8:58 PM
Ushuhuda wa Maisha | Si Rahisi Kwako kwa Hakika Kujijua Mwenyewe

Ushuhuda wa Maisha | Si Rahisi Kwako kwa Hakika Kujijua Mwenyewe

Zhang Rui Mji wa Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang

Niliona katika maneno ya Mungu kwamba Mungu anawapenda watu waaminifu na anawachukia watu wadanganyifu, na ni watu wanyofu tu watakaopata sifa Zake. Kwa hiyo, nilitaka kuwa mtu mnyofu, kwa utambuzi kufanya mazoezi ya kuzungumza kwa usahihi, kuwa bila upendeleo na wa busara, na kutafuta ukweli kutoka kwa mambo ya hakika wakati wa kutoa taarifa juu ya masuala. Katika kazi yangu, kama iwe ni kosa au upungufu, mimi nililielezea kwa undani kwa kiongozi. Pia kwa utambuzi niliuchangua na kuufichua upotovu wangu mwenyewe. Kila wakati nilipoweka hili katika matendo, nilihisi kuwa nilikuwa nimepitia mabadiliko fulani na nilipata mfano kidogo wa kuwa mtu mnyofu.

Katika ushirika kwa mkutano wa hivi karibuni wa wafanyakazi wenza, akizungumza juu ya namna ambayo ni lazima tujifunze kutofautisha kati ya aina mbalimbali za watu katika utumishi wetu kwa Mungu, kiongozi aliniuliza: “Fulani, unafikiri wewe ni mtu wa aina gani?” Nikafikiria mwenyewe: nimepitia mabadiliko kiasi hivi karibuni, hivyo mimi ni kama mtumwa kawaida na wazi kiasi. Kuhusu asili mbaya, najisikia mimi si mbaya vile. Kuhusu asili nzuri, similiki kila maonyesho ya wema, lakini angalau sana najihisi kuwa sahili, mnyofu, na sina moyo mwovu. Kwa hiyo, mimi nilijibu kwa kusema: “Kuzungumza kiasi, mimi ni mtu wa kawaida, na wa asili njema” Kiongozi alisema: “Wewe unafikiri una asili nzuri, kwamba wewe ni mtu wa kawaida kiasi na mnyofu. Hivyo ungethubutu kweli kujieleza na kufichua kila kitu kukuhusu wewe mwenyewe? Wewe kweli huna shaka kwa Mungu kwa asilimia mia? Kweli unathubutu kukubali ya kwamba katika maneno yako na vitendo hakuna malengo ya nia za kibinafsi?” Baada ya kusikia haya, nilijihisi mwasi na nilielezea kwa kujitetea: “Je, ya hapo juu hayakusema kuwa watu wazuri bado wana tabia potovu, kwamba wanaweza kuonyesha kila aina ya upotovu—hili haliuwiani?” Sikuwa radhi kabisa kuachilia maoni yangu mwenyewe.

Baada ya haya kutokea, nilitafakari kwa makini yale aliyoyasema kiongozi: Ningeweza kweli kuthubutu kufichua kila kitu kujihusu mwenyewe? Singeweza. Mambo ambayo niliyaelezea yalikuwa tu masuala yasiyo na thamani ambayo hayakuathiri sifa yangu au umimi. Upotovu wa kibinafsi ambao niliuelezea ulikuwa maonyesho ya upotovu wa kawaida ambao kila mmoja anao, lakini sikuwa nimewahi kuthubutu kueleza na kufichua mambo mabaya na maovu ndani kabisa ya moyo wangu. Nilikuwa kweli sina shaka kwa Mungu kwa asilimia mia? Sikuwa. Wakati kazi yangu haikuzaa matunda, nilipokuwa hasi na dhaifu, nilimwelewa Mungu vibaya na kuamini kuwa mimi nilitoa huduma tu, na ilikuwa bure kuendelea katika utafutiliaji huu. Na sikuamini akatika maneno ya Mungu kwa asilimia mia, katika tabia ya Mungu. Sikuamini kwamba Mungu angewatuza na kuwaadhibu watu kwa mujibu wa maneno Yake, hivyo mimi mara nyingi niliijaribu tabia Yake. Nilipokuwa nje nikienda hapa na pale na kufanya kazi kiasi, yote yalikuwa tu kufanya shughuli na Mungu ili katika siku zijazo ningeweza kubarikiwa na kuzuia maafa; haikuwa kutimiza wajibu ambao kila kiumbe ni lazima autimize. Ingawa kulikuwa na sura ya nje ya tabia njema, hiyo ilikuwa ni ya watu wengine kuona, kuwapa maono mazuri. … Kufikiria kiasi yale hili lilifichua, yote hayakuwa sura ya uongo? Hata hivyo, nilifikiri kwamba nilikuwa mtu sahili kiasi na mnyofu—si huku kweli hii ni kutojijua mwenyewe? Fikiria juu ya kile Mungu alisema: “Ufahamu wa watu wa asili yao wenyewe ni wa juujuu sana, na hutofautiana sana na maneno ya Mungu ya hukumu na ufunuo. Hili si kosa katika lile ambalo Mungu hulifuanua, bali badala yake ni ukosefu wa mwanadamu wa ufahamu wa kina wa asili yake. Watu hawana ufahamu wa kimsingi au wa kutosha wa wao wenyewe, bali badala yake wao wanalenga na kutenga nguvu zao kwa matendo na maonyesho ya nje. Hata kama mtu fulani angelisema jambo mara chache kuhusu kujifahamu, halingekuwa la kina sana. Hakuna mtu aliyewahi kufikiria kwamba yeye ni aina hii ya mtu au ana asili ya aina hii kwa kulitenda jambo kama hili au kulifunua jambo katika mwelekeo fulani. Mungu ameifunua asili na kiini cha mwanadamu, lakini mwanadamu anafahamu kwamba njia yake ya kuyatenda mambo na njia yao ya kusema ni yenye mawaa na yenye kasoro; kwa hiyo ni kazi yenye kutumia juhudi nyingi kwa watu kutia ukweli katika vitendo. Watu wanafikiria kwamba makosa yao ni udhihirisho wa muda tu, ambao unafunuliwa bila kujali, badala ya kuwa ufunuo wa asili yao. … kwa hiyo, wakati wanatia ukweli wao katika vitendo wanaifuata sheria kwa uzembe. Watu hawazioni asili zao wenyewe kama zilizo potovu sana, … lakini kwa kweli, kufuatana na viwango, kuna tofauti kubwa sana, kwa sababu watu wana mazoea fulani tu ambayo kwa nje hayakiuki ukweli, lakini kwa kweli hawatii ukweli katika vitendo” (“Kuifahamu Asili na Kuutia Ukweli Katika Vitendo” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kupitia kupata nuru kutoka kwa maneno ya Mungu, mimi niliona hapo tu kwamba ufahamu wangu juu yangu mwenyewe ulikuwa wa juu juu—nilikuwa nikijaribu kujijua mwenyewe kutoka kwa dhana zangu na mawazo yangu mwenyewe, bila mlingano na maneno ya Mungu kutambua tabia yangu ya kishetani ya kuweza kudanganya na kusema uwongo na kuwa mdanganyifu na asili yangu mwenyewe potovu kutoka kwa ndani ya maneno yake. Niliamini kuwa nilikuwa mtu wa kawaida, mnyofu, na nilikuwa na asili nzuri; lakini ilikuwa tu kwamba kuangalia kutoka nje, nilikuwa sijafanya kitu chochote kuiudhi pakubwa tabia ya Mungu. Katika hali ya kuwa mtu mnyofu nilikuwa nimekomea tu kwa sura ya nje na nilidhani kwamba nikisema ukweli kidogo na kufanya mambo machache halisi ingetosha kutosheleza kiwango cha kuwa mtu mnyofu. Mimi kwa kweli nilikuwa fidhuli sana; kwa kweli sikujijua mwenyewe! Sikujua kwamba sikuwa hata kidogo ninamiliki kiini cha mtu mnyofu, na mimi nilikuwa tofauti sana na kiwango cha Mungu. Wakati huo nilifikiri juu ya Petro akijitambua mwenyewe katika maneno ya Mungu. Yeye daima kwa ukali alijilinganisha na maneno ya Mungu ambamo Yeye aliwafichua watu, hivyo kati ya watu wote, Petro alijua upotovu wake mwenyewe vyema kuliko mtu yeyote na ndiye aliyekuwa na mafanikio zaidi katika uzoefu wake. Nimemfuata Mungu kwa miaka kadhaa na bado sijijui mwenyewe. Uwezo wangu wa kuingia bado una upungufu zaidi; mimi kwa hakika ni aibu.

Natoa shukurani kwa nuru ya Mungu na mwongozo ambavyo vimefanya nione upungufu wangu mwenyewe na kudharaulika, na pia vimenifanya kuelewa kwamba kweli kujijua mwenyewe si kitu rahisi. Uhalisi wa bila mapendeleo tu ni kujijua mwenyewe kupitia kwa maneno ya Mungu. Kutoka siku hii kwendelea, niko tayari kujijua mwenyewe kupitia kwa maneno ya Mungu, na wakati wowote ambapo maneno ya Mungu yanaifichua asili potovu ya watu nitakuwa radhi kujipima mwenyewe kwa ukali dhidi ya hilo. Sitajipima mwenyewe tena kutoka kwa msimamo wangu mwenyewe, nitafuatilia mabadiliko katika tabia, na nitaufariji moyo wa Mungu kwa kuwa kweli mtu mnyofu.

 

Chanzo:  Ushuhuda wa Maisha | Si Rahisi Kwako kwa Hakika Kujijua Mwenyewe

Ninaona njia ya kumjua MunguBaadhi ya Makala: 

 

Views: 76 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Maneno ya Mungu, tabia ya Mungu, ukweli | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar