9:36 PM
Wimbo wa dini | "Ni Wakati Tu Ambapo Mungu Anakuwa Mwili Ndipo Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwandani Wake"

Wimbo wa dini | "Ni Wakati Tu Ambapo Mungu Anakuwa Mwili Ndipo Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwandani Wake"

Ni Wakati tu Mungu anapojinyenyekeza kwa kiwango fulani,
kumaanisha Anakuwa mwili ili kuishi kati ya wanadamu,
ndipo wataweza kuwa wasiri Wake,
ndipo watakuwa marafiki Zake wa karibu.
Mwanadamu anawezaje kupata sifa ya kuwa mwandani wa Mungu
Wakati Mungu ni wa Roho, metukuka na mgumu kumwelewa?
Ni kwa kuwa tu mwili ulioumbwa sawa na mwanadamu
mwanadamu ataweza mapenzi Yake, na kupatwa na Yeye.

Mungu hunena na kufanya kazi katika mwili,
Akishiriki furaha, huzuni na dhiki ya mwanadamu,
Akiishi katika dunia yao, Akiwalinda na kuwaongoza,
hivyo Akiwatakasa wapate baraka Yake na wokovu.
Mwanadamu anawezaje kupata sifa ya kuwa mwandani wa Mungu
Wakati Mungu ni wa Roho, metukuka na mgumu kumwelewa?
Ni kwa kuwa tu mwili ulioumbwa sawa na mwanadamu
mwanadamu ataelewa mapenzi Yake, na kupatwa na Yeye.

Kupitia haya, mwanadamu anaweza kuelewa mapenzi ya Mungu
na kuwa mwandani Wake; hili tu ndo la utendaji.
Kama Mungu angekuwa asiyeonekana na asiyeguswa na mwanadamu,
mwanadamu angekuwaje mwandani Wake? Je, fundisho hili ni bure?
Mwanadamu anawezaje kupata sifa ya kuwa mwandani wa Mungu
Wakati Mungu ni wa Roho, metukuka na mgumu kumwelewa?
Ni kwa kuwa tu mwili ulioumbwa sawa na mwanadamu
mwanadamu ataelewa mapenzi Yake, na kupatwa na Yeye.
Ni Wakati tu Mungu anapokuwa mwili, ndipo mwanadamu takuwa msiri Wake.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Unaweza Pia Kupenda: Mwenyezi Mungu Amekuwa Ameketi Kwenye Kiti Kitukufu cha Enzi | Kwaya ya Injili

Views: 53 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: mapenzi ya Mungu, Wimbo wa dini, Kupata Mwili | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar