8:00 PM
Ushuhuda wa Injili | Mapambano ya Kufa na Kupona

Ushuhuda wa Injili | Mapambano ya Kufa na Kupona

Chang Moyang Mjini Zhengzhou, Mkoani Henan

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: “Ukiasi dhidi ya mwili wako, bila shaka kutakuwa na vita ndani yako. Shetani atajaribu kukufanya ufuate mwili wako, atakufanya ufuate dhana za kimwili na kutekeleza maslahi ya kimwili—ila maneno ya Mungu yatakupa nuru na kukuangazia kwa ndani, na wakati huu itakuwa juu yako ikiwa utamfuata Mungu au utamfuata Shetani. Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu anawagusa watu ndani, na kuendeleza kazi Yake ndani yao, na kwa hivyo katika tukio lolote kuna vita: kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Mtu anashindwa kujua ama acheke au alie” (“Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila mara niliposoma kifungu hiki kutoka maneno ya Mungu, ningetafakari kuhusu yafuatayo: Je, kutenda ukweli ni kugumu kiasi hicho? Wakati watu hawauelewi ukweli, hawawezi kuutenda. Mara wanapouelewa, kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu hakutatosha? Je kungeweza kuwa kwenye uzito kweli kama “ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona”? Haikuwa hadi baadaye, kupitia uzoefu wangu halisi, kuwa niliona kwamba kutenda ukweli si rahisi kwa kweli. Aliyosema Mungu yanalingana kabisa na ukweli; hayajatiwa chumvi hata kidogo.

Muda fulani uliopita, nilihisi kuwa dada aliyefanya kazi nami alikuwa mwenye kiburi na kunidharau; sikuweza kujizuia ila kuzama katika hali isiyo sahihi. Nilianza kujiweka katika vikwazo kwa sababu yake. Sikuweza kulisahau jambo hili katika kazi yangu; nilikuwa mnyenyekevu katika maneno yangu na mwangalifu katika vitendo vyangu kiasi kwamba, baada ya muda mfupi, ningetazama sura yake wakati nilipozungumza au kufanya kitu, na sikuwa nikiubeba mzigo wa kazi yangu. Nilikuwa nikiishi gizani kabisa. Sikuweza kujinasua hata ingawa nilijua kuwa hali yangu ilikuwa hatari. Katikati ya mateso, nilimwomba Mungu mara kwa mara tena, na polepole nilipata kuwa na nuru na mwongozo wa Mungu ndani yangu:: Kuwa na mazungumzo ya dhati na dada yako, tafuta njia ya nuru. Lakini nilipofika kwa mlango wa dada yangu, nilikuwa na wazo tofauti: Dada yangu atafikiri nini nitakapozungumza kuihusu? Je, atasema kuwa kuna mambo mengi madogo mno akilini mwangu, mimi ni mzigo sana, mgumu sana kushughulika naye? Mara tu baada ya kuwa na wazo hili, ilikuwa ni kama kwamba nilikuwa nimeona ule mtazamo usio sawa katika macho yake, ule mtazamo wa kudharau. Ghafla, ujasiri wangu ulipotea tu na nikafifia, kana kwamba mwili wangu wote ulikuwa umekakamaa. kwa mara nyingine tena, maneno ya Mungu yaniletea nuru ya ndani: Ungekuwa na masuala mengi ya faragha uliyoyaona kuwa vigumu kuyazungumzia, ingekuwa vigumu kupambana kutoka katika giza. Ungekuwa radhi kuendelea hivyo? Nilijitia moyo kwa kimya: Kuwa mjasiri, kuwa mnyofu na wazi. Kutenda ukweli si kitu cha kuaibikia! Lakini wakati uo huo, hisia ya namna nyingine ilinivuta kwa ghafla: Usiseme kitu chochote—watu wengine labda wanafikiri kuwa uko sawa. Ikiwa utayazungumzia watafikiri kuwa una mambo mengi madogo mno akilini mwako na hawatakupenda tena. Wai! Ni afadhali kutosema chochote, basi! Nilipositasita kwa mara nyingine tena, Mungu aliniongoza tena: Kuwa mtu mwaminifu inamaanisha huwezi kuwa mwenye haya na hofu! Kupata nuru ya Mungu kulinisisimua, lakini kwa mshangao wangu, mara tu nilipopata nguvu kidogo, mawazo ya Shetani kwa mara nyingine tena yakafoka: Ukiyazungumzia watu wengine watajua hali yako halisi, na utakuwa mwenye taabu! Moyo wangu ghafla ukajikaza sana. Ilikuwa ni kwa njia hii ndio moyo wangu ulikuwa umevutwa huku na huko katika mapambano kati ya uzuri na hasi, nyeusi na nyeupe. Nilijua kwa uwazi: Mimi kutotaka kuzungumza ilikuwa ni haja ya kujiepusha na aibu na ubatili. Lakini kwa njia hii, hali yangu haingetatuliwa na haingekuwa na manufaa kwa kazi yangu. Kutafuta ushirika tu kutatua suala hili tu ndiyo ingekuwa na manufaa kwa kazi yangu na kuwa sambamba na mapenzi ya Mungu. Lakini wakati fikira hiyo ilinijia kuwa mara tu angejua, angeweza kuniheshimu kidogo zaidi kuliko awali, nilipoteza ujasiri wa kutenda ukweli. Nilihisi kama kwamba ningezungumza kuhusu ubaya wangu mwenyewe, singeweza kuendelea kuishi! Kwa muda mfupi nilifadhaishwa sana, na moyo wangu ulikuwa katika maumivu makubwa kama kwamba unachomwa na moto. Hii ilikuwa ngumu kama kwamba nilikuwa nimekabiliwa na uchaguzi wa uzima au kifo, na bila kujua nikalia, na yote ambayo ningefanya ni kumlilia Mungu moyoni mwangu bila kujiweza. Katika wakati huo wa kipeo, maneno ya Mungu kwa mara nyingine yalimemeteka katika akili yangu: “(Vijana) hawapaswi kuwa bila ukweli, wala kuficha unafiki na udhalimu…. Vijana wanapaswa kuwa na ujasiri wa kutoshindwa na ukandamizaji wa nguvu za giza na kubadili umuhimu wa uwepo wao” (“Maneno kwa Vijana na Wazee” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yaliniwezesha hatimaye kutuliza moyo wangu wenye wahaka: Haijalishi nini, siwezi tena kuwa chini ya dhihaka ya Shetani! Siwezi tena kumuasi Mungu; ni lazima nijinyime na kutenda ukweli. Mara nilipofanya uamuzi huo kutafuta dada yangu na kuwa na ushirika wa dhati naye, matokeo yalizidi matarajio yangu sana. Dada yangu hakukosa kunidharau tu, lakini alikiri upotovu wake mwenyewe, akatafakari na kugundua upungufu wake na kuniomba radhi, akisema kwamba katika siku za mbele shida inapotokea, tunapaswa kushiriki kuhusu ukweli mimi na yeye ili tupate kuelewana, kuona kutii ukweli kama kanuni yetu, kujifunza kutoka uwezo wa mwingine ili kufidia upungufu wetu binafsi, kufanya kazi ya kanisa pamoja vizuri. Hivi ndivyo jinsi mapambano hayo yasiyo na silaha yaliisha. Shida yangu ilikuwa imetatuliwa na moyo wangu kuchangamshwa. Nilipokumbuka mapambano makali katika moyo wangu wakati huo na kuonja mateso katika mapambano yaliyofanana na ya kufa na kupona, ni hapo tu ndipo nilijua jinsi masikitiko yangu ya kujiepushia aibu yalikuwa bure. Ilikuwa ni sehemu ya maisha yangu kiasi kwamba nilikuwa naishi gizani, nikikabiliana na mwito baada ya mwito kutoka kwa Mungu lakini sikuweza kujinasua. Niliuelewa ukweli lakini sikuweza kuutenda; kwa kweli nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani! Pia nilipata uzoefu kabisa kuwa kutenda ukweli na kuwa mtu mwaminifu si rahisi.

Ilikuwa tu baada ya kupitia haya ndiyo nilielewa maneno ya Mungu: “Kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, … ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona.” Maneno haya yalisemwa kuhusu hali potovu ya binadamu kwa sababu asili ya kishetani ya watu imekita mizizi kabisa katika mwili. Mwanadamu amefungwa na amezuiliwa nayo, na imekuwa maisha yetu. Tunapotenda ukweli, tunapoacha maisha yetu ya kimwili, mchakato huu ni sawa na kuzaliwa tena, kama kufa na kufufuliwa. Kwa kweli ni mashindano na mapambano ya kufa na kupona, na ni mchakato wa uchungu sana. Wakati kwa kweli hatujui asili yetu wenyewe na hatuna ridhaa ya kuteseka au kulipa gharama, bila shaka hatuwezi kutenda ukweli. Katika siku za nyuma nilidhani kuwa kutenda ukweli kulikuwa rahisi—hii ilikuwa ni kwa sababu sikuwa na ufahamu wa asili yangu potovu na sikujua jinsi upotovu wangu ulivyokuwa wa kina. Katika siku zijazo, niko radhi kujifahamu mwenyewe kwa kina zaidi kupitia uzoefu, kutafuta kutenda ukweli katika vitu vyote, na kujinyima!

Chanzo: Ushuhuda wa Injili | Mapambano ya Kufa na Kupona

Views: 134 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: mapenzi ya Mungu, Kanisa, Maneno ya Mungu, Ushuhuda wa Injili | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar