3:55 PM
Ufahamu Kiasi Kuhusu Kuokolewa

Lin Qing   Jijini Qingzhou, Mkoa wa Shandong

Kwa miaka hii mingi ya kumfuata Mungu, nimeacha familia yangu na raha za mwili, na nimekuwa na shughuli nyingi siku nzima nikitimiza wajibu wangu kanisani. Kwa hiyo niliamini: Mradi tu nisiache kazi yangu katika kanisa, nisimsaliti Mungu, nisiache kanisa, na kumfuata Mungu hadi mwisho, nitahurumiwa na kuokolewa na Mungu. Niliamini pia kuwa nilikuwa nikitembea katika njia ya wokovu na Mungu, na yote niliyokuwa niyafanye ni kumfuata Yeye mpaka mwisho.

Lakini siku chache zilizopita, niliona maandishi fulani kutoka kwa “Ni Wale Tu Ambao Wanapata Ukweli na Kuingia Katika Uhalisi ndio Wanaookolewa Kweli”: “Kuokolewa na Mungu si rahisi kama watu wanavyofikiria. Lazima tupitie hukumu na kuadibu pamoja na majaribio na usafishaji kutoka kwa neno la Mungu hatua kwa hatua. Lazima tufuate kwa makini kila hatua ya kazi ya Mungu, na hatimaye kupata ukweli na kufikia mabadiliko katika tabia kuwa kiumbe kipya, na kuwa na uwezo wa kutegemea ukweli ili kushinda dhidi ya Shetani na kuvuka mipaka ya dhambi. Lazima tuwe na uwezo wa kuishi kwa ufahamu kwa kutegemea maneno ya Mungu, kumtii Mungu kikamilifu na kulingana na Yeye. Huku tu ndiko kushinda Shetani kwa kweli, kuvuka mipaka ya dhambi, na kupatwa na Mungu. Ikiwa tunaweza kufikia matokeo haya kutokana na kupitia kazi ya Mungu, basi huku tu ndiko kuokolewa na Mungu kwa kweli” (Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha). “Katika njia ya kufuatilia ukweli na kufikia wokovu na Mungu, kuna bado matatizo mengi na vikwazo, kama vile familia kuvunjika, maafa ya asili na ya kuletwa na mwanadamu—kila aina ya jaribio na matatizo ambayo lazima watu wapitie. Kwa hakika sio safari nyororo, na ikiwa watu hawana ukweli, hawawezi kusimama imara, uwezekano wa kumsaliti Mungu ni asilimia 100.” (Ukusanyaji wa Mahubiri—Ruzuku ya Uzima). Baada ya kusoma hili, nilihisi kama kwamba nilikuwa nikiamka kutoka ndotoni. Kwa hiyo, kuokolewa na Mungu hakukuwa rahisi kama nilivyokuwa nimefikiri hata hivyo; inategemea watu kupitia kazi na maneno ya Mungu kila hatua ya njia, kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu, ushughulikiaji na upogoaji, pamoja na kupitia machungu ya kila aina ya maudhi na kero. Ili waweze kufikia ufahamu halisi wa tabia zao potovu na hatua kwa hatua kujiondolea upotovu, na hatimaye waweze kutegemea maneno ya Mungu na kutegemea ukweli kumshinda Shetani na kuvuka mipaka ya nguvu za giza katika kila aina ya mazingira. Kufikia matokeo haya tu ndio kuokolewa na Mungu kwa kweli. Lakini kulinganisha hili na hali yangu halisi, nilikuwa mbali na kufikia matokeo hayo. Kulikuwa na nyakati nyingi sana ambazo hata ingawa nilijua kufuatilia sifa na hadhi haikukubaliwa na Mungu, nilikuwa bado ninajishirikisha katika kufuatilia vitu hivi, na nilikuwa hasi na dhaifu wakati sikuvipata. Ningepoteza motisha yangu kufuatilia ukweli na kuanguka gizani ambamo singeweza kujinasua. Kulikuwa na nyakati nyingi sana ambazo hata ingawa nilijua kumwamini Mungu kunamaanisha napaswa kufuatilia ukweli ili kulipiza upendo Wake na kuwa singeweza kufanya shughuli na Mungu, niliona kwamba kazi ya Mungu ilikuwa ikichukua muda mrefu kumalizika na nikabeba uhasi ndani yangu. Nguvu zangu za nyakati za awali zilipotea tu bila ya kupatikana, na nilikuchukulia kutimiza kazi yangu ovyoovyo. Nilipokumbana na shida katika kazi yangu, ingawa nilijua kuwa hii ilikuwa Mungu akinifanyisha kupitia shida, ndani nilikuwa bado nimejaa kutoelewa na malalamiko kwa Mungu. Nilihisi kuwa kumwamini Mungu kulikuwa kugumu sana, kwa kuchosha sana, na kila mara nilitaka kutoroka, na hata kuacha kazi yangu. Kulikuwa na nyakati nyingi sana ambazo hata ingawa nilijua mazingira na watu wote, masuala, na vitu vilivyonizunguka vilipangwa na Mungu ili kunikamilisha, na kuwa napaswa kutafuta ukweli kutoka kwa vitu hivi, nilipokabiliana na mtu, suala au kitu ambacho hakikuwa sawa na dhana zangu, kila mara ningekipinga na sikutaka kukubali. Nilipowaona watu wengine na familia zenye furaha ilhali nilikuwa nimeachwa na wapendwa wangu na sikuwa na mahali pa kupumzika, mara nyingi nilihisi huzuni na maumivu kutokana na hili, kwa kiasi kwamba mara kadhaa nilitaka kuondoka kwa Mungu. ... Hata hivyo, bado nilidhani kuwa nilikuwa nimechukua njia ya wokovu wa Mungu muda mrefu uliopita. Nikitazama hali zote hizi halisi, ningewezaje kuwa na kimo cha kweli hata kidogo? Nilipokumbwa tu na majaribio fulani madogo au kuvunjwa moyo, nilikuwa katika hatari ya kujikwaa, bila kutaja kuwa na uwezo wa kusimama imara katikati ya dhiki kubwa na mateso. Wakati huo nikaona kuwa ingawa nilikuwa nimemfuata Mungu kwa miaka mingi bila kukata tamaa, sikuwa nimeshika ukweli hakika, na tabia yangu ya maisha haikuwa imebadilika hata kidogo. Nilikuwa bado nikiishi chini ya ushawishi wa giza wa Shetani na nilikuwa mhusika wa ulaghai na utawala wake. Hii ilikuwa mbali kabisa na kiwango cha kuokolewa kwa kweli na Mungu, lakini bado niliamini kuwa nilikuwa nimeingia katika njia ya wokovu kutoka kwa Mungu zamani na nilikuwa karibu kutosha—hii ilikuwa tu kujidanganya.

Ee Mungu, asante! Ilikuwa kupata nuru Kwako na mwongozo ndio uliniruhusu kuona hali yangu ya kweli kwa wazi na kunifanya kuelewa ni nini wokovu wa kweli, kubadilisha maarifa yangu ya uwongo kutoka zamani. Pia ilinifanya nielewe kuwa kama sipati ukweli au kuwa na mabadiliko katika tabia yangu ya maisha, bila kujali miaka mingapi nimemwamini Mungu, sitapata idhini Yako. Kuanzia leo na kuendelea mbele, niko radhi kutunza tunu hii ya wakati ili kujiandaa na ukweli zaidi, na kupitia uzoefu wa kazi Yako, nitajiondolea tabia yangu potovu. Nitaishi kulingana na maneno Yako na kukutii kabisa, na kufikia wokovu wa kweli kupitia Kwako.

Chanzo: Ufahamu Kiasi Kuhusu Kuokolewa

Views: 120 | Added by: hatat1946 | Tags: wokovu wa Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar