8:42 PM
Hatimaye Naishi kwa Kudhihirisha Kiasi Kama Mwanadamu

Xiangwang Mkoa wa Sichuan

Ninahisi kuadibiwa sana moyoni mwangu kila mara ninapoona kwamba maneno ya Mungu yanasema: “Wanadamu dhalimu, wakatili! Kufumba macho na kula njama, kusukumana, kung’ang’ania sifa na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Mungu amezungumza maelfu na mamia ya maneno, ilhali hakuna hata mmoja ambaye amejifahamu. Wanatenda matendo kwa ajili ya familia zao na watoto wao, kazi zao, matarajio, hali katika jamii, majivuno na pesa, kwa sababu ya nguo, kwa sababu ya chakula na mwili—matendo ya nani kwa kweli ni kwa ajili ya Mungu? Hata miongoni mwa wale ambao matendo yao ni kwa ajili ya Mungu, ni wachache tu wanaomfahamu Mungu. Ni wangapi wanaotenda matendo yasiyo kwa maslahi yao? Ni wangapi wasiobagua na kuonea wengine wakiwa na nia ya kudumisha hali yao? Ndivyo Mungu amehukumiwa kifo mara nyingi kwa nguvu, mahakimu katili wasiohesabika wamemhukumu Mungu na mara nyingine tena wakamsulubisha msalabani” (“Waovu Lazima Waadhibiwe” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ninawaza jinsi sikuutafuta ukweli, jinsi katika kutimiza wajibu wangu nilishindana na wenzangu kazini tena na tena, jinsi kwa ajili ya sifa na faida yangu ningekandamiza au kukana yule mwingine—jinsi nilisababisha hasara kwa maisha yangu na pia kwa kazi ya familia ya Mungu. Ingawa Mungu alipanga hali nyingi kuniokoa, nilikuwa bila hisia na nilishindwa kabisa kutambua nia ya Mungu. Lakini Mungu aliendelea kunihurumia, kuniokoa, na ni baada tu ya kuadibu na kuhukumu tena na tena ndipo nilizinduka na kuelewa tamanio la Mungu kutuokoa, nikaweka kando kufukuzia kwangu sifa na hadhi na kuanza kutenda kidogo kama mwanadamu.

Hatimaye Naishi kwa Kudhihirisha Kiasi Kama Mwanadamu | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mnamo mwaka wa 1999, nilikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Wakati huo familia yangu ilitimiza wajibu wetu wa ukarimu na niliona jinsi ndugu fulani waliwasiliana vyema, kuweza kutumia maneno ya Mungu kujibu swali lolote. Sote tulikuwa tayari kushirikiana nao, na tungewasiliana wazi nao kuhusu maswala yoyote. Niliwaonea wivu, nikifikiri: Si ingekuwa vizuri sana iwapo ningeweza kuwa kama wao siku moja, nimezungukwa na ndugu, nikitatua shida zao? Na nikiwa na kusudi hili, nilianza kutimiza wajibu wangu kanisani. Mwaka wa 2007, nilipokea upandishaji na shukrani ya Mungu na nilipewa jukumu la kiongozi wa wilaya. Ndugu zangu walitoa ripoti kwangu iwapo wale waliokuwa chini ya kazi yangu walikuwa katika hali isiyo sahihi, kuhusu matatizo yao wenyewe, na maswala mbalimbali katika wilaya. Nilijihisi kwamba nilikuwa katika udhibiti wa mambo na kwamba miaka yangu ya kazi ilikuwa ya kufaa: Sasa ningeweza kuwasilisha ukweli fulani na kusaidia ndugu zangu na matatizo yao. Na ingawa kazi ilikuwa nyingi kiasi, nilikuwa tayari kufanya kazi kwa bidii. Ili kuendeleza cheo hiki na kutimiza majivuno yangu nilitenda kwa mfano mzuri na namna njema wakati wa kutekeleza wajibu wangu. Pasipo kujali kazi ambayo viongozi walitupa, hata kama wenza wangu kazini walihisi kwamba ilikuwa ngumu au hawakuwa tayari kushirikiana, siku zote mimi niliitikia vyema, na iwapo nilikuwa na matatizo nilinyamaza na kukubaliana nao kwa vitendo. Hata kama kulikuwa na vitu ambavyo sikuelewa nilijifanya kuelewa, ili kupata sifa za viongozi wangu.

Ili viongozi wangu wangeniheshimu na ningejitokeza miongoni mwa wenzangu wa kazi, nilianza kupanga jinsi ningeweza kufikia malengo yangu: Ilikuwa rahisi zaidi kutambulika, kuthibitisha uwezo wangu na kupata sifa ya viongozi wangu, wakati wa kufanya kazi ya injili. Mradi kazi hiyo ilikuwa ya kufaa, haikuwa hoja kubwa kama kazi yako nyingine haikuwa ya kufaa—viongozi hawangenipogoa wala kunishughulikia. Na basi nikaanza kufanya kazi: Nilibadilisha jinsi niliendea kazi ya injili, sikuwaelekeza ndugu zangu kwa uvumilivu tena. Iwapo wangeripoti matatizo yoyote katika kazi ya injili ningewapogoa na kuwashughulikia. Nilianza kuwasukuma na kuwasumbua viongozi wa kanisa kwa ajili ya matokeo, na iwapo matokeo yalikuwa ya kutoridhisha nilikasirika: “Mbona mmepata watu wachache sana? Mnataka kuendelea kuwa na kazi hii? Tusipoona matokeo bora zaidi mwezi ujao itabidi tuwabadilishe!” Sikuzingatia kimo cha ndugu zangu, wala sikutumia ukweli kusuluhisha shida na matatizo waliyoyakumba. Niliwasukuma na kuwasumbua tu na nia ya kudumisha cheo changu mwenyewe. Kwa haraka matokeo yalikuwa mazuri zaidi, ambayo ilinifurahisha sana. Matokeo bora yalimaanisha kwamba nilikuwa kati ya wafamya kazi wenza bora zaidi na nikawa napendezwa na mimi mwenyewe. Muda usio mrefu baadaye ndugu mmoja alipewa kazi kwetu. Alikuwa mwenye sura nzuri na alikuwa mnenaji mzuri na mtu aliyewasiliana vizuri. Alizunguka makanisani na ndugu wote walisifu ushirika wake. Hili lilinikasirisha: Wote walisifu ushirika wake—jambo ambalo lazima limaanishe kwamba wangu haukuwa mzuri! Ingekuwa vyema zaidi ikiwa hangekuwa ametumwa hapa. Nikijipima dhidi yake niligundua kwamba kweli alikuwa bora zaidi kuniliko. Lakini sikuwa tayari kukata tamaa. Wakati huo nilijishughulisha na sifa na faida na sikuvutiwa na shida mbalimbali za kanisa. Nilianza kujali kuhusu nilichovaa, jinsi nilivyoongea na kutenda. Katika mikutano nilionyesha busara yangu kimakusudi ili ndugu zangu wangeniheshimu. Wakati mwingine ningemdunisha ndugu aliyeletwa kufanya kazi nami na kutazama kuona jinsi wale waliokuwa chini ya kazi yetu walinichukulia. Niliishi katika hali mbaya na sikuweza kujiokoa. Katika mambo yote nilijilinganisha na ndugu huyo na nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu kabisa. Muda usio mrefu baadaye, nilibadilishwa kazini. Niliposikia habari ilikuwa kana kwamba kisu kikisokotwa moyoni mwangu—je heshima yangu, hadhi yangu, siku zangu za usoni? Mungu alikuwa ananihukumu na kuniadibu, ilhali sikuwa na ufahamu wowote wa asili yangu. Kinyume nayo nilikisia kuhusu jinsi viongozi wangenichambua katika maeneo mengine: Ningewakabili watu vipi, wale walionijua wangefikiria nini? Nikiwa nimenaswa katika utando wa Shetani, nilianza kulalamika, nikijuta kwamba nilikuwa nimetimiza wajibu wangu kama kiongozi, kwamba ikiwa singekuwa nimechukua jukumu hilo hili halingekuwa limefanyika kamwe. … Kadiri nilivyowaza ndivyo niliteseka zaidi. Chini ya adabu ya Mungu nilikuwa napoteza usingizi na kuwaza mawazo ovyo. Mwishowe nilikuwa karibu navunjika kiroho, na mara kadhaa niliwazia kulala barabarani ili gari linikanyage. Nilijua kwamba wakati huu nilikuwa katika hali hatari, lakini singeweza kujiweka huru na sikuwa na chaguo lingine ila kusimama mbele ya Mungu na kuomba: “Ee Mungu, wakati huu naishi katika giza, nikiwa nimedanganywa na Shetani na kuteseka sana. Sitaki kukubali kila kitu ambacho kimenifanyikia leo, nataka kuhepa adabu na hukumu Yako, na nimelalamika na kukusaliti Wewe. Ee Mungu! Ninakusihi Wewe uulinde moyo wangu, Unifanye niweze kujichunguza na kujifahamu, Unihurumie.” Baada ya hili niliona ushirika wa mtu yule: “Watu wengine Mungu huwatendea na ukarimu na hadhi fulani. Wanapandishwa cheo kuwa viongozi au wafanyikazi, wanapewa kazi muhimu. Lakini watu hawa hawarudishi upendo wa Mungu, wanaishi kwa ajili ya miili, hadhi na sifa zao wenyewe, wakitafuta kujitolea ushuhuda na kupata heshima. Je, matendo haya ni matendo mazuri? Si mazuri. Watu hawa hawaelewi jinsi ya kumtuliza Mungu, hawafikiri mapenzi ya Mungu. Wanatafuta kujiridhisha tu wenyewe. Hawa ni watu wanaoudhuru moyo wa Mungu, wanaotenda maovu pekee, wanaosababisha madhara makubwa sana, madhara mengi sana, kwa moyo wa Mungu. Mungu huwapandisha cheo kama viongozi, kama wafanyikazi, kuwaendeleza, hivyo watakuwa kamili. Lakini hawajali mapenzi ya Mungu na wanatenda tu kwa ajili yao wenyewe. Hawafanyi kazi kuwa na ushuhuda kwa Mungu au kufanya kazi ili wale ambao Mungu amewachagua waweze kuingia katika maisha. Wanafanya kazi ili kujitolea ushuhuda, kutimiza malengo yao wenyewe, kuwa na hadhi miongoni mwa wale ambao Mungu amechagua. Hawa ndio watu wanaompinga Mungu zaidi, wanaoudhuru moyo wa Mungu zaidi. Huu ni usaliti kwa Mungu. Kwa maneno ya mwanadamu ni kushindwa kuthamini yale wanayofanyiwa, kwa maneno ya kiroho hawa ni watu waovu wanaompinga Mungu” (“Maana ya Muhimu ya Kuandaa Matendo Mazuri” katika Ushirika na Mahubiri Kuhusu Kuingia Katika Maisha II). Mawasiliano haya yalihisi kama upanga wenye makali pande zote mbili ukinidunga moyoni, ukiniwacha nimeadibiwa vikali. Ni ukarimu na upandishaji wa Mungu ndio uliniruhusu kuwa kiongozi, na Alikuwa amefanya hivi ili ningeweza kuwa kamili. Lakini sikufikiri kuhusu lengo la Mungu na sikujua kulipiza upendo Wake. Niliishi kwa sababu ya hadhi na sifa, kujitolea ushuhuda, na asili ya hili ilikua kumpinga na kumsaliti Mungu. Mungu alichukia kabisa kila kitu nilichofanya na hivyo Alikomesha huduma yangu, kunionyesha ya kwamba katika familia ya Mungu, Mungu na ukweli yanatawala. Niliwazia kuhusu kile nilichokuwa nimetafuta: Nilifikiri kudumisha uhusiano mzuri na viongozi wangu kungehakikisha kwamba nilihifadhi cheo changu, kwa hivyo nilijinyenyekea mno kwao na kukubali kila neno lao. Lakini na ndugu zangu nilikuwa mkali na wa kukosoa. Jambo la kudharauliwaje! Ningefanya chochote kwa ajili ya hadhi. Nilijaribu kutumia ndugu zangu kutimiza lengo langu la kujitokeza miongoni mwa wengine; sikutimiza wajibu wangu kwa maisha ya ndugu zangu. Nilisukuma na kusumbua, hadi kiwango ambacho wale chini ya kazi yangu waliniogopa na kuepukana nami, wasithubutu kujiweka wazi mbele yangu. Ilhali sikugeuka na kujichunguza. Mungu alikuwa amemtuma ndugu huyo kwangu na kando na kushindwa kujifunza kutoka kwa somo hili, nilipigana kwa nguvu zaidi zaidi kwa ajili ya sifa na faida, nikionyesha mwili wangu na kusababisha Mungu kunichukia na kupoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Na ubadili wangu ulikuwa haki ya Mungu kunijia: hukumu bora zaidi iwezekanayo kwangu, wokovu bora zaidi, upendo mkuu wa Mungu. Vinginevyo ningeendelea kwenye njia ya anayempinga Kristo bila kujua. Mungu alikomesha hatua zangu za dhambi. Nilijuta sana kwamba lengo langu la awali la kufukuzia kwangu halikuwa sahihi na kwamba sikuwa nimelenga kutatua shida hiyo, yote ambayo yalisababisha kushindwa kwa leo. Wakati huo, wakati wowote nilipoimba wimbo wa uzoefu ningelia, machozi yakitiririka usoni mwangu: “Baada ya kukosea tabia Yako niliangukia gizani na kuhisi kikamilifu madhara ya Shetani. Nilihisi mwenye majonzi na asiyeweza kujisaidia, nikishutumiwa na dhamiri yangu, kuteseka zaidi ya kifo, na hapo tu ndipo nilijua furaha ya dhamiri iliyo tulivu. Nilipoteza nafasi ngapi za kuwa kamili, nikishindwa kuona malengo Yako mazuri. Hata nikitoa kila kitu siwezi kufidia madhara ambayo umefanyiwa moyo Wako. Ee Mungu, Mungu wa vitendo, ningependa sana kurudi hapo awali na kuanza upya. Ninawezaje kulingana nawe wakati moyo wangu huficha matamanio badhirifu? Natamani faida za hadhi—basi ninawezaje kukosa kuanguka? Siku zote nilikuwa sijali mapenzi Yako, nilikuwa baridi na wa kukupinga Wewe, na nikiwa nakutumikia pia nilipinga na kudanganya. Isingekuwa huruma Yako, singekuwa hapa leo. Kuzingatia yale ambayo nimefanya kifo hakingenikomboa. Pumzi hizi ninazopumua zimepatikana kupitia uvumilivu Wako. Ee Mungu, Mungu wa vitendo, singefaa kukufanya Wewe uteseke mno kwa ajili yangu. Maneno Yako ya uhai hugusa moyo wangu, ushawishi Wako hunipa nguvu bila mwisho, yakiniruhusu kusimama tena katikati ya kushindwa, kunionyesha thamani ya maisha na mbona niliumbwa. Hivyo nikiwa nimekabiliwa na ombi Lako la mwisho, ningewezaje kuhepa tena? Ninataka kutumia matendo halisi kulipia gharama ambayo Wewe umelipa. Iwapo ninapata baraka au shida, ningependa tu kukuridhisha Wewe, kujitolea kwako Wewe, kukufuata kwa karibu hata kama sipati chochote kama malipo” (“Huruma ya Mungu Ilinipa Kuzaliwa Tena” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Usafishaji huu ulikuwa nami kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja na licha ya mateso ya kufa na kupona, yaliyohisi kama kuchunwa nikiwa hai, nilipata tamaa zangu za hadhi na matazamio yalikuwa yamepunguzwa nguvu, na niliona jinsi usafishaji huu ulikuwa wa thamani.

Mwaka wa 2012 dada mmoja aliyesimamia kazi alinipa mimi na kaka mmoja kazi ya uondoshaji na ufukuzaji mahali fulani. Kwa sababu sikuwa nimefanya kazi ya kanisa kwa muda mrefu, sikuelewa kanuni fulani vizuri zaidi. Nilihisi kwamba shida fulani kanisani na mambo yanayoamua hali ya vitu katika kazi yetu ya uondoshaji na ufukuzaji yalikuwa magumu kwa kiasi fulani. Lakini kaka huyo alikuwa amefanya kazi ya kanisa daima na kufidia ukosefu wangu, akinionyesha yale niliyopaswa kujifunza. Huu ulikuwa upendo wa Mungu—Hakuniwekea mzigo mzito. Kaka huyo alitoa ripoti juu ya kazi yetu, na alifanya mengi ya mawasiliano wakati wa uamuzi wa hali ya vitu. Tulipokutana na wale waliokuwa chini ya kazi yetu yeye alikuwa wa kwanza kuwasiliana na baada ya muda ilikuwa kana kwamba sikuwepo, na kitu ndani yangu kilijitokeza: Wakati tunafanya kazi pamoja, wewe uko bora zaidi katika ushirika, lakini mimi niko bora zaidi katika kazi ya injili. Na haijalishi jinsi ulivyo bora katika ushirika unapaswa kuwa mwenye vitendo. Si wakubwa wetu walisema kwamba kazi ya uondoshaji na ufukuzaji haifai kuwa yenye kuleta hasara kwa kazi ya injili? Unaongea, tena na tena, ukijigamba. Ingekuwa afadhali tukitengana ili nami pia niweze kuonyesha uwezo wangu. Si kwamba sina uwezo. Unaweza kudhani kwamba sina ujuzi vile katika ushirika, lakini niko bora zaidi katika kazi ya vitendo kukuliko wewe, na hata hivyo, kazi ya injili ndio uwezo wangu. Na hapo tulipokea barua kutoka kwa dada aliyesimamia kazi—kwa sababu za uendeshaji tungefaa kutengana, kila mmoja akiwajibikia eneo moja. Na ingawa matokeo ya aina zote za kazi katika eneo nililowajibikia hayakuwa mazuri kama yale ya eneo la kaka yangu, bado nilikuwa na furaha: Nilikuwa na mahali pa kutumia talanta zangu. Na haijalishi kwamba matokeo hayakuwa mazuri sana—subiri hadi wakati nimeshughulikia hilo, nitathibitisha jinsi nilivyo na uwezo. Punde tu tulipotenganishwa nilijibwaga kazini na kuanza kupanga mambo, nikiwasiliana na ndugu kuhusu mipango ya kazi na kutafuta maneno ya Mungu ya kuwasiliana nao. Na mambo yalianza kuwa bora zaidi. Na sikuweza kujizuia kufikiria: Kaka yangu anaendelea vipi? Je, anaendelea vyema zaidi kuliko mimi? Na tulipokutana na nikapata habari kwamba kazi yangu ya injili ilikuwa bora zaidi kuliko yake, kwamba nilikuwa nimepata watu zaidi, nilifurahi kisiri: Mwishowe mimi ni bora kukuliko wewe na ninaweza kujivunia. Na nilipokuwa tu nafurahi, Roho Mtakatifu alinishutumu: “Huibi utukufu wa Mungu?” Nilisononeka. Ndio, kueneza injili ni wajibu na jukumu la kila mteule wa Mungu, lakini nilikuwa nimeiona kama njia ya kuelekea kwa sifa na faida. Na ilikuwa kwa sababu ya ushirikiano wa ndugu zangu, sababu ya baraka ya Mungu, kwamba tulikuwa tumewapata watu wale. Nilikuwa na nini cha kujivunia? Niliona aibu nilipofikiria kuhusu hili. Nilikuwa wa kudharauliwa sana. Utakatifu wa Mungu haukuniruhusu kuwa na upotovu kama huu, na nilipotambua hali zangu nilimshukuru Mungu kwa kunirudishia fahamu. Singetafuta sifa na hadhi tena. Katika siku zilizofuata nililenga kusoma maneno ya Mungu, wakati nilikumbana na hali nilizikubali kama za kutoka kwa Mungu, na polepole tamaa yangu ya sifa na hadhi ilipotea. Nililinganisha tu upendo wangu kwa Mungu na ule wa wenzangu kazini, na kutumia uwezo wa kila mmoja na kufidia mapungufu ya kila mmoja. Muda mfupi baadaye nilipandishwa cheo kutimiza wajibu mwingine. Nilishangaa sana na nilijua huku kulikuwa Mungu kuniinua. Nilithamini wajibu huo, nikitamani kufanya kila niwezalo kumridhisha Yeye.

Mwezi wa Agosti 2012, yule dada aliyesimamia kazi yetu aliwasiliana nami, akinipa kazi kutimiza wajibu wangu eneo lingine. Wakati huo nilikubali kwa hamu, lakini kabla niondoke alisema: “Ni bora zaidi kumtuma yule kaka kufanya kazi nawe, itakuwa bora zaidi kwa kazi ya familia ya Mungu….” Aliulizia maoni yangu, na nilisema: “Hiyo ni sawa, niko tayari kufanya kazi naye.” Na wakati tulionana katika mkutano, alikuwa wazi na mimi: “Sikukubaliana nao kukuchagua, ushirika wako si bora kama wangu!” Hiyo kauli moja iliyotolewa bila kufikiri iliniwacha katika msukosuko mkubwa. Nilifikiri nilikuwa nimeacha nyuma ubaguzi wangu dhidi ya kaka yangu, lakini kwa kusikia hilo kitu kilijitokeza tena ndani yangu: Ni aibu kweli, singekubali kwenda naye. Anajua kasoro zangu zote. Nilikuwa nimefikiri kuwa kwa kufika katika kazi yangu mpya ningetambuliwa vyema zaidi kama mgeni! Lakini sasa hakuna cha kufanywa. Nililazimisha tabasamu na kutenda kana kwamba hakukuwa na chochote kibaya, nikifikiri: Mimi si mstadi katika ushirika, lakini nilichaguliwa kwanza kwa sababu mimi ni bora zaidi kukuliko wewe. Ikiwa huniamini, subiri uone! Tulisafiri hadi eneo letu mpya la kazi na kujibwaga katika kufanya wajibu wetu. Mwanzoni, tukikutana na wale chini ya kazi yetu, niliomba niweze kuunyima mwili, kujizuia kwa ajili ya ubia patanifu. Nilisikiza kwa makini jinsi alivyowasiliana na wale chini ya kazi yetu kuhusu hali zao na nilimwombea, ilhali kuhusu kazi ya injili niliwasiliana nao. Baada ya muda fulani, niliona jinsi mawasiliano yake yalikuwa dhahiri zaidi kuliko yangu. Wakati wa mikutano na wale chini ya kazi yetu sikutaka kusema neno hata moja katika ushirika. Nilitamani mikutano hiyo ingeisha mapema na nilitaka kutoroka. Tulikuwa na jukumu la eneo kubwa wakati huo, na nilifikia wazo: Ikiwa tungefanya kazi kama tumetengana singeteseka sana. Nilipoelezea ndugu yangu hili alikubali: “Ukubwa wa eneo hili unafanya kazi iwe ngumu, ingekuwa sawasawa kutengana.” Wakati nilikutana na waliokuwa chini ya kazi yangu pekee yangu niliweza kuongea kwa kiwango kikubwa sana, kuwasiliana na kupanga, kuchukua “mzigo” mzito kwa ajili yao. Muda mfupi baadaye niliona matokeo katika vipengele vyote vya kazi yangu, wakati kaka yangu hakuwa anafanya vizuri sana vile. Sikufanya chochote kuihusu, kana kwamba haikunihusu. Katika mkutano kiongozi wetu alipata habari kwamba tulikuwa tunafanya kazi tukiwa tumetengana na aliwasiliana nasi majukumu ya kazi yetu na ukweli wa ubia patanifu. Nilikuwa tayari kukubali hili na kutoendelea tena kufanya kazi kwa utengano naye. Lakini tuliendelea kufanya kazi tukiwa tumetengana, tukitumia kisingizio kwamba sote tulijua kazi zetu wenyewe vyema zaidi. Nikiogopa kwamba kiongozi wangu angenikashifu nilienda kwa eneo la kazi la ndugu yangu kuwasiliana na wale waliokuwa chini ya kazi yake, lakini nilihisi nilikuwa nje ya eneo langu mwenyewe. Iwapo ningewasiliana vizuri ilionekana kwamba kaka yangu angepata sifa. Hivyo nilifanya vitu kwa namna isiyo ya dhati na kutoa kisingizio, nikisema kwamba nilikuwa na kazi ya usimamizi ya kufanya, na kutoweka. Kaka yangu aliendelea kutoona matokeo, ilhali sikujilaumu wala kuhisi kuogopa—sikumwogopa Mungu, na hata nilipuuza mawasiliano kadhaa kutoka kwa kiongozi wetu. Hili liliendelea hadi tulikuwa tunatoa ripoti juu ya kazi zetu, wakati nilishangaa: Ingawa eneo langu lilikuwa na watu wengi, wakati maeneo yetu wawili yalijumlishwa idadi ilikuwa kidogo. Hapo tu ndipo niliogopa. Nilikuwa nimejaribu kudhibitisha nilikuwa na uwezo, kutimiza lengo langu la kuonyesha jinsi niliweza kufanya kazi vizuri sana, kwamba nilikuwa bora zaidi kuliko yeye katika kazi ya injili. Lakini kazi ya injili katika eneo lake ilikuwa nusura isimame—na wakubwa wetu walikuwa wamesema hilo halikustahili kutendeka kwa hali yoyote. Nilikuwa nimekuwa kizuizi kilichozuia mapenzi ya Mungu kutekelezwa. Sikuwa na budi ila kutazamia maneno ya Mungu kuona chanzo cha hali hizi. Niliona yafuatayo: “Kila mmoja wenu, kama watu wanaohudumu, lazima muweze kulinda maslahi ya kanisa katika yote mnayofanya, badala ya kuwa macho kwa maslahi yako mwenyewe. Haikubaliki kufanya pekee yako, pale ambapo unamdharau naye anakudharau. Watu wanaotenda kwa njia hii hawafai kumhudumia Mungu! Tabia ya mtu wa aina hii ni mbaya sana; hakuna hata kiasi kidogo cha ubinadamu bado kimebaki ndani yake. Yeye ni Shetani asilimia mia moja! Yeye ni mnyama! Hata sasa mambo kama haya bado yanatokea kati yenu, kwenda mpaka kushambuliana wakati wa ushirika, kutafuta visingizio kwa makusudi, kukasirika mkibishana juu ya jambo fulani dogo, hakuna mtu aliye radhi kujitenga, kila mtu akificha kilicho ndani kutoka kwa mwingine, akimwangalia mwingine na makini na kuwa macho. Je! Tabia ya aina hii ni huduma inayofaa kwa Mungu? Je, kazi kama hiyo yenu inaweza kuwakimu ndugu na dada? Sio tu kuwa huwezi kuwaongoza watu kwenye njia sahihi ya maisha, kwa kweli unaingiza tabia zako za upotovu ndani ya ndugu na dada. Je! Huwaumizi wengine? Dhamiri yako ni mbaya sana, iliyooza kabisa! Huingii katika ukweli, na huutii ukweli katika vitendo. Zaidi ya hayo, bila haya unaonyesha hadharani asili yako ya mbovu sana kwa watu wengine, huoni aibu hata kidogo! Ndugu na dada wamekabidhiwa kwako, lakini unawapeleka kuzimu. Je, si wewe ni mtu ambaye dhamiri yake imeoza? Huna aibu kabisa!” (“Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno makali ya Mungu yalifichua asili yangu ya kweli na yaliniacha na aibu. Ilikuwa ni kwa sababu ya kuinuliwa kwa Mungu na ukarimu Wake ndiyo ningeweza kutimiza wajibu huo, Mungu alikuwa ameniaminia kuwaleta ndugu zangu Kwake. Lakini sikuingia katika uhalisi, sikutenda ukweli, na kwa ajili ya sifa na hadhi nilipuuza maslahi ya familia ya Mungu. Nilipigana na kaka yangu kwa wazi na kisiri, nikifanya kazi pekee yangu. Sasa ni wakati wa kueneza injili, na Mungu anatumai kwamba wale wanaoitafuta kweli watarudi kwa familia ya Mungu hivi punde. Lakini nilikwepa majukumu yangu na sikumpenda Mungu, sikuzingatia tamanio Lake lenye ari kabisa na kuwaleta wale waliotafuta njia ya kweli kwa Mungu. Nilitafuta sifa na hadhi, vitu vile visivyo na thamani, ili kudhibitisha nilikuwa na uwezo, badala ya kuwasaidia wengine. Sikuwasiliana kuhusu shida katika kazi yetu, nikitumai kaka yangu angekuwa nyuma yangu. Nilionea wivu vipengele vya kazi ambapo ndugu yangu alikuwa na uwezo zaidi, au hata nilivipuuza, na nilichukulia kazi kama mchezo ambao kwao nilijionyesha na kujigamba kujihusu na kudunisha ndugu yangu. Nilikuwa mwovu mno, bila utu wowote. Mungu huchukia sana watu kama hawa, na iwapo singebadilika ningewezaje kumtumikia Yeye? Iwapo singeingia katika uhalisi ningewaletaje ndugu zangu kwa Mungu? Nikilia, nilikuja kwa Mungu na kuomba: “Ee Mungu! Nilikuwa nimekosea, yote ilikuwa uasi wangu. Nilishindwa kuzingatia matamanio Yako, na ili kuthibitisha nilikuwa na uwezo nilipigana dhidi ya ndugu yangu, ili kumshinda nilipuuza dhamiri yangu na sikutimiza majukumu yangu. Na sasa kazi ya injili imedhuriliwa na nimetenda dhambi mbele yako. Lakini ningependa kutubu na kubadilika, kufanya kazi kwa njia ya upatanifu na kaka yangu na kufanya kazi ya injili iwe ya utendaji zaidi. Nikiazimia kupata hadhi tena, niadhibu, Mungu. Niko tayari kutazamwa na Wewe, Amina!” Baada ya kuomba nilipanda basi kumwona kaka yangu na kuwasiliana naye wazi, nikikubali jinsi nilikuwa nimetenda kwa uasi mbele ya Mungu na jinsi nilipanga kuwa bora zaidi. Tuliwasiliana juu ya ufahamu wetu wa sisi wenyewe. Baadaye tulifanya kazi pamoja na Mungu kama nafsi moja na kuanza kuboresha palipokuwa na dosari katika kazi yetu, tukitafuta mambo ambayo tulipita na makosa, tukijumlisha uzoefu wenye mafanikio niliokuwa nimepata, na kutenda kwa ukali kulingana na mipango ya kazi. Kazi yetu ya injili punde ilikuwa nzuri zaidi. Kutoka kwa hili niliona tabia ya Mungu ya haki. Utakatifu wa Mungu hauruhusu kuwepo na uchafu wala upotovu ndani yangu, na wakati nilidanganywa na Shetani na singeweza kujiokoa, ni Mungu ndiye alinyosha mkono wa wokovu na kunivuta kutoka ukingoni mwa kifo, Akiniokoa kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuniruhusu kubadilika. Niko tayari kutafuta ukweli na kutokuwa mwasi tena, kuwa mwaminifu kikamilifu katika yote ambayo Mungu huniaminia.

Niliona kwamba neno la Mungu linasema: “Mara chache sana wakati mnafanya kazi pamoja hakuna yeyote kati yenu atasema, Ningependa kukusikia ukishiriki na mimi kuhusu kipengele hiki cha ukweli, kwa sababu bado nina tashwishi kukihusu. Au kusema: una uzoefu zaidi kuliko mimi juu ya jambo hili; unaweza kunipa mwelekeo fulani, tafadhali? Je, si hii ingekuwa njia nzuri ya kufanya hivyo? Nyinyi mlio kwenye viwango vya juu husikia ukweli mwingi, na kuelewa mengi kuhusu huduma. Ikiwa ninyi watu ambao mnaratibu kufanya kazi katika makanisa hamjifunzi kutoka kwa kila mmoja, na kuwasiliana, kufidia mapungufu ya kila mmoja, mnaweza kujifunza masomo kutoka wapi? Mnapokutana na chochote, mnapaswa kushirikiana na kila mmoja, ili maisha yenu yaweze kufaidika. Na mnapaswa kushirikiana kwa makini kuhusu mambo ya aina yoyote kabla ya kufanya maamuzi. Ni kwa kufanya hivyo tu ndio mnakuwa na jukumu kwa kanisa na si kuwa wazembe. Baada ya kutembelea makanisa yote, mnapaswa kukutana na kushiriki juu ya masuala yote mnayotambua na matatizo mnayokabiliwa nayo kazini, na kuwasiliana kuhusu nuru na mwanga ambao mmepokea—huu ni utaratibu wa lazima wa huduma. Lazima mfikie ushirikiano wa upatanifu kwa kusudi la kazi ya Mungu, kwa manufaa ya kanisa, na kwa kuwachochea ndugu na dada kuendelea. Unashirikiana pamoja naye na anashirikiana na wewe, kila mmoja akimbadilisha mwingine, mkifikia matokeo bora ya kazi, ili kutunza mapenzi ya Mungu. Huu tu ndio ushirikiano wa kweli, na watu kama hao tu ndio wana kuingia kwa kweli” (“Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya” katika Neno Laonekana katika Mwili). Katika maneno ya Mungu niliona njia ya kutenda kuingia na nilijua jinsi ya kutumikia pamoja na wengine. Nilielewa matamanio ya Mungu: Kila mtu ana uwezo wake, na Mungu hutaka kila mtu kutumia uwezo huo katika kazi ya familia ya Mungu, na kwa kufanya hivyo upungufu wa kila mtu utafidiwa. Kufanya kazi na ndugu huyo kulikuwa tu nilichohitaji. Nilikuwa na upungufu katika kuwasilisha ukweli, na kwa sababu ya upendo wa Mungu niliwekwa nishiriki naye, hivyo uwezo wake ungeweza kufidia udhaifu wangu. Lakini sikuona hili, na wakati nilikuwa na kaka yangu nilishindwa kuuliza usaidizi wake wakati sikuelewa. Wakati mwingine alipowasiliana nami sikuwa tayari kusikiza. Nilikumbakumba naye ili kupata nafasi nzuri, nikiyadhuru maisha yangu mwenyewe na pia kudhuru kazi ya injili. Katika siku zilizofuata nilitenda kuingia katika kipengele hiki cha ukweli, nikitaka ushauri kutoka kwa kaka yangu kuhusu mambo ambayo sikuelewa au singeweza kuona kwa dhahiri: Ningependa uwasiliane nami juu ya kipengele hiki cha ukweli, kwani sikifahamu vizuri. Pia nilitaka ushauri wake juu ya ugumu katika kazi yangu: Sielewi hili vizuri, unaweza kunishauri? Kutoka hapo kuendelea, tulijifunza kutoka kwa kila mmoja wetu na kufidiana tulipoenda makanisani, na wakati tulikabiliana na shida tuliwasiliana sisi kwa sisi, pamoja tukitafuta maneno ya Mungu ili kutatua shida za makanisa. Tukawa wenza kiroho, tukikubali kila mmoja wetu, kutunzana, kuelewa kila mmoja wetu. Wakati mwingine maoni yetu yangetofautiana, lakini mradi yalifaidi maisha ya ndugu zetu na kazi ya familia ya Mungu, tungeweza kukubaliana. Hata kama tulipata aibu kidogo tungeweza kuweka matamanio yetu kando. Tulifanya kazi pamoja kwa furaha, na kila kipengele cha kazi yetu kiliendelea.

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunibadilisha kupitia hukumu Yake na kuadibu Kwake, kwa kunifanya nione sumu na madhara ya Shetani. Sasa natafuta kile kinachofaa, na kuishi kwa kudhihirisha kama mwanadamu. Ingawa bado nina upotovu mwingi ambao lazima utakaswe na lazima upitie hukumu na kuadibu zaidi, nimeona hukumu na adabu ya Mungu ndiyo wokovu bora zaidi wa mwanadamu, upendo wa ukweli zaidi wa Mungu kwa mwanadamu. Nataka kupitia hili zaidi, nataka hukumu na adabu ya Mungu yafuatane nami ninapoendelea, hadi mwishowe niwe wa kufaa kuwa mtumishi wa Mungu.

Chanzo: Hatimaye Naishi kwa Kudhihirisha Kiasi Kama Mwanadamu

Views: 113 | Added by: hatat1946 | Tags: ushuhuda, Upendo-wa-Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar