8:16 PM
Ushuhuda wa Maisha | Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini

Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini

Xiaohe Mji wa Puyang, Mkoa wa Henan

Hapo awali, kila wakati niliposoma maneno yaliyofichuliwa na Mungu kuhusu jinsi watu hawakubali ukweli, sikuamini kwamba maneno hayo yangetumika kwangu. Nilifurahia kula na kunywa neno la Mungu na kuwasiliana kuhusu neno la Mungu, na niliweza kukubali na kukiri kila kitu ambacho Mungu amesema kuwa ukweli—bila kujali jinsi kilivyoumiza moyo wangu au jinsi hakikuambatana na mawazo yangu. Aidha, bila kujali kiwango cha dosari kaka na dada zangu wangeonyesha, ningekikiri na kukikubali. Sikutafuta kujitetea mwenyewe, hivyo nilidhani kwamba nilikuwa mtu ambaye kwa hakika alikubali ukweli. Ni watu wale tu ambao hasa walikuwa wenye kiburi na majivuno na waliokuwa na mawazo kuhusu neno la Mungu, ambao hawangekiri kuwa neno la Mungu ni ukweli ndio ambao hawangekubali ukweli. Nilikuwa kwa kawaida nikifikiri hivi hadi siku moja nilipokuwa nikisikiliza “Ushirika na Mahubiri kuhusu Kuingia kwa Maisha”, ndipo nilipoelewa kweli kilichomaanisha kukubali ukweli.

Yanasema: “Haitoshi tu kukiri kuwa neno la Mungu ni ukweli, ni lazima ulikubali ndani ya moyo wako na uruhusu ukweli kuwa na nafasi katika maisha yako na utawale. Ni lazima ukite mizizi ndani ya moyo wako na kuwa maisha yako. Haya ndiyo maonyesho ya kweli ya kukubali ukweli. … Je, inamaanisha nini kuukubali ndani ya moyo wako? Moyo wako unakiri kuwa sentensi hii ni ukweli na una utambuzi halisi wa ukweli. Basi ni lazima ukubali ukweli huu kikamilifu na uuruhusu kuwa na nafasi katika moyo wako na ukite mizizi. Baadaye, ni lazima uishi kulingana na ukweli huu na utazame vitu kulingana na ukweli huu. Hii ni kukubali ukweli. … Kula na kunywa neno la Mungu na kukiri kuwa neno la Mungu ni ukweli haimaanishi kuwa mtu amekubali ukweli. Badala yake, ni kutambua kikamilifu kiini cha ukweli katika neno la Mungu na kuukubali katika moyo wako. Ni kukana kikamilifu mawazo yako kuhusu Mungu na fikira potovu za hapo awali ulizoshikilia ili kukubali neno la Mungu kama ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Hii ni kwa hakika kukubali ukweli” (“Jinsi ya Kufahamu kuwa Kristo Ndiye Ukweli, Njia na Uzima” katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha II). Niliposikia hili, moyo wangu ulitetemeka mara moja. Hivyo, hilo silo nililofikiri kuhusu kukubali ukweli. Niliyasikiza kwa makini mara nyingine tena, na kupitia kutafakari na kutafuta, hatimaye nikaelewa kilichomaanisha kukubali ukweli. Kuweza kukiri kwa kinywa kuwa neno la Mungu ni ukweli au kuweza kukubali dosari zilizotajwa na watu wengine haikuwa kwa kweli kukubali ukweli kama nilivyokuwa nimefikiri. Kwa hakika kukubali ukweli humaanisha sio tu kukubali kuwa neno la Mungu ni ukweli, ni pia kutambua kiini cha ukweli na kuukubali kikamilifu ndani ya moyo wako. Ni kukataa kabisa mawazo, mitazamo na fikira potovu zako za hapo awali. Ni kukubali ukweli kukita mizizi katika moyo wako na kuweza kuishi kulingana na ukweli. Hii ni kukubali ukweli kwa hakika.

Baada ya kuelewa haya yote, nilianza kutafakari kujihusu mimi mwenyewe: Ninaamini kuwa mimi ni mtu ambaye hukubali ukweli, lakini je, nimekubali neno la Mungu katika moyo wangu? Je, ukweli unatawala katika moyo wangu? Je, nimekataa mawazo yaliyopita na fikira potovu ambazo zimekuwa katika moyo wangu? Baada ya kujichunguza mimi mwenyewe kwa makini, niligundua kuwa sikuwa nimefanya jambo lolote kati ya haya, Kwa mfano: Mungu amefichua kuwa hakuna upendo wa kweli kati ya wanadamu, na kila mmoja hutafuta kujinufaisha kutoka kwa mwingine. Hata ingawa nilikiri kwa kunena ukweli ambao Mungu amenena, kila wakati nilihisi katika moyo wangu kuwa bibi, watoto na wazazi wangu na mimi mwenyewe sote tulikuwa na upendo wa kweli kwa kila mmoja wetu. Midomo yangu ilikiri ukweli kuwa Mungu hamfanyi mwanadamu kukamilika kwa kuzingatia vyeo vyao, lakini ni kulingana na iwapo wana ukweli au hawana; lakini moyo wangu bado ulishikilia mitazamo yangu ya kibinafsi kuwa jinsi cheo changu kilikuwa cha juu ndivyo Mungu angenifanya mkamilifu zaidi, jinsi cheo changu kilivyokuwa cha juu zaidi ndivyo watu wengi zaidi wangeniheshimu. Nilifikiri kuwa Mungu pia angefurahishwa na mimi. Hivyo, kila wakati nilikuwa na hofu kuhusu kupata au kupoteza cheo, na kwa kawaida nilikuwa na wasiwasi kuhusu jambo hili. Nilikiri kwa kinywa changu kuwa Mungu alisema kwamba shida na usafishaji, na ushughulikiaji na upogoaji ni upendo wa Mungu, ni muhimu zaidi kwa maisha ya mwanadamu. Lakini sikutafuta kuelewa kiini cha ukweli wa maneno haya wala kutambua jinsi Mungu hupenda mwanadamu na jinsi ambavyo upendo wa Mungu hudhihirika, hadi kwa kiwango kuwa sikuwa tayari kumkubali Mungu kuwatumia watu, mambo, na vitu ambavyo havikuwa vinaambatana na mawazo yangu kunisafisha na kunishughulikia, hata kwa kiwango kuwa ningelalamika na kunung’unika kuvihusu. Nilifahamu kuwa ombi la Mungu la watu kuwa waaminifu lilikuwa muhimu, lakini sikusisitiza kuliweka katika vitendo au kuingia ndani yake. Bado ningesema uongo mara nyingi na kudanganya kwa sababu ya heshima yangu mwenyewe. Baada ya hiyo, sikuwa tayari kuonyesha ukweli kwa wazi. Nilipokumbana na tatizo ambalo lingehitaji shida ya kimwili nilipokuwa nikitekeleza wajibu wangu, ningeanza kufanya kazi kwa uzembe na singeweza kujitolea mimi mwenyewe kwa majukumu yangu. Mdomo wangu ungekubali kuwa Mungu alisema tutafute mapenzi yake katika mambo yote na tufanye kulingana na matakwa ya Mungu, lakini katika maisha halisi nilipokumbana na mambo, nilifanya mambo kama nilivyopendelea na kulingana na mapenzi yangu. Nilimpuuza Mungu kabisa. Pia, wakati ambapo watu wengine wangeonyesha dosari zangu wakisema kuwa nilikuwa mwenye kiburi sana na kuwa ningefanya mambo kwa njia yangu mwenyewe, moyo wangu haungekubali ukosoaji wao. Lakini nilikuwa naogopa kuwa wengine wangesema kuwa sikukubali ukweli, hivyo ningekubali kwa ishara ya kichwa na kulikiri kinyume na mapenzi yangu. Lakini kwa hakika, sikuzingatia ukosoaji wao. Kulikuwa na mambo mengi kunihusu yaliyoonyesha kuwa sikuwa nimekubali ukweli. Lakini nilipoona kuwa neno la Mungu hufichua kuwa watu wote hawakubali ukweli, sikukubali neno la Mungu kama ukweli, na sikujaribu kuelewa kiini cha neno la Mungu na kujichunguza mimi mwenyewe. Badala yake, nilidhani kuwa nilikuwa wa kipekee hivyo kutopaswa kufuata neno la Mungu na kujichukulia mimi mwenyewe kuwa mtu ambaye alikuwa amekubali ukweli. Je, haya hayakuwa maonyesho ya dhahiri zaidi ya kutokubali ukweli? Wakati huo, niliona kuwa nilikuwa mtu ambaye hakukubali ukweli kwa njia yoyote. Niliyokuwa nikiyaita maonyesho ya kukubali ukweli yalikuwa matendo ya nje kabisa; yalikuwa uongo uliofichika ambao hata haukuwa karibu na kukubali ukweli. Sikuwa ninajifahamu mimi mwenyewe, kwa hakika sikujifahamu mimi mwenyewe! Baada ya kufahamu hili, singejizuia kuwa na uoga. Nilijua kuwa nilikuwa nimemwamini Mungu miaka hii yote ilhali nilikuwa nimeishi nje ya maneno Yake. Kwa hakika sikuwa nimepokea hukumu na adabu ya Mungu. Nilikuwa tu mtu ambaye hamwamini Mungu ndani ya moyo wangu bila Mungu na bila ukweli katika maisha. Iwapo ningeendelea kuamini kwa njia hii, neno la Mungu kamwe halingeweza kuwa maisha yangu. Kamwe singeweza kujiondoa kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuokolewa na kufanywa kuwa mkamilifu. Kinyume chake, ningelaaniwa na Mungu, na ningeangukia adhabu ya Mungu.

Mungu asifiwe kwa kuniongoza na kuniruhusu kuelewa kinachomaanisha kwa hakika kukubali ukweli; kwa kuniruhusu kuona kuwa maarifa na utendaji wangu ya hapo awali yalikuwa ya kiupumbavu sana na hayakuwa yanaambatana na mapenzi ya Mungu. Ninataka kuanza upya na kuweka pamoja juhudi zangu katika kukubali kiini cha ukweli katika moyo wangu katika yale yote ambayo Mungu amesema na kuyatekeleza katika utendaji wangu. Ninataka kuweza kuishi kulingana na ukweli, kuwa mtu ambaye kwa hakika hukubali ukweli.

Chanzo:  Ushuhuda wa Maisha | Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini

Views: 101 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: neno la Mungu, ukweli, matakwa ya Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar