2:19 PM
Kazi na Kuingia (6)

Kazi na kuingia kwa uhalisia ni vya kiutendaji na vinarejelea kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu. Mwanadamu kukosa kabisa uelewa juu ya sura halisi ya Mungu na kazi ya Mungu kumesababisha shida kubwa katika kuingia kwake. Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu Anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi. Mwanadamu hajui chochote kuhusu lengo la kazi ya Mungu, wala kusudi la mpango wa Mungu kwa ajili ya siku za mwisho. Kwa sababu mbalimbali, watu daima wanakuwa vuguvugu katika kuingia ambako Mungu anataka na wanabakia wenye shaka[1], kitu ambacho kimeleta shida kubwa katika kazi ya Mungu katika mwili. Watu wanaonekana kuwa vizuizi na, leo hii, bado wanakuwa hawana uelewa sahihi. Kwa hiyo Nitazungumza juu ya kazi ambayo Mungu anafanya kwa mwanadamu, na makusudi ya Mungu ya haraka, ili kwamba nyinyi nyote muwe watumishi waaminifu wa Mungu ambao, kama Ayubu, ni bora ufe kuliko kumkataa Mungu na utastahimili kila fedheha, na ambao, kama Petro, mtatoa utu wenu wote kwa Mungu na kuwa wandani ambao Mungu Aliwapata katika siku za mwisho. Ninawasihi kaka na dada kufanya kila kitu kilichopo ndani ya uwezo wao kutoa utu wao wote kwa mapenzi ya mbingu ya Mungu, kuwa watumishi watakatifu katika nyumba ya Mungu, na kufurahia ahadi zisizokuwa na kikomo zilizotolewa na Mungu, ili kwamba moyo wa Mungu Baba ufurahie pumziko la amani. “Kukamilisha mapenzi ya Mungu Baba” kunapaswa kuwe wito wa wote wanaompenda Mungu. Maneno haya yanapaswa kutumika kama mwongozo wa mwanadamu kwa ajili ya kuingia na dira inayoongoza matendo yake. Hili ndilo suluhisho ambalo mwanadamu anapaswa kuwa nalo. Kukamilisha kabisa kazi ya Mungu duniani na kushirikiana na kazi ya Mungu katika mwili—huu ni wajibu wa mwanadamu. Siku moja, kazi ya Mungu itakapokuwa imekamilika, mwanadamu atamuaga Anaporudi mapema kwa Baba yake mbinguni. Je, huu sio wajibu ambao mwanadamu anapaswa kuutimiza?

Wakati ambapo, katika Enzi ya Neema, Mungu alirudi kwa mbingu ya tatu, kazi ya Mungu ya kuwakomboa wanadamu wote ilikuwa kwa kweli tayari imeendelea katika tendo lake la kumaliza. Vyote vilivyobaki duniani vilikuwa msalaba ambao Yesu aliubeba, sanda ya kitani ambayo Yesu alifungiwa ndani, na taji ya miiba na joho la rangi nyekundu ambavyo Yesu alivaa (hivi vilikuwa vitu ambavyo Wayahudi walitumia kumdhihaki Yeye). Yaani, kazi ya kusulubiwa kwa Yesu ilikuwa imesababisha ghasia kwa muda na kisha ikatulia. Tangu wakati huo na kuendelea, wanafunzi wa Yesu wakaanza kuendeleza kazi Yake, wakiyachunga na kunyunyizia katika makanisa kila mahali. Maudhui ya kazi yao yalikuwa haya: kuwafanya watu wote watubu, waungame dhambi zao, na wabatizwe; mitume wote wakieneza hadithi ya ndani ya kusulubiwa kwa Yesu na kile kilifanyika kwa kweli, kila mtu asiweze kujizuia kuanguka chini mbele za Yesu kuungama dhambi zake, na zaidi ya hayo mitume wakieneza kila mahali maneno yaliyonenwa na Yesu na sheria na amri Alizozianzisha. Kuanzia wakati huo ujenzi wa makanisa ulianza katika Enzi ya Neema. Kile ambacho Yesu alizungumzia wakati wa enzi hiyo pia kililenga maisha ya mwanadamu na mapenzi ya Baba wa mbinguni. Ni kwa sababu tu enzi hizo ni tofauti ndiyo nyingi za semi na matendo hayo yanatofautiana sana na ya leo. Lakini kiini cha vyote viwili ni sawa. Yote mawili si chochote ila takriban kazi ya Roho wa Mungu katika mwili. Aina hiyo ya kazi na maneno hayo yameendelea mpaka siku hii, na ndiyo maana kile ambacho bado kinashirikishwa katika makanisa ya leo ya dini ni kitu cha aina hiyo na hakijabadilika kabisa. Wakati ambapo kazi ya Yesu ilifika mwisho, njia sahihi ya Yesu Kristo ilikuwa inaanza kuwa na athari duniani, lakini Mungu alianza mipango ya hatua nyingine ya kazi Yake, jambo la kupata mwili katika siku za mwisho. Kwa mwanadamu, Mungu kusulubiwa kulihitimisha kazi ya Mungu kupata mwili, Aliwakomboa binadamu wote, na Akamruhusu kuteka ufunguo wa Kuzimu. Kila mtu anadhani kwamba kazi ya Mungu imekamilika kikamilifu. Kwa uhalisia, kwa Mungu, ni sehemu ndogo tu ya kazi Yake ndiyo imekamilika. Amemkomboa tu binadamu; Hajamshinda mwanadamu, wala kubadilisha ubaya wa Shetani kwa binadamu. Hiyo ndio maana Mungu Anasema, “Ingawa mwili Wangu ulipitia maumivu ya kifo, hilo sio lengo lote la Mimi kupata mwili. Yesu ni Mwana Wangu mpendwa na Alisulubishwa msalabani kwa ajili Yangu, lakini hakukamilisha kikamilifu kazi Yangu. Alifanya tu sehemu.” Hivyo Mungu Akaanza mpango wa mzunguko wa pili ili kuendeleza kazi ya Mungu kupata mwili. Lengo kuu la Mungu ni kumkamilisha na kumpata kila mmoja aokolewe kutoka katika mikono ya Shetani, hiyo ndiyo sababu Mungu Alijiandaa tena kujihatarisha kuja katika mwili. Kinachoitwa “kupata mwili” kinaashiria kutochukua utukufu (kutochukua utukufu kwa sababu kazi ya Mungu bado haijamalizika), lakini kuonekana katika utambulisho wa Mwana mpendwa, na kwamba Yeye ni Kristo, ambaye Mungu amependezwa naye. Ndiyo maana hili linasemekana kuwa ni kuhatarisha. Mwili ni wa nguvu kidogo sana na lazima utahadhari sana,[2] tofauti sana na mamlaka ya Baba wa mbinguni, na Yeye hutimiza tu huduma ya mwili, Akifanikisha kazi na agizo la Mungu Baba bila kujihusisha katika kazi nyingine. Yeye hufanikisha tu sehemu moja ya kazi. Hii ndiyo maana Mungu anaitwa “Kristo” alipokuja duniani. Hii ndiyo maana ya ndani. Sababu ya kusema kwamba kuja huko kunaandamana na majaribu ni kwa kuwa mradi wa kazi mmoja pekee ndio unafanikishwa. Zaidi ya hayo, sababu Mungu Baba humwita tu “Kristo” na “Mwana mpendwa” na Hajampa utukufu wote ni hasa kwa vile mwili uliokuwa mwili huja kufanya mradi wa kazi moja, sio kumwakilisha Baba aliye mbinguni, bali kutimiza huduma ya Mwana mpendwa. Mwana mpendwa atakapomaliza agizo lote Alilokubali kubeba juu ya mabega Yake, Baba atampa Yeye utukufu kamili pamoja na utambulisho wa Baba. Mtu anaweza kusema kwamba hii ni kanuni ya mbinguni. Kwa sababu Yule ambaye amekuja katika mwili na Baba aliye mbinguni wako katika hali mbili tofauti, hao wawili huonana tu katika Roho, Baba akimtazama kwa makini Mwana mpendwa lakini Mwana asiweze kumwona Baba kutoka mbali. Ni kwa sababu kazi ya mwili ni ndogo sana na Ana uwezo wa kuuawa wakati wowote, kwamba kuja huku kunasemekana kuambatana na hatari kuu. Hii ni sawa na Mungu mara tena kumwachilia Mwana Wake mpendwa na kumweka ndani ya mdomo wa chui mkubwa mwenye milia. Ni hatari kwa maisha kwamba Mungu alimweka Yeye mahali ambapo Shetani amekolea sana. Hata kwa kupata mashaka kama hayo, Mungu bado alimkabidhi Mwana Wake mpendwa kwa watu wa mahali pachafu, fisadi ili wao “wamlee.” Hii ni kwa sababu ni njia pekee ya kazi ya Mungu kuleta maana kabisa na njia pekee ya kutimiza mapenzi yote ya Mungu Baba na kufanikisha sehemu ya mwisho ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Yesu alifanikisha tu hatua moja ya kazi ya Mungu Baba. Kwa sababu ya kizuizi cha mwili uliopata mwili na tofauti katika kazi iliyofanikishwa, Yesu Mwenyewe hakujua kwamba kungekuwa na kurudi kwa pili kwa mwili. Hivyo hakuna yeyote ambaye amesoma maelezo ya historia kumhusu Yeye amewahi kutambua Yesu akitabiri kwamba Mungu anataka kuwa mwili Mwenyewe mara ya pili ili kumaliza kazi Yake yote katika mwili. Kwa vile Yesu hata hakujua kuhusu jambo hili, manabii wakuu na wafafanuzi wa maandiko pia hawajui kwamba Mungu anataka kurudi katika mwili, kumaanisha kuja katika mwili tena ili kufanya sehemu ya pili ya kazi Yake katika mwili. Kwa hivyo, hakuna anayetambua kwamba Mungu alijificha Mwenyewe katika mwili kuanzia zamani sana. Hili linaeleweka kwa sababu ilikuwa tu baada ya Yesu kufufuka na kupaa mbinguni ndiyo Akakubali agizo hili, kwa hiyo kupata mwili kwa Mungu kwa pili hakuna mzizi wala msingi na ni, kama maji yasiyo na asili, vigumu kuyashika. Zaidi ya hayo, ni vigumu kupata marejeo kwalo hata katika Biblia yenye sifa kuu.[3] Katika sura na vifungu vingi vya Biblia yote, hakuna hata sentensi moja au neno linalotaja jambo hili. Lakini kuwasili kwa Yesu duniani kulitabiriwa kitambo sana na zaidi ya hayo kulikuwa kupitia kwa utungaji mimba na Roho Mtakatifu. Hata hivyo, Mungu bado alisema ilikuwa hatari kwa maisha. Basi hilo linasema nini kuhusu leo? Si ajabu Mungu asema kwamba kupata mwili wakati huu kuna hatari mara elfu zaidi kuliko zile za wakati wa Enzi ya Neema. Katika maeneo mengi, Mungu Alitabiri kupata kundi la washindi katika nchi ya Sinim. Ni upande wa Mashariki mwa ulimwengu ambapo washindi wanapatikana, hivyo nchi ambapo Mungu kupata mwili mara ya pili Atatua bila shaka ni nchi ya Sinim, mahali ambapo joka jekundu linaishi. Hapo Mungu Atawapata warithi wa joka kuu jekundu na litashindwa na kuaibishwa. Mungu Anataka kuwaamsha watu hawa walioteseka sana, kuwaamsha kabisa, na kuwafanya waondoke katika ukungu na kulikataa joka kuu jekundu. Mungu Anataka Awaamshe kutoka katika ndoto zao, kuwafanya waelewe tabia ya joka kuu jekundu, kuutoa moyo wao wote kwa Mungu, kuinuka kutoka katika nguvu kandamizi za giza, kusimama Mashariki mwa dunia, na kuwa uthibitisho wa ushindi wa Mungu. Baada ya hapo Mungu Atakuwa Amepata utukufu. Kwa sababu hii tu, kazi ambayo ilisitishwa Israeli Mungu Aliipeleka katika nchi ambapo linakaa joka kuu jekundu na, takribani miaka elfu mbili baada ya kuondoka, Amekuja tena katika mwili ili kuendeleza kazi ya Enzi ya Neema. Mwanadamu anashuhudia kwa macho yake, Mungu Akizindua kazi mpya katika mwili. Lakini kwa Mungu, Anaendeleza kazi ya Enzi ya Neema, kwa mwachano wa miaka elfu kadhaa, na badiliko tu la eneo la kufanyia kazi na mradi wa kazi. Ingawa taswira ya mwili ambayo Mungu Ameichukua katika kazi ya leo ni mtu mwingine tofauti na Yesu, Wanashiriki hulka na mzizi mmoja, na wanatoka katika chanzo kimoja. Pengine wana tofauti za umbo la nje, lakini kweli za ndani za kazi Zao zinafanana kabisa. Hata hivyo, enzi zenyewe, ni tofauti kama ilivyo usiku na mchana. Inawezekanaje kazi ya Mungu isibadilike? Au inawezekanaje kazi ziingiliane?

Yesu alichukua umbo la Myahudi, Alifuata mavazi ya Wayahudi, na Alikua akila chakula cha Kiyahudi. Hii ni hali yake ya kawaida ya kibinadamu. Lakini Mungu katika mwili wa leo Anachukua umbo la watu wa Asia na Anakua Akila chakula cha taifa la joka kuu jekundu. Hii haiingiliani na lengo la Mungu kupata mwili. Badala yake, vinakamilishana, na zaidi vinakamilisha maana ya kweli ya Mungu kupata mwili. Kwa sababu Mungu katika mwili Anarejelewa kuwa “Mwana wa Adamu” au “Kristo,” umbo la nje la Kristo wa leo haliwezi kulinganishwa na Yesu Kristo. Hata hivyo, mwili huu unaitwa “Mwana wa Adamu” na Yupo katika sura ya mwili. Kila hatua ya kazi ya Mungu inahusisha maana ya kina sana. Sababu ya Yesu kuzaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu ni kwa sababu Alipaswa kuwakomboa wenye dhambi. Alitakiwa Asiwe na dhambi. Isipokuwa tu mwishoni Alipolazimishwa kufanana na mwili wa dhambi na kuchukua dhambi za wenye dhambi ndivyo Aliweza kuwaokoa kutoka katika laana ya msalaba ambao Mungu Alitumia kuwaadibu watu. (Msalaba ni zana ya Mungu kwa ajili ya kuwalaani na kuwarudi watu; mitajo ya kulaani na kurudi mahususi inahusu kuwalaani na kuwarudi wenye dhambi.) Lengo lilikuwa ni kuwafanya wenye dhambi wote kutubu na kutumia msalaba kuwafanya waungame dhambi zao. Yaani, kwa ajili ya kuwakomboa binadamu wote, Mungu Alijiweka Mwenyewe katika mwili uliozaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu na Akachukua dhambi za binadamu wote. Namna ya kawaida ya kuelezea hii ni kutoa mwili mtakatifu kwa kubadilishana na wenye dhambi wote, usawa wa Yesu kuwa sadaka ya dhambi umewekwa mbele ya Shetani ili “kumsihi” Shetani kuwarudisha binadamu wote wasio na hatia kwa Mungu. Hivyo ili kukamilisha hatua hii ya kazi ya wokovu kulihitaji utungaji mimba kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hili lilikuwa ni sharti la lazima, “mkataba” wakati wa vita kati ya Mungu Baba na Shetani. Hii ndio maana Yesu Alitolewa kwa Shetani, ni baada ya hapo tu ndipo hatua hii ya kazi ikahitimishwa. Hata hivyo, kazi ya ukombozi ya Mungu leo tayari ni ya umuhimu usio kifani, na Shetani hana sababu ya kufanya madai, hivyo Mungu kufanyika mwili hakuhitaji utungaji mimba kwa njia ya Roho Mtakatifu, maana Mungu kwa asili ni mtakatifu na Asiye na hatia. Hivyo Mungu mwenye mwili wa wakati huu sio tena Yesu wa Enzi ya Neema. Lakini bado Yupo kwa ajili ya mapenzi ya Mungu Baba na kwa ajili ya kutimiza matamanio ya Mungu Baba. Hii inaweza kuchukuliwaje kuwa ni msemo usiokuwa na maana? Je, ni lazima Mungu kupata mwili kufuate kanuni kadhaa?

Watu wengi wanatafuta ushahidi katika Biblia, wakitaka kutafuta unabii wa Mungu kupata mwili. Inawezekanaje fikra hafifu za mwanadamu kujua kwamba Mungu Aliacha “kufanya” kazi muda mrefu kwenye Biblia na “Ameachana” nayo na kufurahia kazi ambayo Alipanga kwa muda mrefu lakini Hakuwahi kumwambia mwanadamu? Watu wanakosa sana ufahamu. Baada tu ya kuonja tabia ya Mungu, kwa kawaida wanasimama kwenye jukwaa refu na kukaa kwenye “kiti mwendo” cha hali ya juu wakikagua kazi ya Mungu, na kwenda mbali zaidi kumfundisha Mungu kwa mazungumzo ya misamiati migumu. “Mzee” akiwa amevaa miwani na kupapasa ndevu zake, anafunua Biblia yake kuukuu ambayo amekuwa akiisoma maisha yake yote. Akimumunya maneno na kupepesapepesa macho, sasa anarudi katika Kitabu cha Ufunuo na sasa katika kitabu cha Danieli, na sasa katika Kitabu kinachojulikana sana cha Isaya. Akikodolea macho ukurasa ulioandikwa maneno mengi madogo, anasoma kimya, akili yake ikizunguka bila kupumzika. Ghafula mkono unaopapasa ndevu unasita na kuanza kuzivuta. Kila mara mtu anasikia sauti ya ndevu zikivunjika. Tabia hiyo isiyo ya kawaida inamstaajabisha mtu. “Kwa nini kutumia nguvu zote hizo? Kilichomkasirisha hivyo ni nini?” Turudi kwa mtu mzee, nyusi zake sasa zimesimama. Nyusi zenye rangi ya fedha zimeanguka kama manyoya ya bata bukini sentimita mbili kamili kutoka katika kope za mzee huyu, kama tu kwa bahati lakini kwa usahihi kabisa, mzee huyu anaendelea kukaza macho yake katika karatasi. Anarudia mtiririko huo wa matendo mara kadhaa, kisha anashindwa kuvumilia bali anasimama na kuanza kuzungumzazungumza kana kwamba anafanya porojo[4] na mtu, ingawa mwanga katika macho yake bado haujatoka katika shajara yake. Ghafula anafunika ukurasa aliokuwa anausoma na kugeukia “ulimwengu mwingine.” Mwendo wake ni wa haraka[5] sana na wa kuogopesha takribani kuwashtua watu. Sasa, panya ambaye ametoka katika shimo lake na ndio tu ameanza “kujisikia yupo huru” wakati wa ukimya wake alishtushwa sana na mizunguko yake isiyoeleweka na kukimbia kurudi kwenye shimo lake, na kutoweka bila kujua alipoelekea. Sasa mkono wa kulia wa mzee uliokuwa umetulia unarudia mwendo wake wa kupapasa ndevu juu chini. Anaondoka kwenye kiti, na kuacha kitabu mezani. Kupitia katika mlango ulio wazi kidogo na dirisha lililo wazi, upepo unaingia ndani, bila kujali unapeperusha kitabu kinajifunika, kisha kinafunguka, kinajifunika, kisha kinafunguka tena. Kuna ukiwa usioweza kuelezeka kuhusu tukio hili, isipokuwa tu kwa sauti ya kurasa za kitabu zinapopeperushwa na upepo, kila kitu kinaonekana kuwa kimya. Yeye, pamoja na mikono aliyojikumbatia kwa nyuma, anatembeatembea chumbani, sasa anasimama, sasa anaanza, anatikisa kichwa chake mara kwa mara, anaonekana kurudia kusema “Ee! Mungu! Unaweza kweli kufanya hivyo?” Muda hadi muda pia anatikisa kichwa, “Ee Mungu! Nani anaweza kuijua kazi Yako? Ni vigumu kiasi gani kuchunguza hatua Zako? Ninaamini Hufanyi vitu visivyokuwa na maana.” Sasa mzee huyu anakunja uso, macho yake anayafumba kwa nguvu, akionyesha sura iliyokasirika, pia anaonyesha maumivu makali kupita kiasi, kana kwamba anataka kutafakari taratibu. Hii kweli inampatia changamoto “mzee huyu.” Katika hatua hii ya maisha yake, “kwa bahati mbaya” amekutana na suala hili. Nini kinaweza kufanyika juu yake? Nami pia sina nguvu ya kufanya kitu chochote. Nani alifanya shajara yake kuwa “ya njano”? Nani alifanya ndevu na nyusi zake kukua bila huruma kama theluji nyeupe katika maeneo mbalimbali ya uso wake? Ni kana kwamba ndevu zake zinawakilisha usuli wake. Lakini nani angejua mwanadamu angekuwa mpumbavu kwa kiasi hiki, akitafuta uwepo wa Mungu katika shajara kuukuu? Shajara hii ya zamani inaweza kuwa na karatasi ngapi? Je, inaweza kweli kurekodi matendo yote ya Mungu? Nani anathubutu kuhakikisha hilo? Mwanadamu kimsingi anatafuta umbo la Mungu na anajaribu kutimiza mapenzi ya Mungu kwa kuchanganua zaidi maneno.[6] Je, kujaribu kuingia katika uzima kwa namna hii, ni rahisi kama inavyosikika? Je, huku sio kufikiri bila mantiki na kimakosa? Huoni hii inachekesha?

Tanbihi:

1. “wenye shaka” inaashiria kwamba watu hawana umaizi dhahiri katika kazi ya Mungu.

2. “Ni wa nguvu kidogo sana na lazima utahadhari sana” inaashiria kwamba matatizo ya mwili ni mengi sana, na kazi inayofanywa ni chache sana.

3. “Yenye sifa kuu” inasemwa kwa dhihaka. Inahusu jinsi wataalamu wengi katika hoja za uwongo za dini huabudu “shajara ya mwaka ya kale” iliyochakaa kuwa ni Mungu.

4. “Porojo” ni istiara kwa ajili ya sura mbaya ya watu wanapochunguza katika kazi ya Mungu.

5. “Haraka” inamaanisha mwendo wa hamu na wa hima wa “mzee” anapoongelea kuhusu Biblia.

6. “Kuchanganua zaidi maneno” kunatumiwa kudhihaki wataalam katika hoja za uwongo, ambao hubishana juu ya tofauti ndogondogo kuhusu maneno lakini hawautafuti ukweli au kujua kazi ya Roho Mtakatifu.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Views: 81 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: kazi ya Ukombozi, Roho Mtakatifu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar