0:26 AM
Kujihusisha katika sherehe ya kidini ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo. Watu wengi sana wanafikiri kwamba ili kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho lazima mtu asali, aombe, ale na anywe maneno ya Mungu, au kujaribu kuelewa maneno ya Mungu. Bila kujali kama kuna matokeo yoyote, au kama kuna kuelewa kwa kweli, watu hawa hulenga tu kufanya mambo yasiyo ya dhati kwa nje, na hawalengi matokeo ni watu wanaoishi ndani ya mila za dini, na si watu wanaoishi ndani ya kanisa, na hata zaidi wao si watu wa ufalme. Sala za mtu wa aina hii, nyimbo zake, na kula na kunywa kwake maneno ya Mungu yote yanafuata amri, wanalazimika kufanya hayo, na yanafanyika katika kufuata mitindo, hayafanyiki kwa hiari wala kufanyika kutoka moyoni. Haijalishi ni kiasi gani watu hawa wanaomba au kuimba, hakutakuwa na matokeo kamwe, kwa sababu yote wanayofanya ni amri na mila za kidini, na wao hawatendi neno la Mungu. Kwa kulenga tu mbinu, na kuchukua maneno ya Mungu kama amri ya kuhifadhi, mtu wa aina hii hatendi neno la Mungu, bali tu anaridhisha mwili, na anafanya vitu ili kujionyesha kwa wengine. Aina hii ya matambiko ya dini na amri yanatoka kwa mwanadamu, si kwa Mungu. Mungu hahifadhi sheria, Hazingatii sheria yoyote; Anafanya mambo mapya kila siku na Anafanya kazi ya vitendo. Kama watu katika Kanisa la Nafsi Tatu ambao wamewekewa mipaka kwa ulinzi wa kila asubuhi, sala ya jioni, kutoa shukrani kabla ya kula, kuonyesha shukrani katika kila kitu, na matendo mengine kama haya, haijalishi ni kiasi gani watu hawa wanafanya, au muda wanatenda, hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kama watu huishi ndani ya amri, na mioyo yao ikiwa katika vitendo, basi Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi, kwa sababu mioyo ya watu inachukuliwa na amri, inachukuliwa na dhana za kibinadamu; kwa hiyo Mungu hana njia ya kufanya kazi; watu daima watakuwa wakiishi tu chini ya utawala wa sheria, mtu wa aina hii kamwe hataweza kupokea sifa za Mungu.

kutoka katika “Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho” katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu wakichukulia ukweli kama mfumo wa imani wa kufuatwa, je, wana uelekeo wa kutumbukia katika utaratibu wa dini? Na tofauti kati ya aina hii ya utaratibu wa dini na Ukristo ni gani? Ingawa kile ambacho kinasemekana huenda kikawa cha kina zaidi na cha kusonga mbele zaidi, kikiwa aina fulani ya mafundisho na aina fulani ya utaratibu, basi si kimekuwa Ukristo? Kuna tofauti kati ya mafundisho ya zamani na mapya, lakini ikiwa mafundisho hayo ni aina ya nadharia tu na yakiwa aina ya utaratibu tu, aina ya mafundisho kwa watu—na, vilevile, hawawezi kupata ukweli kutoka kwayo au kuingia katika uhalisi wa ukweli, basi si imani yao ni sawa na Ukristo? Kimsingi, je, si huu ni Ukristo? (Ndiyo.) Kwa hivyo katika tabia yenu na utendaji wa wajibu wenu, ni vitu gani ambavyo kwavyo mna maoni sawa au yanayofanana na wanaoamini katika Ukristo? Ufuatiliaji wa tabia nzuri ya juujuu, kisha kufanya kila uwezalo kujibunia kisingizio kwa kutumia sura ya mambo ya roho; kuiga mtu wa kiroho; kutoa sura ya kuthamini mambo ya kiroho katika kile unachosema, kufanya, na kufichua; kufanya mambo machache ambayo, katika fikra na mawazo ya watu, yanastahili kusifiwa—yote haya ni ufuatiliaji wa mambo ya kiroho kwa njia ya uongo, na ni unafiki. Unasimama juu ukinena maneno na nadharia, ukiwaambia watu wafanye matendo mema, wawe watu wema, na walenge kufuatilia ukweli, lakini katika tabia yako mwenyewe na utendaji wa wajibu wako, hujawahi kutafuta ukweli, hujawahi kutenda kwa mujibu wa kanuni za ukweli, hujawahi kuelewa kile kinachosemwa katika ukweli, mapenzi ya Mungu ni nini, viwango ambavyo Anahitaji kwa mwanadamu ni vipi—hujawahi kuchukulia yoyote haya kwa uzito. Unapokabiliwa na masuala fulani, wewe hutenda kabisa kulingana na mapenzi yako na kumweka Mungu kando. Je, vitendo hivi vya nje na hali za ndani ni kumcha Mungu na kuepukana na uovu? Ikiwa hakuna uhusiano kati ya imani ya watu na ufuatiliaji wao wa ukweli, bila kujali wanamwamini Mungu kwa miaka mingapi, je, watakuwa na uwezo wa kumcha Mungu na kuepukana na uovu kwa kweli? (La.) Na kwa hiyo watu kama hao wanaweza kuitembea njia gani? Je, wao hutumia siku zao wakijiandaa na nini? Je, si ni kwa maneno na nadharia? Je, wao hutumia siku zao wakijiandaa, wakivalia maneno na nadharia, ili kujifanya kama Mafarisayo zaidi, kama watu ambao hudhaniwa kwamba humtumikia Mungu zaidi? Vitendo hivi vyote ni nini? Wanafanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati; wanapeperusha bendera ya imani na kufanya kaida za dini, wakijaribu kumdanganya Mungu ili kufikia lengo lao la kubarikiwa. Hawamwabudu Mungu hata kidogo. Mwishoni, je, si kundi kama hilo la watu litaishia tu kama wale walio ndani ya kanisa ambao hudhaniwa kwamba wanamtumikia Mungu, na ambao hudhaniwa kwamba wanamwamini na kumfuata Mungu?

kutoka katika “Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Wanadamu wengine wana upendeleo wa kujivutia nadhari. Mbele ya ndugu zao, wanasema kweli ni wadeni wa Mungu, lakini akiwapa kisogo, hawatendi ukweli ila wanafanya tofauti kabisa. Je, hawa si ni Mafarisayo wa dini? Mtu ambaye anampenda Mungu kwa kweli na ana ukweli ni yule ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, lakini bila ya hafichui kwa nje. Yeye yuko tayari kutenda ukweli wakati mambo yanapotokea wala hasemi au kutenda kinyume cha dhamiri yake. Anaonyesha hekima wakati mambo yanapotokea na ni mwenye maadili katika matendo yake, bila kujali hali. Mtu kama huyu ni mtu ambaye anahudumu kwa kweli. Kuna watu wengine ambao mara nyingi shukrani zao kwa kuwa wadeni wa Mungu ni kwa mdomo tu. Siku zao huisha wakiwa na nyuso za wasiwasi, kuonekana wameathiriwa, na kuvalia nyuso za huzuni. Hali ya kuchukiza kweli! Na kama ungewauliza, “Ni kwa njia zipi wewe ni mdeni wa Mungu? Tafadhali niambie!” Hawangeweza kutamka lolote. Kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu, basi usizungumze kuhusu uaminifu wako hadharani, bali tumia matendo yako halisi ili kuonyesha upendo wako kwa Mungu, na kumwomba kwa moyo wa kweli. Wale wanaotumia maneno pekee kushughulika na Mungu ni wanafiki wote! Baadhi yao husema kuwa wao ni wadeni kwa Mungu katika kila sala, na kuanza kulia wakati wowote wanaposali, hata bila kuguswa na Roho Mtakatifu. Watu kama hawa wamepagawa na kaidi na fikira za kidini; wanaishi kulingana na hizo kaidi na fikra, daima wakiamini kwamba matendo kama hayo humpendeza Mungu, na kwamba kumcha Mungu kijuujuu au machozi ya huzuni ndivyo Mungu hupendelea. Ni kitu kipi kizuri kinachoweza kutoka kwa watu kama hao wa kushangaza? Ili kuonyesha unyenyekevu wao, baadhi yao huonyesha neema bandia wakati wanapozungumza mbele ya watu wengine. Baadhi yao kwa makusudi ni wanyonge mbele ya watu wengine, kama mwanakondoo asiye na nguvu yoyote. Je, hii ni tabia ya watu wa ufalme? Mtu wa ufalme sharti awe wa kusisimua na aliye huru, asiye na hatia na aliye na uwazi, mwaminifu na wa kupendeza; mtu aishiye katika hali ya uhuru. Ana tabia za kiajabu na heshima, na anaweza kushuhudia kokote aendako; yeye ni yule anayependwa na Mungu na wanadamu. Wale ambao ni wanafunzi katika imani huwa na matendo mengi ya nje; lazima kwanza wapitie kipindi cha ushughulikiaji na kuvunjwa. Wale ambao wana imani kwa Mungu katika nyoyo zao hawawezi kutofautishwa na wengine kwa nje, lakini vitendo na matendo yao ni ya kupongezwa kwa wengine. Watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza chukuliwa kuwa wanaishi kwa kudhihirisha neno la Mungu. Ukihubiri injili kila siku kwa mtu huyu na yule, ukiwaleta kwa wokovu, ilhali mwishowe, wewe bado unaishi katika sheria na mafundisho, basi wewe huwezi kuleta utukufu kwa Mungu. Watu wa aina hii ni watu wa dini, na wanafiki pia.

kutoka katika “Kumwamini Mungu Kunapaswa Kulenge Uhalisi, Si Kaida za Kidini” katika Neno Laonekana katika Mwili

Shughuli za kishirikina ambazo watu wanashughulika nazo ndizo Mungu anazichukia sana, lakini watu wengi bado hawawezi kuachana nazo, wakifikiri kwamba shughuli hizi za kishirikina zimeamriwa na Mungu, na hata leo bado hawajaziacha kabisa. Mambo kama mipango ambayo vijana hufanya kwa ajili ya sherehe za arusi au mahari, zawadi za pesa, dhifa, na maneno mengine na virai vinavyohusiana na matukio ya sherehe; maneno ya zamani ambayo yamerithishwa; shughuli zote za kishirikina zisizokuwa na maana zinazofanywa kwa niaba ya wafu na taratibu za mazishi; yote haya yanachukiwa sana na Mungu. Hata siku ya ibada (ikiwemo Sabato, kama inavyoadhimishwa na ulimwengu wa dini) inachukiwa naye; mahusiano ya kijamii na mawasiliano ya kidunia kati ya mwanamme na mwanamme pia yanachukiwa na kukataliwa zaidi na Mungu. Hata Sikukuu ya Machipuko na Siku ya Krismasi, ambazo zinajulikana kwa kila mtu, haziamriwi na Mungu, sembuse wanasesere na mapambo (mashairi, keki ya Mwaka Mpya, mafataki, kandili, zawadi za Krismasi, sherehe za Krismasi, na Ushirika Matakatifu) ya sikukuu hizi—je, sio sanamu katika akili za wanadamu? Kumega mkate siku ya Sabato, mvinyo, na kitani nyembamba navyo ni sanamu zaidi. Siku zote za sherehe za kijadi ambazo ni maarufu sana nchini China, kama vile Siku ya kuinua Vichwa vya Joka, Sikukuu ya Mashua ya Joka, Sikukuu ya Majira ya Kati ya Kupukutika, Sikukuu ya Laba, na Siku ya Mwaka Mpya, na sikukuu zisizothibitika katika ulimwengu wa kidini, kama vile Pasaka, Siku ya Ubatizo, na Siku ya Krismasi, zote hizi zimepangwa na kurithishwa kwa watu wengi tangu zama za kale hadi leo, zote hazilingani kabisa na binadamu aliyeumbwa na Mungu. Ni uwezo mkubwa wa fikra za binadamu na dhana bunifu ambazo zimewaruhusu kurithishwa hadi leo. Zinaonekana kuwa hazina kasoro, lakini kwa kweli ni hila ambazo Shetani alifanya kwa binadamu. Kadri Shetani wanavyoishi katika eneo fulani, na kadri eneo hilo lilivyo nyuma kimaendeleo na kutofaa, ndivyo desturi zake za kikabaila zinakuwa nyingi zaidi. Vitu hivi vinawafunga watu kwa nguvu, bila kutoa nafasi kwa ajili ya maendeleo. Sikukuu nyingi katika ulimwengu wa kidini zinaonekana kuonyesha ubunifu mkubwa na zinaonekana kujenga daraja kwa kazi ya Mungu, lakini kweli ni vifungo visivyoshikika ambavyo Shetani hutumia kuwafunga watu ili wasije kumjua Mungu—hizi zote ni hila za ujanja za Shetani. Kwa kweli, hatua ya kazi ya Mungu inapomalizika, tayari Amekwishaharibu zana na mtindo wa wakati huo, bila kuacha alama yoyote. Hata hivyo, “waumini wasalihina” bado wanaabudu vitu hivyo vya kushikika; wakati huo huo wanaacha kile Alicho nacho Mungu, bila hata kukichunguza zaidi, wakionekana wamejawa na upendo wa Mungu lakini kwa uhalisi walimtoa ndani ya nyumba zamani sana na kumweka Shetani mezani kwa ajili ya kumwabudu. Sanamu ya Yesu, Msalaba, Maria, Ubatizo wa Yesu na Karamu ya Mwisho—watu wanavichukulia hivi kama Bwana wa Mbinguni, wanaviabudu wakati wote wakilia kwa sauti kwa kurudiarudia “Mungu Baba.” Je, huu sio utani? …

Njia bora zaidi ya kubadilisha tabia ya mwanadamu ni kuondoa vitu hivi vyenye sumu kubwa katika mioyo ya wanadamu, kuwaruhusu watu kuanza kubadilisha fikira na maadili yao. Kwanza kabisa, watu wanatakiwa kuona waziwazi kwamba kaida zote hizi za kidini, shughuli za kidini, miaka na miezi, na sikukuu zote ni za kumchukiza Mungu. Wanatakiwa kuwa huru kutoka kwa vifungo hivi vya fikira za kishirikina na kuondoa kila alama ya kishirikina iliyozama kabisa ndani. Mambo haya yote ni sehemu ya kuingia kwa mwanadamu.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (3)katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Maisha ya kiroho yanayofaa yanajumuisha kusali, kula na kunywa neno la Mungu, kushiriki kuhusu ukweli, kufanya wajibu wa mtu, na kuimba nyimbo za kidini za sifa vizuri. Matendo haya ni ya manufaa sana kwa watu kuingia katika ukweli na mabadiliko ya tabia. Hata hivyo, kaida za dini, ni kufanya vitu kwa namna isiyo ya dhati tu, kutomaanisha kile anachosema mtu, na kuwa hafifu, mzembe, na mnafiki. Hizi zote ni mbinu za juu juu zinazomdanganya Mungu. Kutekeleza kaida za dini kumetengwa na uhalisi na hauna uhalisi hata kidogo—ni kusema maneno bila sauti tu ili kujionyesha, na ni jambi lisilo na matokeo kabisa. Maisha ya kufaa ya kiroho yanategemezwa kwa uhalisi kabisa; yanafanyika kutokana na kuunganishwa na uhalisi, na aidha, ni uaminifu utokao kwa moyo, na hivyo, ni ya kufaa na hukubaliwa na Mungu kwa furaha. Chukua, kwa mfano, maombi yanayofaa: Yanatoka kwa taabu za kweli za mtu na hutoka kwa mahitaji yake maishani. Yanawakilisha umuhimu wa kweli wa nafsi yake ya ndani, na kwa hiyo hupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hata hivyo, maombi katika muktadha wa kaida za dini hukiuka kanuni hii. Mtu anaweza kwa nasibu kusema mistari michache ya maombi bila sauti wakati wowote au mahali popote bila kuyamaanisha, wakati moyoni mwake anahisi kuchoshwa na kukosa msukumo. Anawezaje kupokea kazi ya Roho Mtakatifu? Ni dhahiri kwamba hataki kuomba lakini anajilazimisha kufanya hivyo—hili ni jambo linalokiuka kanuni. Katika hali za kawaida, haiwezekani kwa mtu kuomba bila kukoma; wakati haombi, mtu anaweza kula na kunywa neno la Mungu na anaweza kushiriki kuhusu ukweli. Hii ni kwa sababu maisha ya kiroho ni jambo ambalo haliwezi kudhibitiwa, lakini yanaamuliwa tu kulingana na hali ya mtu mwenyewe na mahitaji ya kweli. Hii ndiyo njia ya pekee ya kupata matokeo mazuri. Maisha ya kweli ya kiroho ni ya kufaa na yanafanyika wakati mambo yanatokea kwa kawaida. Hayajumuishi hata kidogo kutii kanuni au kufanya kaida. Kaida zote za dini ni kanuni na unafiki uliotengenezwa na watu; hazihusishi kutafuta kwa ari. Hii ndiyo maana Mungu anaziita za kinafiki. Maisha ya kufaa ya kiroho hutukia kwa kupitia kazi ya Mungu, na ni muungano wa kazi ya Roho Mtakatifu na tendo lililoanzishwa na binadamu. Ingawa hakuna kanuni au kaida katika aina hii ya maisha ya kiroho, kweli yanaleta matokeo thabiti ya manufaa. Unapohamia kutoka kwa kaida za dini hadi maisha ya kufaa ya kiroho, ni hapo tu ndipo umeingia kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu.

kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Views: 126 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Kutatua Mchafuko wa Kiroho | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar