8:34 AM
Wimbo wa Dini “Watu Waaminifu Tu Ndio Wana Mfano wa Binadamu” | Asante kwa Upendo na Wokovu wa Mungu

Wimbo wa Dini “Watu Waaminifu Tu Ndio Wana Mfano wa Binadamu” | Asante kwa Upendo na Wokovu wa Mungu

Kwa ajili ya umaarufu na faida niliacha viwango vyote vya kutenda, na bila haya nikatumia udanganyifu kutafuta riziki yangu. Sikujali chochote kuhusu dhamiri au maadili, chochote kuhusu uadilifu au heshima. Niliishi tu kuridhisha tamaa na uroho wangu vilivyozidi kukua. Kwa moyo usio na amani, nilitembea katika matope ya dhambi, bila njia yoyote ya kuepuka giza hii isiyo na mipaka. Utajiri wa maisha na raha za muda mfupi hazingeweza kuficha utupu na maumivu ndani ya moyo wangu. Mbona ni vigumu sana kuwa na uadilifu maishani? Mbona wanadamu ni wenye hila sana, wabaya sana? Hii ni dunia ya aina gani? Nani anayeweza kuniokoa? Hii ni dunia ya aina gani? Nani anayeweza kuniokoa?

Nilisikia sauti ya Mungu na kurudi mbele ya Mungu. Nafaidika sana kutokana na kusoma maneno ya Mungu kila siku. Kwa kuelewa ukweli mwingi, sasa nina kanuni za tabia za kibinadamu. Ni ukweli unaoonyeshwa na Mungu ndio huutakasa upotovu wangu. Maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu yatembea nami maishani mwangu. Kukubali uchunguzi wa Mungu katika mambo yote huufanya moyo wangu uwe mtulivu na wenye amani. Hakuna udanganyifu, hakuna uongo, ninaishi katika nuru. Kwa moyo ulio wazi, mimi ni mtu mwaminifu, na ninaishi kwa kudhihirisha mfano wa kibinadamu mwishowe. Nikipitia majaribio na usafishaji, nimeuona uso wa Mungu, na kupata maisha mapya ndani ya maneno ya Mungu. Sasa naweza kuwa mtu mwaminifu, nitupe hila na udanganyifu wangu. Mimi nina shukrani milele kwa upendo wa Mungu na kwa wokovu wa Mungu! Nina shukrani milele kwa Mwenyezi Mungu. Asante Mwenyezi Mungu!

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Views: 91 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: wokovu wa Mungu, Maneno ya Mungu, upendo wa Mungu, ukweli | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar