8:19 PM
Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Wimbo wa Ufalme

Watu wanishangilia Mimi, watu wananisifu Mimi; midomo yote inataja Mungu mmoja wa kweli, watu wote wainua macho yao kutazama matendo Yangu. Ufalme washuka duniani, nafsi Yangu ni tajiri na yenye wingi. Ni nani hangesherehekea haya? Nani hangecheza kwa furaha kwa ajili ya haya? Ee, Sayuni! Inua bango lako la ushindi ili kunisherehekea Mimi! Imba wimbo wako wa ushindi na ueneze jina Langu takatifu! Vitu vyote duniani! Sasa mjitakase kwa kujitolea Kwangu. Nyota angani! Sasa rudini sehemu zenu na muonyeshe ukuu Wangu mbinguni! Nashughulikia sauti za watu duniani, wakimimina upendo usio na kikomo na uchaji wao Kwangu kwa wimbo! Katika siku hii, wakati vitu vyote vinafanywa upya, Naja kutembea duniani. Katika wakati huu, maua yanachanua, ndege wanaimba, vitu vyote vimejaa furaha! Katika sauti ya saluti ya ufalme, ufalme wa Shetani unaporomoka, ukiharibika katika mdundo wa mwito wa wimbo wa ufalme. Na hautainuka tena!

Ni nani duniani anathubutu kuinuka na kupinga? Ninaposhuka duniani Naleta kuchoma, Naleta ghadhabu, Naleta majanga yote. Falme zote za kidunia sasa ni ufalme Wangu! Juu angani, mawingu yaanguka ghafla na kujongea; chini ya anga, maziwa na mito yanaenda mbele na kutoa wimbo wa kugusa. Wanyama wanaopumzika wanajitokeza kutoka kwa mapango yao, na watu wote walalao wanaamushwa nami. Siku ambayo imesubiriwa na watu wote hatimaye imewadia! Wanatoa nyimbo nzuri zaidi Kwangu!

Kwa wakati huu mzuri, kwa majira haya ya kusisimua,

Mbingu juu na yote chini ya mbingu sasa yasifu.

Nani hangesisimshwa kwa ajili ya hili!

Nani hangefurahia hili!

Nani hangelia wakati huu maalum?

Anga si ile anga sawa, sasa ni anga ya ufalme

Dunia si dunia iliyokuwa, lakini sasa ni dunia takatifu.

Baada ya mvua nzito kupita, dunia chafu ya kale kabisa yabadilishwa.

Milima ikibadilika....maji yakibadilika.....

Watu vile vile wakibadilika, vitu vyote vikibadilika...

Milima tulivu!

Nichezeeni!

Maji yasiyosonga!

Tiririka kwa uhuru!

Wanadamu wanaolala!

Inuka katika kutafuta kwenu!

Nimekuja....na Ninatawala...

Wote wataona kwa macho yao wenyewe uso Wangu, wote watasikia kwa masikio yao wenyewe sauti Yangu,

Wapitie wenyewe maisha katika ufalme...

Matamu sana....mazuri sana....

Yasiyosahaulika....Yasiyosahaulika

Katika kuchoma kwa ghadhabu Yangu, joka kuu jekundu linapambana;

Katika hukumu Yangu adhimu, mapepo yaonyesha hali zao za ukweli;

Kwa ukali wa maneno Yangu, wote wahisi aibu,

Hawathubutu kuonyesha nyuso zao.

Kwa kukumbuka muda uliopita, jinsi walivyonikejeli.

Kila mara wakijiringa, mara kwa mara wakinipuuza.

Leo, nani hataomboleza?

Nani hahisi majuto?

Ulimwengu wote duniani umejawa na machozi... Umejawa na sauti za furaha...umejawa na kicheko...

Furaha isiyoweza kufananishwa....furaha isiyoweza kufananishwa

Mvua rasha ya vishindo ndogondogo....theluji nzito yapepea chini...

Watu wachanganya machungu na furaha....wengine wacheka.....

Wengine wakilia kwikwikwi.....na wengine wakishangilia....

Kana kwamba watu wamesahau....iwapo ni majira ya kuchipua yaliyotanda mawingu na ya mvua,

Majira ya joto ya kuchanua kwa maua, majira ya kupukutika kwa majani ya mavuno mengi,

Majira ya baridi kama barafu na jalidi, hakuna ajuaye....

Angani mawimbi yatangatanga, ulimwenguni bahari zinatokota.

Wana wanapunga mikono yao...watu wasongesha miguu yao katika dansi

Malaika wamo kazini....malaika wanachunga...

Watu wa ulimwengu wanajishughulisha, vitu vyote ulimwenguni vinazidisha.

 

Chanzo: Wimbo wa Ufalme

APP ya Kanisa la Mwenyezi MunguYaliyopendekezwa:

 

Views: 83 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: ufalme, Maneno ya Mungu, Hukumu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar