9:22 AM
Ushuhuda wa Maisha | Asili ya Upendo wa Mungu Ni Nini?

Ushuhuda wa Maisha | Asili ya Upendo wa Mungu Ni Nini?

Siqiu   Mji wa Suihua, Mkoa wa Heilongjiang

Wakati wowote ninapoona kifungu kinachofuata cha neno la Mungu, “Ikiwa daima umekuwa mwaminifu Kwangu na kunipenda, lakini unapitia mateso ya maradhi, misukosuko ya maisha, na kutelekezwa na marafiki na jamaa au kupitia maafa mengine yoyote maishani, basi, uaminifu na mapenzi yako Kwangu yataendelea kuwepo?” (“Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ninahisi hasa bila furaha—hisi ya huzuni hunyatia ndani yangu na moyo wangu husema malalamiko yake yasiyoghuna: Ewe Mungu, Unawezaje kuruhusu wale walio waaminifu Kwako na wanaokupenda Wewe kukutana na msiba wa jinsi hiyo? Matokeo yake, nimekuwa na wakati mgumu kuelewa maana ya mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu ambaye alisema, "Mahitaji ya mwisho ya Mungu ya mtu ni ya kupenda na ya kweli."

Hivi karibuni, dada ambaye nilikuwa nikiratibu naye alishikwa na ugonjwa wa tezi dundumio kufanya kazi kupita kiasi. Hatua kwa hatua, hali yake ilifikia kiwango ambapo ilimbidi ale milo sita kwa siku. Kwa sababu ya msongo wa ugonjwa huu, nguvu zake polepole zilipungua, na aliishi kila siku katika mfadhaiko, udhaifu na uchovu. Mwili wake haukuweza kutimiza tamaa yake ya kutekeleza majukumu yake na ugonjwa wake ukaongezeka zaidi na zaidi. Sikuweza kuelewa ni kwa nini hili lilikuwa linatokea: Dada huyu alikuwa ameacha familia yake na kazi iliyokuwa na mshahara wa juu na faida nzuri ili kujitolea kwa utimizaji wa majukumu yake na alikuwa mwaminifu sana. Inawezekanaje kuwa, kwa yote aliyotoa, angetwishwa mateso ya ugonjwa huu kama malipo? ... Sikufichua hisia zangu kwa nje, lakini moyo wangu ulikuwa katika mfadhaiko—wakati wowote mtu yeyote alipoleta suala hili ningekasirika.

Muda mfupi baadaye, mimi na dada yangu tuliachana, lakini sikusahau kamwe kumhusu. Siku moja, nilimuuliza kiongozi wangu jinsi dada yangu huyo alivyokuwa. Kiongozi huyo akasema: "Mwanzoni alikuwa na hali mbaya sana na alikataa kuitambua kazi ya Mungu. Baadaye, kwa ufahamu alirekebisha hali yake, akitafuta nia ya Mungu ndani ya mateso ya ugonjwa wake. Kupitia maneno ya Mungu, alianza kujijua na kutambua kwamba hakuwa na imani ya kweli. Ndani ya imani yake bado kulikuwa na dalili ya "kubadilishana," bado hamu ya kupata baraka kupitia imani yake kwa Mungu. Pia alitambua dalili zingine nyingi za uasi ndani yake. Mara alipotambua mambo haya kujihusu mwenyewe, afya yake iliboreka sana. Anapona siku kwa siku, amerudia kula milo mitatu kwa siku na hali yake ni bora zaidi. Anaweza hata kuwasaidia ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji wake kurekebisha hali zao ….” Niliposikia habari hii njema, nilishtuka kweli. Nilikuwa nimedhani kwamba mateso ya ugonjwa yangechakaza azimio la dada yangu na kumsababishia mateso makubwa. Akiwa ameumizwa sana na ugonjwa, niliamini kuwepo kwake kwa njia ya kusonga mbele ingekuwa ya giza zaidi na zaidi. Hata nilishuku kwamba hangeweza kuendelea. Leo, akikabiliwa na uhalisi wa hali yake, nilibaki kusimama nikiduwaa. Sio tu kwamba hakuwa amepoteza imani yake, lakini, kwa njia ya kusafishwa kwa ugonjwa wake, kwa kweli alikuwa amekuja kuelewa kazi ya Mungu na kutambua upotovu wake. Alijifunza kutoka kwa uzoefu wake na alikuwa amefanya maendeleo kwa maisha yake. Je, si ugonjwa huu ulikuwa dhihirisho la upendo wa kweli wa Mungu na wokovu wa kweli wa mwanadamu?

Baadaye, nilisoma fungu lifuatalo kutoka kwa ushirika wa mtu: "Nambari ya 5: ‘Ikiwa daima umekuwa mwaminifu Kwangu na kunipenda, lakini unapitia mateso ya maradhi, misukosuko ya maisha, na kutelekezwa na marafiki na jamaa au kupitia maafa mengine yoyote maishani, basi, uaminifu na mapenzi yako Kwangu yataendelea kuwepo?’ (“Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kazi ya Mungu haiambatani na mawazo ya watu. Mungu amefanya kazi kulingana na kanuni hii ili kuleta wokovu kwa watu katika enzi zote. Wale wote ambao wamepitia kazi hii ya Mungu watajua ukweli huu. Watu ni waaminifu na wenye upendo kwa Mungu na Mungu kwa upande mwingine huwapa upendo Wake. ... Kama kwa hakika sisi ni wenye upendo na ni waaminifu kwa Mungu, tunapokutana na taabu za aina zote, hili, pia, ni dhihirisho la upendo wa Mungu. Kama kwa hakika tunaelewa mapenzi ya Mungu, tunapaswa kuwa waaminifu hata zaidi na kumpenda Mungu hata zaidi hadi mwisho. Kama hatuwezi kuona mapenzi ya Mungu katika majaribu na hata kumwelewa Mungu visivyo na kumsaliti Mungu, hakika hatutambui kazi ya Mungu. Hata kama tunampenda na ni waaminifu kwa Mungu, bado kuna dalili za usaliti ndani yetu. Hakuna anayeweza kupinga hilo. Mungu humjaribu na kumsafisha mtu ili kumtakasa na kumwokoa" (kutoka kwa Ushirikiano Kutoka kwa wa Juu). Ni baada tu ya kusoma kifungu hiki cha ushirika nilipotambua kwamba siku zote niliihukumu kazi ya Mungu kulingana na mawazo yangu yaliyounganishwa na mwili. Kwa makosa niliamini kuwa upendo wa Mungu una zawadi nyingi za neema na hakikisho la furaha ya kimwili na amani. Sikuwahi kufikiri kuwa mateso ni aina ya baraka za Mungu. Ni baada tu ya kupata habari ya uzoefu wa dada yangu, nilipoelewa kwamba usafishwaji wa mateso ni dhihirisho la kweli la upendo wa Mungu. Mungu husababisha hali fulani na kutoa maafa kwa watu Wake—iwe kwa njia ya ugonjwa wa kimwili, shida ya kifedha, au matatizo mengine yoyote—sio kwa sababu ya uadui lakini kwa sababu ya wema Wake. Ili kukabiliana na upotovu na upungufu wa mwanadamu, Mungu husababisha kila aina za hali kumjaribu na kumsafisha. Yeye hufanya kazi kupitia mateso haya ili kumsafisha, kumbadilisha na kumpa mwanadamu uzima. Ingawa mwili wa mwanadamu lazima upitie shida ya ajabu katika mchakato wa usafishaji, ambayo inaweza kuonekana kama taabu au jambo gumu kuelewa, hii kwa kweli ni Mungu anayefanya kazi ili kuruhusu mtu kujitambua, kusafisha uchafu wote na kumleta mwanadamu katika uhusiano wa kawaida zaidi na zaidi na Yeye ili apate polepole kuukuza upendo kwa Mungu ndani ya moyo wake. Faida hizo haziwezi kupatikana kupitia maisha ya burudani. Wakati mtu anapopata masomo yaliyopatikana kutoka kwa mateso ya majaribu yake na huakisi nyuma kwa njia ambayo amechukua, hatimaye yeye huelewa kwamba hukumu za Mungu na kuadibu, kupiga Kwake na kufundisha nidhamu vyote vilikuwa vimesambazwa na upendo Wake usio na kikomo. Upendo wa Mungu sio tu wenye kustawisha na wenye huruma. Sio tu kuhusu kutoa manufaa ya kimwili, lakini pia kusafisha kwenye kutia uchungu, kupiga na kufundisha nidhamu.

Ewe Mungu, asante kwa kufanya kazi kupitia vipengele vyote vya mazingira yangu ili kurekebisha njia yangu ya kufikiria iliyo ya upuuzi na iliyopotoka na kuniruhusu kuona kwamba hata kama upendo Wako hauambatani na mawazo yetu, dhihirisho lake daima hulenga kutuboresha na kutuokoa. Matendo Yako ya upendo daima yamejaa kazi ya bidii ya moyo Wako na hekima isiyoelezeka. Nilitambua pia kwamba hapo awali sikuwa na ufahamu juu Yako hata kidogo na sikuelewa kuwa upendo Wako mara nyingi umefichwa katika hali. Ewe Mungu, kwa heshima ya upendo Unayoshiriki na wanadamu, nakupa Wewe sifa na shukrani! Pia ninatumaini kwamba siku moja mimi pia nitapokea aina hii ya upendo. Upendo huu ukiletwa kwangu, naapa kukubali kiwango chochote cha mateso, ili nipate kupitia na kushuhudia upendo Wako.

Chanzo: Ushuhuda wa Maisha | Asili ya Upendo wa Mungu Ni Nini?

Views: 102 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: kazi ya Mungu, upendo wa Mungu, mapenzi ya Mungu, Baraka | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar