Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kujua kile ambacho ni huduma kuu ya Mungu katika mwili katika siku za mwisho, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (katika siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima. Hii ni kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho; Anazungumza tu ili dunia iwe ulimwengu wa maneno, ili kila mtu awe amepewa na kutiwa nuru maneno Yake, na ili roho ya mwanadamu iamshwe na aweze kuona vizuri kuhusu maono yake. Wakati wa siku za mwisho, Mungu katika mwili Amekuja duniani hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno. ... Read more »

Views: 116 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 07.26.2019 | Comments (0)