5:38 PM
Matamshi ya Kristo | Sura ya 47

Mwenyezi Mungu mwenye haki—Mwenyezi! Ndani Yako hakuna chochote kabisa kilichofichwa. Kila fumbo tangu zamani hadi milele, ambalo binadamu hawajawahi kufichua, ndani Yako linadhihirika na kwa jumla kuwa wazi. Hatuhitaji tena kutafuta na kupapasa, kwa maana leo nafsi Yako inadhihirika wazi kwetu, Wewe ndilo fumbo ambalo limefichuliwa, na Wewe ni Mungu aliye hai Mwenyewe, na kwa leo Umekuja uso kwa uso na sisi, na kwa sisi kuona nafsi Yako ni kuona kila fumbo la ulimwengu wa kiroho. Kweli hiki ni kitu ambacho hakuna mtu angeweza kuwaza! Wewe uko miongoni mwetu leo, hata ndani yetu, kwa kweli karibu sana kwa sisi kuelezea; fumbo ndani ya hili ni lisilo na mwisho!

Mwenyezi Mungu amekamilisha mpango Wake wa usimamizi. Yeye ndiye Mfalme mshindi wa ulimwengu. Vitu vyote na mambo yote yanadhibitiwa na mikono Yake. Watu wote wanapiga magoti katika ibada, wakiliita jina la Mungu wa kweli—Mwenyezi. Mambo yote, kwa maneno kutoka katika kinywa Chake, yanafanyika. Kwa nini ninyi ni wazembe sana, msiweze kujielekeza kwa bidii kufanya kazi pamoja na Yeye, kujiunga kwa karibu na Yeye, na kwenda na Yeye katika utukufu? Inawezekana kuwa mko tayari kuteseka? Mko tayari kutupwa nje? Ninyi mnadhani kwamba Sijui ni nani anayejitolea kwa dhati Kwangu, na ni nani ambaye amejitumia kwa dhati kwa ajili Yangu? Wajinga! Wapumbavu! Hamwezi kufahamu nia Zangu, sembuse kuweza kuonyesha huruma kwa mizigo Yangu, daima kunifanya Niwe na wasiwasi kuwahusu, kufanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu. Je, hili litaisha lini?

Kuishi kwa kunidhihirisha katika kila kitu, kunishuhudia katika kila kitu—je, inamaanisha tu kuunga mkono kwa maneno matupu? Hamjui kilicho kizuri kwenu! Mambo mnayofanya mnayafanya bila Mimi, sembuse Mimi kuwa katika maisha yenu ya kila siku. Najua ninyi hamchulii kumwamini Mungu kwa uzito hata kidogo, na hivyo haya ndiyo matunda mnayozaa. Bado hamko macho, na mkiendelea kwa njia hii, mtaliaibisha jina Langu.

Jiulize, unapozungumza, je, Niko pale na wewe? Unapokula au kuvaa nguo zako, je, ahadi Yangu imo humo ndani yake? Ninyi kweli ni wasiojali! Wakati kuna hoja ya kuwasilisha, isipoelekezwa moja kwa moja kwako, unaonyesha jinsi ulivyo kweli, na hakuna yeyote kati yenu anayeshawishika. Isingekuwa namna hii, ninyi mngejiona kuwa wakuu, na kwamba mnamiliki vitu vingi ndani yenu. Je, hamjui kuwa mmejazwa na uovu wa Shetani ndani? Fanyeni kazi na Mimi ili kumwaga vitu hivi vyote nje. Acha kile Nilicho na kile Nilicho nacho kikae ndani yako kabisa, hiyo unaweza kuishi kwa kunidhihirisha Mimi, unishuhudie kwa uhalisi zaidi, muwafanye watu zaidi watii mbele ya kiti Changu cha enzi kwa sababu yenu. Lazima mjue mzigo ulio mabegani mwenu ni mzito kiasi gani: kumtukuza Kristo, kumdhihirisha Kristo, kumshuhudia Kristo, ili watu wengi wapate wokovu na ufalme Wangu ubaki imara na usiotikisika. Ninazungumzia haya yote ili msije mkaboronga tu, bila kuelewa umuhimu wa kazi ya leo.

Kutojiweza mnapokabiliwa na mambo, kama siafu kwenye kikaango kimoto—wakizunguka huku na kule: hii ndiyo tabia yenu. Kwa nje mnaonekana kama watu wazima, lakini maisha yenu ya ndani ni yale ya mtoto, kuweza tu kusababisha shida, kuongezea mzigo Wangu. Ikiwa kuna kitu kidogo zaidi ambacho Sijishughulishi nacho, ninyi husababisha shida, sivyo? Msiwe wenye kujidai. Ninachosema ni ukweli. Msifikirie daima kwamba daima Ninawakaripia bila kukoma, kana kwamba Ninatumia maneno makali. Hali yenu ya kweli iko hivyo.

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Views: 80 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: utukufu wa Mungu, ufalme wa Mungu, neno la Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar