6:50 PM
Utendaji (4)

Amani na furaha Nizungumziayo leo sio sawa na yale ambayo unaamini na kufahamu. Ulikuwa ukifikiri kwamba amani na furaha yalimaanisha kuwa na furaha siku nzima, kutokuwako kwa magonjwa au misiba katika familia yako, kuwa mwenye furaha kila mara ndani ya moyo wako, bila hisia zozote za huzuni, na furaha isiyoelezeka ndani yako haijalishi kiasi cha urefu wa maisha yako mwenyewe. Hilo lilikuwa ni pamoja na nyongeza katika mshahara wa mume wako na mwanao kuingia katika chuo kikuu karibuni. Kufikiria juu ya mambo haya, ulimwomba Mungu, uliona kwamba neema ya Mungu ilikuwa kuu sana, ulikuwa na furaha sana mpaka ukawa na tabasamu kubwa, na hungeacha kumshukuru Mungu. Amani na furaha kama hiyo sio amani na furaha halisi, wala sio amani na furaha ya kuwa na kuwepo kwa Roho Mtakatifu. Ni amani na furaha ya kuridhika kwa mwili wako. Unapaswa kufahamu enzi hii ni gani leo; sasa sio Enzi ya Neema, na sio tena wakati ambapo unatafuta kulijaza tumbo lako kwa mkate. Unaweza kufurahi mno kwa sababu mambo yote yanaendelea vyema katika familia yako, lakini maisha yako yako katika hali mahututi—na hivyo, haijalishi vile furaha yako ilivyo kuu, Roho Mtakatifu hayuko nawe. Kuwa na kuwepo kwa Roho Mtakatifu ni rahisi: fanya unachopaswa kufanywa kwa kufaa, tekeleza wajibu na kazi ya mwanadamu vizuri, uweze kujiandaa mwenyewe na vitu unavyohitaji na ufidie upungufu wako. Ikiwa kila mara unalemewa na mzigo wa maisha yako, na unafurahi kwa sababu umetambua ukweli au umefahamu kazi ya Mungu ya leo, huku kweli ni kuwa na kuwepo kwa Roho Mtakatifu. Unaweza kupatwa na wasiwasi unapopitia kitu fulani ambacho hujui namna ya kukipitia, au wakati ambapo huwezi kutambua ukweli unaowasilishwa kwa karibu—hili linathibitisha kwamba Roho Mtakatifu yuko nawe; hii ni hali ya kawaida katika tukio la maisha. Lazima uelewe tofauti kati ya kuwa na kuwepo kwa Roho Mtakatifu na kutokuwa na kuwepo kwa Roho Mtakatifu, na usiwe wa kawaida mno katika mtazamo wako wa hili.

Hapo awali, ilisemwa kwamba kuwa na kuwepo kwa Roho Mtakatifu na kazi ya Roho Mtakatifu ni tofauti. Hali ya kawaida ya kuwa na kuwepo kwa Roho Mtakatifu inadhihirishwa katika kuwa na mawazo ya kawaida, urazini wa kawaida, na ubinadamu wa kawaida. Tabia ya mtu itabaki kama ilivyokuwa, lakini ndani yake kutakuwa na amani, na nje atakuwa na staha ya mtakatifu. Huu utakuwa wakati ambapo Roho Mtakatifu yuko naye. Wakati ambapo Roho Mtakatifu yuko nao, watu huwa na mawazo ya kawaida. Wao hula wanapotakiwa kufanya hivyo, kama wana njaa wao hutaka chakula, kama wana kiu wao hutaka kunywa maji .... madhihirisho kama haya ya ubinadamu wa kawaida sio kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu, hayo ni mawazo ya kawaida ya watu na hali ya kawaida ya kuwa na kuwepo kwa Roho Mtakatifu. Watu wengine huamini kimakosa kwamba wale walio na kuwepo kwa Roho Mtakatifu huwa hawahisi njaa, kwamba huwa hawahisi uchovu, na zaidi ya hayo, huwa hawana fikira yoyote kwa familia, wakiwa takriban wamejitenga kabisa kutoka kwa mwili. Kwa kweli, kadri Roho Mtakatifu alivyo na watu, ndivyo wanakuwa wa kawaida zaidi. Wanajua kuteseka kwa ajili ya Mungu, kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, na kuwa waaminifu kwa Mungu, wanajua kutelekeza, na, zaidi ya hayo, wanajua kula na kuvaa mavazi. Kwa maneno mengine, hawajapoteza chochote cha ubinadamu wa kawaida wanachopaswa kuwa nacho na, badala yake, wanakuwa hasa na busara. Wakati mwingine, wakati ambapo wanasoma vitabu na kuitafakari kazi ya Mungu, kuna imani ndani ya mioyo yao na wako radhi kufuatilia ukweli. Kwa kawaida, kazi ya Roho Mtakatifu inategemezwa juu ya msingi huu. Kama watu hawana mawazo ya kawaida, basi hawana urazini, ambayo si hali ya kawaida. Watu wanapokuwa na mawazo ya kawaida na Roho Mtakatifu yuko nao, bila kuzuilika wao huwa na urazini wa mwanadamu wa kawaida, kumaanisha wana hali ya kawaida. Katika kupitia kazi ya Mungu, kuna nyakati fulani za kazi ya Roho Mtakatifu, wakati ambapo Roho Mtakatifu yuko mara kwa mara nyakati zote. Maadamu urazini wa watu ni ya kawaida, hali zao ni za kawaida, na mawazo ndani yao ni ya kawaida, basi Roho Mtakatifu yuko nao kwa hakika. Wakati ambapo busara na mawazo ya watu sio ya kawaida, basi ubinadamu wao sio wa kawaida. Ikiwa, wakati huu, kazi ya Roho Mtakatifu iko ndani yako, basi Roho Mtakatifu atakuwa nawe pia kwa hakika. Lakini ikiwa Roho Mtakatifu yuko nawe, sio lazima kwamba kazi ya Roho Mtakatifu itakuwa ndani yako, kwani Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa nyakati maalumu. Kuwa na kuwepo kwa Roho Mtakatifu kunaweza tu kudumisha kuishi kwa kawaida kwa watu, lakini Roho Mtakatifu hufanya kazi tu katika nyakati fulani. Kwa mfano, kama wewe ni mmoja wa wale wanaomfanyia Mungu kazi, unapoenda kwa makanisa Roho Mtakatifu hukupa nuru kwa maneno fulani, na huu ndio wakati ambapo Roho Mtakatifu anafanya kazi. Wakati mwingine unasoma na Roho Mtakatifu anakupa nuru kwa maneno fulani, na unajikuta hasa unaweza kuyatathmini dhidi ya uzoefu wako mwenyewe, na kukupa ufahamu mkuu wa hali yako mwenyewe; umepata nuru, na hii pia ni kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati mwingine, Ninapozungumza na ninyi husikiliza hapa chini, mnaweza kuyatathmini maneno Yangu dhidi ya hali zenu wenyewe, wakati mwingine ninyi huguswa au kutiwa moyo, na hii ni kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wengine husema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao nyakati zote. Hili haliwezekani. Ikiwa wangesema kwamba Roho Mtakatifu yuko nao kila mara, hilo lingekuwa la kweli. Ikiwa wangesema kwamba fikira na hisi zao ni za kawaida nyakati zote, hilo pia lingekuwa la kweli, na lingeonyesha kwamba Roho Mtakatifu yuko nao. Ikiwa wanasema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao kila mara, kwamba wanapata nuru kutoka kwa Mungu na kuguswa na Roho Mtakatifu kila wakati, na wanapata ufahamu mpya kila wakati, basi hili si la kawaida. Ni la rohoni kabisa! Bila tashwishi yoyote, watu kama hao ni pepo wabaya! Hata wakati ambapo Roho wa Mungu huja ndani ya mwili, kuna nyakati ambapo lazima Ale, na lazima Apumzike—sembuse mwanadamu. Wale ambao wamemilikiwa na pepo wabaya huonekana kutokuwa na hisia na udhaifu wa mwili. Wanaweza kutelekeza na kuacha kila kitu, wao ni wenye uwezo wa kustahimili mateso na hawahisi uchovu hata kidogo sana, kana kwamba wamevuka mipaka ya mwili. Je, hili silo la rohoni kabisa? Kazi ya pepo mwovu ni ya rohoni, na mambo haya ni yasiyofikiwa na mwanadamu. Wale wasioweza kutofautisha huwa na wivu wanapoona watu kama hao, na husema kwamba imani yao katika Mungu ni thabiti sana, na wana imani kubwa, na kwamba wao huwa si wadhaifu kamwe. Kwa kweli, hili ni dhihirisho la kazi ya pepo mwovu. Hiyo ni kwa sababu watu wa kawaida huwa na udhaifu wa binadamu usioepukika; hii ni hali ya kawaida ya wale walio na kuwepo kwa Roho Mtakatifu.

Ni nini maana ya kusimama imara katika ushuhuda wa mtu? Watu wengine husema kwamba wao hufuata tu hivi na hawajishughulishi na kama wana uwezo wa kupata uzima, na hawafuatilii uzima, lakini wala hawarudi nyuma. Wanakubali tu kwamba hii hatua ya kazi hutekelezwa na Mungu. Katika haya yote, je, hawajashindwa katika ushuhuda wao? Wao hawana hata ushuhuda wa kushindwa. Wale ambao wameshindwa hufuata haijalishi mengine yote na wanaweza kuufuatilia uzima. Wao hawaamini tu katika Mungu wa vitendo, lakini pia hujua kuifuata mipango yote ya Mungu. Hao ndio huwa na ushuhuda. Wale wasiokuwa na ushuhuda hawajawahi kuufuatilia uzima na bado wanafuata kwa kumaliza jambo kwa kubahatisha. Unaweza kufuata, lakini hili halimaanishi kwamba umeshindwa, kwani hujui lolote kuhusu kazi ya Mungu leo. Kushindwa ni kwenye masharti. Sio wote wanaofuata wameshindwa, kwani ndani ya moyo wako hufahamu chochote kuhusu kwa nini ni lazima umfuate Mungu wa leo, wala hujui vile umefaulu hadi leo, nani amekusaidia wewe mpaka leo. Katika imani yao kwa Mungu, watu wengine hutumia siku nzima katika kiwewe; hivyo, kufuata si lazima kumaanishe kwamba una ushuhuda. Ushuhuda wa kweli ni nini hasa? Ushuhuda uliozungumziwa hapa una sehemu mbili: Moja ni ushuhuda kwa kuweza kushindwa, na ya pili ni ushuhuda kwa kuweza kufanywa mkamilifu (ambako, kwa kawaida, ni ushuhuda unaofuata majaribio makuu zaidi na majonzi ya siku za usoni). Kwa maneno mengine, ikiwa unaweza kusimama imara wakati wa majonzi na majaribio, basi umekuwa na hatua ya pili ya ushuhuda. Kilicho cha maana sana leo ni hatua ya kwanza ya ushuhuda: kuweza kusimama imara wakati wa kila namna ya majaribio ya kuadibu na hukumu. Huu ni ushuhuda kwa kushindwa. Hilo ni kwa sababu leo ni wakati wa ushindi. (Unapaswa kujua kwamba leo ni wakati wa kazi ya Mungu duniani; kazi kuu duniani ya Mungu aliyepata mwili ni matumizi ya hukumu na kuadibu kushinda hili kundi la watu duniani wanaomfuata Yeye.) Kama una uwezo wa kushuhudia kwa kushindwa au la hakutegemei tu kama unaweza kufuata hadi mwisho, lakini, la muhimu zaidi, kama, unapopitia kila hatua ya kazi ya Mungu, una uwezo wa ufahamu wa kweli wa kuadibu na hukumu katika kazi hii, na kama wewe kweli unaiona kazi hii yote. Si jambo ambalo utaweza kulimaliza kwa kubahatisha ikiwa utafuata hadi mwisho kabisa. Lazima uweze kuwa radhi kusalimu amri wakati wa kila namna ya kuadibu na hukumu, lazima uwe na uwezo wa ufahamu wa kweli wa kila hatua ya kazi upitiayo, na lazima uweze kupata ufahamu wa, na utiifu kwa tabia ya Mungu. Huu ni ushuhuda wa msingi wa kushindwa unaotakiwa kwako. Ushuhuda wa kushindwa kimsingi unahusu ufahamu wako wa kupata mwili kwa Mungu. Lenye maana sana, hatua hii ya ushuhuda ni kwa kupata mwili kwa Mungu. Haijalishi kile ambacho unafanya au kusema mbele ya watu wa ulimwengu au wale wanaotawala; kilicho na maana kuliko vyote ni kama unaweza kuyatii maneno yote kutoka kinywani mwa Mungu na kazi Yake yote. Kwa hivyo, hatua hii ya ushuhuda inaelekezwa kwa Shetani na maadui wote wa Mungu—pepo na wenye uadui ambao hawaamini kwamba Mungu atakuwa mwili mara ya pili na kuja kufanya hata kazi kubwa zaidi, na zaidi ya hayo, hawaamini katika ukweli wa kurudi kwa Mungu kwa mwili. Kwa maneno mengine, inaelekezwa kwa wapinga Kristo wote—maadui wote wasioamini katika kupata mwili kwa Mungu.

Kumkosa Mungu na kumtamani sana Mungu hakuthibitishi kwamba umeshindwa na Mungu; hilo linategemea kama unaamini kwamba Yeye ni Neno lililopata mwili, kama unaamini kwamba Neno limepata mwili, na kama unaamini kwamba Roho amekuwa Neno, na Neno limeonekana katika mwili. Huu ndio ushuhuda muhimu. Haijalishi vile wewe unafuata, wala vile unavyojitumia mwenyewe; kilicho muhimu ni kama wewe unaweza kugundua kutoka kwa ubinadamu huu wa kawaida kwamba Neno limepata mwili na Roho wa kweli amepatikana katika mwili—kwamba ukweli wote, uzima, na njia umekuja katika mwili, na Roho amewasili duniani na katika mwili kwa kweli. Ingawa, kijuujuu, hili linaonekana ni tofauti na utungaji mimba kwa Roho Mtakatifu, katika kazi hii mnaweza kuona kwa dhahiri zaidi kwamba Roho tayari amepatikana katika mwili, na, zaidi ya hayo, kwamba Neno limepata mwili, na Neno limeonekana katika mwili, na unaweza kufahamu maana ya kweli ya maneno haya: Hapo mwanzo kulikuwako na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Zaidi ya hayo, lazima ufahamu maneno ya leo ni Mungu, na lazima utazame maneno yakipata mwili. Huu ni ushuhuda bora zaidi unaoweza kuwa nao. Hili linathibitisha kwamba una ufahamu wa kweli wa Mungu kupata mwili—wewe huwezi tu kumjua na kumchambua Yeye, lakini pia unajua kwamba njia unayoifuata leo ni njia ya uzima, na njia ya ukweli. Yesu alifanya hatua ya kazi ambayo ilitimiza tu kiini cha “Neno alikuwako kwa Mungu”: Ukweli wa Mungu ulikuwako kwa Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa na mwili na alikuwa asiyetenganishwa kutoka Kwake, yaani, mwili wa Mungu mwenye mwili ulikuwa na Roho wa Mungu, ambalo ni thibitisho kuu zaidi kwamba Yesu mwenye mwili alikuwa aliyepata mwili wa kwanza wa Mungu. Hatua hii ya kazi ilitimiza maana ya ndani ya “Neno lapata mwili,” ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya “naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu,” na inakuruhusu wewe uamini kwa uthabiti maneno haya kwamba “Hapo mwanzo kulikuwako na Neno.” Ambalo ni kusema, wakati wa uumbaji Mungu alikuwa na maneno, Maneno Yake yalikuwa na Yeye na yasiyotenganishwa kutoka Kwake, na enzi ya mwisho inafanya nguvu na mamlaka ya maneno Yake yawe hata wazi zaidi, na kumkubalia mwanadamu kuyaona maneno Yake yote—kuyasikia maneno Yake yote. Hiyo ndiyo kazi ya enzi ya mwisho. Lazima uyajue mambo haya yote kabisa. Si suala la kuujua mwili, bali la kuujua mwili na Neno. Hiki ndicho kile unachotakiwa kushuhudia, kile ambacho kila mtu lazima akijue. Kwa sababu hii ni kazi ya kupata mwili kwa pili—na mara ya mwisho ambapo Mungu anapata mwili—inakamilisha kwa ukamilifu umuhimu wa kupata mwili, inatekeleza kabisa na kutoa kazi yote ya Mungu katika mwili, na kumaliza enzi ya Mungu kuwa katika mwili. Hivyo, lazima ujue maana ya kupata mwili. Haijalishi unavyokimbia huku na huko, au vile unavyotekeleza vizuri masuala mengine ya nje; kilicho na maana ni kama unaweza kutii kwa kweli mbele ya Mungu mwenye mwili na kuitoa nafsi yako yote kwa Mungu, na kutii maneno yote yatokayo kinywani Mwake. Hili ndilo unalopaswa kufanya, na unalopaswa kutii.

Ushuhuda wa siku za mwisho ni ushuhuda kwa kama unaweza kufanywa mkamilifu au la—ambako ni kusema, ushuhuda wa mwisho ni kwamba, kwa kuwa umekubali maneno yote yatokayo kinywani mwa Mungu mwenye mwili, na kwa kuwa umekuja kupata ufahamu wa Mungu na kuwa na hakika kumhusu Yeye, unaishi kwa kudhihirisha maneno yote kutoka kinywani mwa Mungu, na kutimiza masharti ambayo Mungu anakwambia—mtindo wa Petro na imani ya Ayubu, kiasi kwamba unaweza kutii hadi kufa, kujitoa mwenyewe kabisa Kwake, na hatimaye kutimiza mfano wa mwanadamu ambao ni wa juu ya kiwango kilichowekwa—kinachomaanisha mfano wa mtu ambaye ameshindwa, ameadibiwa, amehukumiwa, na kufanywa mkamilifu. Huu ni ushuhuda unaopaswa kuwa na mtu ambaye hatimaye amefanywa mkamilifu. Hizi ni hatua mbili za ushuhuda mnaopaswa kuwa nao, na zinahusiana, kila moja ni ya msingi. Lakini kuna jambo moja unalotakiwa kujua: Ushuhuda Ninaotaka kutoka kwako leo hauelekezwi kwa watu wa ulimwengu, wala kwa mtu yeyote mmoja, lakini kwa kile ambacho Nitakacho kutoka kwako. Kinatathminiwa na kama unaweza kuniridhisha Mimi, na kama unaweza kutimiza kabisa viwango vya masharti Yangu kwa kila mmoja wenu. Hili ndilo mnalopaswa kufahamu.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

 

Views: 81 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Matamshi ya Kristo, Mungu Kupata Mwili | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar