9:10 PM
Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

 
Mwenyezi Mungu anasema, “Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo. Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa binadamu. Binadamu kuingia rahani kunamaanisha kwamba binadamu wote wataishi ndani ya mwangaza wa Mungu na chini ya baraka Zake; hakutakuwa na upotovu wowote wa Shetani, wala maovu yoyote kutokea. Binadamu wataishi kama kawaida duniani, na wataishi chini ya ulinzi wa Mungu. Mungu na mwanadamu waingiapo rahani pamoja, kutamaanisha kwamba binadamu wameokolewa na kwamba Shetani ameangamizwa, kwamba kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu imemalizika kabisa. Mungu hataendelea tena kufanya kazi miongoni mwa mwanadamu, na mwanadamu hataendelea tena kumilikiwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu hatakuwa shughulini tena, na mwanadamu hatakimbiakimbia tena; Mungu na mwanadamu wataingia rahani wakati huo huo.“
 
 
Tazama Video: Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote
 
 
Yaliyopendekezwa: APP ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
 
 
 
 
 
 
Views: 56 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: neno la Mungu, Roho Mtakatifu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar