10:20 PM
Matamshi ya Kristo-Utendaji (2)

Matamshi ya Kristo-Utendaji (2)

Katika nyakati zilizopita, watu walijifundisha wenyewe kuwa na Mungu na kuishi katikati ya roho kila wakati, ambao, ukilinganishwa na utendaji wa leo, ni mafundisho rahisi ya kiroho tu. Utendaji kama huu huja kabla ya kuingia kwa watu katika njia sahihi ya maisha, na ni mbinu ya juujuu zaidi na rahisi zaidi kati ya mbinu zote za utendaji. Ni utendaji wa hatua za mwanzoni kabisa za imani ya watu kwa Mungu. Ikiwa watu wataishi kila mara kwa utendaji huu, watakuwa na hisia nyingi sana, na hawataweza kuingia katika uzoefu ambao ni wa kina na wa kweli. Wataweza tu kuzifundisha roho zao, kuifanya mioyo yao iweze kusonga kwa kawaida karibu na Mungu, na kupata kila mara furaha nyingi mno katika kuwa na Mungu. Watakuwa wamejiwekea mipaka kwa ulimwengu mdogo wa kuwa na mshikamano na Mungu, wasiweze kuelewa kile kilicho katika vina vya ndani kabisa. Watu ambao huishi katika mipaka hii pekee hawana uwezo wa kupiga hatua yoyote kubwa. Wakati wowote, wanaweza kulia, “Aa! Bwana Yesu. Amina!” Wanapokula, wao hulia, “Ee Mungu! Nala na Wewe unakula....” Na ni hivi karibu kila siku. Huu ni utendaji wa nyakati zilizopita, ni utendaji wa kuishi ndani ya roho kila wakati. Huo sio utovu wa adabu? Leo, kama ni wakati wa kutafakari juu ya maneno ya Mungu, unapaswa kuyatafakari, kama ni wakati wa kutia ukweli katika vitendo unapaswa kuuweka katika vitendo, na wakati ni muda wa kutekeleza wajibu wako, unapaswa kuutekeleza. Kufanya utendaji hivyo ni huru kabisa, kunakufungua wewe. Sio kama vile wazee wa dini huomba na kusema neema. Bila shaka, hapo awali, hivi ndivyo watu walioamini katika Mungu walitakiwa kutenda—lakini kutenda kwa njia hii kila mara ni kuliko nyuma kimaendeleo kabisa. Utendaji wa wakati uliopita ni msingi wa utendaji wa leo. Ikiwa kungekuwa na njia kwa utendaji wa nyakati zilizopita, utendaji wa leo utakuwa rahisi zaidi. Kwa hiyo, leo, tunapozungumza juu ya “kumleta Mungu katika maisha halisi,” ni hali gani ya utendaji inatajwa? “Maisha halisi” hasa yanahitaji watu wawe na ubinadamu wa kawaida; kile ambacho watu wanapaswa kuwa nacho ni kile ambacho Mungu anataka kutoka kwao leo. Kuyaleta maneno ya Mungu katika maisha halisi ndiyo maana halisi ya “kumleta Mungu katika maisha halisi.” Leo, watu wanapaswa hasa kujiandaa wenyewe na yafuatayo: Kuhusu suala moja, lazima waendeleze uhodari wao, wafunzwe, waongeze msamiati wao, na kuendeleza ustadi wao wa kusoma; na katika lingine, lazima waishi maisha ya watu wa kawaida. Umerudi tu mbele ya Mungu kutoka ulimwenguni, na lazima kwanza uifunze roho yako, kuufunza moyo wako kuwa na amani mbele ya Mungu. Hili ndilo la msingi kabisa, na pia ni hatua ya kwanza katika kutimiza mabadiliko. Watu wengine ni wepesi kubadilika katika utendaji wao; wao hutafakari ukweli huku wakifua nguo zao, wakielewa ukweli wanaopaswa kuelewa na kanuni wanazopaswa kuweka katika vitendo kwa uhalisi. Katika suala moja, lazima uwe na maisha ya kawaida ya ubinadamu, na katika lingine lazima kuwe na kuingia katika ukweli. Huu ni utendaji bora zaidi kwa maisha halisi.

Zamani, watu walipitia magumu mengi sana, lakini mengine yalikuwa yasiohitajika kwa kweli, kwani mengine yalikuwa mambo ambayo hayakuhitajika kutendwa na mwanadamu. Wanapomleta Mungu katika maisha yao halisi, Mungu kimsingi anahitaji kwamba watu wamwabudu Mungu, wafuatilie ufahamu wa Mungu, na kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu katikati ya ubinadamu wa kawaida. Hawahitajiki kumwomba Mungu mara tu wanapoanza kufagia sakafu, wakihisi ni wadeni Wake wasipofanya hivyo. Utendaji wa leo sio hivyo; ni uliolegezwa na rahisi! Watu hawaambiwi watii mafundisho ya dini. Kila mmoja anapaswa kutenda kulingana na kimo chake mwenyewe: Ikiwa mume wako haamini, mchukulie kama mtu asiyemwamini Mungu, na ikiwa yeye huamini mchukulie kama muumini. Usisisitize kuhusu upendo na uvumilivu, bali kuhusu hekima. Watu wengine huenda kununua mboga, na wanapokuwa wakitembea wao hunong’ona: Ee Mungu! Ni mboga gani ambazo unanikubalia ninunue leo? Naomba usaidizi Wako. Je, nichague ninaponunua? Kisha wao hufikiria: Sitachagua; Mungu ananiambia kwamba nimtukuze Yeye, kwamba nilitukuze jina Lake katika mambo yote, na kwamba watu wote wawe na ushuhuda, kwa hiyo muuzaji akinipa kitu fulani cha kitambo na kilichokauka, bado nitampa Mungu shukrani—nitavumilia! Sisi tuaminio katika Mungu hatuchagui ni mboga gani za kununua. Unafikiri kwamba kufanya hivi ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na baada ya kutumia yuan[a] moja kununua mboga ya kitambo iliyo na kuvu, bado unaomba na kusema: Ee Mungu! Bado nitaila mboga hii iliyooza—maadamu Unikubali, nitaila. Je, utendaji kama huu sio wa kipumbavu? Je, huko sio kufuata mafundisho ya dini? Hapo awali, watu walizifundisha roho zao na waliishi ndani ya roho kila wakati, na hili lilihusiana na kazi iliyofanywa katika Enzi ya Neema. Uchaji Mungu, unyenyekevu, upendo, uvumilivu, kutoa shukrani kwa mambo yote—haya ndiyo yaliyotakiwa kutoka kwa kila muumini katika Enzi ya Neema. Wakati huo, watu walimwomba Mungu katika mambo yote; wangeomba waliponunua nguo, na walipofahamishwa juu ya mkutano, pia wangeomba na kusema: Ee Mungu! Je, Unanikubalia niende au la? Ikiwa unanikubalia kwenda, basi nitayarishie njia iliyonyooka, acha kila kitu kifanyike kwa urahisi. Na ikiwa hunikubalii kwenda, basi nifanye nianguke chini. Walipoomba, walimsihi Mungu. Baada ya kuomba walihisi wasio na utulivu, na hawakuenda. Pia kulikuwa na dada ambao, kwa vile waliogopa kupigwa na waume wao wasiomwamini Mungu wakati ambapo wangerudi, walihisi wasio na utulivu walipoomba—na kwa vile walihisi wasio na utulivu, hawakuenda kwa mkutano. Waliamini hayo yalikuwa mapenzi ya Mungu, ilhali kweli ni kwamba, iwapo wangeenda, hakuna chochote ambacho kingefanyika. Matokeo ni kwamba walikosa mkutano. Haya yote yalisababishwa na ujinga wa watu wenyewe. Watu wanaofanya utendaji kwa njia hii huishi kwa hisia zao wenyewe. Njia hii ya utendaji ina kosa na ni ya kipumbavu, haina udhahiri, na hisia na mawazo yao wenyewe kwa wingi sana. Ukiambiwa kuhusu mkutano, basi nenda, na usipoambiwa, basi usiende; unapoambiwa kuuhusu, hakuna haja ya kumwomba Mungu. Je, hili si rahisi? Ikiwa, leo, unahitaji kununua kipande fulani cha mavazi, basi nenda ukafanye hivyo. Usimwombe Mungu na kusema: Ee Mungu! Leo napaswa kununua kipande fulani cha mavazi, je, Unanikubalia niende au la? Ni aina gani ya mavazi ninayopaswa kununua? Je dada mmoja akija hapa nikiwa nimeenda? Kwa kuomba na kutafakari, unajiambia mwenyewe: “Sitaki kwenda leo, huenda dada fulani akaja hapa.” Ilhali matokeo ni kwamba, kufikia jioni, hakuna aliyekuja hapo, na umekosa mengi. Hata katika Enzi ya Neema, njia hii ya utendaji ilikuwa na makosa na isiyo sahihi. Kwa hiyo, ikiwa watu watafanya utendaji kama katika nyakati zilizopita, hakutakuwa na mabadiliko katika maisha yao. Watakuwa tu watiifu, na hawatatilia maanani upambanuzi, na hawatafanya lolote ila kutii na kuvumilia pasipo kufikiria. Katika wakati huo, watu walisisitiza kuhusu kumtukuza Mungu—lakini Mungu hakupata utukufu wowote kutoka kwao, kwani hawakuwa wameishi kwa kudhihirisha lolote, na hawakuwa wamebadilika. Walijitiisha tu na kujiwekea mipaka wenyewe kulingana na dhana zao wenyewe, na hata miaka mingi ya utendaji haikuleta mabadiliko katika maisha yao; walijua tu kuvumilia, kuwa wanyenyekevu, kupenda, na kusamehe, na hawakupata nuru hata kidogo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Wangemjuaje Mungu?

Watu wataingia tu kwa njia sahihi ya imani katika Mungu ikiwa watamleta Mungu ndani ya maisha yao halisi, na katika maisha yao ya kawaida ya ubinadamu. Leo, maneno ya Mungu yanawaongoza ninyi, na hakuna haja ya kutafuta na kupapasa kama nyakati zilizopita. Wakati ambapo unaweza kutenda kulingana na maneno haya, na unaweza kujichunguza na kujitathmini mwenyewe kulingana na hali ambazo Nimetaja, basi utaweza kubadilika. Haya siyo mafundisho ya dini, lakini kile ambacho Mungu anamtaka mwanadamu afanye. Leo, Nakwambia kiini cha jambo: Jishughulishe tu na kutenda kulingana na maneno Yangu. Matakwa Yangu kwako ni kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, na Nimekwambia hilo tayari; ikiwa unasisitiza kabisa kutenda kwa njia hii, utaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Siku hii ndio wakati wa kuishi katika maneno ya Mungu: Maneno ya Mungu yameeleza yote, yote yamefafanuliwa wazi, na maadamu unaishi kwa maneno ya Mungu, utaishi maisha yaliyo huru kabisa na yaliyokombolewa. Hapo awali, ulipomleta Mungu katika maisha yako halisi, ulipitia mafundisho ya dini na sherehe nyingi sana, ulimwomba Mungu hata katika mambo madogo sana, uliyaweka maneno dhahiri upande mmoja, kutoyasoma, na ukajitolea juhudi zako zote kwa kutafuta—na matokeo kwamba hakukuwa na athari. Chukua mfano wa, kile ulichovaa: Wakati ambapo uliomba, uliliweka jambo hili mikononi mwa Mungu, ukiomba kwamba Mungu achague kitu kinachofaa kwa wewe kuvaa. Mungu aliyasikia maneno haya na kusema: “Unaniomba Nijishughulishe Mimi na tondoti hafifu kama hizi? Ubinadamu wa kawaida na urazini Nilivyokuumbia vimeenda wapi?” Wakati mwingine, mtu fulani atafanya makosa katika matendo yake, na ataamini kwamba amemkosea Mungu, naye huanza kufungwa. Hali za watu wengine ni nzuri sana, lakini wanapofanya kitu fulani kidogo kwa njia isiyo sahihi wao huamini kwamba Mungu anawaadibu. Kwa kweli, hii si kazi ya Mungu, lakini ya akili za watu wenyewe. Wakati mwingine, huwa hakuna kosa lolote na vile unavyopitia tukio, laini wengine husema kwamba unapitia tukio kwa njia isiyo sahihi, na hivyo unategwa—unakuwa mbaya, na mwenye giza ndani. Mara kwa mara, watu wakiwa baridi kwa njia hii, wao huamini kwamba wanaadibiwa na Mungu, lakini Mungu husema: “Sifanyi kazi ya kuadibu ndani yako, ungenilaumuje Mimi hivyo?” Watu ni wabaya sana. Wao pia ni wepesi kuhisi sana mara kwa mara na wao hulalamika kuhusu Mungu mara kwa mara. Mungu hakutaki wewe uteseke, ilhali wewe unajiacha uingie katika hali hiyo. Hakuna thamani katika kuteseka kwa aina hii. Kwa sababu watu hawajui kazi inayofanywa na Mungu, katika mambo mengi wao ni wajinga, na hawawezi kuona kwa dhahiri. Katika nyakati kama hizo, wao hunaswa katika mawazo yao wenyewe, wakiendelea kutegwa zaidi milele. Watu wengine husema kwamba vitu vyote na mambo yote yamo mikononi mwa Mungu—kwa hiyo Mungu hangejua watu wanapokuwa wabaya? bila shaka Mungu hujua. Wakati ambapo unategwa katika dhana za binadamu, Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi ndani yako. Wakati mwingi, watu wengine hutegwa katika hali mbaya, lakini Mimi bado huendelea na kazi Yangu. Kama wewe ni mbaya au mtendaji, Mimi sizuiliwi na wewe—lakini unapaswa kujua kwamba maneno mengi Ninenayo, na kiasi kikubwa sana cha kazi Nifanyayo, huja kwa wingi na haraka kulingana na hali ya watu. Wakati ambapo wewe ni mbaya, hili halizuii kazi ya Roho Mtakatifu. Katika nyakati za kuadibu na kifo, watu wote walitegwa ndani ya hali mbaya, lakini hili halikuizuia kazi Yangu; ulipokuwa mbaya, Roho Mtakatifu aliendelea kufanya kilichohitajika kufanywa ndani ya wengine. Unaweza kuendelea kusimama kwa mwezi mmoja, lakini Naendelea kufanya kazi—chochote ufanyacho katika siku za baadaye au sasa, hakiwezi kuizuia kazi ya Roho Mtakatifu. Hali nyingine mbaya hutokana na udhaifu wa binadamu; wakati ambapo watu hawawezi kweli kufanya jambo au kulielewa, wao huwa wabaya. Kwa mfano, katika nyakati za kuadibu, maneno ya Mungu yalizungumza kuhusu kumpenda Mungu kwa kiwango fulani wakati wa kuadibu—lakini wewe uliamini kwamba huwezi. Wakati wa hali hii watu walihisi hasa wenye huzuni na wakaomboleza, walisikitika kwamba miili yao ilikuwa imepotoshwa vikali na Shetani, na kwamba uhodari wao ulikuwa mbaya sana, walihisi kwamba ilisikitisha kuwa walizaliwa katika mazingira haya. Watu wengine walihisi kwamba wakati ulikuwa umepita sana wa kuamini katika Mungu na kumjua Mungu, na kwamba walikuwa hawastahili kufanywa wakamilifu. Hizi zote ni hali za kawaida.

Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za kutotii, ni mchafu ya kusikitisha, ni kitu kichafu. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi, kuna maonyesho mengi sana ya mwili, na kwa hiyo Mungu hudharau mwili kwa kiwango fulani. Watu wanapoacha uchafu, mambo potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini wakibaki bila kuweza kuachana na uchafu na upotovu, basi bado watamilikiwa na Shetani. Kula njama, udanganyifu, na uhalifu wa watu ni mambo ya Shetani; kwa kukuokoa wewe, Mungu hukutenganisha na mambo haya na kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa, na yote ni kwa sababu ya kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unaishi ukimilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na hutapokea urithi wa Mungu. Mara tu umetakaswa na kufanywa kamili, utakuwa mtakatifu, na utakuwa wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na wa kufurahisha kwa Mungu. Kazi inayofanywa na Mungu leo ni wokovu, na, zaidi ya hayo, ni hukumu, kuadibu, na laana. Ina hali nyingi. Je, maneno mengine ya Mungu sio hukumu na kuadibu tu, bali pia laana? Nazungumza ili kutimiza athari fulani, kuwafanya watu wajijue wenyewe, na sio kuwafisha watu; Moyo Wangu ni kwa ajili yenu. Kuzungumza ni mbinu mmojawapo ambayo Mimi hufanyia kazi, Natumia maneno kuonyesha tabia ya Mungu, na kukuruhusu wewe kuelewa mapenzi ya Mungu. Mwili wako waweze kufa, lakini una roho na nafsi. Kama watu wangekuwa na mwili tu, basi hakungekuwa na maana ya wao kuamini katika Mungu, wala hakungekuwa na maana kwa kazi hii yote ambayo Nimefanya. Leo, Nazungumza juu ya jambo moja na kisha lingine, wakati mmoja Ninachukia mno watu, na wakati mwingine Ninapenda kwa hali ya juu; Nafanya hili kuzibadilisha tabia zako, na kuzigeuza dhana zako.

Siku za mwisho zimefika, na nchi nyingi kutoka upande mmoja wa ulimwengu hadi mwingine ziko katika machafuko, kuna vurugu ya kisiasa, njaa, ndwele, mafuriko, na ukame unaonekana kila mahali, kuna maangamizi katika ulimwengu wa mwanadamu, na Mbingu imetuma msiba hapa chini. Hizi ni ishara za siku za mwisho. Lakini kwa watu, unaonekana kama ulimwengu wa uchangamfu na fahari, ambao unaendelea kuwa hivyo zaidi na zaidi. Watu wanapotazama ulimwengu, mioyo yao inavutiwa nao, na wengine hawawezi kujinasua kutoka kwa ulimwengu; idadi kubwa itadanganywa na wale wanaoshiriki katika hila na uchawi. Usipojitahidi ili kuendelea mbele, na huna maadili, utapeperushwa na wimbi hili lenye dhambi. China ni nchi iliyo nyuma sana kimaendeleo kuliko zote, ni nchi ambayo joka kuu jekundu limelala likiwa limejiviringisha, ina watu wengi zaidi wanaoabudu sanamu na kushiriki katika uchawi, hekalu nyingi zaidi, na ni mahali ambapo pepo wachafu huishi. Ulizaliwa ndani yake, unafurahia manufaa yake, na unapotoshwa na kuteswa nalo, lakini baada ya kupitia kujichungua unaachana nalo na unapatwa kabisa na Mungu. Huu ni utukufu wa Mungu, na kwa hiyo hatua hii ya kazi ina umuhimu mkubwa. Mungu amefanya kazi ya kiwango kikubwa hivi, amenena maneno mengi sana, na hatimaye Atawapata ninyi kabisa—hii ni sehemu moja ya kazi ya usimamizi wa Mungu, na ni “mateka ya ushindi” ya vita dhidi ya Shetani. Kadri watu hawa wanavyokuwa bora na kadri maisha ya kanisa yanavyokuwa thabiti, ndivyo joka kuu jekundu linavyotiishwa. Haya ni mambo ya ulimwengu wa kiroho, ni vita vya ulimwengu wa kiroho, na Mungu anapokuwa mshindi, Shetani ataaibishwa na kuanguka chini. Hatua hii ya kazi ya Mungu ina umuhimu wa ajabu. Kazi ya kiwango kikubwa hivyo huokoa kabisa kikundi hiki cha watu; unaponyoka kutoka kwa ushawishi wa Shetani, unaishi katika nchi takatifu, unaishi katika nuru ya Mungu, na hapo kuna uongozi na mwongozo wa nuru, na kisha kuna maana katika kuwa kwako hai. Mnachokula na kuvaa ni tofauti na wao; mnafurahia maneno ya Mungu, na kuishi maisha yenye maana—na wao hufurahia nini? Wao hufurahia tu urithi wa babu zao na “roho ya kitaifa.” Hawana hata dalili ndogo kabisa ya ubinadamu! Mavazi, maneno, na matendo yenu vyote ni tofauti na vyao. Hatimaye, mtaacha kabisa uchafu, hamtategwa tena na ushawishi wa Shetani, na mtapata upaji wa Mungu wa kila siku. Mnapaswa kila mara kuwa waangalifu. Ingawa mnaishi mahali pachafu hamjawekwa mawaa na uchafu na mnaweza kuishi ubavuni mwa Mungu, mkipokea ulinzi Wake mkuu. Mmechaguliwa miongoni mwa wote walio katika nchi hii ya manjano. Je, ninyi sio watu waliobarikiwa zaidi? Kama kiumbe aliyeumbwa, unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu na uishi katika mwili mchafu, basi wewe siye mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kama binadamu, unapaswa kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso. Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu, kama Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kinachotolewa na ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya Shetani, na kukanyagiwa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au njia ya kweli, basi ni nini maana ya maisha yako? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale wanaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Views: 55 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Matamshi ya Kristo | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar