7:31 PM
Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu Maneno ya Mungu katika

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X  Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu

 

Matamshi ya Mwenyezi Mungu

Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini? Baada ya Mungu kuumba vitu vyote na baada ya kuwepo wanadamu, Mungu alichagua kundi la watu ambao walimfuata, na wanaitwa tu “wateule wa Mungu.” Kuna mipaka maalum na umuhimu katika uchaguzi wa Mungu wa watu hawa. Mipaka ni kwamba kila wakati Mungu anafanya kazi muhimu ni lazima waje—ambacho ni kitu cha kwanza kati ya vinavyowafanya maalum. Na umuhimu wao ni gani? Kuchaguliwa kwao na Mungu kunamaanisha kuwa wana umuhimu mkubwa. Yaani, Mungu angelipenda kuwafanya hawa watu timilifu, na kuwafanya wakamilifu, na baada ya kazi Yake ya usimamizi kuisha, Atawachukua watu hawa. Je, umuhimu huu si mkubwa? Kwa hiyo, hawa wateule ni wa umuhimu mkubwa kwa Mungu, kwa kuwa ni wale ambao Mungu anakusudia kuwapata. Lakini watendaji huduma—vyema, hebu tuachane na uamuzi uliokwisha kufanywa na Mungu, na kwanza tuzungumzie asili yao. Maana ya kawaida ya “mtendaji huduma” ni mtu anayehudumu. Wanaohudumu ni wa kupita; hawahudumu kwa muda mrefu, au milele, ila wanaajiriwa au kuandikwa kwa muda mfupi. Wengi wao wanachaguliwa kutoka miongoni mwa wasioamini. Wajapo duniani ndipo inapoamriwa kwamba watachukua nafasi ya watendaji huduma katika kazi ya Mungu. Wanaweza kuwa walikuwa mnyama katika maisha yao yaliyopita, lakini pia wanaweza kuwa walikuwa mmoja wa wasioamini. Hiyo ndiyo asili ya watendaji huduma.

Unaweza Pia Kupenda:  Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki "Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19"

 

Views: 113 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Mungu Mwenyewe, Maneno ya Mungu, Mamlaka ya Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar