9:20 PM
Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima-Sura ya 2

Kufuata kuanza kazi kwa mtazamo mpya, kutakuwa na hatua mpya katika kazi Yangu. Kama ilivyo katika ufalme, Nitafanya mambo moja kwa moja kupitia kwa uungu, Nikiongoza kila hatua ya njia, sahihi hadi kwa maelezo madogo, na bila kutiwa najisi na nia za binadamu hata kidogo. Yafuatayo yanaeleza kwa muhtasari namna ya utekelezaji halisi: Kwa vile ni kupitia katika ugumu na usafishaji ndiyo wamepata jina la “watu”, na kama walivyo watu wa ufalme Wangu, lazima Niwafanye watii kwa mahitaji kali, ambayo ni ya juu kushinda mbinu za kazi Yangu kwa vizazi vilivyopita. Huu sio tu uhalisi wa maneno, bali pia la muhimu zaidi ni uhalisi wa kutenda, na hili lazima kwanza litimizwe. Katika kila neno na matendo, ni lazima watosheleze viwango vinachohitajika kwa watu wa ufalme, na mkosaji yeyote ataondolewa mara moja, ili kuzuia aibu kulijia jina Langu. Hata hivyo, wale wasiojua ambao hawawezi kuona kwa dhahiri, na hawawezi kuelewa ni wa kipekee. Katika ujenzi wa ufalme Wangu, tilia maanani kula na kunywa maneno Nisemayo, uilelewe hekima Yangu, na kuthibitisha kupitia kazi Yangu. Yeyote anayetilia maanani maneno ya kitabu kisicho Changu hahitajiki na Mimi kabisa; huyu ni kahaba anayeniasi. Kama mtume, mtu hapaswi kuishi nyumbani kwa muda mrefu. Kama hili haliwezi kufanyika, Nitamtupilia mbali na Sitamtumia tena. Simlazimishi. Kwa kuwa mitume hawako nyumbani kwa muda mrefu, ni kwa kushinda kanisani kwa muda mrefu ndiyo wanarekebishwa maadili. Kwa kila mikusanyiko miwili ya kanisa, mitume wanapaswa kuhudhuria angalau mara moja. Kwa hivyo, mikutano ya wafanyikazi wenza lazima ikuwe ya kawaida (mikutano ya wafanyakazi wenza inajumuisha: mikusanyiko yote ya mitume, mikusanyiko yote ya wakuu wa kanisa, na mikusanyiko yote ya watakatifu walio na utambuzi ulio wazi). Angalau wengine wenu mtaweza lazima wahudhurie kila mkusanyiko, na mitume wanatilia maanani tu kuchunga makanisa. Mahitaji yaliyowekwa awali kwa watakatifu yamekuwa ya undani zaidi. Kwa wale waliotenda makosa kabla Nilishuhudie jina Langu, kwa ajili ya kujitoa kwao Kwangu, bado Nitawatumia baada ya wao kujaribiwa na Mimi. Hata hivyo, kwa wale wanaotenda kosa tena baada ya ushuhuda Wangu na wanakusudia wa kuanza ukurasa mpya wa maisha yao, watu kama hao hubaki tu ndani ya kanisa. Bado, hawawezi kuwa wavivu na watukutu, badala yake wawe wanaojizuia zaidi ya wengine. Na kwa wale wasiorekebisha mienendo yao baada ya Mimi kunena sauti Yangu, Roho Wangu atawaacha mara moja, na kanisa litakuwa na haki ya kutekeleza hukumu Yangu, na kuwafanya kutoka kanisani. Hili ni bila shaka, na hakuwezi kuwa na nafasi zaidi ya kufikiria. Mmoja akizirai katika majaribu, yaani, akiondoka, hakuna mtu anapaswa kujishughulisha na mtu huyo, ili kuepuka kunijaribu Mimi na kumruhusu Shetani kuingia kanisani kwa wendawazimu. Hii ndiyo hukumu Yangu kwake. Yeyote anayetenda udhalimu na kutenda kulingana na hisia zake mwenyewe pia hatahesabiwa miongoni mwa watu Wangu, sio tu yule aliyeasi. Kazi nyingine ya mitume ni kulenga kuisambaza injili. Bila shaka, watakatifu pia wanaweza kufanya kazi hii, lakini lazima wawe wenye hekima katika kufanya hivyo, na pia lazima wajizuie kutokana na kuamsha shida. Yaliyotajwa hapa juu ndiyo mbinu ya sasa ya kutenda. Pia tena kama kumbusho, unafaa kuweka maanani kufanya mahubiri yako kuwa yenye undani zaidi, ili kwamba wote waweze kuingia katika ukweli wa maneno Yangu. Lazima uyafuate maneno Yangu kwa ukaribu na kuyafanya yawe kwamba watu wote wapate kuyaelewa vizuri, na bila utata. Hili ni la muhimu sana. Wale kati ya watu Wangu wanaohodhi mawazo ya usaliti lazima waondolewe, na wasiruhusiwe kukaa katika nyumba Yangu kwa muda mrefu, wasije wakaleta tusi kwa jina Langu.

Februari 21,1992

 

Chanzo: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima-Sura ya 2 

Kanisa la Mwenyezi MunguTufuate: Asili ya

 

Views: 133 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Kanisa, neno la Mungu, Hukumu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar