10:02 PM
5. Ni nini hasa imani ya kweli katika Mungu? Ni kwa jinsi gani mtu anafaa kumwamini Mungu ili kupata sifa Zake?

Maneno Husika ya Mungu:

“Imani katika Mungu” inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu si sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni aina ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini. Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtawekwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu.

kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili

Imani ya kweli katika Mungu si kuhusu kumwamini Yeye ili kuokolewa na hata zaidi si kuhusu kuwa mtu mzuri. Pia si kuhusu kumwamini Mungu tu kwa ajili ya kuwa na mfanano wa binadamu. Kwa kweli, watu hawapaswi kuona imani kama tu kusadiki kwamba kuna Mungu; si kwamba unapaswa kuamini tu kuwa Mungu ni ukweli, njia, uhai na hakuna zaidi. Wala si tu ili umkubali Mungu nakuamini kwamba Mungu ni Mtawala juu ya kila kitu, kwamba Mungu ni mwenyezi, kwamba Mungu aliumba vitu vyote katika dunia, kwamba Mungu ni wa kipekee na mkuu. Si kukufanya tu kuamini ukweli huu, mapenzi ya Mungu ni kwamba nafsi yako yote na moyo wako unapaswa kupewa Mungu na kumtii Mungu; yaani, unapaswa kumfuata Mungu, kumruhusu Mungu akutumie, kuwa mwenye furaha kumfanyia huduma, na kwamba unapaswa kufanya kitu chochote kwa ajili ya Mungu.

kutoka katika “Ukimbizaji wa Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Leo, imani ya kweli kwa Mungu ni nini? Ni kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha yako na kumjua Mungu kutoka kwa neno Lake ili uufikie upendo wa kweli Kwake. Kuondoa tashwishi: Imani katika Mungu ni ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—hicho ndicho kiasi cha chini zaidi unachopaswa kuwa nacho katika imani yako kwa Mungu. Imani kwa Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha katika mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu, kutoka maisha ya kiasili kwenda kwa maisha katika nafsi ya Mungu, ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata. Kula na kunywa neno la Mungu ni kwa ajili ya kumjua Mungu na kumtosheleza Mungu. Kula na kunywa neno la Mungu kunakupa maarifa kubwa ya Mungu, na ndipo tu utakapoweza kumtii Mungu. Unapomjua tu Mungu ndipo unapoweza kupenda Mungu, na kupatikana kwa lengo hili ndilo lengo la pekee mwanadamu anapaswa kuwa nalo katika imani yake kwa Mungu. Iwapo katika imani yako kwa Mungu, unajaribu kila wakati kuona ishara na maajabu, basi mtazamo wa imani hii kwa Mungu si sahihi. Imani kwa Mungu ni hasa kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha. Ni kuweka tu katika matendo maneno ya Mungu kutoka kwa kinywa Chake na kuyatekeleza mwenyewe ndiko kupatikana kwa lengo la Mungu. Katika kuamini Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu, kuweza kujiwasilisha kwa Mungu, na kumtii Mungu kikamilifu. Iwapo unaweza kumtii Mungu bila kulalamika, kuyajali mapenzi ya Mungu, kupata kimo cha Petro, na kuwa na mtindo wa Petro ilivyozungumziwa na Mungu, basi hapo ndipo utakuwa umefanikiwa katika imani kwa Mungu, na itadhihirisha kuwa umepatwa na Mungu.

kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kwa sababu unamsadiki Mungu, lazima ule na kunywa neno Lake, upitie neno Lake, na uishi kwa kudhihirisha neno Lake. Huku tu ndiko kunaweza kuitwa imani katika Mungu! Kama unasema unamsadiki Mungu na kinywa chako ilhali huwezi kutia maneno Yake yoyote katika vitendo, au kutoa uhalisi wowote, huku hakuitwi kumwamini Mungu. Badala yake, ni “kuutafuta mkate ili kuikabili njaa.” Kuzungumzia tu ushuhuda mdogo mdogo, masuala ya upuuzi na masuala ya juujuu, bila hata kuwa na kiwango kidogo cha uhalisi: haya hayamaanishi imani katika Mungu, na hasa bado hujang’amua njia sahihi ya kumwamini Mungu. Kwa nini lazima ule na kunywa zaidi ya maneno ya Mungu? Usipokula na kunywa maneno Yake bali utafute tu kupaa mbinguni, je, huko ni kumwamini Mungu? Ni nini hatua ya kwanza kwake yule anayesadiki neno Lake Mungu? Ni katika njia gani ndiyo Mungu humkamilisha binadamu? Unaweza kufanywa kuwa mtimilifu bila ya kula na kunywa neno la Mungu? Unaweza kuchukuliwa kuwa mtu wa ufalme bila ya neno la Mungu kuwa uhalisi wako? Imani katika Mungu inamaanisha nini hasa? Wanaomwamini Mungu wanafaa kumiliki tabia nzuri kwa nje, angalau, na kilicho na umuhimu mkubwa zaidi ni kuwa na neno la Mungu. Haijalishi ni nini, huwezi kuligeuka neno la Mungu. Kumjua Mungu na kutimiza mapenzi Yake vyote vinafanikishwa kupitia kwa neno Lake. Kila taifa, dhehebu, dini, na sekta zitashindwa kupitia kwa neno katika siku za usoni. Mungu ataongea moja kwa moja, na watu wote watashikilia neno la Mungu katika mikono yao; kupitia haya wanadamu watakamilishwa. Ndani na nje, neno la Mungu limeenea kotekote: Binadamu huongelea neno la Mungu kwa vinywa vyao, kutenda kulingana na neno la Mungu, na kulishika neno la Mungu ndani mwao kwa ndani na hata kwa nje, wanarowekwa katika neno la Mungu. Hivi ndivyo binadamu watakamilishwa. Wale wanaotimiza mapenzi ya Mungu na wanaweza kumshuhudia Yeye ndio wale walio na neno la Mungu kama uhalisi.

kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

Unaweza kufikiri kuamini katika Mungu ni kuhusu mateso, au kufanya mambo mengi kwa ajili Yake, au kwa ajili ya amani ya mwili wako, au ni kwa ajili ya kila jambo kwenda vyema kwako, kwa ajili ya kila jambo kuwa la kustarehesha—lakini hakuna kati ya haya ambayo ni madhumuni ambayo watu wanapaswa kuwa nayo kwa ajili ya kuamini katika Mungu. Kama hayo ndiyo unayoamini, basi mtazamo wako si sahihi na huwezi kukamilishwa kabisa. Matendo ya Mungu, tabia ya Mungu ya haki, hekima Yake, maneno Yake, na maajabu Yake na kutoeleweka kwa kina Kwake yote ni mambo ambayo watu wanapaswa kuelewa. Tumia uelewa huu kuachana na maombi ya kibinafsi na pia matumaini ya mtu binafsi na dhana zilizo moyoni mwako. Ni kwa kuondoa haya tu ndiyo unaweza kukidhi masharti yanayotakiwa na Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio unaweza kuwa na uzima na kumridhisha Mungu. Kumwamini Mungu ni kwa ajili ya kumridhisha Yeye na kuishi kwa kudhihirisha tabia ambayo Yeye anahitaji, ili matendo na utukufu Wake viweze kudhihirishwa kupitia kundi hili la watu wasiostahili. Huo ndio mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu, na pia lengo unalopaswa kutafuta. Unapaswa kuwa na mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu na kutafuta kupata maneno ya Mungu. Unahitaji kula na kunywa maneno ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli, na hasa kuona matendo Yake ya utendaji, kuona matendo Yake ya ajabu kotekote katika ulimwengu mzima, pamoja na kazi ya vitendo Yeye hufanya katika mwili. Kwa njia ya uzoefu wao halisi, watu wanaweza kufahamu ni jinsi gani hasa Mungu hufanya kazi Yake kwao na mapenzi Yake kwao ni yapi. Haya yote ni ili kuondoa tabia yao potovu ya kishetani. Jiondolee uchafu na udhalimu ndani yako, ondoa nia zako mbaya, na unaweza kuendeleza imani ya kweli katika Mungu. Kwa kuwa tu na imani ya kweli ndiyo unaweza kweli kumpenda Mungu. Unaweza tu kweli kumpenda Mungu kwa msingi wa imani yako Kwake. Je, unaweza kufanikisha kumpenda Mungu bila kumwamini? Kwa kuwa unaamini katika Mungu, huwezi kukanganyika kuhusu jambo hilo. Baadhi ya watu hujawa na nguvu mara tu wanapoona kwamba imani katika Mungu itawaletea baraka, lakini hupoteza nguvu zote mara tu wanapoona wanafaa kupitia kusafishwa. Je, huko ni kuamini katika Mungu? Mwishowe, imani katika Mungu inahusu utiifu kamili na mzima mbele Yake. Unaamini katika Mungu lakini bado una madai Kwake, una mawazo mengi ya kidini ambayo huwezi kuyapuuza, maslahi ya kibinafsi huwezi kuacha, na bado unatafuta baraka za mwili na unataka Mungu auokoe mwili wako, kuiokoa nafsi yako—haya yote ni maonyesho ya watu wenye mtazamo usio sahihi. Hata kama watu wenye imani za kidini wana imani katika Mungu, hawatafuti mabadiliko ya tabia, hawafuatilii maarifa ya Mungu, na wanatafuta tu maslahi ya miili yao. Wengi kati yenu wana imani ambazo ni za kikundi cha kusadiki kidini. Hiyo siyo imani ya kweli katika Mungu. Kuamini katika Mungu lazima watu wamiliki moyo wa kuteseka kwa ajili Yake na radhi ya kujitoa wenyewe. Isipokuwa wakikidhi haya masharti mawili haihesabiki kama imani katika Mungu, na hawatakuwa na uwezo wa kufikia mabadiliko ya tabia. Ni watu tu wanaotafuta ukweli kwa kweli, wanaotafuta maarifa ya Mungu, na kufuatilia maisha ndio wale ambao kweli wanaamini katika Mungu.

kutoka katika “Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na ukosefu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake wa Mungu. Je, huu si upendo mkamilifu wa Mungu? Je, hii si ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo wa Mungu. Kama mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki, basi yeye ni kiumbe wa Mungu mwenye sifa inayostahili, na hakuna kitu kinachokidhi mapenzi ya Muumba bora zaidi ya hiki. Fikiria kwamba wewe unaweza kumfanyia Mungu kazi, ilhali wewe humtii Mungu, na huna uwezo wa kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa njia hii, wewe hutakuwa tu umekosa kutimiza wajibu wa kiumbe cha Mungu, lakini pia utalaaniwa na Mungu, kwa kuwa wewe ni mtu ambaye hana ukweli, ambaye hana uwezo wa kumtii Mungu, na ambaye si mtiifu kwa Mungu. Wewe unajali tu kuhusu kumfanyia Mungu kazi, na hujali kuhusu kuweka ukweli katika vitendo, ama kujifahamu. Wewe humfahamu ama kumjua Muumba, na humtii ama kumpenda Muumba. Wewe ni mtu ambaye asilia si mtiifu kwa Mungu, na hivyo watu kama hawa hawapendwi na Muumba.

kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro katika kumwamini Mungu, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi zaidi na muhimu zaidi ya utendaji. Hili ndilo alilofanya Petro baada ya kumwona Bwana Yesu, na ni kwa kutenda kwa njia hii tu ndio mtu hupata matokeo bora zaidi. Kujitolea kwa moyo wote kwa maneno ya Mungu hasa kunamaanisha kutafuta ukweli, kutafuta nia ya Mungu ndani ya maneno Yake, kuzingatia kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na kuelewa na kupata ukweli zaidi kutoka kwa maneno ya Mungu. Wakati wa kusoma maneno Yake, Petro hakuwa anazingatia kuelewa mafundisho ya dini na hata alikuwa anazingatia kwa kiasi kidogo kupata maarifa ya teolojia; badala yake, alikuwa anazingatia kuelewa ukweli na kufahamu mapenzi ya Mungu, na kutimiza ufahamu wa tabia yake na uzuri wake. Pia alijaribu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na kuelewa asili potovu ya mwanadamu na dosari halisi za mwanadamu, akitimiza kila hali yote ya madai anayotaka Mungu kutoka kwa mwanadamu ili kumridhisha Yeye. Alikuwa na utendaji mwingi sahihi ndani ya maneno ya Mungu; hili linalingana sana na mapenzi ya Mungu, na ni ushirikiano bora zaidi wa mwanadamu katika uzoefu wake wa kazi ya Mungu. …

Ikiwa mtu anaweza kweli kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu kutokana na mambo na maneno yanayohitajika na Yeye, basi atakuwa mtu aliyekamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yanafaa kabisa kwa mtu huyu, kwamba maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake, anapata ukweli, na anaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili asili ya mwili wake, yaani, msingi wa kuwepo kwake kwa asili, utatikisika na kuanguka. Baada ya mtu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yake anakuwa mtu mpya. Maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake; maono ya kazi ya Mungu, matakwa yake kwa mwanadamu, ufunuo wake kwa mwanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anahitaji mwanadamu kutimiza vinakuwa maisha yake—anaishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, na mtu huyu anageuka kukamilishwa na maneno ya Mungu. Anapitia kuzaliwa upya na anakuwa mtu mpya kupitia maneno Yake. Hii ni njia ambayo Petro aliitumia kuufuatilia ukweli; Ilikuwa njia ya kukamilishwa, kukamilishwa na maneno ya Mungu, na kupata uzima kutoka kwa maneno ya Mungu. Ukweli ulioonyeshwa na maneno ya Mungu ulikuwa maisha yake, na wakati huo tu ndipo alikuwa mtu aliyepata ukweli.

kutoka katika “Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Imani katika Mungu ndiyo hatua ya kwanza katika kumjua Mungu. Harakati ya kusonga kutoka katika imani ya mwanzo katika Mungu mpaka imani kuu kwa Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na harakati ya kuipitia kazi ya Mungu. Iwapo unaamini kwa Mungu kwa ajili tu ya kuamini kwa Mungu, na huamini kwa Mungu kwa ajili ya kumjua Mungu, basi hakuna ukweli katika imani yako, na haiwezi kuwa safi—kuhusu hili hakuna tashwishi. Iwapo, wakati wa harakati anapopata uzoefu wa kazi ya Mungu mwanadamu anapata kumjua Mungu polepole, basi hatua kwa hatua tabia yake itabadilika pia, na imani yake itaongezeka kuwa ya kweli zaidi. Kwa njia hii, wakati mwanadamu anafaulu katika imani yake kwa Mungu, ataweza kumpata Mungu kwa ukamilifu. Mungu alijitoa pakubwa kuingia katika mwili mara ya pili na kufanya kazi Yake binafsi ili mwanadamu apate kumjua Yeye, na ili mwanadamu aweze kumwona. Kumjua Mungu[a] ndiyo matokeo ya mwisho yanayofikiwa katika mwisho wa kazi ya Mungu; ndilo hitaji la mwisho la Mungu kwa mwanadamu. Anafanya hili kwa ajili ya ushuhuda Wake wa mwisho, na ili kwamba mwanadamu mwishowe na kwa kikamilifu aweze kumgeukia Yeye. Mwanadamu anaweza tu kumpenda Mungu kwa kumjua Mungu, na ili ampende Mungu lazima amjue Mungu. Haijalishi vile anavyotafuta, au kile anachotafuta kupata, lazima aweze kupata ufahamu wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumridhisha Mungu.

kutoka katika “Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

a. Nakala ya kwanza inasema “Kazi ya kumjua Mungu.”

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Views: 71 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: kumjua mungu, Kufuata Mapenzi ya Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar