10:29 PM
10. Mtu kutekeleza wajibu wake ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Kutimiza wajibu wako ni ukweli. Kutimiza wajibu wako katika nyumba ya Mungu sio tu kutimiza masharti fulani au kufanya kitu unachopaswa kufanya. Ni kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa anayeishi kati ya mbingu na dunia! Ni kutimiza majukumu na wajibu wako mbele ya Bwana wa uumbaji. Majukumu haya ni majukumu yako ya kweli. Linganisha kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa na kuwa na upendo kwa wazazi wako—ni kipi ndicho ukweli? Kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa ndio ukweli; ni wajibu wako unaotarajiwa kutimiza.

kutoka katika “Uhalisi wa Ukweli ni Nini?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya

Kristo

Wajibu wako hausimamiwi na wewe; si shughuli yako au kazi yako mwenyewe. Ni kazi ya Mungu ambayo inahitaji ushirikiano wako, na hivyo kuibua wajibu wako. Kazi ya Mungu ya usimamizi imetekelezwa hadi leo, na sehemu ambayo lazima watu washirikiane katika kazi Yake ni wajibu wa mwanadamu. Bila kujali unatenda wajibu wa aina gani, si shughuli yako au biashara yako binafsi. Ni kazi ya nyumba ya Mungu, ni sehemu moja ya mpango wa Mungu wa usimamizi, na ni agizo ambalo Mungu amekupa. Hivyo basi, unapaswa kuchukulia vipi wajibu wako? …

Katika kutenda wajibu wako lazima kwanza utafute matakwa ya Mungu. Kutenda wajibu wako si kuchagua upendeleo wako binafsi au kufanya chochote ambacho ungependa kufanya, na si kufanya chochote ambacho unafurahi na kuridhika unapokifanya au chochote kitakachokufanya uonekane kuwa mzuri. Ukimlazimishia Mungu kwa nguvu upendeleo wako au kutenda upendeleo wako mwenyewe kama kwamba ni ukweli, ukiyafuata kana kwamba ni kanuni za ukweli, basi si hilo ni kosa? Huko si kutekeleza wajibu wako na kutekeleza wajibu wako kwa njia hakutakumbukwa na Mungu.

kutoka katika “Unaweza tu Kutekeleza Wajibu Wako Vizuri kwa Kutafuta

Kanuni za Ukweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

6. Unapaswa kufanya yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu, na kutenda wajibu wako, na kutimiza majukumu yako, na kushikilia jukumu lako. Kwa sababu unaamini katika Mungu, unapasa kutoa mchango wako kwa kazi ya Mungu; kama huwezi, basi wewe hufai kula na kunywa maneno ya Mungu, na hufai kuishi katika nyumba ya Mungu.

kutoka katika “Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu

katika Enzi ya Ufalme Wazitii” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mwanadamu kufanya wajibu wake ni, kwa uhakika, kutimiza yote yaliyo ya asili yake, yaani, yale yawezekanayo kwa mwanadamu. Hapo ndipo wajibu wake hutimizika. Dosari za mwanadamu wakati wa huduma ya mwanadamu hupunguzwa taratibu kupitia kwa uzoefu uongezekao na mchakato wa uzoefu wake wa hukumu; hayazuii au kuathiri wajibu wa mwanadamu. Wanaoacha kutoa huduma au kuzalisha na kurudi nyuma kwa kuogopa makosa yanayoweza kuwepo katika huduma ndio waoga zaidi miongoni mwa wanadamu wote. Ikiwa mwanadamu haonyeshi anachopaswa kuonyesha wakati wa kutoa huduma au kutimiza kile kilicho katika uwezo wake kiasili, na badala yake huzembea na kufanya tu bila ari yoyote, atakuwa amepoteza majukumu yake ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo. Mwanadamu kama huyu anachukuliwa kuwa mtu hafifu na duni apotezaye nafasi; itakuaje kwamba mtu kama huyu aitwe kiumbe? Je, hao si ni vyombo vya upotovu ving’aavyo kwa nje ila vimeoza kwa ndani?

kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana. Acha Niwaambie hiki kitu kimoja: Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake.

kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Hivyo basi, kila mtu anapaswa kutekeleza wajibu gani? Wajibu ambao kila mtu anapaswa kutekeleza ni ukweli ambao kila mtu anapaswa kutenda, na ukweli unaopaswa kutekeleza ni wajibu unaopaswa kutekeleza, faradhi unayopaswa kutimiza. Ukitenda ukweli ambao unaufahamu na unapaswa kutenda, basi utakuwa umetimiza wajibu wako vizuri. Usipotenda ukweli, basi hutimizi wajibu wako. Unacheza cheza, unamdanganya Mungu, na wewe ni mzembe tu kwa Mungu. Hivyo, utendaji wa wajibu wako ni lazima uunganishwe na ukweli, unapaswa kuunganika kwa karibu na ukweli. Unapaswa kuweka katika vitendo ukweli wote ambao unaelewa na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli. Kuishi kwa kuridhisha uhalisi wa ukweli ni uwakilishi wa sura ya kweli ya mwanadamu. Mungu alipomuumba mwanadamu, ilikuwa kwa msingi wa sura hii, hivyo ukiishi kwa kudhihirisha sura ya ukweli utamridhisha Mungu. Mungu atafurahi Akuangaliapo, Atakubariki, Atakupa maisha ya milele, Atakuruhusu uishi milele. Lakini iwapo huishi kwa kudhihirisha sura ya ukweli, basi hustahili kuitwa mwanadamu, na Mungu akuangaliapo, Atafikiri huna hali ya kiroho, na kwamba huna pumzi yoyote ya maisha ambayo Mungu amekupa. Ataamuru kwamba taka kama hiyo iondolewe. Hivyo, kutekeleza wajibu kwenyewe ni kutenda ukweli. Usipotenda ukweli unapotekeleza wajibu, basi hutekelezi wajibu wako kwa kweli. Unacheza cheza tu, kumdanganya Mungu, na kuwa mzembe kwa Mungu. Unafuata tu utaratibu. Hivyo, iwapo unamwamini Mungu, unapaswa kupitia na kutenda ukweli ambao Mungu amewapa wanadamu, na hatimaye unapaswa kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa neno la Mungu. Huku ni kutekeleza wajibu wako. … Iwapo ukweli hauhusishwi unapotekeleza wajibu wako, basi ni wa uongo, ni uzembe, ni wa uongo na wa kudanganya; unapitia tu urasmi, unafuata tu utaratibu. Ili kutekeleza wajibu wako kwa kweli, ni lazima utende ukweli unapoutekeleza wajibu, hii ni njia ya pekee ya kutekeleza wajibu wako kwa kiwango kilichowekwa, hii ni njia ya pekee kuwa mwanadamu kwa kweli. Na aina yoyote ya kazi unayofanya, inahusisha kutenda ukweli, na unapotenda ukweli unatimiza majukumu yako. Hii ni faradhi na wajibu wako, hivyo ni lazima utekeleze vizuri. Tunamaanisha hii kwa kutenda ukweli. Kwa hivyo uhusiano wa kweli kati ya kutekeleza wajibu wao na kutenda ukweli ni upi? Ni njia mbili tofauti ya kueleza kitu sawa. Kwa nje, inaonekana kama wajibu ukitekelezwa, lakini kiasili, ni ukweli unatendwa. Hivyo, iwapo huelewi ukweli unapotekeleza wajibu wako, utaweza kutekeleza kazi yako vizuri? Hutaweza. Kwanza kabisa, hutakuwa na ufahamu wazi wa maana ya kutekeleza wajibu wako, ama jinsi ya kutekeleza wajibu wako vizuri. Hutakuwa na ufahamu wazi wa mambo haya. Pili, siku itakuja ambapo una ufahamu wazi lakini bado utakosa kutekeleza wajibu wako vizuri, bado utakuwa na makosa mengi. Wakati huo, utagundua kwamba ubinadamu wako una dosari, kwamba unatenda makosa mengi katika mambo unayofanya, kwamba umejaa upotovu. Wakati huo utaanza kutafuta ukweli ili kuondoa upotovu huu, na punde utakapouondoa, utaanza kutekeleza wajibu wako kwa kufaa. Punde unapoondoa upotovu wako na kuufahamu ukweli, wakati huo utatekeleza wajibu wako kwa usahihi na vizuri, si kwa jina tu, lakini pia kwa uhalisi. Ukimiliki ukweli unapotekeleza wajibu wako, iwapo hakuna upotovu hata kidogo unaonyeshwa unapoutekeleza, basi matokeo yanayostahili yatatimizwa katika utendaji wako. Utakuwa pia umetekeleza wajibu wako kwa kiwango kilichowekwa. Huu ni kweli kabisa. Hivyo, wakati wowote unapotekeleza wajibu wako, jinsi unatafuta ukweli ni muhimu sana. Usipotafuta ukweli, basi ni hakikisho kwamba utendaji wa wajibu wako hautafikia kiwango kilichowekwa.

kutoka katika “Ni Kama Tu Mtu Hutenda Ukweli katika Kufanya Wajibu Wake

Ndipo Atapata Baraka ya Mungu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia

Katika Maisha V

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Views: 105 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: neno la Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar