9:50 PM
Juu ya Hatua za Kazi ya Mungu

Kutoka nje, inaonekana kwamba hatua za kazi ya Mungu katika kipindi hiki tayari zimemalizwa, na kwamba wanadamu tayari wamepitia hukumu, kuadibu, kuangamizwa, na usafishaji wa maneno Yake, na kwamba wamepitia hatua kama vile jaribio la watendaji huduma, kusafisha kwa nyakati za kuadibu, jaribio la kifo, jaribio la foili[b], na nyakati za[a] kumpenda Mungu. Ingawa watu wamepitia mateso makubwa katika kila hatua bado hawajaelewa mapenzi ya Mungu. Kama tu jaribio la watendaji huduma, kile ambacho watu walipata kutoka kwa hilo, kile walichoelewa kutoka hilo, na matokeo gani Mungu alitaka kutimiza kupitia kwa hilo—watu bado hawaelewi kuhusu masuala haya. Inaonekana kutokana na mwendo wa kazi ya Mungu, kwamba kulingana na kiasi cha sasa watu bila shaka hawawezi kuendelea. Inaweza kuonekana kutoka kwa hili kwamba Mungu anafichua kwanza hatua hizi za kazi Yake kwa wanadamu, na Hahitaji kwa lazima kufikia kiwango ambacho watu wanaweza kufikiria katika hatua yoyote, lakini Anajaribu kutumia hili kufafanua suala. Ili Mungu amkamilishe mtu kuweza kupatwa Naye kweli, lazima Atekeleze hatua zilizoelezwa hapo juu. Lengo la kufanya kazi hii ni kuwafanya watu waone ni hatua zipi Mungu anahitaji kutekeleza ili kulikamilisha kundi la watu. Kwa hiyo, ikiangaliwa kutoka nje, hatua za kazi ya Mungu zimemalizwa, lakini kimsingi Ameanza tu rasmi kuwakamilisha wanadamu. Hili ni jambo ambalo watu wanapaswa kuona kwa dhahiri—ni kwamba hatua za kazi Yake zimetimizwa, sio kwamba kazi Yake imetimizwa. Lakini kile ambacho watu huamini kutokana na fikira zao ni kwamba hatua za kazi ya Mungu zimefichuliwa kwa wanadamu, na hilo bila shaka ni kwamba kazi Yake imemalizika. Njia hii ya kuyaona mambo ni mbaya kabisa. Kazi ya Mungu hailingani na fikira za watu, ni jibu la mapigo dhidi ya fikira za watu mara kwa mara, na hatua za kazi Yake hazilingani hasa na fikira za watu; hii inaonyesha hekima ya Mungu. Inaweza kuonekana kutoka hili kwamba fikira za watu ni za kuvuruga mara kwa mara, na yote ambayo watu wanaweza kuyafikiria ni mambo ambayo Mungu anataka kuyalipizia kisasi. Huu ni utambuzi kutoka kwa uzoefu halisi. Watu wote hudhani kwamba Mungu hufanya kazi haraka sana, na wao hudhani kwamba wakiwa bado hawana ufahamu na bado wamepumbazika na kuchanganyikiwa kazi ya Mungu imemalizika bila ya watu kujua. Kila hatua ya kazi Yake iko hivi. Watu wengi sana huamini kwamba Mungu anawachezea watu, lakini kusudi la kazi Yake si hivyo. Mbinu Yake ya kufanya kazi ni kupitia kutafakari, kwanza kufanya kazi kutoka kwa kiwango cha jumla, halafu kuchunguza kwa utondoti, na baada ya hilo kusafisha tondoti hizo kwa ukamilifu. Hili huwashangaza watu kwa ghafla. Watu wote hutaka kumdanganya Mungu, na wao hufikiria kwamba wakiishi tu wataweza kufikia kiwango ambapo wanaweza kumridhisha Yeye, lakini kwa kweli, ingewezekanaje kwa Mungu kuweza kuridhishwa kwa ajili ya majaribio ya wanadamu ya kuishi. Mungu hufanya kazi kupitia kwa mbinu ya kuwashangaza watu kwa ghafla na kuwashtua ili kupata matokeo makubwa zaidi na kuwafanya watu wajue vizuri hekima Yake na kuelewa vizuri haki Yake, uadhama, na tabia yake isiyokosewa.

Mungu sasa ameanza rasmi kuwakamilisha watu. Ili kufanywa kuwa kamili, watu lazima wapitie ufunuo, hukumu, na kuadibu kwa maneno ya Mungu, na kupitia majaribio na usafishaji wa maneno Yake (kama vile jaribio la watendaji huduma). Kuongezea, watu lazima waweze kustahimili jaribio la kifo. Yaani, mtu ambaye kweli hufanya mapenzi ya Mungu anaweza kutoa sifa kutoka ndani ya kina cha moyo wake katikati ya hukumu ya Mungu, kuadibu, na majaribio, na anaweza kutii Mungu kwa ukamilifu na kujitelekeza mwenyewe, hivyo kumpenda Mungu kwa moyo wa uaminifu, nia moja, na utakatifu; huyo ndiye mtu kamili, na pia ni kazi ambayo Mungu anataka kufanya, na kile ambacho Mungu anataka kutimiza. Watu hawawezi kufanya uamuzi kwa urahisi kuhusu mbinu za Mungu za kufanya kazi, na wanaweza tu kufuatilia kuingia katika maisha. Huu ndio msingi. Usichunguze siku zote mbinu za Mungu za kufanya kazi; hili litazuia tu matazamio yako ya baadaye. Ni kiasi gani ulichoona sasa cha mbinu Zake za kufanya kazi? Ni vipi ambavyo umekuwa mtiifu? Ni kiasi gani ulichopata kutoka kwa kila mbingu ya kufanya kazi? Je, uko radhi kukamilishwa na Mungu? Je, uko tayari kuwa mtu mkamilifu? Haya ni mambo ambayo mnapaswa kuelewa kikamilifu. Ni mambo ambayo mnapaswa kuingia ndani yake.

Tanbihi:

a. Maandishi ya asili hayana maneno “nyakati za.”

b. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

 

 

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

1. Ni jinsi gani mtu anafaa kuitambua sauti ya Mungu? Je, mtu anawezaje kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi? Endelea Kusoma: 

 

Views: 37 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: mapenzi ya Mungu, kazi ya Mungu, Hukumu ya Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar