4:58 PM
37. Mabadiliko ya tabia ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Je, mabadiliko katika tabia ni nini? Lazima uwe mpenzi wa ukweli, lazima uikubali hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu unapopitia kazi Yake, na kupitia aina zote za mateso na usafisho, ambayo kwayo unatakaswa kutokana na sumu za kishetani zilizo ndani yako. Haya ndiyo mabadiliko katika tabia. … Mabadiliko katika tabia yanamaanisha kuwa mtu, kwa sababu anapenda na anaweza kuukubali ukweli, hatimaye huja kujua asili yake ya uasi inayompinga Mungu; anaelewa kuwa upotovu wa binadamu ni wenye kina zaidi na kutambua upumbavu na udanganyifu wa mwanadamu. Anatambua uduni wa mwanadamu na kusikitisha kwake, na hatimaye anaelewa kiini na asili ya mwanadamu. Kwa kujua haya yote, anaweza kujikana na kujinyima kabisa, kuishi kwa neno la Mungu, na kutenda ukweli katika kila kitu. Huyu ni mtu anayemjua Mungu; huyu ni mtu ambaye tabia yake imebadilishwa.

kutoka katika “Jinsi ya Kuijua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za

Maongezi ya Kristo

Mabadiliko katika tabia hasa huhusu mabadiliko katika asili ya watu. Mambo ya asili ya mtu hayawezi kuonekana kutoka kwa mienendo ya nje; yanahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuwepo kwao. Yanahusisha moja kwa moja maadili ya mtu katika maisha, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi yake, na kiini chake. Mtu ambaye hawezi kukubali ukweli hatakuwa na mabadiliko katika hali hizi. Ni kwa kupitia kazi ya Mungu pekee, kuingia kikamilifu katika ukweli, kubadili maadili na mitazamo yake kuhusu kuwepo na maisha, kulinganisha msoni yake na ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zake zinaweza kusemekana zimebadilika.

kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika

Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Hiyo si kusema kwamba mtu aliyekomaa katika ubinadamu wake lazima atakuwa na mabadiliko katika tabia; labda hufanyika wakati baadhi ya sumu za kishetani katika asili ya mtu zinabadilika kwa sababu ya maarifa yao kuhusu Mungu na ufahamu wao wa ukweli. Hiyo ni kusema, sumu hizo zinatakaswa na ukweli unaoonyeshwa na Mungu unaanza kustawi ndani ya mtu huyo, unakuwa maisha yake, nao unakuwa msingi wa kuwepo kwake. Hapo tu ndipo anakuwa mtu mpya, na hivyo tabia yake inabadilika. Hivi si kusema kwamba tabia yake ya nje ni ya upole kuliko hapo awali, kuwa alikuwa na kiburi lakini sasa maneno yake ni ya busara, kwamba hakuwa anamsikiza mtu yeyote lakini sasa anaweza kuwasikiza wengine—mabadiliko haya ya nje hayawezi kusemwa kuwa ni mabadiliko katika tabia. Bila shaka mabadiliko katika tabia yanajumuisha hali hizi, lakini jambo lililo muhimu zaidi ni kuwa maisha yake ya ndani yamebadilika. Ukweli unaoonyeshwa na Mungu unakuwa maisha yake hasa, baadhi ya sumu za kishetani zilizo ndani zimetolewa, mtazamo wa mtu huyo umebadilika kabisa, na hakuna chochote kati ya hali hizo kinachokubaliana yale ya dunia. Anaona waziwazi njama na sumu za joka kubwa jekundu; amefahamu kiini cha kweli cha maisha. Kwa hivyo maadili ya maisha yake yamebadilika—hili ndilo badiliko la muhimu zaidi na kiini cha mabadiliko katika tabia.

kutoka katika “Tofauti Kati ya Mabadiliko ya Nje na Mabadiliko katika Tabia”

katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Asili ni nini? Ni kiini cha mwanadamu. Tabia ya mtu ni mambo ambayo yanafichuliwa katika asili ya mtu, na tabia iliyobadilika ina maana kwamba mambo maovu ambayo yalikuwa ndani yako hayataonekana tena kamwe, na kwamba yamebadilishwa na ukweli. Sio mambo ya asili ya mtu ambayo yamebadilika, lakini ni mambo maovu yanayofichuliwa ndiyo ambayo yamebadilika, na mambo yanayohusiana na tabia ya mtu ambayo yamefichuliwa katika hali ya mtu ndiyo yamebadilika. Shetani humpotosha mwanadamu, na mwanadamu amekuwa mfano wa Shetani, amekuwa kitu kinachopinga Mungu, na mwanadamu anaweza kabisa kumsaliti Mungu. Kwa nini inahitajika kwa watu kwamba tabia yao ibadilike? Katika watu ambao hatimaye wamekamilishwa, kunaongezwa mengi ya ujuzi wa Mungu, na mengi ambayo yanalingana na mapenzi ya Mungu. Katika siku za nyuma, watu walipokuwa na tabia potovu, kila kitu walichofanya kilikuwa kibaya, na kila kitu walichofanya kilimpinga Mungu. Sasa wana ukweli, wanaweza kufanya mengi ambayo yanalingana na mapenzi ya Mungu. Lakini hiyo sio kusema kwamba hawamsaliti Mungu; bado wana uwezo wa kumsaliti Mungu. Inawezekana kubadili sehemu ya yale yanayofichuliwa na asili ya watu, na sehemu inayobadilishwa ni sehemu yako ambayo ina uwezo wa kutenda kulingana na ukweli. Lakini kuweza kuweka ukweli katika vitendo leo hakumaanishi kwamba asili yako imebadilika. … Kwa hiyo huku “kubadilika” kunamaanisha nini? Kunamaanisha kwamba, unapoelewa mapenzi ya Mungu, utaweza kutii. Ikiwa huelewi mapenzi ya Mungu, wewe bado utatenda kulingana na matakwa yako mwenyewe na bado utaamini kwamba matendo yako yanalingana na mapenzi ya Mungu; huu ni usaliti, na ni kitu kilicho katika asili yako. Bila shaka, hakuna mipaka katika mabadiliko ya tabia. Kadiri ulivyopata ukweli mwingi zaidi—ambayo ni kusema, ujuzi wako kumhusu Mungu ulivyo wa kina zaidi—ndivyo uwezekano wako wa kumpinga na kumsaliti Mungu ulivyo mdogo zaidi. Ufuatiliaji wa mabadiliko katika tabia hasa hutatuliwa kwa ufuatiliaji wa ukweli. Maarifa ya kiini cha asili ya watu pia yanatimizwa kwa kuelewa ukweli. Wakati watu wamepata ukweli hakika, basi matatizo yote huyatatatuliwa.

kutoka katika “Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika

Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Kwa kifupi, mabadiliko katika tabia ya maisha hugeuka kutoka kumpinga na kumsaliti Mungu hadi hatimaye kuwa mtiifu na mwaminifu kwa Mungu, na kumwabudu—huo ndio mchakato. Wakati ambapo watu wanaweza kumtii na kumwabudu Mungu wanao ukweli na ubinadamu. Huyu ndiye aina ya mtu ambaye amepitia mabadiliko katika tabia yake ya maisha. Kwa hiyo, mchakato wa mabadiliko katika tabia ya maisha ni mchakato wa kuingia katika ukweli na kupata ukweli, mchakato wa kukubali ukweli kama uzima, na pia mchakato wa mtu kumjua Mungu. Mtu aliye na maarifa ya kweli kumhusu Mungu ambaye moyo wake umemilikiwa kabisa na neno la Mungu, ambaye anaweza kumpenda na kuwa mwaminifu kwa Mungu, kufanya kila kitu ili kumridhisha Mungu, na ambaye anaweza kuwa wa moyo na akili moja na Yeye ni aina ya mtu anayepatwa na Mungu. Ikiwa mtu hawezi kumpenda na kumtii Mungu kutoka moyoni mwake kwa sasa, inaonyesha kwamba moyo wake bado unatwaliwa na Shetani, na kwamba bado unadhibitiwa na sumu na falsafa ya Shetani. Wakati ambapo mtu amepata ukweli wote ambao anapaswa kuwa nao na kuukubali wote moyoni mwake, atapata maisha mapya. Akiwa na maisha mapya, utiifu wa mtu kwa Mungu, kumpenda Mungu, na kumwabudu Mungu kutafuata; wakati huu tabia ya maisha ya mtu itakuwa imebadilika kabisa. Mchakato wa mabadiliko katika tabia ya maisha pia ni mchakato wa kufanywa upya kwake. Moyo wa mtu huyo ulidhibitiwa na Shetani mwanzoni, na maisha na sumu ya Shetani vikawa asili yake. Sasa, vitu hivi vinavunjika kutokana na ukweli wote ambao ameukubali. Moyo wake unatawaliwa na ukweli, ukweli umekuwa bwana wa moyo wake, kwa hiyo tabia yake inayodhihirishwa katika maisha pia hubadilika, hivi ndivyo mabadiliko ya tabia ya maisha yalivyo. Wakati ambapo Shetani alikuwa na mamlaka ndani yako mwanzoni, ulikuwa ukimtii na ungemridhisha katika vitu vyote; vyote vilifanywa kulingana na Shetani. Hivi leo ni ukweli ambao una mamlaka ndani yako; unafuata ukweli pekee na kumridhisha Mungu. Mchakato wa Mungu kumpata mtu ni kama ufuatao: Mwanzoni, ilikuwa rahisi sana kwako kumpenda Shetani lakini vigumu kumpenda Mungu, lakini sasa kuna ukweli ndani yako na unapenda ukweli, kwa hiyo kumpenda Mungu kumekuwa rahisi. Unapoombwa kumpenda Shetani, lolote lisemwalo ili kukushawishi, hutalifanya. Kwa hivyo, mara ukweli unapoingia ndani ya mtu, yeye hubadilisha kabisa na kuwa mtu mpya. Kwa hivyo inaweza kusemekana kuwa tabia ya maisha ya mtu hubadilishwa hasa kwa kufuatilia na kupata ukweli.

kutoka katika “Nini Mabadiliko ya Tabia na Michakato Minne ya Mabadiliko ya

Tabia” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha IV

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

 

Views: 120 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: kumjua mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar