6:00 PM
Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Mbili”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Mbili”

Matamshi ya Mungu:

Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo. Kwa sababu dunia nzima imefunikwa kwa ukungu, Ninapotazama kutoka mawinguni, kuwepo Kwangu hakujawahi kutambuliwa na mwanadamu; mwanadamu anatafuta kitu fulani duniani, anaonekana akichakura, anayo nia, inaonekana, ya kusubiri kurudi Kwangu—ilhali yeye hajui siku Yangu, na anaweza tu kutegemea mara kwa mara mwanga unaong’aa mashariki. Miongoni mwa watu wote, Ninatafuta wale wanaoupendeza moyo Wangu kwa kweli. Natembea miongoni mwa watu wote, na kuishi miongoni mwa watu wote, lakini mwanadamu yuko salama salimini duniani, na kwa hivyo hakuna wanaopendeza nafsi Yangu kwa kweli. Watu hawajui jinsi ya kuyajali mapenzi Yangu, hawawezi kuona matendo Yangu, na hawawezi kutembea katika mwanga na kumulikwa na mwanga huo. Hata ingawa mwanadamu daima anayathamini maneno Yangu, yeye hana uwezo wa kuona katika mikakati ya udanganyifu ya Shetani; kwa kuwa kimo cha mwanadamu ni kidogo sana, hana uwezo wa kufanya vile ambavyo moyo wake unatamani. Mwanadamu hajawahi kunipenda kwa dhati. Ninapompandisha, yeye hujiona asiyefaa, lakini hili halimfanyi awe na ari ya kuniridhisha. Yeye hushikilia tu kituo Nilichompa mikononi mwake na kukichunguza; bila hisia yoyote kwa uzuri Wangu, yeye anasisitiza badala yake kujijaza na baraka za kituo chake. Je, huu sio upungufu wa mwanadamu? Milima inaposonga, je, inaweza kubadili mkondo kwa ajili ya kituo chako? Maji yanaposonga, je, yanaweza kukoma tu kabla ya kufikia kituo chako? Je, mbingu na dunia zinaweza kubadilishwa na kituo chako? Wakati mmoja Nilikuwa mwenye huruma kwa mwanadamu, mara kwa mara—ilhali hakuna anayependa kwa dhati wala kuthamini haya, waliyasikiliza tu kama hadithi, au waliisoma tu kama tamthilia. Je, maneno Yangu hayauguzi moyo wa mwanadamu? Je, matamshi Yangu kwa kweli hayaleti mabadiliko yoyote? Inawezekana kuwa hakuna anayeamini katika kuwepo Kwangu? Mwanadamu hajipendi mwenyewe; badala yake, anaungana na Shetani ili kunivamia Mimi, na kumtumia Shetani kama “chombo” cha kunitumikia Mimi. Nitapenyeza katika mipango yote ya Shetani, na kuwazuia watu wote wa duniani dhidi ya kukubali uongo wa Shetani, ili wasije wakaniasi Mimi kwa ajili ya kuwepo kwa Shetani.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu hutoa ushuhuda wa mamlaka Yake, tabia yenye haki, kiini kitakatifu, kupelekea binadamu kumwelewa Mungu Mwenyewe wa peke na kuanza kutembea kwenye njia ya kumjua!

Unakaribishwa kupakua programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu.

Views: 96 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: matamshi ya Mungu, Kusikia Sauti ya Mungu, Maneno ya Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar