12:30 PM
Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Siku hizi watu wengi hawatilii maanani mafunzo yapi yanayopaswa kusomwa wakati wa upatano na wengine. Nimegundua kuwa wengi wenu hawawezi kujifunza mafunzo hata kidogo wakati wa ushirikiano na wengine. Wengi wenu mnashikilia maoni yenu mwenyewe, na wakati mnafanya kazi kanisani, unatoa maoni yako na yeye anatoa yake, moja uhusiano na mingine, bila kushirikiana kabisa. Mnajihusisha tu katika kutoa umaizi wenu wenyewe wa ndani, unaingia tu katika kuachilia huru “mizigo” ndani yenu, si kutafuta uzima hata kidogo. Inaonekana kwamba unafanya tu kazi hiyo kwa kutimiza wajibu, daima ukiamini kwamba unapaswa kufuata njia yako mwenyewe bila kujali jinsi watu wengine walivyo, na kwamba unapaswa kushiriki jinsi Roho Mtakatifu anavyokuongoza, bila kujali jinsi watu wengine walivyo. Hamna uwezo wa kugundua uwezo wa wengine, na hamuwezi kujichunguza. Njia yenu ya kupokea vitu ni yenye makosa sana. Inaweza kusemwa kwamba hata sasa bado mnaonyesha kujidai kwingi, kana kwamba ugonjwa huo wa zamani umerejea tena. Hamuwasiliani nyinyi kwa nyinyi ili kufikia uwazi kamili, au ni katika matokeo ya aina gani mmepata katika makanisa fulani, au jinsi hali yako ya ndani imekuwa hivi karibuni, na kadhalika—ninyi hamuwasiliani tu kwa namna hii. Nyinyi kimsingi hamna mazoea kama vile kuacha dhana zenu wenyewe au kujitelekeza. Viongozi na wafanyakazi wanafikiri tu kuhusu kuwachangamsha na kuwapa nguvu ndugu kwa njia ya ushirika wao, na wale wanaofuata wanajua tu kufuatilia peke yao. Kimsingi hamuelewi huduma ni nini au ushirikiano ni nini, na mnadhani tu kuhusu kuwa na dhamira nyinyi wenyewe kuulipiza upendo wa Mungu, wa kuwa na dhamira ya nyinyi wenyewe kuishi kwa kudhihirisha mtindo wa Petro, na si kuhusu kitu kingine chochote. Hata unasema, bila kujali jinsi watu wengine walivyo, hamtatii kwa upofu hata hivyo, na bila kujali watu wengine walivyo, ninyi wenyewe unatafuta ukamilifu na Mungu, na hiyo itatosha. Kwa kweli, dhamira yako hayajapata maonyesho thabiti katika uhalisi hata kidogo. Je! Hii sio aina yote ya tabia mnayoonyesha siku hizi. Kila mmoja wenu anashikilia imara utambuzi wenu wenyewe, na ninyi nyote mnataka kufanywa wakamilifu. Ninaona kwamba mmetumikia kwa muda mrefu sana na hamjaendelea sana, hasa katika somo hili la kufanya kazi pamoja kwa maelewano hamjaendelea kabisa! Kuenda kwenye makanisa unawasiliana kwa njia yako, na yeye anafanya ushirika kwa njia yake. Kuna uratibu wa upatanifu kwa nadra sana. Na watu walio chini ambao wanafuata wako namna hii hata zaidi. Ambayo ni kusema kwamba ni watu wachache sana miongoni mwenu wanaelewa kumtumikia Mungu ni nini, au jinsi mtu anapaswa kumtumikia Mungu. Mmechanganyikiwa, na kuchukulia masomo ya aina hii kama suala dogo sana, kwa kiasi kwamba watu wengi hawatendi tu kipengele hiki cha ukweli, wanafanya mabaya kwa kujua. Hata watu ambao wametumikia kwa miaka mingi kwa kweli wanapigana na kugombana miongoni mwao. Je! Hiki si kimo chako halisi? Ninyi watu mnaohudumu pamoja kila siku ni kama Waisraeli ambao walimtumikia Mungu Mwenyewe katika hekalu kila siku. Inawezekanaje kuwa ninyi watu ambao ni kama makuhani hamjui jinsi ya kushirikiana na jinsi ya kutumikia?

Wakati ule, Waisraeli walimtumikia Yehova moja kwa moja hekaluni. Utambulisho wao ulikuwa ule wa makuhani. (Bila shaka, si kila mtu alikuwa kuhani; ni baadhi tu waliomtumikia Yehova katika hekalu ndio walikuwa na utambulisho wa makuhani). Wangevalia taji ambazo walipewa na Yehova (kunamaanisha walifanya taji kulingana na matakwa ya Yehova, sio kwamba Yehova aliwapa taji moja kwa moja). Wangevalia mavazi yao ya kikuhani ambayo walipewa na Yehova, bila viatu kumtumikia Yehova moja kwa moja hekaluni, tangu asubuhi hadi usiku. Utumishi wao kwa Yehova haukuwa usio na mipangilio au wa kutenda makosa wapendavyo; yote ilikuwa kulingana na sheria, ambazo hakuna mtu aliyemtumikia Yehova moja kwa moja angeweza kukiuka. Wote walilazimika kufuata sheria hizi; vinginevyo, kuingia hekaluni kulikatazwa. Ikiwa yeyote kati yao alivunja sheria za hekalu, yaani, kama mtu yeyote aliasi amri za Yehova, ilikuwa lazima apate kutendewa kulingana na sheria zilizotolewa na Yehova, na hakuna mtu aliyeruhusiwa kupinga, na hakuna mtu aliyeruhusiwa kumtetea. Haijalishi ni miaka mingapi ambayo walikuwa wamemtumikia Mungu, wote walipaswa kufuata sheria. Hii ndio sababu makuhani wengi walivalia nguo za kikuhani kila wakati na kumtumikia Yehova kwa njia hii mwaka mzima, ingawa Yehova hakuwatendea kwa njia yoyote maalum, na hata walikwenda mbele ya madhabahu au hekalu maisha yao yote. Hivyo ndivyo ulivyokuwa uaminifu wao na utii wao. Haishangazi kwamba Yehova aliwabariki kwa njia hii; ilikuwa yote kutokana na uaminifu wao kwamba walipata kibali na kuyaona matendo yote ya Yehova. Wakati ule ambapo Yehova alifanya kazi katika Israeli, watu Wake waliochaguliwa, matakwa Yake juu yao yalikuwa makali sana. Wote walikuwa watiifu sana na walizuiliwa na sheria, ambazo zilitumika kuwalinda ili kwamba wamheshimu Yehova. Hizi zote zilikuwa amri za utawala za Yehova. Ikiwa miongoni mwa wale makuhani kulikuwa na yeyote ambaye hakuishika Sabato au ambaye alikiuka amri za Yehova na aligunduliwa na watu wa kawaida, huyo mtu angeletwa mara moja mbele ya madhabahu na kupigwa kwa mawe hadi kufa. Haikuruhusiwa kuweka maiti zao katika hekalu au karibu na hekalu. Yehova hakukubali hilo. Ikiwa mtu alifanya hivyo, angetendewa kama wale ambao hutoa “dhabihu zenye kukufuru,” na kutupwa katika shimo kubwa na kuuawa. Bila shaka, watu wote kama hao wangepoteza maisha yao, hakuna aliyeachwa hai. Kulikuwa hata na wale ambao walitoa “moto wa kukufuru,” kwa maneno mengine, wale watu ambao hawakutoa dhabihu katika siku zilizotolewa na Yehova wangeteketezwa na moto wa Yehova pamoja na vitu vyao vya dhabihu, hawaruhusiwi kubaki juu ya madhabahu. Mahitaji kwa makuhani yalikuwa: hawakuruhusiwa kuingia hekaluni, na hata ua wa nje wa hekalu, bila ya kwanza kuosha miguu yao; hakuna kuingia hekaluni ikiwa hujavalia vazi za kikuhani; hakuna kuingia hekaluni ikiwa hujavalia taji za kikuhani; hakuna kuingia hekaluni ikiwa umechafuliwa na maiti; hakuna kuingia hekaluni baada ya kuugusa mkono wa mtu asiye haki bila ya kwanza kuosha mikono yake mwenyewe; hakuna kuingia hekaluni baada ya mahusiano ya ngono na wanawake (hii haikuwa milele, kwa muda wa miezi mitatu tu), hawakuruhusiwa kuuona uso wa Yehova, wakati ulipokuwa umeisha, ikimaanisha kwamba ni baada ya miezi mitatu tu ndio wangeweza kuruhusiwa kuvaa mavazi safi ya kikuhani, na kuhudumu katika ua wa nje kwa siku saba kabla ya kuweza kuingia katika hekalu ili kuuona uso wa Yehova; waliruhusiwa kuvaa mavazi yote ya kikuhani ndani ya hekalu tu na hawaruhusiwi kuyavaa nje ya hekalu, ili kuepuka kulichafua hekalu la Yehova; iliwapasa wote waliokuwa makuhani kuwaleta wahalifu ambao wamekiuka sheria za Yehova mbele ya madhabahu ya Yehova ambako wangeuawa na watu wa kawaida, vinginevyo moto ungeanguka juu ya kuhani ambaye alishuhudia. Kwa hiyo walikuwa waaminifu kwa Yehova daima, kwa sababu sheria za Yehova zilikuwa kali juu yao, na hawangeweza kabisa kuthubutu kukiuka kikawaida amri Zake za utawala. Waisraeli walikuwa waaminifu kwa Yehova kwa sababu walikuwa wameuona moto Wake, walikuwa wameuona mkono ambao Yehova alitumia kuwaadibu watu, na pia kwa sababu hapo awali walimheshimu Yehova mioyoni mwao. Kwa hivyo kile walichopata sio moto wa Yehova tu; pia walipata utunzaji na ulinzi kutoka kwa Yehova, na kupata baraka za Yehova. Uaminifu wao ni kwamba walifuata maneno ya Yehova katika yale waliyofanya, bila mtu yeyote kuasi. Ikiwa mtu yeyote angekosa kutii, watu bado wangetekeleza maneno ya Yehova, na kuwaua waliokwenda kinyume na Yehova, bila njia yoyote ya kuficha. Hasa wale ambao walikiuka Sabato, wale waliokuwa na hatia ya uasherati, na wale walioiba sadaka kwa Yehova wangeadhibiwa vikali zaidi. Wale ambao walikiuka Sabato waliuawa kwa mawe nao (watu wa kawaida), au walipigwa viboko hadi kufa, bila yeyote kuachwa. Wale waliofanya vitendo vya uasherati, hata wale waliomtamani mwanamke mzuri, au wale waliokuwa na mawazo ya kiasherati baada ya kumwona mwanamke mwovu, au waliokuwa na tamaa ya kimapenzi baada ya kumwona mwanamke mwenye umri mdogo—kila mtu wa aina hii angeuawa. Ikiwa mwanamke mdogo yeyote ambaye hakuvaa nguo ya kufunika au utaji alimjaribu mwanaume katika kitendo cha tabia mbaya, mwanamke huyo angeuawa. Ikiwa ilikuwa ni kuhani (wale watu ambao walihudumu katika hekalu) ndiye aliyekiuka sheria za aina hii, angesulubiwa au kunyongwa. Hakuna mtu wa aina hii angeweza kuruhusiwa kuishi, na hakuna hata mtu mmoja angeweza kupata kibali mbele za Yehova. Jamaa za mtu wa aina hii hawangeruhusiwa kutoa dhabihu kwa Yehova mbele ya madhabahu kwa miaka mitatu baada ya kifo chake, na hawangeruhusiwa kugawana dhabihu ambazo Yehova aliwapa watu wa kawaida. Wakati tu ulipopita ndio wangeweka ng’ombe au kondoo wa daraja la juu kwenye madhabahu ya Yehova. Ikiwa kulikuwa na kosa lingine lolote, walipaswa kufunga kwa siku tatu mbele za Yehova, wakiomba neema Yake. Kuabudu kwao Yehova hakukuwa tu kwa sababu sheria za Yehova zilikuwa kali sana na za shuruti sana; badala yake ilikuwa ni kwa sababu ya neema ya Yehova, na pia ilikuwa kwa sababu walikuwa waaminifu kwa Yehova. Hivyo, huduma yao hadi leo imekuwa ya uaminifu vilevile, na hawajawahi kuvunja maombi yao mbele ya Yehova. Katika siku hizi watu wa Israeli bado wanapata utunzaji na ulinzi wa Yehova, na hata leo Yehova bado ni neema kati yao, na daima hukaa nao. Wote wanajua jinsi wanapaswa kumheshimu Yehova, na jinsi wanapaswa kumtumikia Yehova, na wote wanajua jinsi wanapaswa kuwa ili kupokea na kulindwa na Yehova, kwa sababu wote wanamcha Yehova mioyoni mwao. Siri ya mafanikio ya huduma yao yote si nyingine isipokuwa uchaji. Lakini nyinyi nyote mko namna gani leo? Je! Mnafanana na watu wa Israeli kwa vyovyote? Je! unafikiri kwamba huduma ya leo ni kama kufuata uongozi wa kielelezo mkubwa wa kiroho? Hamna tu uaminifu na uchaji wowote. Mnapokea neema nyingi, nyinyi ni sawa na makuhani wa Israeli, kwa sababu nyote mnamtumikia Mungu moja kwa moja. Ingawa hamuingii hekaluni, yale mnayopokea na mnayoona ni mengi zaidi kuliko kile ambacho makuhani waliomtumikia Yehova katika hekalu walipokea. Lakini bado mnaasi na mnapinga mara nyingi kuliko walivyofanya. Uchaji wenu ni mdogo sana, na hivyo mnapokea neema ndogo sana. Ingawa mnajitolea kidogo sana, mmepata mengi zaidi kuliko Waisraeli hao. Je! Huku sio kuwatendea nyinyi kwa wema? Wakati wa kazi katika Israeli, hakuna mtu angethubutu kumhukumu Yehova kama alivyotaka. Na nyinyi je? Kama si kwa sababu kazi Ninayofanya miongoni mwenu ni kuwashinda, Ningewezaje kuvumilia kutenda kwenu ovyo ovyo kuliaibisha kwa jina Langu? Ikiwa enzi mnayoishi ingekuwa Enzi ya Sheria, hakuna hata mmoja wenu angekuwa hai, kutokana na matendo yenu na maneno yenu. Uchaji wenu ni mdogo sana! Nyinyi daima mnanilaumu kwa kutowapa kibali kikubwa, na hata kusema kuwa sikuwapa maneno ya baraka ya kutosha, kwamba Nina laana tu kwenu. Je, hamjui kwamba kwa uchaji mdogo hivyo haiwezekani kwenu kukubali baraka Zangu? Je! Hamjui kwamba Mimi huwalaani mara kwa mara na kuwahukumu kwa sababu ya hali mbovu ya huduma yenu? Je, ninyi nyote mnajihisi kuwa mmekosewa? Ninawezaje kuwapa baraka Zangu kikundi cha watu ambao ni waasi na hawatii? Ninawezaje kutoa neema Yangu kwa watu ambao huleta aibu kwa jina Langu? Matendo kwa nyinyi watu tayari ni yenye huruma sana. Ikiwa Waisraeli wangekuwa waasi kama mlivyo leo, Ningalikuwa Nimewaangamiza muda mrefu uliopita. Ilhali Mimi siwatendei kwa vyovyote ila kwa huruma. Je! Huu sio wema? Je! Mnataka baraka nyingi zaidi kuliko hii? Wale pekee ambao Yehova anawabariki ni wale wanaomheshimu Yeye. Yeye huwaadibu wale wanaoasi dhidi Yake, Hamsamehei mtu yeyote kamwe. Je, si ninyi watu wa leo ambao hamjui jinsi ya kutumikia mko na haja zaidi ya kuadibiwa na hukumu, ili mioyo yenu iweze kurekebishwa kikamilifu? Je, kuadibiwa na hukumu ya aina hii sio baraka bora zaidi kwenu? Je! Sio ulinzi wenu bora? Bila hiyo, je, yeyote kati yenu angeweza kuvumilia moto wa Yehova unaochoma? Ikiwa kweli mngetumikia kwa uaminifu kama watu wa Israeli, je, hamngekuwa pia na neema kama rafiki yenu daima? Je, hangekuwa pia na furaha na neema ya kutosha? Je, nyote mnajua jinsi mnapaswa kutumikia?

Leo mahitaji ya nyinyi kufanya kazi pamoja kwa upatanifu ni sawa na jinsi Yehova alivyowataka Waisraeli kumtumikia. Vinginevyo, huduma yenu itafikia tamati. Kwa sababu nyinyi ni watu wanaomtumikia Mungu moja kwa moja, kwa kiwango cha chini zaidi mnapaswa kuweza kuwa waaminifu na watiifu katika huduma yenu, na lazima muweze wa kujifunza masomo kwa njia ya vitendo. Hasa wale wanaofanya kazi kanisani, je, yeyote kati ya ndugu na dada walio chini angethubutu kushughulika na nyinyi? Je, mtu yeyote angethubutu kuwaambia makosa yenu uso kwa uso? Mko juu ya yote, nyinyi kweli mnatawala kama wafalme! Hata hamjifunzi au kuingia katika somo la matendo kama hilo, na bado mnazungumza juu ya kumtumikia Mungu! Kwa sasa unaulizwa kuongoza makanisa kadhaa, na sio tu kwamba unakata tamaa mwenyewe, hata unashikilia mawazo na maoni yako, na kusema mambo kama “Nadhani jambo hili linafaa lifanyike kwa njia hii, kwani Mungu amesema kuwa hatupaswi kuzuiwa na wengine, na kwamba siku hizi hatupaswi kutii kwa upofu.” Kwa hiyo kila mmoja anashikilia maoni yake mwenyewe, na hakuna mtu anayemtii mwingine. Ingawa unafahamu wazi kwamba huduma yako iko katika shida kubwa, bado unasema, “Vile ninavyoona, yangu haiko mbali sana. Kwa hali yoyote sisi kila mmoja ana upande mmoja; unazungumza kuhusu yako, na mimi kuhusu yangu; unashiriki kuhusu maono yako na ninazungumza juu ya kuingia kwangu.” Huchukui jukumu kwa vitu vingi ambavyo vinapaswa kushughulikiwa, au unamudu tu, kila mtu akieleza maoni yake mwenyewe, kwa busara akilinda hali yake mwenyewe, sifa na uso wake. Hakuna mtu aliye tayari kujinyenyekesha, hakuna mtu atakayejitoa kwa ari kumrekebisha mwingine na kurekebishwa ili maisha yaendelee kwa haraka zaidi. Wakati mnafanya kazi pamoja, wachache kati yenu husema: “Ningependa kukusikia ukishiriki na mimi kuhusu kipengele hiki cha ukweli, kwa sababu bado nina tashwishi kukihusu.” Au kusema: “Una uzoefu zaidi kuliko mimi juu ya jambo hili; unaweza kunipa mwelekeo fulani, tafadhali?” Je, si hii ingekuwa njia nzuri ya kufanya hivyo? Nyinyi mlio kwenye viwango vya juu husikia ukweli mwingi, na kuelewa mengi kuhusu huduma. Ikiwa ninyi watu ambao mnaratibu kufanya kazi katika makanisa hamjifunzi kutoka kwa kila mmoja, na kuwasiliana, kufidia mapungufu ya kila mmoja, mnaweza kujifunza masomo kutoka wapi? Mnapokutana na chochote, mnapaswa kushirikiana na kila mmoja, ili maisha yenu yaweze kufaidika. Na mnapaswa kushirikiana kwa makini kuhusu mambo ya aina yoyote kabla ya kufanya maamuzi. Ni kwa kufanya hivyo tu ndio mnakuwa na jukumu kwa kanisa na si kuwa wazembe. Baada ya kutembelea makanisa yote, mnapaswa kukutana na kushiriki juu ya masuala yote mnayotambua na matatizo mnayokabiliwa nayo kazini, na kuwasiliana kuhusu nuru na mwanga ambao mmepokea—huu ni utaratibu wa lazima wa huduma. Lazima mfikie ushirikiano wa upatanifu kwa kusudi la kazi ya Mungu, kwa manufaa ya kanisa, na kwa kuwachochea ndugu na dada kuendelea. Unashirikiana pamoja naye na anashirikiana na wewe, kila mmoja akimbadilisha mwingine, mkifikia matokeo bora ya kazi, ili kutunza mapenzi ya Mungu. Huu tu ndio ushirikiano wa kweli, na watu kama hao tu ndio wana kuingia kwa kweli. Kunaweza kuwa na hotuba fulani isiyofaa wakati wa ushirikiano, lakini hiyo haijalishi. Shirikiana juu yake baadaye, na mpate ufahamu wa wazi kulihusu; msipuuze suala hilo. Baada ya aina hii ya ushirika unaweza kufidia mapungufu kwa ndugu na dada. Ni kwa kuenda kwa kina zaidi tu kwa namna hii katika kazi yako ndio unaweza kufikia matokeo bora. Kila mmoja wenu, kama watu wanaohudumu, lazima muweze kulinda maslahi ya kanisa katika yote mnayofanya, badala ya kuwa macho kwa maslahi yako mwenyewe. Haikubaliki kufanya pekee yako, pale ambapo unamdharau naye anakudharau. Watu wanaotenda kwa njia hii hawafai kumhudumia Mungu! Tabia ya mtu wa aina hii ni mbaya sana; hakuna hata kiasi kidogo cha ubinadamu bado kimebaki ndani yake. Yeye ni Shetani asilimia mia moja! Yeye ni mnyama! Hata sasa mambo kama haya bado yanatokea kati yenu, kwenda mpaka kushambuliana wakati wa ushirika, kutafuta visingizio kwa makusudi, kukasirika mkibishana juu ya jambo fulani dogo, hakuna mtu aliye radhi kujitenga, kila mtu akificha kilicho ndani kutoka kwa mwingine, akimwangalia mwingine na makini na kuwa macho. Je! Tabia ya aina hii ni huduma inayofaa kwa Mungu? Je, kazi kama hiyo yenu inaweza kuwakimu ndugu na dada? Sio tu kuwa huwezi kuwaongoza watu kwenye njia sahihi ya maisha, kwa kweli unaingiza tabia zako za upotovu ndani ya ndugu na dada. Je! Huwaumizi wengine? Dhamiri yako ni mbaya sana, iliyooza kabisa! Huingii katika ukweli, na huutii ukweli katika vitendo. Zaidi ya hayo, bila haya unaonyesha hadharani asili yako ya mbovu sana kwa watu wengine, huoni aibu hata kidogo! Ndugu na dada wamekabidhiwa kwako, lakini unawapeleka kuzimu. Je, si wewe ni mtu ambaye dhamiri yake imeoza? Huna aibu kabisa!

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Views: 70 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: hukumu ya siku za mwisho, Matamshi ya Kristo, upendo wa Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar