6:49 PM
Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?

Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu. Una uwezo wa kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu kila unapofanya chochote; hata kama huelewi mapenzi ya Mungu, bado ni lazima utimize wajibu na majukumu yako kadri ya uwezo wako. Hujachelewa sana kusubiri mapenzi ya Mungu yafichuliwe kwako na kisha kuyaweka katika vitendo. Wakati uhusiano wako na Mungu umekuwa wa kawaida, basi pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu. Kila kitu kimejengwa juu ya msingi wa maneno ya Mungu. Kupitia katika kula na kunywa maneno ya Mungu, tenda kulingana na mahitaji ya Mungu, weka sawa maoni yako, usitende mambo yanayompinga Mungu au kuingilia kati mambo ya kanisa. Usifanye vitu visivyo na manufaa kwa maisha ya ndugu, usiseme maneno yasiyosaidia wengine, usifanye vitu vya kufedhehesha. Kuwa mwadilifu na mwenye heshima unapofanya mambo yote na kuyafanya ya kupendeza mbele ya Mungu. Hata ingawa kutakuwa na nyakati ambazo mwili ni dhaifu, unaweza kushikiza umuhimu mkubwa kabisa kwa kufaidi familia ya Mungu, kutotamani faida yako mwenyewe, na kutekeleza haki. Ikiwa unaweza kutenda kwa njia hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.

Kila unapofanya chochote, lazima uchunguze iwapo motisha yako ni sahihi. Ikiwa unaweza kutenda kulingana na matakwa ya Mungu, basi uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida. Hiki ndicho kigezo cha chini zaidi. Iwapo, unapochunguza motisha yako, kunatokea zile zisizo sahihi, na iwapo unaweza kuzikwepa na kutenda kulingana na maneno ya Mungu, basi utakuwa mtu ambaye ni mwema mbele ya Mungu, kitu ambacho kitaonyesha kuwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, na kwamba kila unachofanya ni kwa ajili ya Mungu, na sio kwa sababu yako binafsi. Ni lazima uuweke moyo wako sawa kila unapofanya ama kusema chochote, uwe mwenye haki katika matendo yako, na usiongozwe na hisia zako, au utende kulingana na mapenzi yako: Haya ndiyo maadili ambayo wale wanaoamini katika Mungu wanatenda kulingana nayo. Motisha za mtu na kimo chake vinaweza kufichuliwa katika kitu kidogo, na hivyo, kwa watu kuingia kwa njia ya kufanywa wakamilifu na Mungu, ni lazima kwanza wasuluhishe motisha yao wenyewe na uhusiano wao na Mungu. Ni pale ambapo tu uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida ndipo utaweza kufanywa mkamilifu na Mungu, na ni hapo tu ndipo ushughulikiaji, upogoaji, nidhamu, na usafishaji wa Mungu kwako utaweza kupata matokeo yanayotakiwa. Hiyo kusema, watu wanaweza kuwa na Mungu mioyoni mwao, wasitafute maslahi binafsi, wasifikirie kuhusu maisha yao binafsi ya baadaye (ikirejelea kufikiri juu ya mwili), lakini badala yake wanabeba mzigo wa kuingia katika maisha, wanajitahidi wawezavyo kufuatilia ukweli, na kuitii kazi ya Mungu. Kwa namna hii, makusudi unayoyatafuta ni sahihi, na uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Inaweza kusemwa kwamba kuutengeneza uhusiano wako na Mungu ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia kwako katika safari ya kiroho. Ingawa hatima yako iko mikononi mwa Mungu, na imeshaamuliwa kabla na Mungu, na haiwezi kubadilishwa na wewe mwenyewe, kwamba unaweza au huwezi kufanywa mkamilifu au kupatwa na Mungu kunategemea na kama uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au la. Pengine kuna sehemu ndani yako ambazo ni dhaifu au zenye kutotii—lakini bora tu mtazamo wako wa nje ni sawa na motisha yako ni sahihi, na bora tu umeuweka uhusiano wako na Mungu sawa na kuufanya wa kawaida, basi utafuzu kufanywa mkamilifu na Mungu. Iwapo huna uhusiano sahihi na Mungu, na unatenda kwa ajili ya mwili, au familia yako, basi haijalishi kiwango cha kazi unayofanya kwa bidii, itakuwa bure. Iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, basi kila kitu kingine kitakuwa sawa. Mungu haangalii chochote kingine, bali anaangalia tu iwapo mitazamo yako kwa kuamini kwa Mungu ni sawa: unayemwamini, ni kwa ajili ya nani unaamini, na ni kwa nini unaamini. Iwapo unaweza kuona vitu hivi kwa udhahiri, na unaweza kuweka mitazamo yako iwe sawa na kuweza kutenda, basi maisha yako yatapiga hatua, na una uhakika wa kuweza kuingia kwenye njia sahihi. Iwapo uhusiano wako na Mungu sio wa kawaida, na mitazamo yako kwa kuamini katika Mungu inakiuka maadili, basi haya yatazuia mengine yote. Haijalishi jinsi unavyoamini katika Mungu, hutafaidi chochote. Iwapo tu uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida ndipo utasifiwa na Mungu unapoupa mwili kisogo, unapoomba, unapoteseka, unapostahimili, unapotii, unapowasaidia ndugu na dada zako, unaweka juhudi zaidi kwa Mungu, na kadhalika. Iwe kitu unachofanya kina thamani na umuhimu au hakina hutegemea iwapo makusudi yako ni sahihi na iwapo mitazamo yako ni sahihi. Siku hizi, imani ya watu wengi kwa Mungu ni kama kutazama saa kubwa huku vichwa vyao vikiwa vimeelekezwa upande mmoja—mitazamo yao imekengeuka. Kila kitu kitakuwa kizuri ikiwa mwelekeo mpya unaweza kufanyika hapa, kila kitu kitakuwa sawa ikiwa hili litatatuliwa, wakati hakutafanyika kitu ikiwa hili halitatatuliwa. Baadhi ya watu wanakuwa na tabia nzuri katika uwepo Wangu, lakini nyuma Yangu kile wanachofanya ni kupinga. Haya ni maonyesho yaliyopotoka na ya udanganyifu na aina hii ya mtu ni mtumwa wa Shetani, ni mfano halisi wa namna ile ile ya Shetani kumjaribu Mungu. Wewe ni mtu sahihi tu ikiwa unaweza kuitii kazi Yangu na maneno Yangu. Ilimradi unaweza kula na kunywa maneno ya Mungu, ilimradi kila kitu unachofanya kinapendeza mbele ya Mungu, ilimradi hufanyi mambo ya aibu, usifanye mambo ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya watu, ilimradi unaishi katika mwanga, hunyonywi na Shetani, basi uhusiano wako na Mungu utawekwa sawa.

Katika kumwamini Mungu, makusudi na mitazamo yako yanapaswa kuwekwa sawa; unapaswa kuwa na ufahamu sahihi na utendeaji sahihi wa maneno ya Mungu, kazi ya Mungu, mazingira yaliyopangwa na Mungu, mtu aliyeshuhudiwa na Mungu, na wa Mungu wa vitendo. Hupaswi kutenda kulingana na mawazo yako binafsi, au kufanya mipango yako midogo mwenyewe. Unapaswa kuweza kutafuta ukweli katika kila kitu na kusimama katika sehemu yako kama uumbaji wa Mungu na kuzitii kazi zote za Mungu. Kama unataka kutafuta kukamilishwa na Mungu na kuingia katika njia sahihi ya maisha, basi moyo wako siku zote unapaswa kuishi katika uwepo wa Mungu, usiwe fisadi, usimfuate Shetani, usimwachie Shetani fursa yoyote kufanya kazi yake, na usimruhusu Shetani kukutumia. Unapaswa kujitoa kikamilifu kwa Mungu na kumwacha Mungu akutawale.

Upo radhi kuwa mtumishi wa Shetani? Upo radhi kunyonywa na Shetani? Je, unamwamini Mungu na kumtafuta Mungu ili kwamba uweze kukamilishwa na Yeye, au ni ili uwe foili[a] katika kazi ya Mungu? Je, upo radhi kupatwa na Mungu na kuishi maisha ya maana, au upo radhi kuishi maisha tupu na yasiyo na thamani? Upo radhi kutumiwa na Mungu, au kunyonywa na Shetani? Upo radhi kuacha maneno ya Mungu na ukweli kukujaza, au kuacha dhambi na Shetani kukujaza? Litafakari na kulipima hili. Katika maisha yako ya kila siku, unapaswa kuyaelewa maneno hayo uyasemayo na mambo hayo uyafanyayo ambayo yatasababisha uhusiano wako na Mungu kuwa usio wa kawaida, halafu ujirekebishe na kuingia katika tabia sahihi. Yachunguze maneno yako, vitendo vyako, kila mwenendo wako, na fikra zako na mawazo wakati wote. Ielewe hali yako ya kweli na ingia katika njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwa njia hii tu ndipo unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Kwa kupima iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kurekebisha makusudi yako, kuielewa asili na kiini cha mwanadamu, na kujielewa mwenyewe kweli; kupitia hili, utaweza kuingia katika uzoefu halisi, na kujinyima kwa kweli, na kupata tamaa ya kutii. Katika masuala hayo kama unapokuwa unapitia iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kupata fursa za kukamilishwa na Mungu, utaweza kuelewa hali nyingi, ambazo kwazo Roho Mtakatifu Anafanya kazi, na utaweza kubaini mengi ya udanganyifu na njama za Shetani. Ni kupitia njia hii tu ndipo unaweza kukamilishwa na Mungu. Unaweka uhusiano wako na Mungu sawa ili kwamba ujisalimishe mwenyewe mipangilio yote ya Mungu. Ni ili utaingia kwa kina zaidi katika uzoefu halisi, na kupata kazi zaidi ya Roho Mtakatifu. Unafanya mazoezi ya kuwa na uhusianao wa kawaida na Mungu, muda mwingi, utapata huu kupitia kuunyima mwili na kupitia ushirikiano wako wa kweli na Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba “bila moyo wa ushirikiano, ni vigumu kupokea kazi ya Mungu; ikiwa mwili haupati mateso, hakuna baraka kutoka kwa Mungu; ikiwa roho haihangaiki, Shetani hataaibishwa.” Ikiwa unazitenda na kuzielewa vizuri kanuni hizi, mitazamo yako juu ya imani kwa Mungu itawekwa sawa. Katika matendo yenu ya sasa, mnapaswa kuacha mtazamo wa “kutafuta mkate ili kutuliza njaa,” mnapaswa kuacha mtazamo wa “kila kitu kinafanywa na Roho Mtakatifu na watu hawawezi kuingilia.” Watu wanaozungumza namna hii wote wanafikiri, “Watu wanaweza kufanya chochote kile ambacho wako radhi kukifanya, na muda utakapofika Roho Mtakatifu atafanya kazi na watu hawatakuwa na haja ya kuushinda mwili, hawatakuwa na haja ya kushirikiana, watakuwa wanahitaji tu Roho Mtakatifu kuwashawishi.” Mitazamo hii yote ni ya kipuuzi. Katika mazingira haya, Roho Mtakatifu hawezi kufanya kazi. Ni mtazamo wa aina hii ndio unakuwa kizuizi kikubwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Mara nyingi, kazi ya Roho Mtakatifu inapatikana kupitia ushirikiano wa watu. Watu wasiposhirikiana na wakikosa kusudi, na kutaka kubadilisha tabia zao, kupata kazi ya Roho Mtakatifu, na kupata mwangaza na nuru kutoka kwa Mungu, hizi zote ni fikra za kupita kiasi. Huku kunaitwa “kujifurahisha mwenyewe na kumsamehe Shetani.” Watu kama hawa hawana uhusiano wa kawaida na Mungu. Umepata dalili nyingi za Shetani ndani yako, na katika matendo yako ya zamani, kuna mambo mengi ambayo yamepingana na matakwa ya sasa ya Mungu. Je, unaweza kuyatelekeza sasa? Pata uhusiano wa kawaida na Mungu, fanya kulingana na makusudi ya Mungu, kuwa mtu mpya na kuwa na maisha mapya, usitazame dhambi zako za zamani, usiwe mwenye majuto kupita kiasi, kuwa na uwezo wa kusimama na kushirikiana na Mungu, na kutimiza majukumu ambayo unapaswa kufanya. Kwa njia hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.

Ikiwa unakubali tu maneno haya kwa mdomo baada ya kuyasoma lakini hayajaingia moyoni mwako, na huko makini kuhusu kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi inathibitisha kwamba huweki umuhimu mkubwa kwenye uhusiano wako na Mungu, mitazamo yako bado haijawekwa sawa, makusudi yako bado hayajaelekezwa kwa kumruhusu Mungu akupate, na kumkubalia Mungu utukufu, badala yake yameelekezwa kwa kuruhusu njama za Shetani kushinda na kwa kupata malengo yako binafsi. Mtu wa aina hii ana makusudi na mitazamo isiyo sahihi. Bila kujali kile ambacho Mungu amesema au namna kilivyosemwa, hawajali na hakuna mabadiliko yanayoweza kuonekana. Mioyo yao haihisi woga wowote na hawaoni aibu. Mtu wa aina hii ni mtu aliyekanganyikiwa bila roho. Kwa kila tamshi la Mungu, baada ya kulisoma na kupata ufahamu, utaliweka katika vitendo. Bila kujali ulivyokuwa ukitenda kabla—pengine huko nyuma mwili wako ulikuwa dhaifu, ulikuwa muasi, na ulipinga—hili silo jambo kubwa, na haliwezi kuzuia maisha yako yasikue leo. Ilimradi unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu leo, basi kuna tumaini. Ikiwa kwa kila wakati unaposoma maneno ya Mungu, unakuwa na mbadiliko na kuruhusu watu wengine kuona kwamba maisha yako yamebadilika kuwa mazuri, inaonyesha kwamba una uhusiano wa kawaida na Mungu na kwamba umewekwa sawa. Mungu hashughulikii watu kulingana na dhambi zao. Ilimradi unaweza kutoasi tena na hupingi tena baada ya wewe kuelewa na kufahamu, basi Mungu atakuwa bado Ana huruma na wewe. Unapokuwa na ufahamu huu na nia ya kutafuta kukamilishwa na Mungu, basi hali yako katika uwepo wa Mungu itakuwa ya kawaida. Bila kujali unachofanya, zingatia: Mungu atafikiri nini ikiwa nitafanya hiki? Je, kitawafaidi ndugu? Je, kitakuwa cha faida kwa kazi ya nyumba ya Mungu? Chunguza makusudi yako katika maombi, ushirika, usemi, kazi na kuhusiana na watu, na chunguza endapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au si wa kawaida. Ikiwa huwezi kutofautisha makusudi yako na fikra zako, basi huna ubaguzi, kitu ambacho kinathibitisha kwamba unaelewa kidogo sana kuhusu ukweli. Ikiwa unaweza kuwa na ufahamu ulio wazi wa kila kitu ambacho Mungu hufanya, vitazame vitu kulingana na neno la Mungu na vitazame vitu kwa kusimama katika upande wa Mungu, basi mitazamo yako itakuwa sahihi. Kwa hiyo, kujenga uhusiano mzuri na Mungu ni kipaumbele cha juu kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kuichukulia kama kazi muhimu na kama tukio lao kubwa la maisha. Kila kitu unachofanya kinapaswa kipimwe dhidi ya iwapo una uhusiano wa kawaida na Mungu au la. Ikiwa uhusianao wako na Mungu ni wa kawaida na makusudi yako ni sahihi, basi kifanye. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, hupaswi kuogopa kupoteza maslahi binafsi, hupaswi kumruhusu Shetani kushinda, hupaswi kumruhusu Shetani kupata kitu dhidi yako, na hupaswi kumruhusu Shetani kukufanya uwe kichekesho. Kusudi kama hili ni udhihirisho kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Si kwa ajili ya mwili, badala yake ni kwa ajili ya amani ya roho, ni kwa ajili ya kupata kazi ya Roho Mtakatifu na kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ili kuingia katika hali sahihi, unapaswa kujenga uhusiano mzuri na Mungu, unapaswa kuweka sawa mtazamo wako wa imani kwa Mungu. Ni kumruhusu Mungu kukupata, kumruhusu Mungu kufichua matunda ya maneno Yake kwako na kukuangazia na kukupatia nuru zaidi. Kwa namna hii utaingia katika tabia nzuri. Endelea kula na kunywa maneno ya Mungu ya sasa, ingia katika njia ya sasa ya kazi ya Roho Mtakatifu, fanya kulingana na matakwa ya Mungu ya sasa, usifuate mazoea ya kale, using’ang’anie njia za zamani za kufanya mambo, na haraka ingia katika namna ya kazi ya leo. Kwa njia hii uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida kabisa na utaingia katika njia sahihi ya kumwamini Mungu.

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Views: 34 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Matamshi ya Kristo, kazi ya Roho Mtakatifu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar