9:49 PM
Sura ya tatizo la mwanadamu kutokubali ukweli ulioonyeshwa na Kristo ni ipi? Matokeo ya mtu kutomchukua Kristo kama Mungu ni yapi?

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Yesu akawaambia, … Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na mtatimiliza tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo, na hakudumu katika ukweli, kwa sababu ukweli haupo ndani yake. Anaponena uwongo, anazungumza yaliyo yake mwenyewe: kwani yeye ni mwongo, na baba wa uwongo. Na kwa kuwa nawaambieni ukweli, hamniamini. … Yule ambaye ni wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu: nyinyi kwa hivyo hamyasikii, kwa kuwa nyinyi si wa Mungu” (Yohana 8:42-45, 47).

“Kupitia hili ninyi mnajua Roho wa Mungu; Kila roho inayokubali kuwa Yesu Kristo amefika katika mwili ni ya Mungu: Na kila roho isiyokubali kuwa Yesu Kristo amefika katika mwili si ya Mungu: na hii ndiyo ile roho ya anayempinga Kristo” (1 Yohana 4:2-3).

“Kwa kuwa walaghai wengi wameingia ulimwenguni, ambao hawakubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili. Huyu ni mlaghai na anayempinga Kristo” (2 Yohana 1:7).

Maneno Husika ya Mungu:

Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu?

kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa

na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Yeyote asiyemwamini Mungu wa mwili—yaani, yeyote asiyeamini kazi na hotuba ya Mungu anayeonekana na haamini Mungu anayeonekana lakini badala yake anaabudu Mungu asiyeonekana mbinguni—hana Mungu katika moyo wake. Ni watu wasiomtii na wanaompinga Mungu. Watu hawa hawana ubinadamu na fahamu, kusema chochote kuhusu ukweli. Kwa watu hawa Mungu anayeonekana na kushikika hawezi kuaminika zaidi, lakini Mungu asiyeonekana wala kushikika ni Mungu wa kuaminika na pia Anayefurahisha nyoyo zao. Wanachotafuta si ukweli wa uhalisi, wala si kiini cha kweli cha uhai, wala nia za Mungu; badala yake, wanatafuta msisimko. Mambo yoyote yanayoweza kuwaruhusu kufikia tamaa zao ni, bila shaka, imani na shughuli zao. Wamwamini Mungu tu ili kuridhisha tamaa zao, si kutafuta ukweli. Hawa watu si watenda maovu? Wanajiamini sana, na hawaamini kwamba Mungu aliye mbinguni atawaangamiza, hawa “watu wazuri.” Badala yake, wanaamini kwamba Mungu atawaruhusu kubaki na, zaidi ya hayo, Atawatuza vizuri sana, kwani wamemfanyia Mungu mambo mengi na kuonyesha kiwango kikubwa cha “uaminifu” Kwake. Kama wangemtafuta Mungu anayeonekana, wangelipiza kisasi mara moja dhidi ya Mungu na kukasirika wakati hawatapata tamaa zao. Hawa ni watu waovu wanaotaka kuridhisha tamaa zao; si watu wa uadilifu wanaosaka ukweli. Watu kama hao ni wale wanaojulikana kama waovu wanaomfuata Kristo. Wale watu wasioutafuta ukweli hawawezi kuamini ukweli. Hawawezi kabisa kutambua matokeo ya baadaye ya binadamu, kwani hawaamini kazi ama hotuba yoyote ya Mungu anayeonekana, na hawawezi kuamini hitimisho la baadaye la binadamu. Hivyo, hata wakimfuata Mungu anayeonekana, bado wanatenda maovu na hawatafuti ukweli, wala hawatendi ukweli Ninaohitaji.

kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tatizo kubwa zaidi la mwanadamu ni kwamba anaweza kupenda tu vitu ambavyo hawezi kuviona au kuvigusa, vitu ambavyo ni vya siri kubwa na vya kushangaza, na kwamba haviwezi kufikiriwa na mwanadamu na haviwezi kufikiwa na mwanadamu. Kadiri vitu hivi vinavyokuwa si halisi, kadiri vinavyochambuliwa na mwanadamu, ambaye anavifuata bila kujali kitu chochote, na hujaribu kuvipata. Kadiri vinavyokuwa si halisi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kuvichunguza na kuvichambua zaidi, hata kwenda kwa kiwango cha kufanya mawazo yake ya kina kuyahusu. Kinyume chake, jinsi vitu vinavyokuwa halisi zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kuvipuuza; huviangalia kwa dharau, na hata huvitweza. Huu hasa si mtazamo weni juu ya kazi halisi Ninayoifanya leo? Kadiri mambo hayo yanavyokuwa halisi, ndivyo unavyozidi kuyadharau. Wala hutengi muda kwa ajili ya kuyachunguza, bali unayapuuza; unayadharau mambo haya halisi, yenye matakwa ya moja kwa moja, na hata unakuwa na dhana nyingi kuhusu Mungu huyu ambaye ni halisi sana, na huwezi tu kuukubali uhalisi na ukawaida Wake. Kwa njia hii, huamini katika hali isiyo dhahiri? Una imani thabiti katika Mungu asiye dhahiri wa wakati uliopita, na wala hupendi kumjua Mungu wa kweli wa leo. Hii si kwa sababu Mungu wa jana na Mungu wa leo wanatoka katika enzi tofauti? Si pia kwa sababu Mungu wa jana ni Mungu wa mbinguni aliyeinuliwa, wakati Mungu wa leo ni mwanadamu mdogo wa duniani? Aidha, si pia kwa sababu Mungu anayeabudiwa na mwanadamu ni yule aliyetokana na dhana zake, wakati Mungu wa leo ni mwili halisi uliotengenezwa duniani? Hata hivyo, si kwa sababu Mungu wa leo ni halisi sana kiasi kwamba mwanadamu hamfuatilii? Maana kile ambacho Mungu wa leo anamtaka mwanadamu afanye ni kile ambacho mwanadamu hayupo radhi kabisa kukifanya, na ambacho kinamfanya ahisi aibu. Huku sio kufanya mambo yawe magumu kwa mwanadamu? Je, hili halionyeshi makovu yake hapa? Kwa namna hii, wengi wao ambao hawafuati uhalisi wanakuwa maadui wa Mungu mwenye mwili, wanakuwa wapinga Kristo. Huu si ukweli dhahiri? Hapo zamani, wakati Mungu alikuwa hajawa mwili, inawezekana ulikuwa mtu wa dini, au msahilina. Baada ya Mungu kuwa mwili, wasahilina wengi kama hao waligeuka bila kujua na kuwa wapinga Kristo. Unajua ni nini kinachoendelea hapa? Katika imani yako kwa Mungu, hujikiti katika uhalisi au kuufuatilia ukweli, bali unashikilia sana uongo—je, si hiki ndicho chanzo wazi cha uadui wako na Mungu mwenye mwili? Mungu mwenye mwili anaitwa Kristo, hivyo sio kwamba wote ambao hawamwamini Mungu mwenye mwili ni wapinga Kristo? Je, yule unayemwamini na kumpenda ni huyu Mungu mwenye mwili kweli? Je, kweli ni huyu Mungu aliye hai ambaye ni wa halisi zaidi na ambaye ni wa kawaida kabisa? Malengo ya ufuatiliaji wako, zako ni yapi hasa? Yako mbinguni au duniani? Je, ni dhana au ni ukweli? Je, ni Mungu au ni kiumbe fulani asiyekuwa wa kawaida?

kutoka katika “Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe kawaida na wenye kutojali katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu?

kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati

Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana

katika Mwili

Wale ambao huamini tu katika Yesu Kristo lakini hawaamini katika Mungu mwenye mwili wa leo wote wamehukumiwa. Wote ni Mafarisayo wa kisasa kwa sababu hawamtambui Mungu wa leo, na wote humpinga Mungu. Bila kujali imani yao katika Yesu ni ya kujitolea kiasi gani, itakuwa bure; hawatapata sifa ya Mungu.

kutoka katika “Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu”

katika Neno Laonekana katika Mwili

Mnaamini kuwepo kwa Mungu aliye mbinguni lakini mnakataa yule Mungu aliye duniani. Hata hivyo, Sikubaliani na maoni yenu. Nawapongeza tu wale wanadamu wanaosimama imara na kumtumikia Mungu wa duniani, kamwe sio wale wasiomkiri Kristo aliye duniani. Bila kujali jinsi wanadamu kama hawa walivyo waaminifu kwa Mungu aliye mbinguni, mwishowe, hawatauepuka mkono Wangu unaoadhibu waovu. Wanadamu kama hawa ni waovu; ni wale waovu wanaompinga Mungu na hawajawahi kumtii Kristo kwa furaha. Bila shaka, idadi yao inajumuisha wale wote wasiomjua na, zaidi, wasiomkiri Kristo. Unaamini kwamba unaweza kutenda utakavyo kwa Kristo alimradi wewe ni mwaminifu kwa Mungu aliye mbinguni? Makosa! Kutomjua Kristo kwako ni kutomjua Mungu aliye mbinguni. Bila kujali uaminifu wako kwa Mungu aliye mbinguni, ni maneno matupu tu na kujifanya, kwani Mungu aliye duniani si muhimu tu kwa mwanadamu kupokea ukweli na ufahamu mkubwa zaidi, lakini hata zaidi ni muhimu kwa lawama ya mwanadamu na baadaye kwa kuushika ukweli kuwaadhibu waovu. Umeelewa matokeo yenye faida na yanayodhuru hapa? Umepata kuyapitia? Ningependa siku moja hivi karibuni ninyi muelewe ukweli huu: Kumjua Mungu, mnapaswa kumjua sio tu Mungu wa mbinguni lakini, hata muhimu zaidi, Mungu aliye duniani. Msiyachanganye yaliyo kipaumbele ama kuruhusu yaliyo ya pili kuchukua nafasi ya yaliyo ya msingi. Ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kujenga uhusiano mzuri na Mungu, kuwa karibu na Mungu, na kupeleka moyo wako karibu na Yeye. Kama umekuwa wa imani kwa miaka nyingi na kushirikiana na Mimi kwa muda mrefu, lakini bado unabaki mbali na Mimi, basi Nasema kwamba ni lazima iwe kuwa mara nyingi unaikosea tabia ya Mungu, na mwisho wako utakuwa mgumu sana kufikiria. Kama miaka mingi ya ushirikiano na Mimi haijakubadilisha kuwa mwanadamu aliye na ubinadamu na ukweli, ila badala yake imeingiza njia zako ovu ndani ya asili yako, na huna maono maradufu ya uwongo kuhusu fahari kuliko awali pekee lakini kutonielewa kwako kumeongezeka pia, kiasi kwamba unakuja kunichukulia kuwa rafiki yako mdogo wa kando, basi Nasema kwamba mateso yako si ya juujuu tena, lakini yamepenya ndani kwa mifupa yako. Yote yaliyosalia ni wewe kusubiri matayarisho ya mazishi yako kufanywa. Huhitaji kunisihi basi Niwe Mungu wako, kwani umetenda dhambi inayostahili kifo, dhambi isiyosameheka. Hata kama Ningeweza kuwa na huruma nawe, Mungu aliye mbinguni Atasisitiza kuchukua maisha yako, kwani kosa lako dhidi ya tabia ya Mungu si shida ya kawaida, lakini lile lililo kubwa sana kiasili. Wakati utakapofika, usinilaumu kwa sababu ya kutokujulisha mbeleni. Yote yanarudia haya: Wakati unashirikiana na Kristo—Mungu aliye duniani—kama mwanadamu wa kawaida, yaani, unapoamini kwamba Mungu huyu si chochote ila ni mwanadamu, ni hapo basi ndipo utaangamia. Hili ndilo onyo Langu la pekee kwenu nyinyi nyote.

kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika

Mwili

Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa

Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Views: 72 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: siku za mwisho, Njia ya Uzima wa Milele | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar