5:33 PM
Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho? Hakuna kati yenu aliye wazi sana juu ya hili. Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo. Watu wengi sana wanafikiri kwamba ili kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho lazima mtu asali, aombe, ale na anywe maneno ya Mungu, au kujaribu kuelewa maneno ya Mungu. Bila kujali kama kuna matokeo yoyote, au kama kuna kuelewa kwa kweli, watu hawa hulenga tu kufanya mambo yasiyo ya dhati kwa nje, na hawalengi matokeo ni watu wanaoishi ndani ya mila za dini, na si watu wanaoishi ndani ya kanisa, na hata zaidi wao si watu wa ufalme. Sala za mtu wa aina hii, kuimba kwake, na kula na kunywa kwake maneno ya Mungu yote yanafuata amri, wanalazimika kufanya hayo, na yanafanyika katika kufuata mitindo, hayafanyiki kwa hiari wala kufanyika kutoka moyoni. Haijalishi ni kiasi gani watu hawa wanaomba au kuimba, hakutakuwa na matokeo kamwe, kwa sababu yote wanayofanya ni amri na mila za kidini, na wao hawatendi neno la Mungu. Kwa kulenga tu mbinu, na kuchukua maneno ya Mungu kama amri ya kuhifadhi, mtu wa aina hii hatendi neno la Mungu, bali tu anaridhisha mwili, na anafanya vitu ili kujionyesha kwa wengine. Aina hii ya matambiko ya dini na amri yanatoka kwa mwanadamu, si kwa Mungu. Mungu hahifadhi sheria, Hazingatii sheria yoyote; Anafanya mambo mapya kila siku na Anafanya kazi ya vitendo. Kama watu katika Kanisa la Nafsi Tatu ambao wamewekewa mipaka kwa ulinzi wa kila asubuhi, sala ya jioni, kutoa shukrani kabla ya kula, kuonyesha shukrani katika kila kitu, na matendo mengine kama haya, haijalishi ni kiasi gani watu hawa wanafanya, au muda wanatenda, hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kama watu huishi ndani ya amri, na mioyo yao ikiwa katika vitendo, basi Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi, kwa sababu mioyo ya watu inachukuliwa na amri, inachukuliwa na dhana za kibinadamu; kwa hiyo Mungu hana njia ya kufanya kazi; watu daima watakuwa wakiishi tu chini ya utawala wa sheria, mtu wa aina hii kamwe hataweza kupokea sifa za Mungu.

Maisha ya kawaida ya kiroho ni kuishi maisha mbele ya Mungu. Wakati wa kuomba mtu anaweza kutuliza moyo wake mbele ya Mungu, na kwa njia ya sala anaweza kutafuta kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, kujua maneno ya Mungu, na anaweza kuelewa mapenzi ya Mungu. Wakati wa kula na kunywa maneno ya Mungu mtu anaweza kuelewa zaidi na kuwa udhahiri zaidi juu ya ni nini Mungu anataka kufanya sasa hivi, na mtu anaweza kuwa na njia mpya ya matendo na asiwe wa kushikilia ukale, ili matendo ya mtu yote ni kwa lengo la kufanikisha maendeleo katika maisha. Kwa mfano, sala ya mtu si kwa ajili ya kusema baadhi ya maneno mazuri, au kupiga kelele mbele ya Mungu kuonyesha deni ya mtu, bali ni kwa kufanya mazoezi ya kutumia roho ya mtu, kutuliza moyo wa mtu mbele ya Mungu, kufanya mazoezi ya kutafuta uongozi wa maneno ya Mungu katika mambo yote, kufanya moyo wa mtu uwe moyo wa kuvutiwa na mwanga mpya kila siku, kutokuwa wa kukaa tu wala mvivu, na kuingia kwenye njia sahihi ya kutenda maneno ya Mungu. Kwa sasa watu wengi wanalenga mbinu, na hawajaribu kufuata ukweli ili kufikia maendeleo katika maisha; hapa ndipo watu hupotoka. Pia kuna baadhi ya watu ambao, hata kama wao wana uwezo wa kupokea mwanga mpya, taratibu zao hazibadiliki, wao huunganisha fikra za dini za zamani ili kupokea neno la Mungu leo, na wanayoingiza bado ni kanuni ambayo hubeba fikra za dini kwa pamoja, na hawaingiziwi mwanga wa leo kabisa. Kwa hivyo, matendo yao ni machafu wanafanya matendo yale yale kwa jina jipya, na haijalishi matendo yao ni mazuri kiwango gani, bado ni ya unafiki. Mungu huongoza watu kufanya mambo mapya kila siku, na Anahitaji watu kuwa na umaizi mpya na ufahamu mpya kila siku, na si kuwa na mienendo ya zamani au wasiobadilika. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, ila mbinu zako hazijabadilika kamwe, kama bado wewe ni wa shauku na mwenye shughuli nyingi kwa nje, na wala huji mbele za Mungu kufurahia maneno Yake kwa moyo mtulivu, basi hutaweza kupata chochote. Wakati wa kupokea kazi mpya wa Mungu, kama hutaunda mpango mpya, kama hutatenda katika njia mpya, kama hutatafuta ufahamu mpya, lakini badala yake kushikilia mambo mazee ya zamani na kupokea kiasi kidogo tu cha mwanga mpya bila kubadili jinsi unavyotenda, basi mtu wa aina hii ingawa yu ndani ya mkondo huu kwa kawaida kwa kweli ni Mfarisayo wa dini nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu.

Kama unataka kuishi maisha ya kawaida ya kiroho, unahitaji kupata mwanga mpya kila kuchao, kutafuta ufahamu wa kweli wa maneno ya Mungu, na kufikia udhahiri kuelekea ukweli. Unahitaji kuwa na njia ya kufanya matendo kwa vyote vile, na kwa kusoma maneno ya Mungu kila siku unaweza kupata maswali mapya na kugundua upungufu wako mwenyewe. Hili litaleta moyo ulio na kiu na unaotafuta, ambao utaweka nafsi yako yote katika mwendo, na wewe utakuwa na uwezo wa kuwa kimya mbele ya Mungu wakati wowote, na kuwa na hofu kubwa ya kuachwa nyuma. Kama mtu anaweza kuwa na moyo huu wa kutamani na kutafuta, na pia awe na nia ya kuingia ndani kwa kuendelea, basi yupo katika njia sahihi kwa ajili ya maisha ya kiroho. Wale wote ambao wanaweza kukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu, ambao wanatamani kufanya maendeleo, ambao wako radhi kutafuta kukamilishwa na Mungu, wale ambao wanatamani kuelewa kwa undani maneno ya Mungu, na ambao hawatafuti vitu visivyo vya kawaida lakini wanalipa gharama ya vitendo, kuonyesha kwa vitendo kufikiria mapenzi ya Mungu, kuingia ndani kwa vitendo, kufanya uzoefu wao kuwa wa kweli zaidi na halisi zaidi, ambao hawatafuti maneno matupu ya kanuni, na ambao pia hawatafuti hisia isiyo ya kawaida, wala kumwabudu mtu yeyote mkubwa mtu wa aina hii ameingia katika maisha ya kawaida ya kiroho. Kila kitu anachofanya ni kwa lengo la kufanikisha maendeleo zaidi katika maisha, kufanya upya roho yake na wala si palepale, na daima awe na uwezo wa kuingia ndani kwa wema. Kwa mfano, aombapo kabla ya kula, halazimishwi kufanya hivyo, lakini badala yake anatuliza moyo wake mbele ya Mungu, kumshukuru Mungu katika moyo wake, yuko tayari kuishi kwa ajili ya Mungu, kuweka muda wake katika mikono ya Mungu, na yuko tayari kushirikiana na Mungu na kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu. Kama moyo wake hauwezi kuwa kimya mbele ya Mungu, ni afadhali asile bali azidi kutenda, basi hii si kufuata sheria, lakini ni kutenda neno la Mungu. Baadhi ya watu, wanapoomba kabla ya kula, kwa kujua wao hujifanya ili kuweka matendo ya kujionyesha, ambayo yanaweza kuonekana kama kumcha Mungu, lakini akili zao huwaza: “Kwa nini nahitaji kufanya matendo kwa njia hii? Si mambo ni mazuri bila kuomba? Mambo yangali vile baada ya kuomba, hivyo kwa nini kujisumbua?” Mtu wa aina hii hufuata amri, na ingawa maneno yake yanasema kwamba yuko tayari kumridhisha Mungu, moyo wake haujaja mbele za Mungu. Haombi namna hii ili afanye mazoezi ya kutuliza moyo wake mbele ya Mungu, bali hufanya hivyo ili kuwadanganya watu wengine na ili watu wengine waone. Mtu wa aina hii ni mnafiki kabisa, kama mchungaji wa dini ambaye anaweza kuombea tu wengine lakini hawezi mwenyewe kuingia ndani; mtu wa aina hii ni ofisa wa kidini, kabisa! Kila siku Mungu ananena mambo mapya, Anafanya mambo mapya, lakini wewe unafuata amri kila siku, ukijaribu kumdanganya Mungu, kushughulikia Mungu bila uangalifu, hivyo si wewe ni mtu ambaye anamwasi Mungu? Je, unaweza kupokea baraka wakati unazingatia amri na kumwasi Mungu? Si wewe utaadibiwa na Mungu?

Kazi ya Mungu kwa kasi inaendelea ikitupa washiriki wa dini na madhehebu mbalimbali na watu mashuhuri wanaoshikilia misa ya kanisa kwa umbali sana, na pia kutawanya kwa pande zote nne wale wataalamu kati yenu ambao hasa hupenda kufuata kanuni. Kazi ya Mungu haisubiri, haitegemei kitu chochote nawala haizembei. Haivuti au kuburuta mtu yeyote; kama huwezi kustahimili basi utaachwa, bila kujali ni miaka ngapi umefuata. Haijalishi wewe ni mkongwe anayestahili kiasi kipi, kama wewe hufuata amri basi lazima uondolewe. Ninamshauri mtu wa aina hii kuwa na maarifa fulani ya kibinafsi, kwa hiari kuchukua kiti cha nyuma, na kutoshikilia kilicho cha kale; kuwalazimu wengine kutenda neno la Mungu kwa mujibu wa kanuni zako za vitendo si hii ni kujaribu kushinda mioyo ya watu? Utendaji wako ni kufuata sheria, na kuwafundisha watu kufuata ibada ya kanisa. Mara zote wewe huwafanya watu wafanye mambo kulingana na matakwa yako, hivyo huku si kutengeneza vikundi? Hivyo huku si kugawanya kanisa? Basi wewe una ujasiri wa kusema kuwa unafikiria mapenzi ya Mungu vipi? Ni kipi kinakuwezesha kusema kwamba hili ni kuwakamilisha wengine? Ukiendelea kuongoza kwa njia hii, si hii ni kuwaongoza watu ndani ya matambiko ya kidini? Kama mtu ana maisha ya kawaida ya kiroho, kama anapata ufunguliaji na uhuru katika roho zao kila siku, basi anaweza kutenda maneno ya Mungu bila kuzuiwa kumridhisha na, hata anapoomba hapitii tu kanuni au kufuata mchakato, na anao uwezo wa kustahimili mwanga mpya kila siku. Kwa mfano: Wakati anafanya mazoezi ya kutuliza moyo wake mbele za Mungu, anaweza kufanya moyo wake kweli uwe tulivu mbele ya Mungu na hakuna mtu anayeweza kumvuruga, na hakuna mtu, tukio au kitu kinaweza kuzuia maisha yake ya kawaida ya kiroho. Aina hii ya matendo ni kwa lengo la kufanikisha matokeo, si tu kuwapa watu kanuni fulani za kuzingatia. Aina hii ya matendo si kufuata sheria, ila kuendeleza maendeleo ya watu katika maisha. Kama wewe ni mfuataji amri tu, basi maisha yako kamwe hayatabadilika, ingawa wengine wanaweza kufanya matendo kwa njia hii, kama wewe ufanyavyo, mwishowe, wengine wanaweza kustahimili kasi za kazi ya Roho Mtakatifu, wakati utaondolewa kutoka kwa mkondo wa Roho Mtakatifu. Hivyo basi je, hujidanganyi? Madhumuni ya maneno haya ni kuwaruhusu watu watulize mioyo yao mbele ya Mungu na kurejea kwa Mungu, kuruhusu kazi ya Mungu kutekelezwa kwa watu bila kizuizi, na ili itimize matokeo. 

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Views: 27 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: Matamshi ya Kristo, Chakula cha Kiroho cha Kila Siku | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar