Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Katika sala zao hapo awali walikuwa wakifanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati na kufanya mchezo tu, na hakuna mtu aliyeupeana moyo wake kwa ukamilifu mbele ya Mungu na kumwomba Mungu kweli. Watu humwomba Mungu tu wakati kitu kinawatendekea. Katika wakati huu wote, umewahi kweli kumwomba Mungu? Je, umewahi kutoa machozi ya uchungu mbele ya Mungu? Je, umewahi kujijua mwenyewe mbele ya Mungu? Je, umewahi kumwomba Mungu maombi ya kutoka? Kuomba hufanyiwa mazoezi polepole: Ikiwa kwa kawaida huombi nyumbani, basi hutakuwa na njia yoyote ya kuomba kanisani, na kama kwa kawaida huombi wakati wa mikusanyiko midogo, basi hutaweza kusali wakati wa mikusanyiko mik ... Read more »

Views: 128 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 08.31.2019 | Comments (0)

Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili. Kabla Aanze kutekeleza kazi ya huduma Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bila kuonyesha ishara ya uungu Wake, na ni baada tu ya kuanza rasmi kutekeleza huduma Yake ndipo uungu Wake uliwekwa wazi. Maisha na kazi Zake katika ile miaka ishirini na tisa yote ilidhihirisha kuwa Alikuwa mwanadamu halisi, mwana wa Adamu, mwili; kwani huduma Yake ilianza tu kwa dhati baada ya umri wa miaka ishirini na tisa. Maana ya ... Read more »

Views: 93 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 08.30.2019 | Comments (0)

Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii hasa kwamba mwili wa mwanadamu umepotoshwa ndiyo maana Mungu amemfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mlengwa wa upotovu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa pekee wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, ni lazima Mungu awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi. Mungu lazima awe mwili ili Aweze kufanya kazi Yake kwa ufanisi kwa sababu mwanadamu ... Read more »

Views: 102 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 08.29.2019 | Comments (0)

Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu punde mwanadamu alipopotoshwa. Kwa maneno mengine, usimamizi wa Mungu wa mwanadamu ulianza kutokana na kazi ya kum ... Read more »

Views: 115 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 08.28.2019 | Comments (0)

Kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, bila shaka, ikirejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu. Sizungumzii kazi ambayo inatokana na matakwa ya mwanadamu bali kazi ya mitume, watendaji kazi au ndugu wa kawaida waliopo katika mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu. Hapa, kazi ya mwanadamu hairejelei kazi ya Mungu mweny ... Read more »

Views: 124 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 08.27.2019 | Comments (0)

Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. Mara chache watu humwamini Mungu ili waishi maisha ya maana, wala hamna wale ambao wanaamini kwamba kwa kuwa mwanadamu yu hai, anapaswa ampende Mungu kwa kuwa ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya dunia kufanya hivyo, na ni wito wa asili wa mwanadamu. Kwa njia hii, ingawa watu tofauti kila mmoja hufu ... Read more »

Views: 113 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 08.26.2019 | Comments (0)

Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde unapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia kwako kutakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kufuatilia kwako. Kwa njia hiyo, uzoefu na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua taswira nzima kwa ukamilifu, hutapoteza kitu maishani na hutapotea. Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo. Huwezi kugeuka baada ya siku chache tu na hutaweza kuipata njia mwafaka hata katika majuma machache. Je, si hili linakur ... Read more »

Views: 107 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 08.25.2019 | Comments (0)

Kazi ya Mungu mwenye mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na wakamsulubisha Yesu msalabani. Mara ya pili, pia, watu pia hawakuamini ndani Yake, wala kumfahamu, na kwa mara nyingine wakamsulubisha Kristo msalabani. Je, mwanadamu si adui wa Mungu? Kama mwanadamu hamjui Yeye, mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Na anawezaje kuwa na sifa za kumshuhudia Mungu? Je, si madai ya kumpenda Mungu, kumtumikia Mungu, kumtukuza Mungu yote ni udanganyifu? Kama unayatoa maisha yako kwa haya mambo yasiyokuwa na uhalisi, yasiyoweza kutekelezeka, huoni kama unafanya kazi bure? Unawezaje kuwa mwandani wa Mun ... Read more »

Views: 101 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 08.24.2019 | Comments (0)

Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala A ... Read more »

Views: 102 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 08.23.2019 | Comments (0)

Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo hayo yote na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani. Kadri aina hii ya kuadibu na kuhukumu inavyozidi, ndivyo moyo wa binadamu unavyoweza kujeruhiwa zaidi na ndivyo roho yake inavyoweza kuzinduliwa zaidi. Kuzindua roho za watu hawa waliopoto ... Read more »

Views: 101 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 08.22.2019 | Comments (0)

« 1 2 ... 14 15 16 17 18 ... 28 29 »