7:53 AM
Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima-Sura ya 17

Mwenyezi Mungu anasema, Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya. Wakati mwangaza hafifu unaanza kuonekana Mashariki, watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao. Lakini, hakuna aliyewahi kutambua kwamba siku imewadia mwangaza Wangu unaposhuka duniani. Wanadamu wengi wanashtuliwa na ujio wa ghafla wa mwangaza; baadhi yao, kwa macho ya kuvutiwa ya dadisi, wanaangalia mwendo wa mwangaza na kutoka upande upi unasongea; ama wengine wanasimama tayari wakitazama mwangaza, ili waweze kuelewa wazi zaidi palipotoka mwangaza. Iwe ilivyo, kuna yeyote aliyewahi kugundua thamani ya mwangaza wa leo? Kuna yeyote aliyewahi kufahamu ajabu ya mwangaza huu? Wanadamu wengi wamechanganyikiwa tu; wamejeruhiwa machoni na kutupwa chini matopeni na mwangaza. Mtu anaweza kusema kwamba, chini ya mwangaza huu usiokuwa na ufasili, dunia imefunikwa na vurugu, ikifanya mtazamo wa kusikitisha usiovumilika ambao, ukichunguzwa kwa kina, unamtesa mtu na huzuni nyingi. Kutoka hapa, mtu anaelewa kwamba, wakati mwangaza una nguvu kabisa, hali ya dunia itakuwa kwamba haiwezi kumruhusu mwanadamu kusimama mbele Yangu. Binadamu uko katika mng’ao wa mwangaza; tena, binadamu uko katika wokovu wa mwangaza lakini kwa wakati huo huo pia chini ya majeraha yanayotokana na mwangaza: Kuna yeyote asiye chini ya mapigo yanayoua ya mwangaza? Kuna yeyote anayeweza kutoroka kuchoma kwa mwangaza? Nimetembea kote duniani, kutawanya mbegu za Roho Wangu, ili binadamu wote duniani kwa sababu hii wataongozwa nami. Kutoka kwa urefu wa juu wa mbingu, Naangalia chini kwa dunia yote, Nikitazama matukio ya ajabu na yasiyo ya kawaida ya viumbe wa dunia. Sehemu ya juu ya bahari inaonekana kuteswa na mshtuko wa tetemeko la ardhi: Ndege wa bahari wanaruka hapa na pale, wakitafuta samaki wa kumeza. Wakati huo huo, hii haijulikani chini ya bahari, ambayo hali ya sehemu ya juu haiwezi kabisa kuzindua fahamu, kwa sababu chini ya bahari kutulia kama mbingu ya tatu: Hapa viumbe vilivyo hai vikubwa na vidogo vinaishi pamoja kwa amani, bila kushiriki katika “migogoro ya mdomo na ulimi” hata mara moja. Miongoni mwa matukio ya ajabu na ya kichekesho, binadamu ndio unaoona ni vigumu sana kuniridhisha. Hii ni kwa sababu hadhi Niliyompa mwanadamu ni ya juu sana, na hivyo tamaa yake ni kubwa mno, na ndani ya macho yake daima kuna kiwango cha uasi. Ndani ya nidhamu Yangu kwa mwanadamu, ndani ya hukumu Yangu kwake, kumekuwa na mengi yenye maumivu, mengi yaliyo na huruma, lakini kwa mambo haya mwanadamu hana habari hata kidogo. Sijawahi kumshughulikia mwanadamu yeyote kwa ukali: Nimepeana tu marekebisho mwafaka, wakati mwanadamu hajatii, na tu, wakati mwanadamu amekuwa mdhaifu, Nimetoa msaada mwafaka. Lakini, wakati binadamu unaendelea kujitenga nami na zaidi ya hayo unatumia mipango danganyifu ya Shetani kuasi dhidi Yangu, Nitamwangamiza mwanadamu mara moja, Nikiwaacha wanadamu bila nafasi ya kufanya maonyesho makuu ya ujuzi wao mbele Yangu, ili wasiweze tena kujigamba na madoido na hali, wakionea wengine, duniani.

Natumia mamlaka Yangu duniani, Nikidhihirisha kazi Yangu yote. Yote yaliyo katika kazi Yangu yanajitokeza duniani; mwanadamu hajawahi, duniani, kuweza kuufahamu mwendo Wangu mbinguni, wala kutafakari kabisa mizunguko na njia za Roho Wangu. Wanadamu wengi wanaelewa tu maelezo madogo yaliyo nje ya roho, bila kuweza kuelewa hali halisi ya roho. Matakwa Yangu kwa binadamu hayatoki kwa Mimi wa mbinguni Nisiye dhahiri, ama kwa Mimi wa dunia Nisiyekadiriwa: Natoa matakwa ya kufaa kulingana na kimo cha mwanadamu. Sijawahi kumweka yeyote kwa matatizo, wala Sijawahi “kukamua damu ya mtu yeyote” ili kujiridhisha: Inaweza kuwa kwamba matakwa Yangu yamezuiwa na masharti haya pekee? Kwa viumbe lukuki duniani, ni yupi asiyetii tabia za maneno yaliyo mdomoni Mwangu? Ni yupi kati ya viumbe hawa, wanaokuja mbele Yangu, hajachomwa kabisa kupitia maneno Yangu na moto Wangu unaochoma? Ni yupi kati ya viumbe hawa anayethubutu kujigamba mbele Yangu? Ni yupi kati ya viumbe hawa hainami mbele Yangu? Mimi ni Mungu anayelazimisha tu ukimya kwa viumbe? Kwa mambo lukuki katika uumbaji, Nachagua yale yanaoridhisha nia Yangu; kwa wanadamu lukuki, Nawachagua wale wanaotunza roho Yangu. Nachagua bora zaidi kwa nyota zote, hivyo Naongeza mwangaza hafifu kwa ufalme Wangu. Natembea duniani, Nikitawanya harufu Yangu nzuri kila mahali, nami Naacha umbo Langu kila mahali. Kila pahali panatingika kwa mvumo wa sauti Yangu. Watu kila mahali wanadumu kwa hamu ya mambo waliyozea ya urembo wa mandhari ya jana, kwani binadamu wote wanakumbuka siku za nyuma …

Binadamu wote wanatamani kuona uso Wangu, lakini Nishukapo Mwenyewe duniani, wote wanakirihishwa na ujio Wangu, wote wanaufukuza mwangaza usije, kana kwamba Mimi ni adui ya mwanadamu mbinguni. Mwanadamu ananisalimu na mwangaza wa kujikinga machoni mwake, na daima anabaki katika tahadhari, akihofia sana kwamba Naweza kuwa na mipango mingine kwake. Kwa sababu binadamu wananiona kama rafiki asiyejulikana, wanahisi kwamba Nina nia ya kuwaua bila kujali. Katika macho ya mwanadamu, Mimi ni adui wa mauti. Baada ya kuonja joto Langu katikati ya msiba, mwanadamu hata hivyo bado hafahamu pendo Langu, na bado ameamua kunifukuza na kunikaidi. Mbali na kujinufaisha na yeye kuwa katika hali hii ili kuchukua hatua dhidi yake, Namfunika mwanadamu na joto la kumbatio, Najaza mdomo wake na utamu, na kuweka chakula anachohitaji tumboni mwake. Lakini, wakati hasira Yangu ya ghadhabu inapotingiza milima na mito, Sitamtawaza mwanadamu aina mbalimbali za msaada, kwa sababu ya woga wake. Wakati huu, Nitakuwa na ghadhabu, Nikiwanyima viumbe hai fursa ya kutubu na, kuachana na matumaini yote ya mwanadamu, Nitasambaza adhabu anayostahili sana. Wakati huu, radi na umeme vinang’aa ghafla na kunguruma, kama mawimbi ya bahari yakisonga kwa hasira, kama milima elfu kumi ikigonga chini. Kwa ajili ya uasi wake, mwanadamu anaangushwa na radi na umeme, viumbe wengine wanafutwa katika milipuko ya radi na umeme, ulimwengu mzima unazorota ghafla katika machafuko, na uumbaji huwezi kupata pumzi muhimu ya uhai. Majeshi lukuki ya binadamu hayawezi kutoroka kishindo cha radi, katikati ya nuru ya ghafla ya umeme, wanadamu, makundi mengi sana, wanaanguka ndani ya mto unaobubujika haraka, kutokomezwa na mafuriko yanayotiririka chini kutoka milima. Ghafla, panakutana dunia ya “wanadamu” badala ya hatima ya binadamu. Maiti wanasongasonga juu ya bahari. Binadamu wote wanaenda mbali nami kwa sababu ya ghadhabu Yangu, kwani mwanadamu amekosea dhidi ya kiini cha Roho Wangu, uasi wake umenichukiza Mimi. Lakini, mahali ambapo hakuna maji, wanadamu wengine bado wanafurahia, wakicheka na kuimba, ahadi ambazo Nimewapa.

Binadamu wote wanapotulia, Natoa kimulimuli cha mwangaza mbele ya macho yao. Hapo, wanadamu wanakuwa na uwazi wa akili na uangavu wa jicho, na wanakoma kuwa na nia ya kukimya; hivyo, hisia ya kiroho inakusanywa ndani ya mioyo yao mara moja. Wakati huu, binadamu wote wanafufuka. Wakiweka kando malalamiko yao, wanadamu wote wanakuja mbele Yangu, baada ya kushinda nafasi nyingine ya kusalimika kupitia maneno Ninayotangaza. Hii ni kwa sababu wanadamu wote wanataka kuishi duniani. Lakini nani miongoni mwao amewahi kuwa na nia ya kuishi kwa ajili Yangu? Nani miongoni mwao amewahi kufichua mambo mazuri ndani yake kunipa furaha? Nani miongoni mwao amewahi kugundua harufu ya kuvutia Kwangu? Wanadamu wote ni vitu hafifu na visivyotakaswa: Nje, wanaonekana kuangaza macho, lakini kwa nafsi zao muhimu hawanipendi kwa dhati, kwa sababu ndani ya nafasi ya kina cha moyo wa binadamu hakujawahi kuwa hata na kiasi kidogo cha Mimi. Mwanadamu anakosa sana: Kumlinganisha nami Mwenyewe, ingeonekana kwamba tuko mbali sana kama dunia kutoka kwa mbingu. Lakini, hata hivyo, Simshambulii mwanadamu katika sehemu zake dhaifu na zenye kasoro, wala Simcheki kudharau upungufu wake. Mikono Yangu imekuwa ikifanya kazi[a] duniani kwa maelfu ya miaka, na wakati huo wote macho Yangu yamelinda binadamu wote. Lakini Sijawahi kuchukulia mzaha maisha ya binadamu hata mmoja kana kwamba ni kitu cha kuchezea. Nachunguza damu ya moyo wa mwanadamu, nami Naelewa bei ambayo amelipa. Anaposimama mbele Yangu, Sitamani kujinufaisha na kutokuwa na ulinzi kwa mwanadamu ili kumwadibu, wala kumtawaza vitu visivyohitajika. Badala yake, Nimemtunza tu mwanadamu, na kumpa mwanadamu, wakati huu wote. Kwa hivyo, yote anayofurahia mwanadamu ni neema Yangu, yote ni fadhila inayotoka kwa mkono Wangu. Kwa sababu Niko duniani, mwanadamu hajawahi lazimika kuteseka mateso ya njaa. Badala yake, Namruhusu mwanadamu kupokea kutoka mikono Yangu mambo ambayo anaweza kufurahia, na kumruhusu mwanadamu kuishi ndani ya baraka Zangu. Je, wanadamu wote hawaishi chini ya kuadibu Kwangu? Kama vile milima inavyoshikilia ndani ya vina vyao mambo ya mengi na wingi, na maji katika ukubwa wake vitu vya kufurahisha, je, watu wanaoishi ndani ya maneno Yangu leo wanavyo, hata zaidi, chakula wanachopenda na kuonja? Niko duniani, na mwanadamu anafurahia baraka Zangu duniani. Niachapo dunia nyuma, ambapo ndipo pia kazi Yangu itafika ukamilishaji wake, wakati huo, wanadamu hawatapata tena hisani yoyote kutoka Kwangu kwa sababu ya udhaifu wao.

Machi 16, 1992

 

Chanzo: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima-Sura ya 17

Kanisa la Mwenyezi MunguTufuate: Asili ya

 

Views: 136 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Sauti ya Mungu, neno la Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar