11:22 AM
Kazi na Kuingia (7)

Imemchukua mwanadamu mpaka siku hii kutambua kwamba kile mtu anachokosa si tu kuruzukiwa maisha ya kiroho na uzoefu wa kumjua Mungu, lakini, muhimu zaidi, mabadiliko katika tabia yake. Kutokana na ujinga kamili wa mwanadamu wa historia na utamaduni wa kale wa wanadamu, hana ujuzi wa kazi ya Mungu hata kidogo. Mwanadamu hutumaini kuwa ndani kabisa ya moyo, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu sana, lakini kwa sababu ya upotovu mkubwa mno wa mwili wa mwanadamu, pamoja na kutojali na upumbavu, mwanadamu ameshushwa kuwa asiye na ufahamu wa Mungu hata kidogo. Mungu Anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa maelfu ya miaka. Kupitia fursa hii, Atamfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Yaani, kupitia maarifa ya mwanadamu, Atabadilisha namna wanavyomfahamu na mitazamo yao Kwake, ili kwamba maarifa yao juu ya Mungu, yaweze kuanza katika rekodi safi, na mioyo yao itakuwa imesafishwa upya na kubadilishwa. Kushughulika na nidhamu ni njia, na ushindi na kufanya upya ni malengo. Kuondoa mawazo ya kishirikina aliyonayo mwanadamu kuhusu Mungu asiye dhahiri ndilo limekuwa kusudi la Mungu milele, na hivi karibuni limekuwa suala la haraka kwake. Ni matumaini Yangu kwamba watu wote watalifikiria hili zaidi. Wabadilishe jinsi kila mtu anavyopitia uzoefu ili kwamba kusudi hili la haraka la Mungu liweze kufanyika hivi karibuni na hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu duniani iweze kuhitimishwa kwa matokeo mazuri. Onyesheni uaminifu wenu kama mnavyopaswa, na ufariji moyo wa Mungu kwa mara ya mwisho. Ni matumaini Yangu kwamba hakuna mtu yeyote miongoni mwa kaka na dada atakayekwepa jukumu hili au kuzungukazunguka tu. Mungu Anakuja katika mwili wakati huu kwa mwaliko, na kutokana na hali ya mwanadamu. Yaani, Anakuja kumpatia mwanadamu kile alichokuwa anahitaji. Atakuja kumwezesha kila mwanadamu, wa tabia yoyote au jamii, kuona neno la Mungu na, kutoka katika neno Lake, kuona uwepo na udhihirishaji wa Mungu na kukubali ukamilishaji wa Mungu. Neno lake litabadilisha mawazo na mitazamo ya mwanadamu ili kwamba sura ya kweli ya Mungu ikite mizizi kabisa katika moyo wa mwanadamu. Hili ndilo tamanio pekee la Mungu duniani. Haijalishi jinsi gani asili ya mwanadamu ilivyo, jinsi gani asili yake ilivyo duni, au matendo yake yalivyokuwa huko nyuma, Mungu Hajali haya. Anatumainia tu mwanadamu kuisafisha kabisa taswira ya Mungu aliyonayo moyoni mwake na kuijua asili ya binadamu, na hapo Atakuwa Amebadilisha mtazamo wa kiitikadi wa mwanadamu. Anatarajia mwanadamu kuwa na shauku ya kina kwa Mungu na kuwa na mahusiano ya milele na Yeye. Hiki ndicho Mungu Anachomwomba mwanadamu.

Maarifa ya maelfu kadhaa ya miaka ya utamaduni wa kale na historia vimefunga fikra na dhana na akili ya mwanadamu kwa nguvu sana kiasi cha kutoweza kupenyeka na kutoweza kubadilishwa.[1] Mwanadamu anaishi katika ngazi ya kumi na nane ya kuzimu, kana kwamba wamefukuziwa chini na Mungu, wasiweze kuona mwanga tena. Fikra za kishirikina zimemkandamiza mwanadamu kiasi kwamba mwanadamu anaweza kupumua kwa shida sana na hivyo kufa kwa kukosa hewa. Hawana nguvu hata kidogo ya kupinga, kimya kimya wanaendelea kuvumilia na kuvumilia... Hakuna hata mmoja aliyewahi kujaribu kupigana au kusimama kwa ajili ya uadilifu na haki; wanaishi maisha ambayo hayana tofauti na maisha ya mnyama, huku wakinyanyaswa na kushambuliwa na mabwana wa ushirikina, mwaka baada ya mwaka, siku baada ya siku. Mwanadamu hajawahi kufikiria kumtafuta Mungu ili kufurahia furaha duniani. Ni kana kwamba mwanadamu amepigwa, kama majani yaliyoanguka ya majira ya kupukutika, yaliyonyauka na kukauka kabisa. Mwanadamu amepoteza kumbukumbu na anaishi bila matumaini kuzimu kwa jina la ulimwengu wa kibinadamu, akisubiri ujio wa siku ya mwisho ili kwamba waweze kupotea pamoja na kuzimu, kana kwamba siku ya mwisho wanayoitamani sana ni siku watakayofurahia pumziko la amani. Maadili ya kishirikina yamempeleka mwanadamu “Kuzimu,” kiasi kwamba mwanadamu anakuwa na uwezo mdogo wa kupinga. Ukandamizaji wa aina mbalimbali umemlazimisha mwanadamu taratibu kuzama chini kabisa Kuzimu na kutanga mbali kabisa na Mungu. Sasa, Mungu Amekuwa mgeni kabisa kwa mwanadamu, na mwanadamu bado anafanya haraka kumwepuka wanapokutana. Mwanadamu hamtilii maanani na anamtenga kana kwamba mwanadamu hajawahi kumwona hapo kabla. Mungu amekuwa akisubiri kotekote katika safari ndefu ya maisha ya binadamu lakini hajawahi kuelekeza ghadhabu Yake isiyodhibitika kwa mwanadamu. Amekuwa Akisubiri tu kimya kwa mwanadamu kutubu na kuanza upya. Mungu zamani alikuja kwenye ulimwengu wa binadamu na Huvumilia mateso hayo hayo kama mwanadamu. Ameishi na mwanadamu kwa miaka mingi na hakuna aliyegundua kuwepo Kwake. Mungu amekuwa Akivumilia kimya taabu za ulimwengu wa binadamu huku Akifanya kazi Aliyoleta pamoja Naye. Kwa kuwa mapenzi ya Mungu Baba na mahitaji ya wanadamu, Amevumilia, Akipitia maumivu ambayo kamwe mwanadamu hajawahi kupitia. Mbele ya mwanadamu, Amewahudumia kimya kimya na kujinyenyekeza Mwenyewe, kwa ajili ya mapenzi ya Mungu Baba na mahitaji ya wanadamu. Maarifa ya utamaduni wa kale kwa taratibu yamemwondoa mwanadamu kutoka katika uwepo wa Mungu na kumweka mwanadamu kwa mfalme wa mashetani na wana wake. Vitabu Vinne na Maandiko ya Kale ya Kiyunani Matano vimepeleka fikra na mawazo ya mwanadamu katika enzi nyingine ya uasi, na kumfanya mwanadamu kuendelea kuwaabudu wale walioandika Vitabu hivyo na Maandiko ya Kiyunani, wakikuza zaidi mitazamo yao juu ya Mungu. Mfalme wa mashetani bila huruma alimtupa Mungu nje kutoka katika moyo wa mwanadamu bila wao kujua, huku akifurahia kuuchukua moyo wa mwanadamu. Baada ya hapo na kuendelea mwanadamu akawa na roho mbaya na ya uovu akiwa na sura ya mfalme wa mashetani. Chuki juu ya Mungu ilijaza kifua chao na sumu ya mfalme wa mashetani ikasambaa ndani ya mwanadamu hadi alipomalizwa kabisa. Mwanadamu hakuwa na uhuru tena na hakuweza kuvunja vifungo vya mfalme wa mashetani. Kwa hiyo, mwanadamu angeweza kuendelea kukaa pale tu na kufungwa, kujisalimisha kwake na kujitiisha kwake. Amepanda zamani sana mbegu ya kutoamini kuwa kuna Mungu ndani ya moyo mchanga wa mwanadamu, akimfundisha mwanadamu dhana za uongo kama vile, “kujifunza sayansi na teknolojia, kutambua Vipengele Vinne vya Usasa, hakuna Mungu duniani.” Si hivyo tu, ametangaza kwa kurudiarudia, “Hebu tujenge makazi mazuri sana kwa kufanya kazi kwa bidii,” akiwaomba wote kujiandaa toka wakiwa watoto kutumikia nchi yao. Mwanadamu amepelekwa mbele yake bila kujitambua, na bila kusita akajichukulia sifa (akimrejelea Mungu akiwa Ameshikilia binadamu mzima katika mikono Yake). Hajawahi kuhisi aibu au kuwa na hisia yoyote ya aibu. Aidha, bila aibu amewanyakua watu wa Mungu na kuwaweka katika nyumba yake, wakati akirukaruka kama panya mezani na kumfanya mwanadamu amwabudu kama Mungu. Ni ujahili kabisa huu Anaropoka tuhuma hizo za kushtua, “Hakuna Mungu duniani. Upepo upo kwa ajili ya sheria za asili; mvua ni unyevunyevu unaoganda na kudondoka chini kama matone; tetemeko la ardhi ni mtikisiko wa uso wa ardhi kwa sababu ya mabadiliko ya jiolojia; ukame ni kwa sababu ya ukavu hewani kwa mwingiliano wa kinyuklia katika uso wa jua. Haya ni matukio ya asili. Ni sehemu gani ambayo ni tendo la Mungu?” Hata anaropoka[a] kauli kama hizi zisizo na aibu: “Mwanadamu alitokana na sokwe wa zamani, na dunia leo imeendelea kutoka katika jamii ya kale ya takribani miaka bilioni moja iliyopita. Ama nchi inaendelea au inaanguka inaamuliwa na mikono ya watu wake.” Mwanadamu amemning’iniza ukutani miguu juu kichwa chini na kumweka mezani ili kutunzwa vizuri na kuabudiwa. Anapokuwa anapiga kelele kwamba “Hakuna Mungu,” anajichukulia mwenyewe kuwa ni Mungu, na kumsukumia mbali Mungu nje ya mipaka ya dunia bila huruma. Anasimama katika sehemu ya Mungu na kutenda kama mfalme wa mashetani. Ni upuuzi mkubwa kiasi gani! Anamsababisha mtu kuteketezwa na chuki yenye sumu. Inaonekana kwamba Mungu ni adui wake mkubwa na Mungu Hapatani naye kabisa. Anafanya hila zake za kumfukuza Mungu wakati anabakia huru na hajapatikana.[2] Huyo kweli ni mfalme wa mashetani! Tunawezaje kuvumilia uwepo wake? Hatapumzika hadi awe ameisumbua kazi ya Mungu na kuiacha katika matambara na kuwa katika hali ya shaghalabaghala kabisa,[3] kana kwamba anataka kumpinga Mungu hadi mwisho, hadi mmoja kati yao awe ameangamia. Anampinga Mungu kwa makusudi na kusogea karibu zaidi. Sura yake ya kuchukiza imefunuliwa toka zamani na sasa imevilia damu na kugongwagongwa,[4] ipo katika hali mbaya sana, lakini bado hapunguzi hasira zake kwa Mungu, kana kwamba anatamani kummeza Mungu kabisa kwa mara moja ili kutuliza hasira moyoni mwake. Tunawezaje kumvumilia, huyu adui wa Mungu anayechukiwa! Ni kumalizwa kwake na kuondolewa kabisa ndiko kutaleta mwisho wa matamanio yetu ya maisha. Anawezaje kuruhusiwa kuendelea kukimbia ovyoovyo? Amemharibu mwanadamu kwa kiwango ambacho mwanadamu hajui ’mahali pa raha zote, na anakuwa mfu na hajitambui. Mwanadamu amepoteza uwezo wa kawaida wa kufikiri wa kibinadamu. Kwa nini tusijitoe sadaka uhai wetu wote kumwangamiza na kumchoma na kuondoa kabisa hofu ya hatari inayobakia na kuruhusu kazi ya Mungu kuufikia uzuri usiotarajiwa hivi karibuni? Genge hili la waovu limekuja miongoni mwa wanadamu na kusababisha hofu na shida kubwa. Wamewaleta wanadamu wote katika ukingo wa jabali, wakipanga kwa siri kuwasukumia chini wavunjike vipande vipande na kumeza maiti zao. Wana matumaini ya kuharibu mpango wa Mungu na kushindana na Mungu katika pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda.[5] Hiyo kwa vyovyote vile ni rahisi! Msalaba umeandaliwa, mahususi kwa ajili ya mfalme wa mashetani ambaye ni mwenye hatia ya makosa maovu sana. Mungu si wa msalaba tena na Amekwishamwachia Shetani. Mungu Aliibuka mshindi muda mrefu uliopita, Hahisi tena huzuni juu ya dhambi za binadamu. Ataleta wokovu kwa binadamu wote.

Kutoka juu hadi chini na kuanzia mwanzo hadi mwisho, amekuwa akisumbua kazi ya Mungu na kutenda kinyume Chake. Mazungumzo yote ya “urithi wa utamaduni wa kale,” “maarifa ya thamani ya utamaduni wa kale,” “mafundisho ya imani ya Tao na imani ya Confucius,” na “maandiko ya kale ya Confucius na ibada ya kishirikina” vimempeleka mwanadamu kuzimu. Sayansi na teknolojia ya kisasa, vilevile maendeleo ya viwanda, kilimo, na biashara havionekeni popote. Badala yake, anasisitiza ibada za kishirikina zilizoenezwa na “masokwe” wa kale kwa makusudi kabisa kuingilia, kupinga na kuharibu kazi ya Mungu. Sio tu amemtesa mwanadamu hadi leo hii, bali anataka kummaliza[6] mwanadamu kabisa. Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. Kuna wachache sana ambao wapo tayari kumpokea Mungu na kukaribisha kwa furaha ujio wa Mungu. Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii; wakiwa na visu na mapanga mikononi, wanajipanga katika pambano kumwangamiza Mungu. Sanamu zimetapakaa nchi nzima ya shetani ambapo mwanadamu anafundishwa kuwa hakuna Mungu. Juu ya nchi hii kunatoka harufu mbaya sana ya karatasi linaloungua na ubani, ni harufu nzito sana inayomaliza hewa. Inaonekana kuwa ni harufu ya uchafu unaopeperuka wakati joka anapojisogeza na kujizungusha, na ni harufu ambayo mwanadamu hawezi kuvumilia bali kutapika tu. Licha ya hiyo, kunaweza kusikika pepo waovu wakikariri maandiko. Sauti inaonekana kutoka mbali kuzimu, na mwanadamu hawezi kujizua kusikia baridi ikiteremka chini ya uti wake. Katika nchi hii sanamu zimetapakaa, zikiwa na rangi zote za upinde wa mvua, ambazo zinaibadilisha nchi kuwa ulimwengu unaometameta, na mfalme wa mashetani amekenua, kana kwamba njama zake ovu zimefanikiwa. Wakati huo mwanadamu hana habari naye, wala mwanadamu hajui kwamba shetani amekwishamharibu kwa kiwango ambacho amekuwa hawezi kuhisi na ameshindwa. Anatamani kumfutilia mbali Mungu mara moja, na kumtukana na kumwangamiza, na kujaribu kuchana na kuvuruga kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu “akiingilia” kazi miongoni mwa wanadamu? Anawezaje kumruhusu Mungu kufichua uso wake wa chuki? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu anayevimba kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kutawala nguvu yake duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake? Akiwa na roho mbaya, bado anaamini kwamba yeye ni mzuri kupita kiasi. Genge hili la washiriki jinai![7] Wanakuja miongoni mwa walio na mwili wa kufa na kuendeleza starehe na kuvuruga mpangilio. Usumbufu wao unaleta kigeugeu duniani na kusababisha hofu katika moyo wa mwanadamu, na wamemharibu mwanadamu kiasi kwamba mwanadamu anafanana na wanyama wabaya wasioweza kuvumilika, wala hana tena hata chembe ya mwanadamu asilia mtakatifu. Hata wanatamani kutawala kama madikteta duniani. Wanakwamisha kazi ya Mungu ili kwamba isiweze kusonga mbele na kumfunga mwanadamu kana kwamba wapo nyuma ya kuta za shaba na chuma cha pua. Baada ya kufanya dhambi nyingi sana na kusababisha shida nyingi sana, wanawezaje kutarajia kitu chochote tofauti na kusubiri kuadibu? Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo. Kwa makusudi wanapinga ukweli licha ya kuuelewa vizuri. Wana wa uasi! Ni kana kwamba, sasa mfalme wao amepanda kwenda katika kiti cha enzi cha kifalme, wamekuwa wa kuridhika nafsi na kuwatendea wengine wote kwa dharau. Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakuongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi na kuchomeka vichwa vyao na kuchochea vurugu.[8] Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu wa wafalme wote, bila kutambua kwamba si chochote zaidi ya nzi katika kitu kilichooza. Si hivyo tu, wanatoa maoni ya kashfa dhidi ya uwepo wa Mungu kwa kutegemea nguruwe na mbwa wa wazazi wao. Nzi wadogo wanadhani wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi mwenye meno.[9] Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, wazazi wao ni nguruwe na mbwa wachafu mara bilioni kuliko wao wenyewe? Hawatambui uduni wao, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na majivuno na kiburi juu ya uzuri wao na mvuto wao, kwa siri kabisa wanamtupia mwanadamu uchafu wao. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao, na hivyo wanautesa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea kisa cha ndani cha ulimwengu wa kidini). Mwanadamu anajua kidogo kwamba, ingawa mbawa za nzi ni nzuri za kupendeza, hata hivyo ni nzi mdogo tu aliyejaa uchafu na kujazwa na vijidudu. Kwa kutegemea uwezo wa nguruwe na mbwa wa wazazi wao, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya uungwaji mkono mkubwa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliopitiliza. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza kazi yao tena ya utesaji, wakiendeleza kazi yao yenye umri wa maelfu kadhaa ya miaka. Kikundi hiki cha waliopotoka ni hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu sana. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani imfanye Mungu kulia kwa sauti kuu, na Anajizuia sana kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize. Kwa mwanadamu kumpenda Mungu ni lazima aelewe mapenzi Yake na furaha Yake na huzuni, vilevile na kile Anachokichukia zaidi. Hii itakuza zaidi kuingia kwa mwanadamu. Kadri mwanadamu anavyoingia kwa haraka, ndivyo moyo wa Mungu unavyoridhika; kadri mwanadamu anavyomtambua kwa uwazi mfalme wa mashetani, ndivyo mwanadamu anavyosogea karibu zaidi kwa Mungu, ili kwamba matamanio yake yaweze kutimizwa.

Tanbihi:

1. “Kutoweza kubadilishwa” imenuiwa kama tashtiti hapa, kumaanisha kwamba watu ni wagumu katika ufahamu, utamaduni na mitizamo yao ya kiroho.

2. “Huru na hajapatikana” inaonyesha kwamba shetani anapagawa na kucharuka.

3. “Hali ya shaghalabaghala kabisa” inahusu jinsi tabia ya shetani ya ukatili haivumiliki kuona.

4. “Imevilia damu na kugongwagongwa” inahusu sura mbaya ya kutisha ya mfalme wa pepo.

5. “Pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda” ni istiara ya mipango mibaya ya shetani yenye kudhuru kwa siri, ya uovu. Inatumiwa kwa dhihaka.

6. “Kummaliza” inahusu tabia ya kidhalimu ya mfalme wa pepo, ambaye huwaangamiza watu wote.

7. “Washiriki jinai” ni wa namna moja na “kundi la majambazi.”

8. “Kuchochea vurugu” inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

9. “Nyangumi mwenye meno” imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

a. Maandishi ya asili yanasoma “Baadhi hata hupiga kelele.”

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Views: 73 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Matamshi ya Kristo | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar