Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama ... Read more »

Views: 112 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 09.10.2019 | Comments (0)

Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale am ... Read more »

Views: 102 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 09.09.2019 | Comments (0)

Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushirikiane kuhusu mada ya kumfuata Mungu. Lakini, lazima Niwakumbushe wote wanaoyasoma maneno haya kwamba neno la Mungu huelekezwa kwa wale wanaomtambua na wale wanaomfuata Mungu, na sio kwa watu wote wa ulimwengu, wakiwemo wale wasiomtambua Mungu. Ikiwa unaamini kuwa Mungu Anazungumza na halaiki, ya kuwa ... Read more »

Views: 103 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 09.08.2019 | Comments (0)

Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi ambayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi. Watu, ambao wamepotoshwa, wote huishi katika mtego wa Shetani, wao kuishi katika mwili, kuishi katika tamaa za ubinafsi, na hakuna hata mmoja kati yao anayelingana na Mimi. Kuna wale ambao wanasema kwamba wao wanalingana na Mimi, lakini ambao wote huabudu sanamu zisizo yakini. Ingawa wanakubali jina Langu kama takati ... Read more »

Views: 84 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 09.07.2019 | Comments (0)

Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati ya hawa wafuasi wote, kuna wale wanaohudumu kama makuhani, wale wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Nawagawa katika makundi haya tofauti kwa msingi wa uaminifu wanaonionyesha. Wakati wanadamu wote wameainishwa kulingana na aina zao, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu. Moja baada ya mwingine, Nayaita makundi ya wale Ningependa kuwaokoa kurejea katika nyumba Yangu, kisha Nawaruhusu watu hawa wote wakubali kaz ... Read more »

Views: 105 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 09.06.2019 | Comments (0)

Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kii ... Read more »

Views: 106 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 09.05.2019 | Comments (0)

Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Ilikuwa kwa sababu ya upotovu wa binadamu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake, na ilikuwa pia kwa sababu ya uasi wa malaika mkuu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake. Iwapo Mungu hatamshinda Shetani na kuokoa binadamu, ambao wamepotoshwa, Mungu hatawahi tena kuweza kuingia rahani. Mungu anako ... Read more »

Views: 106 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 09.04.2019 | Comments (0)

Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo; mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kusimamia vitu mwenyewe, na huna ustadi juu yako mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinashikiliwa katika mikono Yake. Kama kazi ya Mungu ilimkimu mwanadamu kwa kumpa hatima, hatima ya ajabu, kabla ya wakati, na kama Mungu alitumia hii kumshawishi mwanadamu na kusababisha mwanadamu kumfuata Yeye—kama Yeye alifanya mpan ... Read more »

Views: 89 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 09.03.2019 | Comments (0)

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya M ... Read more »

Views: 107 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 09.02.2019 | Comments (0)

Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu. Hivyo basi, mwanadamu hana uwezo wa kujitenga na ... Read more »

Views: 87 | Added by: flickrpinquorettfb | Date: 09.01.2019 | Comments (0)

« 1 2 ... 13 14 15 16 17 ... 28 29 »