8:55 AM
Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii

Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii

1. Mwanadamu hapaswi kujitukuza wala kujipa sifa. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu.

2. Unapaswa kufanya lolote ambalo lina manufaa kwa kazi ya Mungu, na hupaswi kufanya chochote ambacho kitaleta madhara kwa manufaa ya kazi ya Mungu. Unapaswa kutetea jina la Mungu, ushahidi Wake, na kazi ya Mungu.

3. Pesa, vitu vya dunia, na mali yote ambayo yako katika kaya ya Mungu ni sadaka ambazo zinapasa kutolewa na binadamu. Sadaka hizi hazifai kufurahiwa na binadamu yeyote ila kasisi na Mungu Mwenyewe, kwani sadaka zinazotolewa na binadamu ni za kufurahiwa na Mungu, Mungu pekee ndiye Anayeweza kumgawia kasisi sadaka hizi, na hakuna mwingine yeyote aliyehitimu wala kuwa na haki ya kufurahia sehemu yoyote ya sadaka hizi. Sadaka zote zinazotolewa na mwanadamu (ikiwemo pesa na vitu vinavyoweza kufurahiwa) vinapewa Mungu, na sio kwa mwanadamu. Na hivyo, vitu hivi havipaswi kufurahiwa na mwanadamu; iwapo mwanadamu angevifurahia vitu hivi, basi angekuwa anaiba sadaka. Yeyote yule atakayefanya hili ni msaliti kama Yuda, kwa kuwa, zaidi ya Yuda kuwa msaliti. Yuda alijitwalia vilivyokuwa katika mfuko wa hela.

4. Mwanadamu anayo tabia ya upotovu na, zaidi ya hayo, amejawa na hisia. Kwa hivyo, ni marufuku kabisa kwa watu wa jinsia mbili tofauti kufanya pamoja kazi wakati wa kumtumikia Mungu. Yeyote yule atakayepatikana na kosa hili atatupiliwa mbali, bila ubaguzi—na hakuna atakayeepuka hili.

5. Hupaswi kumhukumu Mungu, au kujadili kwa kawaida mambo yanayomuhusu Mungu. Unapaswa kutenda vile mwanadamu anavyopaswa kutenda, na kuzungumza jinsi mwanadamu anapasa kuzungumza, na hupaswi kuvuka upeo wako wala kuvuka mipaka yako. Uchunge ulimi wako na uwe mwangalifu na hatua zako. Yote haya yatakuzuia kufanya jambo lolote linaloweza kukosea tabia ya Mungu.

6. Unapaswa kufanya yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu, na kutenda wajibu wako, na kutimiza majukumu yako, na kushikilia jukumu lako. Kwa sababu unaamini katika Mungu, unapasa kutoa mchango wako kwa kazi ya Mungu; kama huwezi, basi wewe hufai kula na kunywa maneno ya Mungu, na hufai kuishi katika nyumba ya Mungu.

7. Katika kazi na mambo yanayohusiana na kanisa, kando na kumtii Mungu, katika kila kitu unapaswa kufuata maagizo ya mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu. Hata kosa lolote hata liwe dogo kivipi halikubaliwi. Lazima uwe mkamilifu katika kutii kwako, na hupaswi kuchunguza kati ya mazuri na mabaya; yaliyo mazuri au mabaya hayakuhusu. Unapaswa kujishughulisha tu na utiifu kamili.

8. Watu wanaoamini katika Mungu wanapaswa kumtii na kumwabudu. Hupaswi kusifu au kumwabudu mtu yeyote; hupaswi kumpa Mungu nafasi ya kwanza, binadamu unayemheshimu nafasi ya pili, kisha wewe mwenyewe nafasi ya tatu. Mtu yeyote asishikilie nafasi yoyote moyoni mwako, na hufai kuzingatia watu—hasa wale unaowaenzi—kuwa katika kiwango sawa na Mungu, kuwa sawa na Yeye. Mungu hawezi kustahimili hili.

9. Mawazo yako yanapasa kuwa ya kazi ya kanisa. Unapaswa kuweka kando matarajio ya mwili wako, uwe na msimamo thabiti kuhusu mambo ya kifamilia, na ujitoe kwa moyo wako wote kwa kazi ya Mungu, na uiweke kazi ya Mungu kwanza kisha maisha yako katika nafasi ya pili. Huu ndio mwenendo mwema wa utakatifu.

10. Jamaa zako (watoto, mke au mume, dada zako au wazazi wako na kadhalika) wasio wa imani yako hawapaswi kulazimishwa kuja kanisani. Nyumba ya Mungu haina ukosefu wa washirika, na hakuna haja ya kuijaza na watu wasiokuwa na maana katika nyumba Yake. Wale wote wasioamini kwa moyo mchangamfu, hawapaswi kuongozwa kuingia kanisani. Amri hii inaelekezwa kwa kila mwanadamu. Kuhusu hili jambo mnapaswa kuchunguza, mfuatilie na mkumbushane, na hakuna anayepasa kukiuka amri hii. Hata jamaa wako wasio wa imani yako wanapoingia kanisani shingo upande, hawapaswi kupatiwa jina jipya wala kupewa vitabu vya kanisa; watu kama hao si wa kaya ya Mungu, na kuingia kwao kanisani kunapaswa kukomeshwa kwa udi na uvumba. Iwapo matatizo yataletwa kanisani kwa sababu ya uvamizi wa mapepo, basi wewe mwenyewe utafukuzwa au kuwekewa vikwazo. Kwa ufupi, kila mmoja analo jukumu katika hili jambo, lakini pia hupasi kuwa asiyejali, wala kutumia jambo hili kulipiza kisasi cha kibinafsi.

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Views: 78 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme, maisha ya kanisa, ujio wa pili wa Yesu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar