2:45 PM
Mungu Anakamilisha Wale Wanaoufuata Moyo Wake

Kundi la watu ambao Mungu anataka kupata sasa ni wale ambao wanajitahidi kushirikiana na Mungu, wanaoweza kuiheshimu kazi Yake, na wanaoamini kuwa maneno Anayonena Mungu ni ya kweli, wale wanaoweza kuweka mahitaji ya Mungu katika vitendo. Ni wale walio na uelewa wa kweli katika mioyo yao. Ni hao ndio wanaoweza kukamilishwa, na wale ambao bila shaka watatembea katika njia ya ukamilisho. Wale wasio na uelewa wa wazi wa kazi ya Mungu, wale wasiokula na kunywa neno la Mungu, wale wasiotilia maanani neno la Mungu, na wale wasio na upendo wowote kwa Mungu katika mioyo yao—watu kama hao hawawezi kufanywa wakamilifu. Wale walio na shaka na Mungu mwenye mwili, wale wanaobaki bila uhakika juu Yake, wale ambao hawachukulii kazi ya Mungu kwa uzito, na wale ambao daima wanamdanganya Mungu, hao watu wanakataa Mungu na ni wa Shetani—hakuna njia ya kukamilisha watu kama hao.

Kama unataka kufanywa mkamilifu, lazima kwanza uwe na neema ya Mungu, kwa sababu Mungu anawakamilisha wale ambao Amewapa neema, wale wanaoupendeza moyo Wake. Kama unataka kuupendeza moyo wa Mungu, lazima uwe na moyo unaotii kazi Yake yote, lazima ujitahidi kuufuata ukweli, na lazima uukubali uchunguzi wa Mungu katika kila kitu. Je, kila kitu unachofanya kimepitia uchunguzi wa Mungu? Je, nia yako iko sawa? Kama nia yako iko sawa, Mungu Atakubaliana nawe; kama nia yako sio sawa, hii inathibitisha kwamba kile moyo wako unapenda sio Mungu, ni mwili na Shetani. Kwa hiyo lazima ukubali uchunguzi wa Mungu katika kila kitu kupitia maombi. Unapoomba, ingawa nafsi Yangu haiko hapo, Roho Mtakatifu yuko pamoja nawe, na unapoomba kwa mtu huyu, pia unaomba kwa Roho wa Mungu. Kwa nini unaamini katika mwili huu? Kwa sababu Yuko na Roho wa Mungu. Unaweza kumwamini mtu huyu bila Roho wa Mungu. Unapoamini katika mtu huyu, unaamini katika Roho wa Mungu. Unapomwogopa mtu huyu, unamwogopa Roho wa Mungu. Imani katika Roho wa Mungu ni imani katika mtu huyu, imani katika mtu huyu pia ni imani katika Roho wa Mungu. Unapoomba, unahisi Roho wa Mungu akiwa pamoja nawe, Mungu yuko mbele yako, kwa hivyo unamwomba Roho wa Mungu. Leo, watu wengi wanaogopa sana kuyaleta matendo yao mbele za Mungu, na ingawa unaweza kuudanganya mwili wa Mungu, huwezi kumdanganya Roho wa Mungu. Yale yote ambayo hayawezi kustahimili uchunguzi wa Mungu hayakubaliani na ukweli nayo lazima yawekwe kando, ama unatenda dhambi dhidi ya Mungu. Kwa hivyo, haijalishi kama ni wakati unaomba, unaponena na kushiriki na ndugu na dada zako, ama unapofanya wajibu wako na kufanya biashara yako, lazima uuweke moyo wako mbele za Mungu. Unapoitimiza kazi yako, Mungu yuko nawe, na bora nia yako iwe sawa, nayo iko kwa ajili ya kazi ya nyumba ya Mungu, Mungu atakubali kila kitu ufanyacho, kwa hivyo ni lazima uweke bidii kwa dhati kujishughulisha na kuitimiza kazi yako. Unapoomba, kama una upendo kwa Mungu katika moyo wako, na kama unatafuta utunzaji wa Mungu, ulinzi, na uchunguzi, kama haya ndio nia yako, maombi yako yatafaulu. Unapoomba katika mikutano, ndivyo unafaa kufungua moyo wako na kuomba Mungu, ambia Mungu kile kilicho moyoni mwako, na bila kuongea uongo, basi maombi yako yatafaulu. Kama unampenda Mungu moyoni mwako kwa dhati, basi fanya kiapo kwa Mungu: “Mungu, uliye mbinguni na nchini na vitu vyote, naapa Kwako: Hebu Roho Wako achunguze kila kitu ninachofanya na unilinde na kunijali kila wakati. Kinafanya kila kitu nifanyacho kiweze kusimama katika uwepo Wako. Ikiwa moyo wangu utawahi kukoma kukupenda ama kukusaliti Wewe, nipe adhabu Yako na laana kali zaidi. Usinisamehe katika dunia hii ama inayofuata!” Unaweza kuthubutu kula kiapo kama hiki? Kama huwezi, hii inadhibitisha kuwa wewe ni mwoga, na kwamba bado unajipenda. Je, mnao uamuzi huu? Kama kweli huu ndio uamuzi wako, lazima ufanye kiapo hiki. Kama una azimio la kula kiapo kama hiki, Mungu ataridhisha uamuzi wako. Unapoapa kwa Mungu, Mungu anasikiza. Mungu Anaamua kama wewe ni mwenye dhambi ama mwenye haki kupitia maombi yako na matendo yako. Huu sasa ni mchakato wa kuwakamilisha, na kama kweli unayo imani katika kukamilishwa kwako na Mungu, utaleta kila kitu ufanyacho mbele za Mungu na kuukubali uchunguzi wa Mungu, nawe ukitenda jambo la kikatili ama kumsaliti Mungu, Mungu “atakukamilisha” kulingana na kiapo chako, na kisha haijalishi kitakachokufanyikia, iwe kuangamia ama kuadibu, ni shida yako mwenyewe. Ulikula kiapo, basi lazima ukitekeleze. Ukila kiapo, lakini ukose kukitekeleza, utaangamia. Unapokula kiapo, Mungu atakukamilisha kulingana na kiapo chako. Wengine wanaogopa baada ya kuomba, na kusema, “Ee, jamani, nafasi yangu katika ufisadi imepotea, nafasi yangu kufanya mambo maovu imepotea, nafasi yangu ya kujiingiza katika ulafi wangu wa kidunia imepotea!” Watu hawa bado wanaipenda dunia na dhambi, nao ni hakika wataangamia.

Kuwa muumini katika Mungu kunamaanisha kuwa kila kitu ufanyacho lazima kiletwe mbele za Mungu na kupitia uchunguzi wa Mungu. Kama kile ufanyacho kinaweza kuletwa mbele za Roho wa Mungu lakini sio mbele ya mwili wa Mungu, hii inadhibitisha kuwa hujajitiisha katika uchunguzi wa Roho wa Mungu. Roho wa Mungu ni nani? Mtu aliyetolewa ushahidi na Mungu ni nani? Je, Wote hawako ndani ya nafsi moja? Wengi Huwaona kama wawili, wakiamini Roho wa Mungu ni Wake pekee, naye mtu aliyetolewa ushahidi na Mungu ni mwanadamu tu. Lakini umekosea, sivyo? Je, mtu huyu anafanya kazi kwa niaba ya nani? Wale ambao hawaujui mwili wa Mungu hawana uelewa ya kiroho. Roho wa Mungu na mwili Wake ni mmoja, kwa sababu Roho wa Mungu anatokea kwa mwili. Kama mtu huyu si mwema kwako, Roho wa Mungu Atakuwa mwema? Ni nini kimekuchanganya? Leo, hakuna asiyekubali uchunguzi wa Mungu anaweza kupokea idhini ya Mungu, na yeyote asiyemjua Mungu mwenye mwili hawezi kukamilishwa. Jiangalie nawe ujiulize kama kila kitu unachofanya kinaweza kuletwa mbele ya Mungu. Iwapo huwezi kuleta kila kitu unachofanya mbele za Mungu, hii inaonyesha kuwa wewe ni mtenda maovu. Je, watenda maovu wanaweza kufanywa wakamilifu? Kila kitu unachofanya, kila tendo, kila nia, na kila jibu lazima kiletwe mbele za Mungu. Hiyo ni, maisha yako ya kawaida ya kiroho, maombi yako, ukaribu wako na Mungu, kula na kunywa neno la Mungu, ushirika na ndugu na dada zako, kuishi maisha yako katika kanisa, na hata huduma yako katika ushirikiano wako ni vitu vyote ambavyo lazima viletwe mbele za Mungu na kuchunguzwa na Yeye. Ni matendo kama hayo ndiyo yatakayokusaidia kustawi katika maisha. Mchakato wa kukubali uchunguzi wa Mungu ni mchakato wa kutakaswa. Kadri unavyoukubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyotakaswa zaidi, kadri unavyokuwa katika uwiano na matakwa ya Mungu, ili kwamba hutasikia wito wa uasherati na ubadhirifu, na moyo wako utaishi katika uwepo wa Mungu; kadri unavyokubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyomuaibisha Shetani na kuutelekeza mwili. Kwa hivyo, kukubali uchunguzi wa Mungu ni njia ambayo watu wanafaa kutenda. Haijalishi kile unachokifanya, hata katika ushirika na ndugu na dada zako, ukiyaleta matendo yako mbele za Mungu na kutafuta uchunguzi wa Mungu, na kama nia yako ni kumtii Mungu Mwenyewe, unachotenda ni sahihi zaidi. Kama tu wewe ni mtu anayeleta kila kitu anachofanya mbele za Mungu na kukubali uchunguzi wa Mungu ndipo utakapokuwa mtu anayeishi kwa hakika katika uwepo wa Mungu.

Wale wasio na uelewa wa Mungu hawawezi kumtii Mungu kikamilifu. Watu kama hao ni wana wa uasi. Ni wenye kutaka makuu sana, na kunao uasi mwingi sana ndani mwao, kwa hivyo wanajitenga na Mungu na hawana nia ya kukubali uchunguzi wa Mungu. Watu kama hao hawawezi kufanywa wakamilifu na Mungu kwa urahisi. Watu wengine wana uchaguzi katika vile wanavyokula na kunywa neno la Mungu na katika hali yao ya kulikubali. Wanakubali sehemu za neno la Mungu zinazolingana na dhana zao wakikataa zile zisizokubaliana nazo. Je, hawamwasi na kumkataa Mungu kwa uwazi? Kama mtu anaamini katika Mungu kwa miaka mingi bila kupata uelewa hata kidogo wa Mungu, yeye ni mtu asiyeamini. Wale walio tayari kukubali uchunguzi wa Mungu ni wale wanao tafuta uelewano wa Mungu, walio tayari kukubali neno la Mungu. Ni wale ambao watapokea uridhi wa Mungu na mibaraka, nao ni wale waliobarikiwa zaidi. Mungu analaani wale wasio na nafasi Yake katika mioyo yao. Anawaadibu na kuwaacha watu kama hao. Kama humpendi Mungu, Mungu atakuacha, na kama hutasikia Ninachosema, Naahidi kwamba Roho wa Mungu atakuacha. Jaribu hili iwapo hauniamini! Leo Nawaambia njia ya kufuata, lakini kama utafanya hivyo ni juu yako. Kama huna imani, kama hutatenda, utaona kama Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako au la! Kama hautatafuta uelewano wa Mungu, Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani mwako. Mungu anafanya kazi ndani ya wale wanaotafuta na kulithamini neno la Mungu. Kadri unavyolithamini neno la Mungu, ndivyo Roho wa Mungu atakavyofanya kazi zaidi ndani mwako. Kadri mtu anavyolithamini neno la Mungu, ndivyo nafasi yake ya kukamilishwa na Mungu inavyokuwa kubwa. Mungu anawakamilisha wale ambao wanampenda Yeye kwa kweli. Anawakamilisha wale ambao mioyo yao iko katika amani mbele Yake. Ukiithamini kazi yote ya Mungu, ukiuthamini mwanga wa Mungu, ukiuthamini uwepo wa Mungu, ukithamini kujali na kuwekwa kwa Mungu, ukithamini jinsi neno la Mungu linakuwa ukweli wako na utoaji wa maisha, unafuata zaidi moyo wa Mungu. Ukiithamini kazi ya Mungu, ukiithamini kazi yote ambayo Mungu Amefanya juu yako, Mungu Atakubariki na kufanya kila kitu kilicho chako kuongezeka. Usipoithamini kazi ya Mungu, Mungu Hatafanya kazi kwako, Atakuruhusu tu nyakati za neema kwa imani yako, ama kukubariki na utajiri kidogo ama usalama kwa familia yako. Lazima utie bidii kuyafanya maneno ya Mungu kuwa ukweli wako ili umridhishe Yeye na kuupendeza moyo Wake, sio tu kutia bidii kufurahia neema ya Mungu. Hakuna kitu muhimu zaidi kwa waumini kama kupokea kazi ya Mungu, kupata ukamilifu, na kuwa anayefanya mapenzi ya Mungu. Hili ndilo lengo unalofaa kufuata.

Kila ambacho mwanadamu alitafuta katika Enzi ya Neema sasa hakiko tena, kwa sababu kiwango cha juu cha kufuata kimetokea, kufuata kitu ambacho ni cha kujivunia na cha matendo, harakati ambayo inaweza kukidhi zaidi kile ambacho mwanadamu anahitaji ndani. Kwa wale walio katika enzi zilizopita, Mungu hakufanya kazi ya leo kwao, Hakunena nao sana jinsi Amenena leo, wala mahitaji Yake kwao hayakuwa ya juu kama ya leo. Kwamba Mungu anainua vitu hivi kwenu kunathibitisha kuwa nia ya mwisho ya Mungu, kumelengwa kwenu, kundi hili. Iwapo kweli unataka kufanywa mkamilifu na Mungu, basi lifuate kama lengo lako kuu. Haijalishi kama unakimbia, unagharimika, unatenda wajibu, ama umeaminiwa na Mungu, ni lazima utafute kukamilishwa na kuridhisha mapenzi ya Mungu. Lazima utafute haya kwa kila kitu ufanyacho. Mtu akisema kuwa hafuati kukamilishwa na Mungu ama kuingia katika maisha, lakini anafuata tu amani na furaha ya kimwili, basi yeye ni kipofu kabisa. Wale wasiofuata ukweli wa maisha, lakini wanafuata maisha ya milele pekee katika maisha ya baadaye na usalama katika maisha haya ni vipofu kabisa. Kwa hivyo, kila kitu ufanyacho lazima kifanywe kwa madhumuni ya kufanywa mkamilifu na kupatwa na Mungu.

Kazi ambayo Mungu anafanya kwa watu ni kuwakimu kulingana na mahitaji yao tofauti. Kadri maisha ya mwanadamu yalivyo makubwa, ndivyo anavyohitaji mengi zaidi, na ndivyo anavyotafuta zaidi. Kama katika awamu hii huna harakati, inathibitisha kuwa Roho Mtakatifu amekuacha. Wale wote wanaofuata maisha hawatawahi kuachwa na Roho Mtakatifu, wao hufuata kila wakati, wanatamani kila wakati. Watu kama hao hawatosheki kamwe kupumzika mahali walipo. Kila awamu ya kazi ya Roho Mtakatifu inalenga kufikia athari ndani mwako, lakini ukikua wa kutojali, kama hauhitaji tena, kama huikubali kazi ya Roho Mtakatifu, Yeye atakuacha. Watu wanahitaji uchunguzi wa Mungu kila siku, wanahitaji kupewa kwa wingi kutoka kwa Mungu kila siku. Je, watu wanaweza kuishi bila kula na kunywa neno la Mungu kila siku? Kama mtu anahisi kuwa hawezi kula ama kunywa neno la Mungu vya kutosha, kama analitafuta kila siku na kuwa na njaa na kiu kwake, Roho Mtakatifu atafanya kazi juu yao. Kadri mtu anavyotamani, ndivyo atakavyokuwa na ushirika kuhusu vitu vya hakika. Kadri mtu anavyoutafuta ukweli sana, ndivyo maisha yake yanavyokua kwa haraka, yakimpa uzoefu wa hali ya juu na kumfanya tajiri katika nyumba ya Mungu.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Views: 74 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwish | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar