9:36 AM
Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII ” Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII ” Sehemu ya Kwanza

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.

Maudhui ya video hii:

Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu. Kuhusiana na kumjua Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, sehemu ya kwanza tuliyoijadili ni ipi? (Mamlaka ya Mungu.) Ya pili ilikuwa ni ipi? (Tabia ya haki ya Mungu.) Na ya tatu? (Utakatifu wa Mungu.) Tumejadili mara ngapi kuhusu mamlaka ya Mungu? Je, imewacha wazo kwako? (Mara mbili.) Je kuhusu tabia ya haki ya Mungu? (Mara moja.) Idadi ya safari tulizojadili utakatifu wa Mungu pengine imeacha wazo kwako, lakini maudhui mahususi tuliyojadili kila mara yamewacha wazo kwako? Katika sehemu ya kwanza “mamlaka ya Mungu,” kitu kipi kimeacha wazo wa kina sana kwako, ni sehemu gani imekuwa na matokeo makubwa kwako? (Mungu kwanza alizungumza juu ya mamlaka na nguvu ya neno la Mungu; Mungu ni mwema kama neno Lake na neno Lake litakuwa kweli. Hiki ndicho kiini kabisa cha Mungu.) (Mamlaka ya Mungu yapo katika uumbaji Wake wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Hakuna mtu anaweza kugeuza mamlaka ya Mungu. Mungu ni Mtawala wa vitu vyote na Anadhibiti vitu vyote.) (Mungu anatumia upinde wa mvua na maagano pamoja na mwanadamu.) Haya ni maudhui mahususi. Kulikuwa na kitu kingine? (Maagizo ya Mungu kwa Shetani kwamba anaweza kumjaribu Ayubu, lakini hawezi kuchukua uhai wake. Kutokana na hili tunayaona mamlaka ya neno la Mungu.) Huu ni uelewa mlioupata baada ya kusikia ushirika. Je, kuna kitu kingine cha kuongeza? (Hasa tunatambua kwamba mamlaka ya Mungu yanawakilisha hali na nafasi ya kipekee ya Mungu, na hakuna viumbe vilivyoumbwa au ambavyo havijaumbwa vinaweza kuwa na mamlaka Yake.) (Mungu anazungumza kuweka agano na mwanadamu na Anazungumza kuweka baraka Zake juu ya mwanadamu, hii yote ni mifano ya mamlaka ya neno la Mungu.) (Tunayaona mamlaka ya Mungu katika uumbaji wa mbingu na nchi, na vitu vyote kupitia neno Lake, na kwa Mungu katika mwili tunaona pia neno Lake linabeba mamlaka ya Mungu, hizi zote ni alama za upekee wa Mungu. Tunaona pale ambapo Bwana Yesu alimwamuru Lazaro kutoka kaburini kwamba uhai na kifo vipo chini ya udhibiti wa Mungu, ambavyo Shetani hana uwezo wa kudhibiti na kwamba haijalishi kazi ya Mungu inafanyika katika mwili au katika Roho, mamlaka Yake ni ya pekee.) Je, mna kitu chochote kingine cha kuongezea? (Tunaona kwamba awamu sita ya maisha huamuliwa na Mungu.) Vizuri sana! Tunapozungumza kuhusu mamlaka ya Mungu, mnaelewa nini kuhusu neno “mamlaka”? Ndani ya mawanda ya mamlaka ya Mungu, katika kile ambacho Mungu anafanya na kufichua, watu wanaona nini? (Tunauona ukuu na hekima ya Mungu.) (Tunaona kwamba mamlaka ya Mungu yapo siku zote na kwamba kweli, kweli yapo.) (Tunayaona mamlaka ya Mungu kwa upana kwenye utawala Wake juu ya mbingu, na tunayaona kwa ufinyu kadri anavyodhibiti maisha ya binadamu. Kutoka kwa awamu sita ya maisha tunaona kwamba Mungu kweli anapanga na kudhibiti kila kipengele cha maisha yetu.) (Aidha, tunaona kwamba mamlaka ya Mungu yanamwakilisha Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, na hakuna viumbe vilivyoumbwa au ambavyo havijaumbwa vinaweza kuwa nayo. Mamlaka ya Mungu ni alama ya hadhi Yake.) “Alama za hadhi ya Mungu na nafasi ya Mungu,” mnaonekana kuwa na uelewa wa kimafundisho wa maneno haya. Nimewauliza swali gani, mnaweza kulirudia? (Katika kile ambacho Mungu anafanya na kufichua, tunaona nini?) Unaona nini? Inaweza kuwa unaona tu mamlaka ya Mungu? Je, mlihisi tu mamlaka ya Mungu? (Tunauona uhalisia wa Mungu, hali ya ukweli wa Mungu, hali ya uaminifu wa Mungu.) (Tunaiona hekima ya Mungu.) Hali ya uaminifu wa Mungu, hali ya ukweli wa Mungu, na mtu fulani alisema hekima ya Mungu. Kuna kingine kipi? (Uweza wa Mungu.) (Kuiona haki na wema wa Mungu.) Bado hamjagusa kiini chenyewe, hivyo fikirieni kidogo zaidi. (Mamlaka na nguvu za Mungu vinafichuliwa na kuakisiwa katika kumwajibikia, kumwongoza, na kumsimamia binadamu. Hii ni halisi kabisa na kweli. Siku zote anafanya kazi Yake na hakuna viumbe vilivyoumbwa na ambavyo havikuumbwa vinaweza kuwa na mamlaka na nguvu hizi.) Ninyi nyote mnaangalia kwenye matini zenu? Je, kweli una maarifa yoyote ya mamlaka ya Mungu? Kuna yeyote kati yenu ambaye kweli ameelewa mamlaka Yake? (Mungu ametuangalia na kutulinda tangu tukiwa wadogo, na tunayaona mamlaka ya Mungu katika hilo. Hatukujua kuhusu hatari zilizotupata, lakini Mungu siku zote alikuwa anatulinda kisiri; haya pia ni mamlaka ya Mungu.) Vizuri sana, imesemwa vyema.

Views: 73 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Utakatifu wa Mungu, neno la Mungu, Mamlaka ya Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar