasi sana, huwezi kuokolewa! Watu kama hao hawataondolewa? Je, wakati ambapo kazi Yangu inamalizika si wakati ambapo siku yako ya mwisho itakuja? Nimefanya kazi nyingi sana na kusema maneno mengi kati yenu—ni kiasi gani cha hayo kilichoingia ndani ya masikio yenu? Ni kiasi gani cha hayo ambacho mmewahi kutii? Wakati kazi Yangu itaisha ndio pia utakuwa wakati unapoacha kunipinga na kusimama dhidi Yangu. Wakati wa kazi Yangu, daima nyinyi hutenda dhidi Yangu, hamyatii maneno Yangu kamwe. Ninafanya kazi Yangu, na wewe unafanya kazi yako mwenyewe, unatengeneza ufalme wako mdogo mwenyewe—nyinyi kundi la mbweha na mbwa, kila kitu mnachofanya ni dhidi Yangu! Nyinyi daima mnajaribu kuwaleta wale wanaowapenda tu katika kumbatio lenu —uko wapi uchaji wenu? Kila kitu mnachofanya ni kidanganyifu! Hamna utii au uchaji, kila kitu mnachofanya ni udanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hao wanaweza kuokolewa? Wanaume zinzi, wa kiasherati daima hutaka kuwavuta kwao wale makahaba wabembe kwa ajili ya raha yao wenyewe. Sitawaokoa mapepo wenye uasherati kama hao, Nawachukia ninyi mapepo wachafu, uasherati wenu na kupiga bemba kwenu kumewatumbukiza kuzimu—mna nini cha kusema kujihusu? Ninyi pepo mchafu na roho wabaya ni waovu sana! Nyinyi ni wa kuchukiza! Takataka kama nyinyi mnawezaje kuokolewa? Je, wale waliotegwa katika dhambi bado wanaweza kuokolewa? Ukweli huu, njia hii, na maisha haya hayapendezi kwenu; mnavutiwa na dhambi, pesa, hadhi, umaarufu na faida, ridhaa za mwili, maumbile mazuri ya wanaume na ubembe wa wanawake. Ni nini kinachowapa sifa zinazostahili kuingia katika ufalme Wangu? Taswira yenu ni kubwa zaidi kuliko Mungu, hali yenu ni ya juu zaidi kuliko Mungu, kutosema chochote cha sifa yenu kati ya wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hamjabadilika kuwa malaika mkuu? Wakati mwisho wa watu unafichuliwa, ambao pia ni wakati kazi ya wokovu inafikia kikomo, wengi wenu mtakuwa maiti ya maiti ambayo haiwezi kuokolewa na lazima muondolewe. Wakati wa kazi ya wokovu, Mimi ni mwenye huruma na mwema kwa watu wote. Wakati kazi inamalizika, mwisho wa watu wa aina tofauti utafichuliwa, na wakati huo Sitakuwa mpole na mwema, kwa maana mwisho wa watu utakuwa umefichuliwa, kila mmoja atakuwa ameainishwa kulingana na aina, na hakutakuwa na maana katika kufanya kazi yoyote zaidi ya wokovu. Ni hasa kwa sababu enzi ya wokovu itakuwa imepita; kwa kuwa itakuwa imepita, haitarudi tena.

Tanbihi:

a. Nakala ya asili inacha "kiovu."

b. Nakala ya asili inaacha "unapaswa kujua."

c. Nakala ya asili inaacha "Watu walidhani kwamba."

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

 

Views: 24 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: siku za mwisho, kumjua mungu, Matamshi ya Kristo | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar