8:36 PM
Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa

Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa. Ingawa Yeye huvumilia shida ambazo watu wanaweza kupata ugumu kuvumilia, ingawa Yeye kama Mungu mkuu ana unyenyekevu wa kuwa mtu wa kawaida, hakuna kipengele cha kazi Yake kimecheleweshwa, na mpango Wake haujatupwa katika mchafuko hata kidogo. Anafanya kazi kulingana na mpango Wake wa awali. Mojawapo ya madhumuni ya kupata mwili huku ni kuwashinda watu. Mengine ni kuwakamilisha watu Anaowapenda. Yeye hutamani kuwaona kwa macho Yake mwenyewe watu Anaowakamilisha, na Yeye hutaka kujionea Mwenyewe jinsi watu Anaowakamilisha humshuhudia. Sio mtu mmoja ambaye hukamilishwa, na sio wawili. Hata hivyo, ni kikundi cha watu wachache sana. Kikundi hiki cha watu huja kutoka nchi mbalimbali za dunia, na kutoka kwa makabila mbalimbali ya ulimwengu. Kusudi la kufanya kazi hii nyingi ni kukipata kikundi hiki cha watu, kupata ushuhuda ambao kikundi hiki cha watu humtolea, na kupata utukufu ambao Yeye hupata kupitia kwa kikundi hiki cha watu. Yeye hafanyi kazi ambayo haina umuhimu, wala hafanyi kazi ambayo haina thamani. Inaweza kusemwa kuwa, kwa kufanya kazi nyingi sana, lengo la Mungu ni kuwakamilisha watu wote ambao Yeye anataka kuwakamilisha. Katika wakati wowote wa ziada Alio nao nje ya hili, Atawaondosha wale walio waovu. Jua kwamba Haifanyi kazi hii kubwa kwa sababu ya wale walio waovu; kwa kinyume, Yeye hufanya kadri Awezavyo kwa sababu ya idadi hiyo ndogo ya watu ambao hawana budi kukamilishwa na Yeye. Kazi ambayo Yeye hufanya, maneno ambayo Yeye hunena, siri ambayo Yeye hufichua, na hukumu Yake na adhabu zote ni kwa ajili ya idadi hiyo ndogo ya watu. Yeye hakupata mwili kwa sababu ya wale walio waovu, sembuse wao kuchochea ghadhabu kubwa ndani Yake. Yeye husema ukweli, na huzungumzia kuingia, kwa sababu ya wale watakaokamilishwa, Alipata mwili kwa sababu yao, na ni kwa sababu yao Yeye hutoa ahadi na baraka Zake. Ukweli, kuingia, na maisha katika ubinadamu ambayo Yeye huzungumzia si kwa ajili ya wale walio waovu. Yeye hutaka kuepuka kuzungumza na wale walio waovu, na hutaka kuwapa wale ambao watakamilishwa ukweli wote. Lakini kazi Yake inahitaji kwamba, kwa sasa, wale walio waovu waruhusiwe kufurahia baadhi ya utajiri Wake. Wale ambao hawatekelezi ukweli, ambao hawamridhishi Mungu, na ambao hukatiza kazi Yake wote ni waovu. Hawawezi kukamilishwa, na wanachukiwa kabisa na kukataliwa na Mungu. Kwa kinyume, watu ambao hutia ukweli katika vitendo na wanaweza kumridhisha Mungu na ambao hujitolea wenyewe kabisa katika kazi ya Mungu ndio watu ambao watakamilishwa na Mungu. Wale ambao Mungu hutaka kuwakamilisha sio wengine bali ni kikundi hiki cha watu, na kazi ambayo Mungu hufanya ni kwa ajili ya watu hawa. Ukweli ambao Yeye huzungumzia unaelekezwa kwa watu ambao wako tayari kuutia katika vitendo. Yeye huwa hazungumzi na watu ambao hawatii ukweli katika vitendo. Ongezeko la umaizi na ukuaji wa utambuzi ambao Yeye huzungumzia umelengwa kwa watu ambao wanaweza kutekeleza ukweli. Anapozungumza juu ya wale ambao watakamilishwa Yeye anazungumzia watu hawa. Kazi ya Roho Mtakatifu inaelekezwa kwa watu ambao wanaweza kutenda ukweli. Mambo kama kumiliki hekima na kuwa na ubinadamu yanaelekezwa kwa watu ambao wako tayari kutia ukweli katika vitendo. Wale ambao hawatekelezi ukweli wanaweza kuusikia ukweli mwingi na wanaweza kuuelewa ukweli mwingi, lakini kwa sababu wao ni miongoni mwa watu waovu, ukweli ambao wao huuelewa huja kuwa tu mafundisho na maneno, na hauna umuhimu kwa mabadiliko yao ya tabia au kwa maisha yao. Hakuna hata mmoja wao aliye mwaminifu kwa Mungu; wao wote ni watu wanaomwona Mungu lakini hawawezi kumpata, na wote wamehukumiwa na Mungu.

Roho Mtakatifu ana njia ya kutembea katika kila mtu, na humpa kila mtu fursa za kukamilishwa. Kupitia uhasi wako unajulishwa upotovu wako mwenyewe, na kisha kwa njia ya kuacha uhasi utapata njia ya kutenda, na huku ndiko kukamilishwa kwako. Aidha, kwa njia ya mwongozo na mwangaza wa siku zote wa mambo fulani chanya ndani yako, utatimiza shughuli yako kwa kuamili na kukua katika umaizi na kupata utambuzi. Wakati hali zako ni nzuri, uko tayari hasa kusoma neno la Mungu, na hasa tayari kumwomba Mungu, na unaweza kuyahusisha mahubiri unayoyasikia na hali zako mwenyewe. Kwa nyakati kama hizo Mungu hukupatia nuru na kukuangaza ndani, na kukufanya utambue mambo fulani ya kipengele chanya. Huku ni kukamilishwa kwako katika kipengele chanya. Katika hali hasi, wewe ni dhaifu na hasi, na huhisi kuwa huna Mungu moyoni mwako, lakini Mungu hukuangaza, akikusaidia kupata njia ya kutenda. Kutoka nje ya hili ni kupata ukamilisho katika hali chanya. Mungu anaweza kumkamilisha mwanadamu katika vipengele hasi na chanya. Inategemea kama unaweza kupata uzoefu, na kama wewe hufuatilia kukamilishwa na Mungu. Kama kwa hakika unatafuta kukamilishwa na Mungu, basi kilicho hasi hakiwezi kukufanya upoteze, lakini kinaweza kukuletea mambo ambayo ni halisi zaidi, na kinaweza kukufanya uweze zaidi kujua kile kilichopunguka ndani yako, uweze zaidi kufahamu sana hali zako halisi, na kuona kwamba mtu hana kitu, wala si kitu; kama hupitii majaribio, hujui, na daima utahisi kuwa wewe ni wa hadhi ya juu kuliko wengine na bora kuliko kila mtu mwingine. Kwa njia hii yote utaona kwamba yote yaliyotangulia yalifanywa na Mungu na kulindwa na Mungu. Kuingia katika majaribio hukuacha bila upendo au imani, huna sala, na huwezi kuimba nyimbo—na, bila kulitambua, katikati ya hili unakuja kujijua. Mungu ana njia nyingi za kumkamilisha mwanadamu. Yeye hutumia mazingira ya kila aina ili shughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia vitu mbalimbali ili kumuweka mwanadamu wazi; katika suala moja Yeye humshughulikia mwanadamu, katika jingine Yeye humuweka mwanadamu wazi, na katika jingine Yeye humfichua mwanadamu, kuzichimbua na kuzifichua “siri” katika vina vya moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kuzifichua hali zake nyingi. Mungu humkamilisha mwanadamu kupitia mbinu nyingi—kupitia ufunuo, ushughulikiaji, usafishwaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa vitendo.

Ni nini mnachokitafuta sasa? Labda ni kukamilishwa na Mungu, kumjua Mungu, kumpata Mungu, au ni mtindo wa Petro wa miaka ya tisini, ama kuwa na imani kubwa zaidi ya ile ya Ayubu. Mnaweza kutafuta mengi, iwe ni kutafuta kuitwa wenye haki na Mungu na kufika mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, au kuweza kumdhihirisha Mungu duniani na kuwa na ushuhuda wa nguvu na mkubwa sana kwa Mungu. Bila kujali mnachokitafuta, kwa jumla, ni kwa ajili ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Haijalishi kama unatafuta kuwa mtu mwenye haki, au unatafuta mtindo wa Petro, ama imani ya Ayubu, au kukamilishwa na Mungu, chochote unachokitafuta, kwa muhtasari, yote ni kazi ya Mungu. Hivyo ni kusema, bila kujali unachokitafuta, yote ni kwa ajili ya kukamilishwa na Mungu, yote ni kwa ajili ya kupitia neno la Mungu, ili kuuridhisha moyo wa Mungu; yote ni kwa ajili ya kugundua uzuri wa Mungu, yote ni kwa ajili ya kutafuta njia ya kutenda katika uzoefu halisi kwa lengo la kuweza kuiacha tabia yako ya uasi, kufanikisha hali ya kawaida ndani yako mwenyewe, kuweza kufuata kabisa mapenzi ya Mungu, kuwa mtu sahihi, na kuwa na nia sahihi katika kila kitu unachokifanya. Sababu ya wewe kupitia vitu hivi vyote ni kufikia kumjua Mungu na kufanikisha ukuaji wa maisha. Ingawa kile unachokipitia ni neno la Mungu, na kile unachokipitia ni matukio halisi, watu, mambo, na vitu katika mazingira yako, hatimaye unaweza kumjua Mungu na kukamilishwa na Mungu. Kutafuta kuitembea njia ya mtu mwenye haki au kutafuta kutia neno la Mungu katika vitendo, hizi ndizo njia. Kumjua Mungu na kukamilishwa na Mungu ndiyo hatima. Kama unatafuta sasa kukamilishwa na Mungu, au kumshuhudia Mungu, kwa ujumla, hatimaye ni ili kumjua Mungu; ni ili kwamba kazi Anayoifanya ndani yako sio ya bure, ili hatimaye uje kuujua uhalisi wa Mungu, kujua ukuu Wake, vivyo hivyo hata zaidi kuujua unyenyekevu wa Mungu na hali Yake ya kutoonekana, na kujua kazi nyingi ambazo Mungu hufanya ndani yako. Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani, kufanya kazi Yake katika watu hawa wachafu na wapotovu, na kukikamilisha kikundi hiki cha watu. Mungu hakupata mwili tu ili kuishi na kula kati ya watu, kuwalisha watu, kutoa wanachohitaji watu. Jambo muhimu zaidi ni kwamba Yeye hufanya kazi Yake kubwa ya wokovu na ushindi kwa watu hawa walio na upotovu usiovumilika. Alikuja katika kiini cha joka kubwa jekundu ili kuwaokoa watu hawa wapotovu mno, ili watu wote waweze kubadilishwa na kufanywa wapya. Tatizo kubwa ambalo Mungu huvumilia siyo tu shida ambayo Mungu mwenye mwili huvumilia, lakini hasa ni kwamba Roho wa Mungu hupitia udhalilishaji uliokithiri—Yeye hujinyenyekeza na kujificha Mwenyewe sana kiasi kwamba Yeye huwa mtu wa kawaida. Mungu alipata mwili na kuchukua mfano wa mwili ili watu waone kwamba Ana maisha ya kawaida ya binadamu, na kwamba ana mahitaji ya kawaida ya binadamu. Hili linatosha kuthibitisha kwamba Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani. Roho wa Mungu hufanyika katika mwili. Roho Wake ni wa juu sana na mkuu, lakini Yeye huchukua mfano wa mwanadamu wa kawaida, wa mwanadamu asiye muhimu ili kufanya kazi ya Roho Wake. Ubora wa tabia, umaizi, hisi, ubinadamu, na maisha ya kila mmoja wenu vinaonyesha kwamba hamfai kweli kupokea kazi ya Mungu ya aina hii. Hakika hamfai kumruhusu Mungu kuvumilia shida kama hiyo kwa ajili yenu. Mungu ni mkubwa sana. Yeye ni mkuu sana, na watu ni duni sana na wa hali ya chini, lakini Yeye bado huwafanyia kazi. Yeye hakupata mwili tu ili kuwaruzuku watu, kuzungumza na watu, Yeye hata huishi pamoja na watu. Mungu ni mnyenyekevu sana, wa hupendeka sana. Ikiwa punde upendo wa Mungu unapotajwa, mara tu neema ya Mungu inapotajwa, unatoa machozi unapotamka sifa kubwa, ukifika katika hali hii, basi una maarifa ya kweli ya Mungu.

Kuna kuchepuka katika kutafuta kwa watu siku hizi; wao hutafuta tu kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu, lakini hawana maarifa yoyote juu ya Mungu, na wametelekeza nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu ndani yao. Hawana maarifa ya kweli ya Mungu kama msingi. Kwa njia hii wanapoteza nguvu wakati uzoefu wao unapoendelea. Wale wote wanaotafuta kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu, ingawa wakati wa zamani hawakuwa katika hali nzuri, walielekea kwa uhasi na udhaifu, na mara nyingi walitoa machozi, wakaingia katika kukata tamaa, na wakavunjika moyo; sasa hali zao zinakuwa bora kwa kukithiri wanapopata uzoefu zaidi. Baada ya uzoefu wa kushughulikiwa na kuvunjwa, au kupitia kisa cha kusafishwa, wamekuwa na maendeleo makubwa. Hali kama hizo hazionekani zikiwafika tena, tabia zao zimebadilika, na upendo wa Mungu unaishi kwa kudhihirika ndani yao. Kuna kanuni kwa kukamilishwa kwa watu na Mungu, ambayo ni kwamba Yeye hukupa nuru kwa kutumia sehemu yako inayofaa ili uwe na njia ya kutenda na unaweza kujitenga na hali zote hasi, ikisaidia roho yako kupata uhuru, na ikikufanya uweze kumpenda zaidi. Kwa njia hii, unaweza kuiacha tabia potovu ya Shetani. Wewe huna hila na uko wazi, ukiwa tayari kujijua, na ukiwa tayari kutia ukweli katika vitendo. Mungu huona kwamba uko tayari kujijua na uko tayari kutia ukweli katika vitendo, kwa hiyo unapokuwa dhaifu na hasi, Yeye hukupa nuru maradufu, Akikusaidia kujijua zaidi, kuwa tayari kujitubia, na kuweza zaidi kutenda mambo ambayo unapaswa kuyatenda. Ni kwa njia hii tu ambapo moyo wako unahisi amani na utulivu. Mtu ambaye kwa kawaida huzingatia kumjua Mungu, ambaye huzingatia kujijua, ambaye huzingatia vitendo vyake mwenyewe ataweza kupokea kazi ya Mungu mara kwa mara, mara kwa mara kupokea mwongozo na nuru kutoka kwa Mungu. Hata ingawa yuko katika hali hasi, anaweza kugeuka mara moja, iwe ni kwa sababu ya matendo ya dhamiri au kwa sababu ya nuru kutoka kwa neno la Mungu. Mabadiliko ya tabia ya mtu hufanikishwa daima anapojua hali yake mwenyewe halisi na kujua tabia na kazi ya Mungu. Mtu ambaye yuko tayari kujijua na yuko tayari kuwasiliana ataweza kutekeleza ukweli. Aina hii ya mtu ni mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, na mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu ana ufahamu wa Mungu, uwe ni wa kina au wa juu juu, haba au maridhawa. Hii ni haki ya Mungu, na ni kitu ambacho watu hupata, ni faida yao wenyewe. Mtu ambaye ana maarifa ya Mungu ni yule ambaye ana msingi, ambaye ana maono. Mtu wa aina hii ana hakika kuhusu mwili wa Mungu, na ana hakika kuhusu neno la Mungu na kazi ya Mungu. Bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi au kuzungumza, au jinsi watu wengine husababisha vurugu, anaweza kushikilia msimamo wake, na kuwa shahidi kwa Mungu. Kadiri mtu alivyo katika njia hii ndivyo anavyoweza kutekeleza zaidi ukweli anaouelewa. Kwa sababu daima anatenda neno la Mungu, yeye hupata ufahamu zaidi wa Mungu, na analo azimio la kuwa shahidi kwa Mungu milele.

Kuwa na utambuzi, kuwa na utii, na kuwa na uwezo wa kubaini mambo ili uwe hodari katika roho ina maana kuwa maneno ya Mungu yanakuangaza na kukupa nuru ndani mara tu unapokabiliwa na kitu fulani. Huku ni kuwa hodari katika roho. Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya kusaidia kufufua roho za watu. Kwa nini Mungu daima husema kuwa watu ni wa kujijali na wajinga? Ni kwa sababu roho za watu zimekufa, na wamekuwa wa kutojali kiasi kwamba hawajui kabisa mambo ya roho. Kazi ya Mungu ni kuyafanya maisha ya watu yaendelee na ni kusaidia roho za watu zichangamke, ili waweze kubaini mambo ya roho, na wao daima waweze kumpenda Mungu mioyoni mwao na kumridhisha Mungu. Ufikaji mahali hapa huonyesha kwamba roho ya mtu imefufuliwa, na wakati mwingine atakapokabiliwa na kitu fulani, anaweza kuonyesha hisia mara moja. Yeye huitikia mahubiri, na kuonyesha hisia haraka kwa hali mbalimbali. Huku ndiko kufanikisha uhodari wa roho. Kuna watu wengi ambao wana majibu ya haraka kwa tukio la nje, lakini mara tu kuingia katika uhalisi au mambo kinaganaga ya roho yanapotajwa, wao huwa wa kutojali na wajinga. Wao huelewa kitu tu kikiwa ni dhahiri. Hizi zote ni ishara za kuwa wa kutojali kiroho na mjinga, za kuwa na uzoefu kidogo wa mambo ya roho. Watu wengine ni hodari wa roho na wana utambuzi. Mara tu wanaposikia kitu kinachoelekezwa kwa hali zao hawapotezi muda kukiandika. Wanakitumia kwa uzoefu wao wa baadaye, na kwa kujibadilisha. Huyu ni mtu ambaye ni hodari katika roho. Na kwa nini anaweza kuonyesha hisia haraka sana? Kwa sababu yeye hulenga vipengele hivi katika maisha ya kila siku, na mara tu mojawapo ya vipengele hivi kinapotajwa, kinatokea kufanana na hali yake ya ndani, na anaweza kukipokea mara moja. Ni sawa na kumpa mtu mwenye njaa chakula; anaweza kula mara moja. Ukimpa chakula mtu asiye na njaa, hana haraka kuonyesha hisia. Daima wewe humwomba Mungu, na kisha unaweza kuonyesha hisia mara moja unapokabiliwa na kitu fulani: kile Mungu huhitaji katika jambo hili, na jinsi unavyopaswa kutenda. Mungu alikuongoza juu ya suala hili mara ya mwisho; unapokabiliwa na kitu cha aina hii leo unajua jinsi ya kuingia katika hali hii kuuridhisha moyo wa Mungu. Daima ukitenda kwa njia hii na daima upate uzoefu kwa njia hii, wakati fulani utakuwa stadi kwayo. Wakati unasoma neno la Mungu unajua ni mtu wa aina gani Mungu anamzungumzia, unajua ni aina gani ya hali za roho Anayozungumzia, na unaweza kuelewa jambo muhimu na kulitia katika vitendo; hii inaonyesha kuwa unaweza kupata uzoefu. Kwa nini watu wengine hawana jambo hili? Ni kwa sababu hawaweki jitihada nyingi katika kipengele cha kutenda. Ingawa wako tayari kutia ukweli katika vitendo, hawana umaizi wa kweli katika utondoti wa huduma, katika utondoti wa ukweli katika maisha yao. Wanachanganyikiwa jambo linapotokea. Kwa njia hii, unaweza kupotoshwa nabii wa uongo au mtume wa uongo anapokuja. Haikubaliki kupuuza utambuzi. Ni lazima uzingatie mambo ya roho daima: kile Mungu husema, jinsi Mungu hufanya kazi, yale yaliyo matakwa Yake kwa watu, ni watu wa namna gani unapaswa kuwasiliana nao, na ni watu wa aina gani unapaswa kuwaepuka. Ni lazima usisitize mambo haya wakati wa kula na kunywa neno la Mungu na wakati wa uzoefu halisi. Daima ukiwa na uzoefu wa neno la Mungu kwa njia hii, utaelewa ukweli na uelewe vizuri vitu vingi, na utakuwa na utambuzi pia. Ni nini kufundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu, ni nini lawama inayotokana na nia ya mwanadamu, ni nini mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini mpango wa mazingira, ni nini maneno ya Mungu yanatolea nuru ndani, kama huna uhakika juu ya mambo haya, hutakuwa na utambuzi. Unapaswa kujua kile ambacho huja kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini tabia ya uasi, jinsi ya kulitii neno la Mungu, na jinsi ya kuacha uasi wako mwenyewe; unapaswa kuelewa utondoti wa ukweli huu wote, ili jambo linapotukia, una ukweli unaofaa wa kulinganisha nalo, una maono yanayofaa kama msingi, una kanuni katika kila jambo ufanyalo na unaweza kutenda kulingana na ukweli. Halafu maisha yako yatajazwa na nuru ya Mungu, yatajazwa na baraka za Mungu. Mungu hatamtendea vibaya mtu yeyote ambaye humtafuta kwa kweli. Hatamtendea vibaya mtu yeyote ambaye huishi kwa kumdhihirisha na ambaye hushuhudia kwa ajili Yake, na hatamlaani mtu yeyote ambaye kwa kweli anaweza kuona kiu ya ukweli. Ikiwa, unapokula na kunywa maneno ya Mungu, unaweza kuzingatia hali yako mwenyewe ya kweli, kuzingatia vitendo vyako mwenyewe, na kuzingatia ufahamu wako mwenyewe, basi, unapokabiliwa na tatizo, utapokea nuru na utapata ufahamu wa utendaji. Kisha utakuwa na njia ya kutenda na utakuwa na utambuzi kwa kila kitu. Mtu aliye na ukweli si rahisi kudanganywa, na rahisi kutenda kwa vurugu au kutenda kwa kupita kiasi. Kwa sababu ya ukweli amelindwa, na pia kwa sababu ya ukweli yeye hupata ufahamu zaidi. Kwa sababu ya ukweli ana njia zaidi za kutenda, hupata fursa zaidi za Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yake, na hupata fursa zaidi za kukamilishwa.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Views: 31 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Matamshi ya Kristo, kazi ya Roho Mtakatifu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar