7:46 AM
Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Tano”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Tano”

Mwenyezi Mungu anasema, “Machoni Pangu, mwanadamu ndiye mtawala wa vitu vyote. Nimempa mamlaka si haba, Nikimwezesha kusimamia vitu vyote duniani—nyasi iliyo juu ya milima, wanyama katika misitu, na samaki majini. Badala ya kuwa na furaha kwa sababu ya haya, mwanadamu anasumbuliwa na wasiwasi. Maisha yake yote ni yale ya maumivu makali, na kukimbia hapa na pale, na raha kuongezwa kwa utupu, na katika maisha yake yote hakuna uvumbuzi na uundaji mpya. Hakuna anayeweza kujinasua kutoka katika utupu huu wa maisha, hakuna ambaye amegundua maisha ya maana, na hakuna ambaye amepitia maisha ya kweli. Ingawa watu wa leo wote wanaishi chini ya mwanga Wangu unaong’aa, hawajui lolote kuhusu maisha ya mbinguni. Nisipokuwa na huruma kwa mwanadamu na Nisipomwokoa binadamu, basi watu wote wamekuja bure, maisha yao duniani hayana maana, na wataondoka bure, bila chochote cha kujigamba nacho. Watu wa kila dini, nyanja ya jamii, taifa, na dhehebu wote wanajua utupu ulio duniani, na wote wananitafuta na kungoja kurejea Kwangu—ilhali nani ana uwezo wa kunifahamu nitakapofika? Nilitengeneza vitu vyote, niliumba binadamu, na leo nimeshuka kati ya mwanadamu. Mwanadamu, lakini, anagonga nyuma Yangu, na kulipisha kisasi Kwangu. Je, kazi Ninayofanya kwa mwanadamu haina faida yoyote kwake? Je, Mimi hakika sina uwezo wa kumtosheleza mwanadamu? Mbona mwanadamu ananikataa? Mbona mwanadamu ni baridi na hana hisia Kwangu? Mbona ardhi imejawa na ‘maiti’? Je, hii ndiyo hali ya dunia Niliyomtengenezea mwanadamu? Mbona Nimempa mwanadamu mali isiyo ya kufananishwa, ilhali ananipa Mimi mikono miwili mitupu? Mbona mwanadamu hanipendi kwa kweli? Mbona haji kamwe mbele Zangu? Maneno Yangu yote yamekuwa ya bure? Je, maneno yamepotea jinsi joto lipoteavyo kwa maji? Mbona mwanadamu hataki kushirikiana na Mimi? Je, wakati wa kufika kwa siku Yangu ni wakati wa kufa kwa mwanadamu kweli? Je, hakika Ningeweza kumwangamiza mwanadamu wakati ufalme Wangu utatengenezwa? Mbona, wakati wa mpango Wangu wa usimamizi wote, hakuna ambaye ameweza kuelewa nia Zangu? Mbona, badala ya kuyatunza matamshi ya kutoka kwa mdomo Wangu, mwanadamu anayachukia na kuyakataa? Simkashifu yeyote, ila tu Nawafanya watu wote watulie na kutekeleza kazi ya kujiangalia kwa undani.”

Unaweza Pia Kupenda: Ishara za siku za mwisho hukusanya habari kama vile mwezi damu, majanga na vita kujulisha dalili za siku za mwisho zilizotabiriwa katika Biblia zimeonekana moja baada ya yengine, na ni wakati wa kukaribisha kuja kwake Yesu kwa mara ya pili.

Views: 104 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Maneno ya Mungu, Kanisa na Dini, Mamlaka ya Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar