9:45 PM
Ushuhuda wa Injili: Roho ya Majivuno Kabla ya Kuanguka

Baixue Mji wa Shenyang

Kwa sababu ya mahitaji ya kazi,nilihamishiwa hadi sehemu nyingine ya kazi。Wakati huo,nilikuwa na shukurani sana kwa Mungu。Nilihisi kwamba nilikuwa ninapungukiwa sana,lakini kwa njia ya ukuzwaji mtakatifu na  Mungu,nilipewa nafasi ya kutimiza wajibu wangu katika eneo la kazi la ajabu hivyo。Niliweka nadhiri kwa Mungu moyoni mwangu:Ningefanya lote ninaloweza kumlipa Mungu。

Hata hivyo,baada ya kufika,nilitambua utata mwingi katika kazi iliyokuwa ikifanyika。Matokeo yake,nilichukua jukumu mwenyewe la kuanza kukagua kila kitu cha kazi。Nilipokuwa nikitekeleza ukaguzi wangu,nilikuwa pia nikifikiri mwenyewe:“Je,kazi yoyote ilifanyikaje jinsi hii?Hakuna kazi yoyote iliyosimamiwa vizuri!Nilidhani kazi iliyofanyika hapa ingekuwa bora kabisa。Lakini sikuwahi kufikiri ingekuwa mbaya kuliko kazi yangu ya awali。Sasa kwa kuwa niko hapa,ni lazima isimamiwe vyema,hatua kwa hatua,kwa mujibu wa utaratibu wa kazi。Nitawaongoza ndugu wote kuingia katika uzima。“Kwa sababu ya hili,niliungana nawafanyikazi wenzangu,nikaanza kuratibu kila kitu cha kazi,kuwasiliana,kupanga,na kufanya mipangilio。Kote katika mawasiliano yangu,mara nyingi nilifichua hisia zangu za kweli,“Ubora wa kazi hapa uko chini。Kazi yangu kabla haikuwa jinsi yenu ilivyo sasa。Katika mahali pangu pa kazi pa zamani,siku zote tulisimamia kazi kwa namna hii na ile,sisi daima tulifanya vizuri sana。Tulikuwa watiifu kwa Mungu ....“Baada ya mikutano hii,baadhi ya wafanyikazi wenzangu wangesema:”Sawasawa kabisa!Hatujafanya kazi yoyote ya thamani halisi。Wakati huu,tunahitaji kuanza upya na kufanya kazi yetu kwa mujibu wa mahitaji ya Mungu。“Wengine wangesema:”Asante kwa mawasiliano yako makubwa na kwa mipango uliyoifanya leo。Vinginevyo,ukosefu ​​wetu wa uangalifu kwa hatua za usalama ingekuwa hatari sana。“Baada ya kusikia maneno haya,nilifurahi sana。Nilihisi kwamba nilikuwa na nguvu zaidi kuliko kiongozi wao wa awali。Ingawa nilikuwa nikijivunia mwenyewe,pia sikuweza kujizuia kuhisi mwenye hatia kidogo:Je,ilikuwa sahihi kweli kwangu kuongea jinsi hiyo?Kwa nini siku zote nilisema kwamba mahali nilipofanya kazi awali palikuwa bora?Lakini kwa upande mwingine,nilifikiri:Kuna ubaya gani kusema hivyo?Nilikuwa ninajaribu tu kuwafundisha jinsi ya kufanya kazi bora。Kwa njia hii,mimi sikufuata msukumo wa Roho Mtakatifu  kujichunguza mwenyewe。Katika  BIBLIA,Kitabu cha Mithali husema,“Kiburi huja kabla ya maangamizo,na roho ya majivuno hutangulia maanguko”(Mithali 16:18)。Nilipoanza tu kazi yangu bila kusita na kwa matumaini makubwa,nilihisi kwamba,moyoni mwangu,nilikuwa napoteza mawasiliano na Mungu。Kazi yangu haikukosa tu kufanikiwa,lakini pia ufanisi wa kazi yetu ya Injili uliacha kupanda sana hadi kuanza kushuka。Nilianguka katika hali ya uchungu zaidi,lakini sikuwa na uhakika nilichokitenda vibaya。Kwa hiyo,nikaenda mbele ya Mungu kwa sala ili nitafute mwongozo。Wakati huu,nilikumbuka kifungu kutoka kwa mahubiri:“Ili kuwa kiongozi anayemhudumia Mungu,lazima uwe na kanuni。... Kwa hali yoyote ile,bado unahitaji kushuhudia na kumtukuza Mungu Sema kadiri unavyoyaelewa,mtukuze na kutoa ushuhuda kwa Mungu kadiri uwezavyo,na usijitukuze mwenyewe wala kuruhusu wengine kukuabudu kwa hali yoyote ile。Hii ndiyo amri ya kwanza na ya msingi zaidi ya kufuata“(”Mtu Lazima Awe na Kanuni Katika Kumtumikia Mungu“katika Mkusanyiko wa Mahubiri-Ruzuku ya Maisha)。Machozi yalitiririka usoni mwangu。Majuto,hatia,na shukrani vyote vilijaa moyoni mwangu kwa wakati mmoja。Nilikumbuka yote niliyokuwa nimewaambia wafanyikazi wenzangu na nikaona kwamba mimi kweli sikustahili kutukuzwana Mungu。Kanisa liliniandalia kuja hapa kutekeleza wajibu wangu ili nipate kumtukuza na kumshuhudia Mungu,kuwaongoza ndugu mbele ya Mungu,na kuwasaidia kumjua。Na bado,bila aibu nilijionyesha,nikajitukuza,nikajishuhudia mwenyewe,na kujijenga mwenyewe。Nilifanya hivyo ili wengine waniheshimu na kuniabudu。Nilikuwa nimejaa kiburi。Nilijishuhudia mwenyewe na kujijenga mwenyewe kwa kisingizio cha kumpenda na kumridhisha Mungu。Je,mtu wa kudharauliwa hivyo anastahilije kumtumikia Mungu?Je,kazi ya mtu kama huyo inawezaje kubarikiwa na Mungu?Yote niliyokuwa nikifanya ilikuwa ni kuhangaikia umaarufu na cheo:Nilikua natembelea njia ya mpinga Kristo。Nilikuwa natenda kwa kuasi dhidi ya Mungu kabisa,na nilichukiwa na Mungu kwa kweli。Nilivyozidi kufikiri juu ya hilo,ndivyo nilivyozidi kujichukia sana。Sikuweza kujizuia ila kusujudu kwa majuto mbele ya Mungu,na kulia Kwake,“Ee Mungu!Asante kwa adabu na hukumu zako ambazo ziliniamsha,zikiniruhusu kutambua asili yangu ya kishetani。Pia ulifichua mwelekeo wa huduma yangu kwangu,ukinisaidia kuelewa kuwa nikikutukuza na kukushuhudia tu Wewe ndipo ninapoweza kukuridhisha,kuruhusu mapenzi Yako yafanyike,na kutimiza misheni Uliyonipa Wewe kufanya。Nikijitukuza na kuwa na ushuhuda Kwako tu ndio huduma yangu inaweza kuwa ya kupendeza moyo Wako Huo ndio wajibu wangu kama kiumbe kwa Muumba。Ee Mungu!Kuanzia sasa kuendelea,nimeahidi kuchunguza moyo wangu na matilaba kabla nizungumze au kutenda,kukutukuza kwa makusudi na kuwa na ushuhuda  Kwako,nikiwaongoza ndugu kukujua Wewe,na kuufariji moyo Wako kwa kuwa mtu mwenye ukweli na ubinadamu。“

Chanzo:  Roho ya Majivuno Kabla ya Kuanguka

Maudhui Yanayohusiana:  Mwenyezi Mungu  Amekuwa Ameketi Kwenye Kiti Kitukufu cha Enzi 

Views: 72 | Added by: hatat1946 | Tags: Roho Mtakatifu, Ushuhuda wa Injili | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar