8:13 AM
Ushuhuda wa Maisha | Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …

Ushuhuda wa Maisha | Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …

Huimin Mji wa Jiaozuo, Mkoa wa Henan

Kila wakati nilipoona au kusikia kuhusu mtu aliyekuwa amebadilishwa kama kiongozi naye kujisikia mwenye huzuni, dhaifu au mnunaji, basi niliwaangalia kwa dharau. Nilidhani haikuwa kitu zaidi ya watu tofauti waliokuwa na majukumu tofauti ndani ya kanisa, kwamba hakukuwa na tofauti kati ya juu au chini, kwamba sote tulikuwa uumbaji wa Mungu na hakukuwa na sababu ya kuhuzunikia. Kwa hiyo kama nilikuwa nikiwatunza waumini wapya au kuongoza wilaya, sikuwahi kufikiri kuwa nilizingatia sana hadhi yangu, kwamba nilikuwa mtu wa aina hiyo. Singeweza kamwe kufikiri hata katika miaka milioni moja kwamba ningeonyesha tabia ya aibu kama hiyo wakati mimi mwenyewe nilipobadilishwa …

Kwa kuwa kazi yangu haikuwa imeleta matokeo yoyote kwa muda fulani, kiongozi wangu alinibadilisha. Wakati huo, nilidhani kuwa hata kama ubora wa tabia yangu haukuwa umefanywa kuwa kiongozi wa wilaya, hakika ni lazima bado niruhusiwe kufanya kazi ya kunyunyizia. Sikuwahi kutarajia kiongozi wangu anifanye nitunze kazi za kawaida. Nilishangaa basi, nikifikiria kuwa kiongozi wa wilaya mwenye heshima kama mimi leo akitumwa, na kwamba mtu yeyote katika kanisa ambaye angeweza kupeleka ujumbe au ambaye alikuwa na akili kidogo angeweza kufanya kazi hii. Je, si kunilazimisha nifanye kazi hii ulikuwa dhahiri ni uharibifu wa vipaji vyangu? Lakini niliendelea kujiwekea hisia zangu, nikiwa na hofu kwamba dada zangu wangesema sikuwa mtiifu, kwamba nilijali kuhusu hadhi yangu. Lakini mara tu nilipofika nyumbani, nilianguka sawasawa kitandani na kujisikia vibaya sana. Mawazo ya kutokuwa na hadhi kutoka sasa kwendelea na kushangaa ni jinsi gani ndugu zangu wa kike na wa kiume wangeniona yalijaa kichwani mwangu. Na kunifanya nitumwe—ningewezaje kupata umaarufu wangu tena? Nilivyozidi kulifikiria jambo hilo, ndivyo nilivyozidi kujihisi vibaya sana.

Siku chache baadaye, nikamwona dada aliyekuwa amenipangia kazi. Mara tu nilipomwona, alinipa ushirika, akisema, “Kufanya kazi hii inaonekana rahisi, lakini bado ni lazima ifanywe kwa upendo,” kisha akaendelea kuzungumza juu ya ukweli wa vipengele kama vile hekima na utii. Nikanong’ona bila kujihusisha, wakati moyo wangu ukiwa kama moto mkali, nikifikiri, “Unanipa ushirika? Kana kwamba sijui chochote! Si ni mimi niliyekupa ushirika mwanzoni? Sasa wewe ndiwe unayenipa kwa zamu.” Hakuna neno hata moja la yale dada yangu aliyokuwa akishiriki lilioingia ndani; badala yake niliudhiwa tu na maneno yake ya kupita kiasi. Mwishowe nikasema bia subira, “Kuna chochote kingine? Kama hakuna, basi nakwenda zangu!” Mara niliporudi, niliendelea kujiuliza ni kwa nini nilikuwa na mtazamo kama huo kwa dada yangu. Ikiwa hadhi yake ilikuwa ya juu kuliko yangu au sawa na yangu, ningemtendea hivi? La, singefanya hivyo. Bila shaka haingekuwa hivyo! Si ilikuwa ni kwa sababu daima nilikuwa nimemwongoza, na sasa yeye kwa zamu alikuwa akinionyesha mambo ambayo yaliniacha nisiyeshawishika? Si hii inaonyesha kwamba nilikuwa ninaongozwa na fikira za hadhi? Ghafla nilihisi vibaya sana juu ya tabia yangu mwenyewe ya aibu na maneno ya Mungu ya hukumu yalinijia: “Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii ndivyo utavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo zaidi lazima wapitie usafishaji mkubwa. Mtu wa aina hiyo hana thamani kabisa! Lazima ashughulikiwe na ahukumiwe vya kutosha ili aache hilo kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii maisha hawawezi kubadilishwa; wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na kuingia ndani; daima wewe hulenga tamaa zile badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kufika karibu na Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme? Ikiwa kusudi la kufuatilia kwako si kutafuta ukweli, basi afadhali utumie fursa hii na kurudi duniani ili kufanikiwa. Kupoteza muda wako hivi kwa kweli hakuna thamani—kwa nini ujitese?” (“Mbona Huko Tayari Kuwa Foili[a]?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nikiangalia maneno ya Mungu na nikifikiri juu yangu mwenyewe, niligundua kuwa kile nilichokuwa nikifuatilia hakikuwa ukweli kamwe, wala sikuwa nikitafuta kumtosheleza Mungu, lakini badala yake ilikuwa sifa, faida na hadhi. Nikiwa na hadhi, kujiamini kwangu kuliongezeka mara mia moja; bila hadhi, nilikuwa mwenye harara na wa huzuni sana hivi kwamba singeweza kujisumbua kufanya kazi. Kwa kweli nilijisahau kwa hadhi yangu nikiharakisha pote nikijihusisha mchana kutwa na mambo haya yasiyo na maana na yasiyo na thamani na kupoteza wakati mwingi; na nilipata nini mwishowe? Tabia ya aibu niliyoionyesha leo? Nikifikiri juu ya yote ambayo Mungu alikuwa amenifanyia, sikuwa tu nimekosa kuufariji moyo wa Mungu kwa imani ambayo Yeye alikuwa ameweka ndani yangu, lakini kwa kinyume, nilikuwa nimechukia kazi aliyokuwa amenipa Yeye kuwa ni duni mno na sikutaka kuifanya. Kwa hiyo nilikuwa nafuatilia dhamiri yangu mwenyewe? Nilimshukuru Mungu kwa ufunuo Wake ambao uliniruhusu kuona aibu ya kufuatilia umaarufu wangu mwenyewe, faida na hadhi, na kutambua kwamba nilikuwa mwenye kiburi sana, mweye kujigamba sana na kuweka umuhimu mkubwa sana juu ya hadhi. Kisha kukaja kwa fikira wimbo wa maneno ya Mungu: “Ee Mungu! Kama nina hadhi au la, sasa ninajielewa mwenyewe. Hadhi yangu ikiwa juu ni kwa sababu ya kuinuliwa na Wewe, na ikiwa iko chini ni kwa sababu ya mpango Wako. Kila kitu ki mikononi Mwako. Sina chaguzi au malalamishi yoyote. … na ninapaswa tu kuwa mtiifu kabisa chini ya utawala Wako kwa sababu kila kitu ki ndani ya yale Umepanga. … Ukinitumia, mimi ni kiumbe. Ukinikamilisha, mimi bado ni kiumbe. Usiponikamilisha, bado nitakupenda kwa sababu mimi si zaidi ya kiumbe” (Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Niliimba wimbo huu mara kwa mara, machozi yakitiririka kutoka kwa macho yangu, na nikaja kuomba mbele ya Mungu: Ee Mungu! Kupitia kwa maneno Yako nimekuja kuelewa nia Zako. Bila kujali kama hali yangu ni ya juu au ya chini, mimi ni uumbaji Wako na ni lazima nitii kabisa mipangilio unayoifanya Wewe, ni lazima nifanye kila ninaloweza kutekeleza wajibu unaotarajiwa kwa moja ya uumbaji Wako na nisiwe mchaguzi mwangalifu kwa yale uliyoniaminia kufanya. Ee Mungu! Ninapenda tu kuitii mipangilio yako, kuwa mbele Yako na kufanya kazi kama ng'ombe na kuwa chini ya mamlaka Yako, kamwe kutofanya tena mambo ambayo hunisababisha mateso au yanayokuumiza Wewe kwa sababu ya hadhi. Ee Mungu! Mimi natamani tu Wewe unishughulikie na kunihukumu hata zaidi, kunifanya niwe na uwezo wa kuweka chini ufuatiliaji wangu wa hadhi, kuacha mambo hayo ambayo huzuia nikukaribie Wewe na kukupenda Wewe, na kufanya kila ninaloweza kutekeleza wajibu wangu kwa uaminifu wote.

Chanzo:  Ushuhuda wa Maisha | Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …

Views: 96 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Ushuhuda wa Maisha, ukweli, neno la Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar