9:52 PM
maisha ya ushindi | Niko Tayari Kukubali Usimamizi wa Wote

Xianshang Mji wa Jinzhong, Mkoa wa Shanxi

Muda mfupi uliopita, kila wakati niliposikia kwamba viongozi wa ngazi za juu zaidi walikuwa wakija kwa kanisa letu, ningehisi kutaharaki kiasi. Sikufichua hisia zangu kwa nje, lakini moyo wangu ulijaa upinzani wa siri. Nilidhani: “Ingekuwa bora kama nyinyi nyote hamkuja. Mkija, angalau msinyunyizie kanisa na mimi. Vinginevyo, nitakuwa nimewekewa mipaka na kutoweza kuwasiliana kwa karibu.” Baadaye, hali hiyo ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba kwa kweli nilichukia kuja kwao. Hata hivyo, sikufikiri kwamba kulikuwa na kitu kibaya nami na bila shaka sikujaribu kujijua katika mazingira ya hali hii.

Siku moja, nilisoma kifungu kifuatacho katika mpangilio wa kazi “Kanuni juu ya Wajibu wa Viongozi na wafanyikazi wa Kanisa wa Ngazi Zote”: “Lazima watembelee kila kundi la eneo linalotoa maamuzi na kuelewa vizuri kazi zao, watatue makosa na mikengeuko ya kazi yanayotokea kwa kila kundi la eneo linalotoa maamuzi kwa wakati wa kufaa, na hasa kutoa mwelekeo na msaada kwa yale makundi dhaifu kidogo ya kutoa maamuzi ya eneo ili yaweze kufanya kazi zao bora zaidi katika maeneo yao” (Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu). Nilitafakari maana ya kifungu hiki huku nikiwaza hali yangu ya karibuni: Kwa nini nilichukia sana viongozi wa ngazi za juu zaidi kuja kwa kanisa letu? Kwa nini sikuwa tayari kuwaacha wanyunyizie kanisa pamoja nami? Je, haikuwa kwa sababu nilikuwa na wasiwasi kwamba kama wangekuja kanisani, wangetambua kwamba sikuwa nikifanya kazi kulingana na kanuni au mapenzi ya Mungu na wangenishughulikia kuhusu suala hili? Aidha, je, sikuwa na hofu kwamba kuja kwao kungezuia mafanikio ya mipango yangu ya kazi? Je, sikuwa na hofu kwamba wangewasiliana kwa karibu vyema kuniliko na kunisababisha kupoteza hadhi yangu ya heshima katika mioyo ya ndugu zangu wa kiume na wa kike? Kama hawangekuja, ningeendelea na mipango yangu ya kazi kama nilivyotaka. Hata kama mbinu zangu hazikulingana na ukweli wala mapenzi ya Mungu, hakuna yeyote ambaye angejua na hakika hakuna yeyote ambaye angenishughulikia au kunikosoa. Kwa njia hii, hadhi yangu katika mioyo ya ndugu zangu wa kiume na kike ingekuwa tu kubwa zaidi na thabiti zaidi. Ndugu wote wa kiume na wa kike wa kanisa wangeniheshimu sana, kunipenda na kutii amri zangu. Ningekuwa muhimu sana katika kanisa lote. Je, hilo halikuwa kusudi langu la kweli? Je, sikuwa nikipanga njama kumfukuza Mungu kutoka mioyoni mwa ndugu zangu wa kiume na wa kike ili niweze kupata hadhi katika mioyo yao? Je, sikuwa mfano halisi wa hizo sumu za joka kubwa jekundu. “Mfalme mkuu yuko mbali sana kama mbingu,” “Hakuna mfalme ila mimi”? Baadaye, nilisoma neno la Mungu: “Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. … Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii … Anatamani kumfutilia mbali Mungu mara moja, na kumtukana na kumwangamiza, na kujaribu kuchana na kuvuruga kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu ‘akiingilia’ kazi yake miongoni mwa wanadamu wa duniani? Anawezaje kumruhusu Mungu kufichua uso wake wa chuki? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu anayevimba kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kutawala nguvu yake duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake? … Mapepo na roho wa Shetani … wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha!” (“Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ili kudhibiti na kudai mamlaka juu ya wanadamu, joka kubwa jekundu lilipigana na ujio wa Mungu kwa nguvu zote, bila kumruhusu Mungu kuhusika katika masuala ya wanadamu, ili kufichua uso wake katili, kuharibu mipango yake au kutawala katika utawala wake. Kwa hiyo, lilipinga ovyo ovyo, kuvuruga, kuharibu na kuangamiza kazi ya Mungu. Liliota ya kwamba, siku moja, lingeweza kumpokonya Mungu kutoka mioyoni mwa wanadamu na kutimiza lengo lake lenye kustahili dharau la kuwa mpatanishi wa milele wa mwanadamu na kuwalazimisha wanadamu kumwabudu. Kulikuwa na tofauti gani kati ya mawazo yangu mwenyewe na matendo ya joka kubwa jekundu? Kwa sababu nilitaka kudumisha hadhi yangu mwenyewe na kuhakikisha kuwa niliweza kwenda njia yangu mwenyewe na nisizuiliwe katika kazi yangu, sikutaka kuwaruhusu viongozi wengine au wafanya kazi kuisimamia au kuikagua kazi yangu. Sikutaka mtu mwingine yeyote aingilie kazi ya kanisa langu au kuwanyunyizia ndugu zangu wa kiume na wa kike. Kwa nini sikutaka hili? Si ni kwa sababu tu nilitaka kudhibiti na kudai mamlaka juu ya wengine? Si azma yangu ilikuwa ni kujitangaza mfalme na mtawala wa kidunia juu ya ndugu zangu wa kiume na wa kike? Niliona kwamba sumu ya joka kubwa jekundu—kile kiburi kisichozuiliwa na cha kupenda makuu—ilikuwa tayari imepenya kwa kiini cha uhai wangu. Kwa juujuu, nilikuwa ninafanya kazi ili kutimiza wajibu wangu, lakini moyo wangu ulishikilia nia zilizofichika. Kwa kweli, nilitaka kuunda ufalme wangu mwenyewe katika upinzani kwa Mungu na katika kuzuia utekelezaji wa mapenzi ya Mungu. Asili yangu ilikuwa ya kutisha sana! Kama sio kwa ajili ya ufunuo na hukumu kali ya neno la Mungu, singeweza kamwe kujua ni kwa kiwango gani nilikuwa nimepotoshwa na Shetani na nilivyompinga Mungu. Singeweza kamwe kutambua kwamba, ndani kabisa ya nafsi yangu, njama ya kishetani ilikuwa imebuniwa na kwamba asili yangu na kiini changu yalikuwa yamepotoshwa sana.

Asante Mungu kwa ufunuo Wako na kunipa nuru, ambazo zimenikubali kutambua asili yangu ya kishetani. Ninaahidi kutafuta ukweli kwa bidii na kuja kwa ufahamu wa kina wa jinsi sumu ya joka kubwa jekundu huiumiza asili yangu. Ninaapa, zaidi ya hayo, kukubali ukaguzi na usimamizi wa wafanyakazi wengine na viongozi. Nitakubali kushughulikiwa na kupogolewa kwa wote. Nitajiweka chini ya ukaguzi wa mkusanyiko wote wa waumini ili nipate kutekeleza majukumu yangu kwa uangalifu sana ili kuufariji moyo Wako.

Chanzo: maisha ya ushindi | Niko Tayari Kukubali Usimamizi wa Wote

 

Views: 100 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Hukumu ya Mungu, maisha ya kanisa, mapenzi ya Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar