11:19 AM
3. Watu wanafaa kupitiaje hukumu na adabu ya Mungu ili kuokolewa?

Maneno Husika ya Mungu:

Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro katika kumwamini Mungu, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi zaidi na muhimu zaidi ya utendaji. Hili ndilo alilofanya Petro baada ya kumwona Bwana Yesu, na ni kwa kutenda kwa njia hii tu ndio mtu hupata matokeo bora zaidi. Kujitolea kwa moyo wote kwa maneno ya Mungu hasa kunamaanisha kutafuta ukweli, kutafuta nia ya Mungu ndani ya maneno Yake, kuzingatia kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na kuelewa na kupata ukweli zaidi kutoka kwa maneno ya Mungu. Wakati wa kusoma maneno Yake, Petro hakuwa anazingatia kuelewa mafundisho ya dini na hata alikuwa anazingatia kwa kiasi kidogo kupata maarifa ya teolojia; badala yake, alikuwa anazingatia kuelewa ukweli na kufahamu mapenzi ya Mungu, na kutimiza ufahamu wa tabia yake na uzuri wake. Pia alijaribu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na kuelewa asili potovu ya mwanadamu na dosari halisi za mwanadamu, akitimiza kila hali yote ya madai anayotaka Mungu kutoka kwa mwanadamu ili kumridhisha Yeye. Alikuwa na utendaji mwingi sahihi ndani ya maneno ya Mungu; hili linalingana sana na mapenzi ya Mungu, na ni ushirikiano bora zaidi wa mwanadamu katika uzoefu wake wa kazi ya Mungu. Wakati ambapo alipitia mamia ya majaribio kutoka kwa Mungu, alijichunguza kabisa dhidi ya kila neno la hukumu ya Mungu kwa mwanadamu, kila neno la ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, na kila neno la madai Yake kwa mwanadamu, na akajaribu kufikia maana ya maneno ya Mungu. Alijaribu kwa bidii kutafakari na kukariri kila neno ambalo Bwana Yesu alimwambia, na alitimiza matokeo mazuri sana. Kupitia njia hii ya utendaji aliweza kutimiza kujifahamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na hakuja tu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu, lakini pia alikuja kuelewa kiini cha mwanadamu, asili ya mwanadamu, na aina mbalimbali za dosari ambazo mwanadamu anazo—huku ni kujifahamu kwa kweli. Kutoka kwa maneno ya Mungu, hakutimiza tu kujifahamu kwa kweli, lakini kutokana na mambo yaliyoonyeshwa katika neno la Mungu—tabia ya Mungu yenye haki, kile Anacho na alicho, mapenzi ya Mungu kwa kazi Yake, mahitaji Yake kwa wanadamu—kutoka kwa maneno haya alikuja kumjua Mungu kabisa. Alikuja kujua tabia ya Mungu, na asili yake; alikuja kujua na kuelewa kile Mungu anacho na Alicho, uzuri wa Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu. Hata ingawa wakati huo Mungu hakuzungumza sana kama Anavyofanya leo, matunda yalipatikana ndani ya Petro katika hali hizi. Hili lilikuwa jambo adimu na la thamani.

kutoka katika “Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za

Maongezi ya Kristo

Kama unaamini katika utawala wa Mungu, basi lazima uamini kuwa mambo ambayo hutokea kila siku, yawe mema au mabaya, si matukio ya kubahatisha. Sio kwamba mtu fulani ni mkali kwako au anakulenga kwa makusudi; yote kwa kweli husafidiwa na kupangwa na Mungu. Kwa nini Mungu hupanga mambo haya? Sio ili kuzifichua kasoro zako au kukukashifu; kukukashifu si lengo la mwisho. Lengo la mwisho ni kukukamilisha na kukuokoa. Mungu anafanyaje hilo? Kwanza, Anakufanya ufahamu tabia yako potovu, kufahamu asili na hali yako, kasoro zako, na kile unachokosa. Ni kwa kuelewa mambo haya yaliyomo katika moyo wako tu ndiyo utaweza kufuatilia ukweli na kuacha tabia yako potovu hatua kwa hatua. Huku ni Mungu kukupa fursa. Lazima ujue jinsi ya kuitumia fursa hii na usiwe mkaidi kwa Mungu. Hasa unapokabiliwa na watu, matukio, na mambo ambayo Mungu anapanga kando yako, usifikiri kila mara kwamba mambo hayako kama unavyotaka yawe, kila mara ukitaka kutoroka, kila mara ukimlaumu na kumwelewa Mungu visivyo. Huko si kuipitia kazi ya Mungu, na hiyo itafanya iwe vigumu sana kwako kuingia katika uhalisi wa ukweli. Lolote lile ambalo huwezi kulielewa kikamilifu, wakati ambapo una matatizo, lazima ujifunze kutii. Unapaswa kwanza kuja mbele ya Mungu na kuomba zaidi. Kwa njia hiyo, kabla ya wewe kujua kutakuwa na mabadiliko katika hali yako ya ndani na utaweza kutafuta ukweli ili kutatua tatizo lako utaweza kuipitia kazi ya Mungu. Katika kipindi hiki, uhalisi wa ukweli unahemshwa ndani yako, na hivi ndivyo jinsi utakavyoendelea mbele na jinsi mabadiliko katika hali ya maisha yako yatafanyika. Utakapokuwa umepitia mabadiliko haya na kuwa na aina hii ya uhalisi wa ukweli, basi utakuwa na kimo, na kimo huleta uzima. Ikiwa mtu huishi daima kulingana na tabia potovu ya Shetani, basi bila kujali ana shauku au bidii kiasi gani, bado hawezi kufikiriwa kuwa na kimo, au uzima. Mungu hufanya kazi ndani ya kila mtu, na bila kujali mbinu Yake ni ipi, utaratibu ambao kazi Yake inachukua ni upi, au maneno Yake yana sauti ya aina gani, Ana lengo moja tu la mwisho: kukuokoa. Kukuokoa kunamaanisha kukugeuza, na hivyo utakosaje kuteseka kidogo? Ni lazima upate kuteseka. Kuteseka huku kunaweza kuhusisha mambo mengi. Mungu huibua watu, mambo, na vitu ambavyo viko karibu nawe ili kukufunua, kukuwezesha kujitambua, vinginevyo Yeye hukushughulikia moja kwa moja, kukupogoa, na kukufichua. Kama vile tu mtu aliye juu ya meza ya upasuaji–lazima upitie maumivu kiasi kwa ajili ya matokeo mazuri. Kama kila wakati Mungu anapokupogoa na kukushughulikia na kila wakati Anaibua watu, mambo, na vitu, hilo huchochea hisia zako na kukuongezea nguvu, basi kupitia hayo kwa njia hii ni sahihi, na utakuwa na kimo na utaingia katika uhalisi wa ukweli.

kutoka katika “Ili Kufikia Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo,

na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na ukosefu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake wa Mungu. Je, huu si upendo mkamilifu wa Mungu? Je, hii si ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? Kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo wa Mungu. Kama mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki, basi yeye ni kiumbe wa Mungu mwenye sifa inayostahili, na hakuna kitu kinachokidhi mapenzi ya Muumba bora zaidi ya hiki.

kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo

Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ukweli ambao mtu anahitaji kumiliki unapatikana katika neno la Mungu, ukweli ambao ni faida zaidi na manufaa kwa mtu. Ni lishe na riziki ambayo miili yenu inahitaji, kitu ambacho huwasaidia kurejesha ubinadamu wenu wa kawaida, ukweli ambao mnapaswa kujiandaa nao. Zaidi mnavyotenda neno la Mungu, kwa haraka ndivyo zaidi maisha yenu yatachanua; zaidi mnavyotenda neno la Mungu, ndio wazi ukweli unakuwa. Mnavyokua katika kimo, mtaona mambo ya ulimwengu wa kiroho wazi zaidi, na mtakuwa na nguvu zaidi ya ushindi juu ya Shetani. Sehemu kubwa ya ukweli ambao hamuelewi itakuwa wazi wakati unatenda neno la Mungu. Watu wengi wameridhika na kuelewa tu maandiko ya neno la Mungu na kuzingatia katika kujiandaa wenyewe na mafundisho bila kupitia kina chake katika vitendo; si hiyo ni njia ya Mafarisayo? Jinsi gani kirai “Neno la Mungu ni uzima” kikawa ukweli kwao, basi? Wakati tu mtu anatenda neno la Mungu ndio maisha yake yanaweza kweli kuchanua; maisha hayawezi kukua tu kwa kusoma neno Lake. Kama ni imani yako ya kwamba kuelewa neno la Mungu ni kila kinachohitajika kuwa na maisha, kuwa na kimo, basi kuelewa kwako ni potovu. Kuelea kwa kweli neno la Mungu hutokea wakati unatenda ukweli, na ni lazima uelewe ya kwamba “ni kwa kutenda tu ukweli kunaweza kueleweka siku zote.”

kutoka katika “Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa” katika Neno Laonekana

katika Mwili

Ikiwa mtu anaweza kweli kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu kutokana na mambo na maneno yanayohitajika na Yeye, basi atakuwa mtu aliyekamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yanafaa kabisa kwa mtu huyu, kwamba maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake, anapata ukweli, na anaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili asili ya mwili wake, yaani, msingi wa kuwepo kwake kwa asili, utatikisika na kuanguka. Baada ya mtu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yake anakuwa mtu mpya. Maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake; maono ya kazi ya Mungu, matakwa yake kwa mwanadamu, ufunuo wake kwa mwanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anahitaji mwanadamu kutimiza vinakuwa maisha yake—anaishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, na mtu huyu anageuka kukamilishwa na maneno ya Mungu. Anapitia kuzaliwa upya na anakuwa mtu mpya kupitia maneno Yake.

kutoka katika “Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za

Maongezi ya Kristo

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Kazi ya Mungu katika siku za mwishoni kuhukumu kupitia neno Lake. Kisha ikiwa tunataka tabia yetu potovuitakaswe na kufikia wokovu, tunapaswa kwanza kutia jitihadakwa neno la Mungu na kwa kwelikula na kunywa maneno ya Mungu, na kukubali hukumu na ufunuo wa Mungukatika neno Lake. Haijalishi jinsi neno la Mungu linauguza moyo,jinsi lilivyo kali, au ni kwa kiasi gani linatufanya kuteseka, kwanza kuwa na uhakika kwambaneno la Mungu lote ni ukweli, na uhalisi wa maishaambao tunapaswa kuuingia. Maneno yote ya neno la Munguni ya kututakasa na kutubadilisha, kutufanya kuacha tabia yetu potovuna kufikia wokovu, na hata zaidi kutufanya kuelewa ukweliili kufikia maarifa ya Mungu. Kwa hiyo tunapaswa kukubali hukumuna kuadibiwa,kupogolewa na kushughulikiwakwa neno la Mungu. Ikiwa tunataka kupokea ukwelikatika neno la Mungu, lazima tuweze kuteseka kwa kukubalina kutii neno la Mungu na ukweli. Tunapaswa kutafuta ukwelikatika neno la Mungu, kuhisi mapenzi ya Mungu,na kutafakari na kujijua wenyewe, kutafakari juu ya neno la Munguili kujua kiburi, udanganyifu, ubinafsi na kudharaulika kwetu, jinsi sisi hushiriki katika shughuli na Mungu,kumtumia Mungu vibaya,kumdanganya Mungu, kuchezea ukweli,na tabia zingine za kishetani, pamoja na uchafu mbalimbalikatika imani yetu kwa Mungu na nia za kupokea baraka. Kwa njia hii, tunaweza kujua hatua kwa hatua ukweli wa upotovu wetu na kiini cha asili yetu. Baada ya kuelewa ukweli zaidi,ujuzi wetu juu ya Mungu utakua zaidi hatua kwa hatua, na sisi kwa kawaida tutajua ni aina gani ya mtu ambaye Mungu anapenda au hapendi, ni aina gani ya mtu ambaye angeweza kuokoaau kuondosha, ni aina gani ya mtu ambaye angeweza kutumia, na ni aina gani ya mtu ambaye atakayebariki. Mara tu tunapoelewa mambo haya,tutaanza kuelewa tabia ya Mungu. Haya ndiyo matokeo yote ya kupata hukumuna kuadibiwa na neno la Mungu. Wote wanaotafuta ukwelihuzingatia kupata uzoefu wa hukumu na kuadibiwa kwa neno la Mungu, wanakuwa waangalifu kutafuta ukwelikatika kila kitu,na ni makini katika kutenda neno la Munguna kumtii Mungu. Watu kama hao wataweza kuelewahatua kwa hatua ukwelina kuingia katika ukwelikwa kupitia neno la Mungu, na kufanikisha wokovu na kufanywa kamili. Kwa wale ambao hawapendi ukweli, ingawa wanaweza kutambuakuonekana kwa Mungu na kazi kutoka kwa ukweliulioonyeshwa na Mungu, wanafikiri hakikawanaweza kufanikisha wokovu bora tuwaache kila kitu kwa ajili ya Munguna kutimiza wajibu wao. Mwishoni, bado hawawezi kupokea ukwelina uzima baada ya kumwamini Mungu kwa miaka mingi. Wanaelewa tu maneno machache, barua,na mafundisho,lakini wanafikiri wanajua ukwelina wamepata ukweli. Wanajidanganya wenyewena hakika wataondolewa na Mungu.

kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Tunaposoma maneno ya Mungu leo, jambo muhimu kabisa ni kwamba tukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu. Jambo la msingi ni kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, na hili ndilo jambo la muhimu kabisa. … Nyote mnasema kwamba mko tayari kuvumilia mateso ya hukumu na kuadibu. Kwa kuwa mko tayari kuvumilia mateso haya, mtatii vipi? Mtayakubali vipi? Ukiyaona maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu, je, utayakubali kama hukumu ya Mungu kwako? Au utashikilia kwamba maneno haya yanawahukumu wengine, kwamba hayahusiani na wewe, na hivyo kuepuka hukumu na kuadibu kwa Mungu? Utachukua njia ipi? Ikiwa uko tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, basi hufai kuepuka mambo haya unaposoma neno la Mungu. Haijalishi maneno haya ni ya kuumiza au makali kiasi gani, unapaswa kuyakubali yote. Unamwomba Mungu: “Ee Mungu, niko tayari kukubali hukumu na kuadibu Kwako. Maneno Yako ya hukumu yanaelekezwa kwangu. Mimi ni aina hii ya mtu mpotovu, nina shida hizi za upotovu, kwa hiyo napaswa kukubali hukumu na kuadibu Kwako, kwani huu ni upendo Wako kwangu, ni Wewe kuniinua. Nayakubali na kuyatii kabisa, na nina shukrani kwa ajili ya upendo Wako.” Punde unapoomba kwa njia hii, utayakubali kwa urahisi, na hutaona ugumu. Kisha linganisha maneno ya Mungu na hali zako wenyewe ili kuzidisha ufahamu wako. Hivi ndivyo inavyoweza kufanywa. Hili ni onyesho la kutii hukumu na kuadibu kwa Mungu. Lakini ukiyaona maneno ya Mungu ambayo ni makali kiasi, na kusema: “Mungu, maneno haya si hukumu kwangu, ni hukumu ya wengine, ni hukumu ya Shetani. Hayahusiani na mimi, kwa hiyo sihitaji kuyasoma,” basi huku ni kuepuka hukumu na kuadibu kwa Mungu. Ndugu wengine wakikupogoa na kukushughulikia, unapaswa kufanya nini? Unapaswa kuomba haraka kwa Mungu: “Mungu, nakushukuru! Huu ni upendo Wako ukinijia. Umewagusa ndugu zangu wanipogoe na kunishughulikia kwa sababu ya upendo Wako kwangu. Natii.” Lazima uombe. Usipoomba itakuwa rahisi kwako kukataa, rahisi kwa mwili wako kuasi, rahisi kwa wewe kutokubaliana na wengine, rahisi kulalamika na hata itakuwa rahisi zaidi kwako kuwa hasi. Kwa hiyo, lazima uende haraka kuomba. Baada ya kuomba, akili yako itakuwa tulivu, na utaweza kutii. Punde unapoweza kutii kweli, utakuwa na roho moyoni mwako, na utasema: “Wakati huo sikukasirika bali kulikubali. Ilikuwa kwa sababu niliomba. Sasa hatimaye naweza kumtii Mungu.” Unaona dalili ya matumaini na unapata kimo kiasi; hivi ndivyo mtu anakua.

kutoka katika “Jinsi Ambavyo Unapaswa Kula na Kunywa Maneno ya Mungu ili Kufanikisha Matokeo” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha I

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Views: 73 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Hukumu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar