7:48 PM
Asili ya Binadamu Haiwezi Kupimwa kwa Sura

Yang Rui Mji wa Yuci , Mkoa wa Shanxi

Siku moja, nilisikia kwa ghafla kuwa baba yangu alifukuzwa kutoka kwa kanisa. Nilishangaa kabisa wakati huo na sikuweza kuelewa. Katika moyo wangu, baba yangu alikuwa ndiye mtu mkuu mno duniani. Ingawa ana hasira mbaya, alitutunza sana sisi ndugu wa kike na kamwe hakutupiga au kutukemea. Licha ya harakati za familia yetu, hangeturuhusu tuone hasira bila kujali ni shida kiasi gani angepaswa kustahimili. Baada familia yetu yote kuikubali kazi ya Mungu, baba yangu alikuwa aidha amilifu katika kutekeleza wajibu wake, na mara nyingi alitutia moyo kutimiza wajibu wetu vizuri. Ingawa baba yangu alikuwa mkali kidogo wakati mwingine, mara tu palipokuwa na wajibu wa kutimiza, bila kujali upepo na mvua au kiwango cha ugumu, angetafuta njia ya kulikamilisha hilo. Mtu mwema kama huyo angewezaje kufukuzwa? Ikiwa hawezi kupokea wokovu, basi ni nani anayeweza? Hali hiyo iliujaza moyo wangu hasira na mgongano, kwa sababu nilihisi kanisa halikumtendea baba yangu haki. Ingawa sikulisema, niliona vigumu kuutuliza moyo wangu na niliumia vibaya katika mateso.

Siku chache zilizopita, niliona yafuatayo miongoni mwa maneno ya Mungu: “Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kumfanyia tendo mbaya, lakini katika uhusiano wako na Kristo, huwezi … au kutii neno la Kristo; basi Ninasema kwamba wewe ni mdanganyifu mkubwa na mtenda dhambi katika dunia. Kama wewe ni hasa mtu mwema na mwaminifu kwa jamaa yako, marafiki, mke (au mume), wanao, na wazazi, na kamwe hujanyanyasa wengine, lakini huwezi kulingana na kuwa na amani na Kristo, basi hata iwapo utatuma vitu vyako vyote kama misaada kwa jirani zako au umemlinda vizuri baba yako, mama, na kaya, bado Nasema kwamba wewe ni mwovu, na mwenye hila pia. Usifikiri kwamba wewe unalingana na Kristo ikiwa unalingana na mwanadamu au unafanya baadhi ya matendo mema. … Je, unafikiri kwamba matendo mema yanaweza kubadilishwa na utii wako?” (“Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kutafakari juu ya maneno ya Mungu, hatua kwa hatua nilielewa: Kuona kama mtu ni mwenye haki au mwovu, angalia siyo kama tabia yake ya nje ni nzuri au mbaya au jinsi uhusiano wao na watu wengine ulivyo. Badala yake, angalia uhusiano wake na Mungu, na kama ana utii wa kweli kwa Mungu na kumcha. Bila kujali uhusiano mzuri unaofanywa kati ya watu wawili, yeye ni mwovu kama hawezi kulingana na Kristo na hawezi kuyatii maneno Yake. Katika dhehebu lake la zamani, baba yangu alikuwa kiongozi. Baada ya kuikubali hatua hii ya kazi ya Mungu, ndugu wa kiume na wa kike wa kanisa hawakumchagua kuwa kiongozi kwa sababu asili yake ilikuwa ya kiburi mno. Wakati ule alipoonekana akitii juu juu na kufanya chochote alichoambiwa, nia yake ya siri ilikuwa kuwa na uwezo wa kukalia "enzi" ya kiongozi mara nyingine. Baadaye, wakati nia yake haikufanikishwa, alibainisha tabia yake halisi, daima akionyesha majivuno zaidi katika kanisa, kamwe kutomsikiliza mtu yeyote, na daima akiwalazimisha watu kumsikiliza bila kujali chochote. Kama aliona mfanyakazi ambaye hakumpenda, angempima, amdunishe, na kumdhoofisha. ... Je, si hii ni tabia ya waovu? Kama alikuwa kweli amekuwa kiongozi, si hilo lingekuwa kuharibu kanisa na kuwadhuru ndugu wa kiume na wa kike? Sikujua asili ya baba yangu na kiini, na nilikuwa daima nimechanganyikiwa na maneno na matendo yake kwa nje na kupofushwa na upendo wake wa baba. Nilikuwa hafifu sana katika kuwapima watu. Kama tu Mungu alivyosema: “Kiwango ambacho mwanadamu anamhukumu mwanadamu kinatokana na tabia zake; aliye na mwenendo mzuri ni mtu mwenye haki, na aliye na mwenendo wa kuchukiza ni mwovu. Kiwango ambacho Mungu anamhukumu mwanadamu kinatokana na iwapo asili ya mtu inamtii Yeye; anayemtii Mungu ni mtu mwenye haki, na asiyemtii Mungu ni adui na mtu mwovu, bila kujali iwapo tabia ya mtu huyu ni nzuri ama mbaya, na bila kujali iwapo hotuba ya mtu huyu ni sahihi ama si sahihi” (“Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kwa mujibu wa maneno ya Mungu, tabia ya baba yangu haikuwa kutii mpango wa Mungu na utaratibu, pamoja na kusababisha vurugu. Kiini kama hicho ndicho ambacho humpinga Mungu. Lakini nilitumia mwenendo wake kwa nje, kama vile kunitunza na kunijali, kuweza kutimiza wajibu wake, kuamua kuwa yeye ni mtu mwema, kufikiri kwamba kanisa halikustahili kumfukuza. Hata hivyo, matendo yake mema ya nje hayana usawa na kumtii Mungu, na pia hayawezi kuitwa yenye haki. Ni wale tu wanaoutii mpango wa Mungu kwa kweli na kukubali kwa hiari kukubali kuadibiwa na hukumu ya Mungu, na kutafuta mabadiliko ya kitabia, wanaoweza kupokea wokovu. Baba yangu atajilaumu mwenyewe tu kwa kuanguka katika hali ambayo yupo leo. Ilisababishwa na yeye kutotafuta ukweli, na hana mtu mwingine wa kulaumu. Aidha, hili lilikuwa dhihirisho la tabia ya Mungu ya haki.

Ee Mungu! Asante kwa kutumia mazingira haya na kunipa kipengele hiki cha ukweli ili kupindua kabisa maoni yangu mabaya, na kwa ajili ya kufanya nione utakatifu Wako na kwamba tabia Yako ya haki na ya uadhama ni lazima isikosewe na mtu yeyote. Hili limenifanya nielewe kwamba siwezi kutofautisha au kung'amua mambo bila ukweli. Kuanzia sasa na kwendelea, bila kujali ni nini kinachonitokea, sitampima mtu tena kulingana na sura yake ya nje. Ni sharti nichukue mtazamo wa ukweli na kukubali kila kitu Unachokifanya. Hata kama siwezi kung'amua Unayoyafanya, nitaamini kuwa yote Unayoyafanya ni sawa. Sitachambua na kuchunguza tena kutoka kwa mtazamo wa mtu. Nitasimama upande wa ukweli, mara kwa mara nikijitahadharisha kuwa shahidi kwa ajili Yako.

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Views: 127 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: ukweli, Maneno ya Mungu, Kanisa | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar