7:31 PM
Maneno ya Roho Mtakatifu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" (Dondoo 1)

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" (Dondoo 1)

Mwenyezi Mungu anasema, “Usiku uingiapo polepole, mwanadamu huwa hafahamu, kwani moyo wa mwanadamu hauwezi kujua jinsi giza linapokaribia au wapi linakotoka. Usiku unapotoweka polepole, mwanadamu hukaribisha mwanga wa mchana, lakini ikija kwa kulikotoka nuru na jinsi imeliondoa giza la usiku, mwanadamu anajua hata machache na hata ana ufahamu mchache zaidi Mabadiliko haya ya kawaida ya mchana na usiku humpitisha mwanadamu kutoka kipindi kimoja hadi kingine, kutoka kipindi kimoja cha kihistoria hadi kingine, wakati huu wote yakihakikisha kwamba kazi ya Mungu katika kila kipindi na mpango Wake wa kila enzi unatekelezwa. Mwanadamu ametembea katika enzi hizi tofauti pamoja na Mungu, lakini bado hafahamu kwamba Mungu huongoza hatima ya mambo yote na viumbe hai au jinsi Mungu hupanga na kuelekeza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo. Kuhusu sababu, siyo kwa sababu matendo ya Mungu hayafahamiki, au kwa sababu mpango wa Mungu bado haujakamilika, lakini ni kwa sababu moyo na roho ya mwanadamu viko mbali sana na Mungu, kiasi ya kwamba, mwanadamu anabaki katika huduma ya Shetani wakati ule ule anapomfuata Mungu—na hata halitambui hili. Hakuna anayetafuta nyayo za Mungu kwa vitendo au kuonekana Anakoonyesha, na hakuna aliye na hiari ya kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani, yule mwovu, ili kurekebishwa kufuatana na dunia hii na kanuni za kuwepo ambazo watu waovu hufuata. Wakati huu, moyo na roho za mwanadamu hutolewa ushuru kwa shetani na kuwa riziki ya Shetani. Hata zaidi, moyo wa binadamu na roho yake zimekuwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na uwanja wake wa kuchezea unaofaa. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni za kuwa binadamu, na wa thamani na maana ya kuwepo kwa binadamu. Sheria za Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu, na yeye huacha kumtafuta na kumsikiza Mungu. Wakati upitavyo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu na yote yanayotoka kwa Mungu. Mwanadamu kisha huanza kupinga sheria na amri za Mungu na moyo na roho zake hufishwa…. Mungu humpoteza mwanadamu ambaye Alimuumba mwanzoni, na mwanadamu hupoteza mzizi wa mwanzo wake: Hii ndiyo huzuni ya hii jamii ya wanadamu.”

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana. 

Views: 125 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Usomaji wa Maneno ya Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar