1:40 AM
Matamshi ya Kristo  Njia … (6)

Matamshi ya Kristo-Njia … (6)

Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu ndio tumeletwa katika siku hii. Kwa hiyo, sisi sote ni wasaliaji katika mpango wa usimamizi wa Mungu, na kwamba tunaweza kubakizwa mpaka siku hii ni kutiwa moyo kwa hali ya juu kutoka kwa Mungu. Kulingana na mpango wa Mungu, nchi ya joka kuu jekundu inapaswa kuangamizwa, lakini Ninadhani kwamba labda Ameanzisha mpango mwingine, au Anataka kutekeleza sehemu nyingine ya kazi Yake. Kwa hiyo mpaka leo Sijaweza kuueleza kwa dhahiri—ni kama kwamba ni kitendawili kisichoweza kufumbuliwa. Lakini kwa jumla, kundi hili letu limejaaliwa na Mungu, na Ninaendelea kuamini kwamba Mungu ana kazi nyingine ndani yetu. Sote tuiombe Mbinguni hivi: “Mapenzi Yako yatimizwe na Ujitokeze kwetu mara tena na Usijifiche ili tuuone utukufu Wako na uso Wako kwa dhahiri zaidi.” Mimi huhisi kila mara kwamba njia ambayo Mungu hutuongoza kwayo haiendi tu juu moja kwa moja, lakini ni njia ya kupinda iliyojaa mashimo ya barabarani, na Mungu anasema kwamba kadri njia inavyokuwa na miamba mingi ndivyo inavyoweza kufichua mioyo yetu ya upendo zaidi, lakini hakuna mmoja wetu anayeweza kuifungua aina hii ya njia. Katika uzoefu Wangu, Nimetembea njia nyingi zenye miamba, danganyifu na Nimevumilia mateso makuu; wakati mwingine hata Nimepatwa na majonzi mpaka Nilitaka kulia, lakini Nimetembea njia hii mpaka siku hii. Naamini kwamba hii ni njia inayoongozwa na Mungu, kwa hiyo Navumilia uchungu wa mateso yote na kuendelea. Kwani hili ndilo Mungu ameamuru, kwa hiyo nani anaweza kuliepuka? Siombi kupata baraka yoyote; yote Ninayoomba ni kwamba Niweze kutembea njia Ninayostahili kutembea kulingana na mapenzi ya Mungu. Sitafuti kuwaiga wengine au kutembea njia ambazo wanatembea—yote Ninayoomba ni kwamba Niweze kutimiza bidii Yangu ya kutembea njia Yangu teule mpaka mwisho. Siombi msaada wa wengine; kusema kweli, hata Mimi siwezi kumsaidia mtu mwingine. Inaonekana kwamba Mimi ni mwepesi sana kuhisi kuhusu suala hili. Sijui kile ambacho watu wengine hufikiria. Hii ni kwa sababu Nimeamini kila mara kwamba haijalishi vile ambavyo mtu lazima ateseke na vile ambavyo anatakiwa kutembea katika njia yake hii inaamriwa na Mungu na kwamba hakuna anayeweza kumsaidia mwingine. Labda sehemu ya ndugu zetu wenye shauku wanaweza kusema kwamba Nimekosa upendo. Lakini hili ndilo Naamini. Watu hutembea njia zao wakitegemea uongozi wa Mungu, na Naamini kwamba wengi wa ndugu Zangu watafahamu moyo Wangu. Natarajia pia kwamba Mungu atatupa nuru kuu sana katika hali hii ili upendo wetu uweze kuwa safi zaidi na urafiki wetu uweze kuwa wa thamani zaidi. Tusichanganyikiwe kuhusu mada hii, lakini tuelewe tu vizuri ili mahusiano kati yetu yaweze kuanzishwa kwa msingi wa uongozi wa Mungu.

Mungu amefanya kazi katika China bara kwa miaka kadhaa, na Amelipa gharama kuu katika watu wote ili hatimaye kutufikisha tulipo leo. Nafikiri kwamba ili kumwongoza kila mtu katika njia sahihi, kazi hii ni lazima ianzie pale kila mtu ni mnyonge zaidi—ni kwa njia hii tu ndiyo kikwazo cha kwanza kinaweza kushindwa ili iweze kuendelea kusonga mbele. Je, hiyo si bora? Taifa la China ambalo limepotoshwa kwa miaka elfu nyingi limeendelea mpaka leo. Kila aina ya “virusi” vinaendelea kutanuka na vinasambaa kila mahali kama tauni; kutazama tu mahusiano ya watu kunatosha kuona ni virusi vingapi viko ndani ya watu. Ni vigumu mno kwa Mungu kukuza kazi Yake katika sehemu kama hii iliyofungwa kikiki na kuambukizwa virusi. Nafsi, mienendo ya watu, jinsi wanavyofanya mambo, kila kitu wanachoonyesha katika maisha yao na mahusiano yao kati ya watu wawili yote yamevunjika zaidi ya kuaminika na hata maarifa yao na utamaduni wao vyote vimeshutumiwa na Mungu. Bila kutaja matukio mbalimbali waliyojifunza kutoka kwa familia na jamii zao—yote haya yamehukumiwa machoni pa Mungu. Hii ni kwa sababu wale wanaoishi katika nchi hii wamekula virusi vingi sana. Inaonekana kuwa hali ya kawaida kwa watu, na hawafikirii chochote kuhusu hilo. Kwa hivyo, kadri upotovu wa watu ulivyo mahali fulani, ndivyo mahusiano yao kati ya watu wawili yatakuwa yasiyofaa zaidi. Kuna mashindano ya kikatili katika mahusiano ya binadamu—wanafanyiana njama na kuchinjana kama kwamba mahali hapo ni mji wa pepo wachafu wa watu kulana. Ni vigumu isivyosadikika kutekeleza kazi ya Mungu katika mahali pa aina hii panapoogofya sana, ambapo mazimwi huenea pote. Ninaposhughulikia watu, Mimi humsihi Mungu kila mara bila kukoma. Hii ni kwa sababu Mimi kila mara huogopa kushughulikia watu, na mimi huogopa sana kwamba Nitakosea “hadhi” ya wengine na tabia Yangu. Katika moyo Wangu Mimi kila mara huogopa kwamba hawa pepo wachafu watatenda kwa kutojali, kwa hiyo Mimi kila mara humwomba Mungu anilinde. Aina yote ya mahusiano yasiyofaa yanaweza kuonekana kati ya watu hawa walio miongoni mwetu. Mimi huona mambo haya yote na kuna chuki moyoni Mwangu. Hiyo ni kwa sababu watu kila mara hufanya “shughuli” za wanadamu kati yao na hawamzingatii Mungu kamwe. Nachukia matendo ya watu sana. Kinachoweza kuonekana katika watu walio China bara si kingine ila tabia potovu ya kishetani, kwa hiyo katika kazi ya Mungu ndani ya watu hawa, ni takriban vigumu kupata chochote cha maana ndani yao; kazi yote inafanywa na Roho Mtakatifu, na ni kwamba tu Roho Mtakatifu huwasisimua watu zaidi, na Hufanya kazi ndani yao. Ni takriban vigumu kuwatumia watu hao, yaani, kazi ya kusisimuliwa na Roho Mtakatifu pamoja na ushirikiano wa watu haiwezi kufanyika. Roho Mtakatifu hufanya tu kazi kwa bidii kuwasisimua watu, lakini hata hivyo watu ni wazito tu na wasiohisi na hawana habari ni nini ambacho Mungu anafanya. Kwa hiyo, kazi ya Mungu katika China bara inalinganishwa na kazi Yake ya kuumba ulimwengu. Yeye huwafanya watu wote wazaliwe mara ya pili na hubadilisha kila kitu kuwahusu kwa sababu hakuna chochote cha maana ndani ya watu hawa. Ni la kuvunja moyo sana. Mimi mara kwa mara hufanya ombi la sikitiko kwa ajili ya watu hawa: “Mungu, naomba nguvu Zako kuu zifichuliwe kwa watu hawa ili Roho Wako awasisimue sana, na ili watesekaji hawa wazito na wa akili goigoi waweze kuamka, wasilale tena, na waone siku ya utukufu Wako.” Sote tuombe mbele ya Mungu na tuseme: Ee Mungu! Utuonee huruma mara tena na kututunza ili mioyo yetu iweze kukugeukia Wewe kwa ukamilifu na tuweze kuokoka kutoka kwa hii nchi chafu, kusimama, na kukamilisha kile ulichotuaminia sisi. Natarajia kwamba Mungu atatusisimua mara tena ili tupate nuru Yake, na kwamba Atuhurumie ili mioyo yetu iweze kumrudia polepole na Aweze kutupata. Hii ni shauku ambayo tunashirikiana sote.

Njia tuifuatayo imeamriwa yote na Mungu. Kwa jumla, Naamini kwamba Ninaweza kwa uhakika kutembea njia hii mpaka mwisho, na hii ni kwa sababu Mungu kila mara hutabasamu juu Yangu, na ni kana kwamba mkono wa Mungu huniongoza Mimi kila wakati. Kwa hiyo, haijazimuliwa na kitu chochote kingine ndani ya moyo Wangu—Mimi kila mara hujishughulisha na kazi ya Mungu. Mimi hujaribu kila Niwezalo kukamilisha kila kitu ambacho Mungu ameniaminia kwa bidii, na Siingilii kabisa kazi ambazo hajanigawia Mimi, wala Siingilii kazi ambayo mwingine anafanya. Hiyo ni kwa sababu Naamini kwamba kila mtu lazima atembee njia yake mwenyewe bila kuingiliana. Hivi ndivyo Ninavyoyaona. Labda hii ni kwa sababu ya nafsi Yangu mimi, lakini Natarajia kwamba ndugu Zangu watanielewa na kunisamehe kwa sababu Mimi katu Sithubutu kwenda kinyume cha amri za Baba Yangu. Sithubutu kukataa mapenzi ya Mbinguni. Inawezekana kuwa mmesahau kwamba “mapenzi ya Mbinguni hayawezi kukataliwa”? Labda watu wengine hudhani kwamba Mimi ni mwenye ubinafsi sana, lakini Nadhani kwamba Nimekuja hasa kufanya sehemu ya kazi ya usimamizi wa Mungu. Sijakuja kwa ajili ya mahusiano yanayofanywa kati ya watu wawili. Siwezi kabisa kujifunza namna ya kuwa na mahusiano mazuri na watu wengine. Lakini Nina uongozi wa Mungu kuhusu kile ambacho Ameniaminia Mimi, na Nina ujasiri na uvumilivu wa kufanya kazi hii vizuri. Inawezekana kuwa Mimi ni “mwenye ubinafsi” sana. Ni matamanio Yangu kwamba kila mtu angeanza kuhisi upendo wa Mungu usio na uchoyo na kushirikiana na Yeye. Msingojee kuja kwa uadhama wa pili wa Mungu—hili si zuri kwa mtu yeyote. Mimi kila mara hufikiri kwamba jambo tunalopaswa kuzingatia ni hili: “Lazima tufanye kila kinachowezekana kufanya tunachopaswa kufanya ili kumridhisha Mungu. Mungu amemwaminia kila mtu kitu fulani tofauti; tunapaswa kukitimiza vipi?” Unapaswa kujua ni njia gani hasa unayofuata—ni muhimu uelewe hili. Kwa vile nyote mko radhi kumridhisha Mungu, mbona msijitolee kwanza Kwake? Siku ya kwanza Nilipoomba kwa Mungu, Nilimpa Yeye moyo Wangu wote. Watu walio karibu Nami—wazazi, dada, kaka, au wenzi wa kazi—walisahaulika katika akili Yangu kwa uamuzi Wangu, na ni kana kwamba Kwangu hawakuwepo kamwe. Hiyo ni kwa sababu mawazo Yangu kila mara yalikuwa kwa Mungu, maneno Yake, au hekima Yake—mambo haya kila mara yalikuwa muhimu ndani ya moyo Wangu na yakawa mambo ya thamani sana katika moyo Wangu. Kwa hiyo kwa watu waliojawa na falsafa za maisha, Mimi ni kiumbe katili, asiye na hisia. Jinsi Ninavyotenda, jinsi Nifanyavyo mambo, kila mwendo Wangu—haya yote huumiza mioyo yao. Wao hunitupia macho ya ajabu kana kwamba Nimekuwa kitendawili kisichofumbuliwa. Watu wananitathmini kisirisiri ndani ya mioyo yao—hawajui Ninachoenda kufanya. Ningewezaje kuacha kusonga mbele kwa sababu ya kila mwendo wa watu hao? Labda wana wivu, au wamechukizwa, au wanadhihaki—Mimi bado huomba kwa hamu mbele ya Mungu kana kwamba Yeye na Mimi pekee ndio tuko katika ulimwengu mmoja, na hakuna mwingine yeyote. Nguvu za nje kila mara zinanikandamiza karibukaribu sana, lakini hisia ya kusisimuliwa na Mungu pia hutapakaa ndani Yangu. Katika mtanziko huu, Niliinama mbele ya Mungu: “Ee Mungu! Mimi sijawahi kukosa kutaka kufanyia kazi mapenzi Yako. Machoni pako Ninaheshimiwa na kuchukuliwa kama dhahabu ya kupendeza, lakini Siwezi kutoroka kutoka kwa nguvu za giza. Niko radhi kuteseka kwa ajili Yako maishani mwote, Niko radhi kufanya kazi Yako kuwa kazi ya maisha Yangu; Nakusihi Unipe mahali pa kufaa pa kupumzika ili Nijitolee Kwako. Ee Mungu! Niko radhi kujitoa Mwenyewe Kwako. Wewe unajua vizuri udhaifu wa mwanadamu, kwa hiyo kwa nini Unajificha kutoka Kwangu?” Papo hapo Nilihisi kana kwamba Nilikuwa yungiyungi la mlimani linaloachilia harufu nzuri katika upepo mwanana, lakini hakuna aliyejua. Mbinguni ilikuwa inaomboleza na moyo Wangu uliendelea kulia kana kwamba Nilikuwa na maumivu zaidi ndani ya moyo Wangu. Nguvu zote na kuzingira kwa wanadamu vilikuwa kama radi katika siku angavu. Ni nani angeweza kuuelewa moyo Wangu? Kwa hiyo Nilikuja mbele ya Mungu tena na kusema: “Ee Mungu! Hakuna njia yoyote ya kutekeleza kazi Yako katika nchi hii ya uchafu? Ni kwa nini wengine wana utulivu katika mazingira yanayosaidia na yasiyokuwa na mateso, ilhali hawawezi kuufikiria moyo Wako? Hata kama Ningetandaa mabawa Yangu, ni kwa nini Siwezi kupuruka kwenda mbali? Je, hukubali?” Nilitumia siku kadhaa Nikiomboleza juu ya hili, lakini kila mara Niliamini kwamba Mungu angeufariji moyo Wangu wa huzuni. Tangu mwanzo hadi mwisho, hakuna ambaye angeelewa hali Yangu ya moyo ya wasiwasi. Labda ulikuwa ni utambuzi wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu—kila mara Mimi huwa motisha kwa ajili ya kazi Yake na Mimi huwa na wakati wa kupumua kwa shida. Mpaka siku hii Mimi bado huomba: “Ee Mungu! Ikiwa ni mapenzi Yako, Niongoze kutekeleza hata kazi Yako kubwa zaidi ili iweze kupanuka kotekote katika ulimwengu mzima, ifunguke kwa kila taifa, kila dhehebu katika ulimwengu, ili moyo Wangu upate amani kidogo, ili Niishe katika mahali pa amani kwa ajili Yako, na Nikufanyie kazi bila pinzani na Niweze kuutuliza moyo Wangu kukuhudumia maishani Mwangu.” Hii ni shauku ndani ya moyo Wangu. Labda ndugu Zangu watasema kwamba Nina kiburi, kwamba Nina maringo. Nakubali hilo kwa kuwa ni kweli—kile vijana huwa nacho ni kiburi tu. Kwa hiyo Nanena ukweli bila kupinga mambo ya hakika. Ndani Yangu mnaweza kuona nafsi zote za kijana, lakini pia mnaweza kuona pale Nilipo tofauti na vijana wengine—nayo ni utulivu Wangu na upole Wangu. Sitayarishi mada kutoka kwa hili; Naamini kwamba Mungu ananijua bora zaidi kuliko Ninavyojijua Mwenyewe. Haya ni maneno kutoka moyoni Mwangu, na Natarajia kwamba ndugu Zangu hawatachukizwa. Tuzungumze maneno yaliyo mioyoni mwetu, tuangalie kila vitu vyetu tunavyofuatilia, tulinganishe mioyo yetu ya upendo kwa Mungu, tusikilize maneno tunayonong’ona kwa Mungu, tuimbe nyimbo nzuri zaidi ndani ya mioyo yetu, na kuonyesha hisia zetu za fahari ili maisha yetu yawe mazuri zaidi. Sahau yaliyopita, na tutazamie siku zetu za usoni. Mungu atatufungulia sisi njia!

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Endelea Kusoma:  Ifuate Kazi Mpya ya Roho Mtakatifu na Kupata Sifa ya Mungu 

Views: 40 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Kuijua Sauti ya Mungu, Matamshi ya Kristo | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar