7:04 AM
Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Nane”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Nane”

Mwenyezi Mungu anasema: “Yote yatakamilika na maneno Yangu; hakuna mwanadamu atakayekula, na hakuna mwanadamu anayeweza kufanya kazi ambayo Nitaifanya. Nitaifanya hewa ya nchi yote iwe safi na Nitatoa madoadoa yote ya mapepo duniani. Tayari Nimeanza, na Nitaanza hatua ya kwanza ya kazi Yangu ya kuadibu katika makazi ya joka kuu jekundu. Hivyo inaweza kuonekana kuwa kuadibu Kwangu kumeifikia dunia nzima, na lile joka kuu jekundu na mapepo yote machafu yatashindwa kuepuka kuadibu Kwangu, kwa kuwa Ninaziangalia nchi zote. Kazi Yangu duniani itakapokamilika, hapo ndipo, kipindi cha hukumu Yangu kitakamilika, Nitamuadibu kirasmi lile joka kuu jekundu. Watu Wangu wataona kuadibu Kwangu kwa haki kwa lile joka kuu jekundu, watamwaga sifa mbele kwa sababu ya haki Yangu, na milele watalisifu jina Langu takatifu kwa sababu ya haki Yangu. Hivyo basi, mtatenda wajibu wenu kirasmi, na mtanisifu kirasmi kotekote katika nchi, milele na milele!”

Zaidi:  Neno la Mungu “Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?”

Views: 37 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: matamshi ya Mungu, Roho Mtakatifu, hukumu ya siku za mwisho | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar