3:37 PM
Vigezo vya Mtu Aliye Mwema Kwa Kweli

Ushuhuda wa Injili : Vigezo vya Mtu Aliye Mwema Kwa Kweli

 

Moran Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong

Tangu nilipokuwa mtoto, siku zote nilishikiza umuhimu mkubwa kwa jinsi watu wengine walivyoniona na ukadiriaji wao kwangu. Ili niweze kupata sifa kutoka kwa wengine kwa kila kitu nilichokifanya, sikubishana na yeyote asilani wakati wowote kitu chochote kilichoibuka, ili kuepuka kuharibu picha nzuri watu wengine walikuwa nayo kwangu. Baada ya kuikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, niliendelea kwa njia hii, nikizingatia kwa kila njia iwezekanayo picha nzuri ambayo ndugu zangu wa kiume na wa kike walikuwa nayo kwangu. Hapo awali, wakati nilipokuwa ninasimamia kazi, kiongozi wangu mara nyingi angesema kwamba utendaji wangu ulikuwa kama “bwana ndiyo,” wala sio utendaji wa mtu ambaye huweka ukweli katika vitendo. Sikuathiriwa nalo asilani, lakini kwa kinyume kama watu wengine walinifikiria kuwa mtu mzuri, basi nilihisi kuridhika.

Siku moja, nilisoma aya hii: “Ikiwa katika imani yako ya Mungu hufuatilii ukweli, basi hata kama huonekani kuwa ukikosa, bado wewe si mtu mwema kwa dhati. Wale ambao hawafuatilii ukweli bila shaka hawana hisi ya haki, wala hawawezi kupenda kile ambacho Mungu hupenda au kuchukia kile ambacho Mungu huchukia. Hawawezi kusimama kwa upande wa Mungu kabisa, sembuse kulingana na Mungu. Ni vipi basi wale wasio na hisi ya haki wanaweza kuitwa watu wema? Sio tu kuwa wale walioelezwa na watu wa dunia kama ‘watu wazuri’ hawana hisi ya haki, wala hawana malengo katika maisha. Wao ni watu tu ambao hawataki kumkosea yeyote asilani, hivyo wana thamani gani? Mtu mwema kwa dhati huashiria mtu ambaye hupenda vitu vyema, mtu ambaye hufuatilia ukweli na hutamani mwanga, mtu anayeweza kutambua mema na maovu na ambaye ana malengo sahihi katika maisha; ni mtu wa aina hii tu anayependwa na Mungu” (“Kumtumikia Mungu ni Lazima Mtu Ajifunze Jinsi ya Kutambua Watu wa Kila Aina” katika Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu). Baada ya kusoma maneno haya, ghafla niliona mwanga. Sasa nikaona kwamba mtu mzuri hakuwa mtu ambaye ana maongezi ya kirafiki na watu wa kawaida na ambaye habishani au kugombana nao, au mtu anayeweza kuwapa ndugu zake wa kiume na wa kike picha nzuri na kupata ukadiriaji mzuri kutoka kwao. Mtu mwema kwa dhati ni mtu ambaye hupenda vitu vyema na ambaye hutafuta ukweli na haki, mtu ambaye ana malengo halisi katika maisha, ambaye ana hisi ya haki, anayeweza kutambua kati ya mema na maovu, kupenda kile ambacho Mungu hupenda na kuchukia kile ambacho Mungu huchukia; mtu ambaye yuko tayari kufanya liwezekanalo katika utendaji wa wajibu wake na ambaye ana nia na ujasiri kujitolea maisha yake kwa ukweli na haki. Kuhusu matendo yangu mwenyewe, ni wapi kulikuwa na hisi yoyote ya haki? Wakati wowote ambapo ndugu fulani wa kiume alirudi kutoka kueneza injili akizungumzia ilivyokuwa ngumu, sikujizuia kuhisi kuvurugwa nikianza kulalamika, nikihisi kuwa kueneza Injili haikuwa kazi rahisi, kwamba kwa kweli ilikuwa ngumu sana, bila kujua nikichukua upande wa mwili wa mwanadamu na kutotaka kushirikiana tena. Nilipoona machafuko katika kanisa yakihusiana na mambo kama vile usambazaji wa dhana kumwelekeza Mungu, kama yalikuwa mambo mazito, ningefanya ushirika nikitumia maneno ya busara kutatua suala hili, kama hayakuwa mazito, ningelipita suala hilo kwa kulipuuza nikiogopa kwamba mtu mwingine angekuwa na maoni juu yangu kama singezungumza vizuri. Nilipomwona mwenzangu akifanya mambo ambayo hayakuwa na uhusiano wowote na ukweli au kutozingatia mazingira yake, nilitaka kudakiza suala hilo naye, lakini nikawaza, “Je, angelistahimili kama ningelidakiza suala hili? Sio jambo la thamani kuuumiza uhusiano wetu mzuri juu ya jambo dogo kama hilo. Nitasubiri tu hadi wakati mwingine na kulidakiza wakati huo.” Kwa njia hii nilipata visingizio kwa ajili yangu mwenyewe ili niweze kuboronga.

Sasa niliona kwamba nililingana tu na vigezo vya watu wa dunia vya mtu mwema, ambayo ilikuwa tu ni “bwana ndiyo” machoni pa watu wa kawaida: mtu ambaye huwa hataki asilani kumkosea yeyote na yeye si kitu kama mtu mzuri wa furaha ya Mungu ambaye hupenda vitu vyema, hutafuta ukweli na ana hisi ya haki. Niliona maoni ya watu wengine kwangu kuwa muhimu zaidi kuliko kupata ukweli na niliridhika tu kwa kupata wengine kunisifu; ingewezekanaje niweze kuwa mtu mwenye malengo sahihi katika maisha? Je, sifa za wengine zingewakilisha upataji wangu wa ukweli? Je, ukadiriaji mzuri wa wengine kwangu ungewakilisha kwamba nilikuwa na uzima? Kama nilimwamini Mungu lakini sikuwa natafuta ukweli au haki, sikuwa nikitafuta mabadiliko katika tabia yangu, lakini badala yake daima nilikuwa nikifuatilia sifa yangu mwenyewe na kujiepusha na aibu yangu mwenyewe, hili lilikuwa na thamani gani wakati wa kumfuata Mungu? Je, ni nini ningeweza kupata kama ningefuata njia hii hadi mwisho kabisa? Nilikuwa kiumbe mpotovu, kabisa. Kama kwa kweli nilikuwa nimepata heshima ya wote na nilikuwa na hadhi katika mawazo yao, basi si nilikuwa nimekuwa yule malaika mkuu ambaye alishindana na Mungu kwa cheo? Je, si nilikuwa nimekuwa adui halisi wa Mungu? Je, si mtu wa aina hii ni yule ambaye ametenda dhambi ya kufisha mbele ya macho ya Mungu? Wale ambao Mungu huokoa na kukamilisha ni watu wema kwa dhati wanaotafuta ukweli na haki. Hao sio watu wasio na busara ambao hawawezi kutofautisha mema na maovu, wasio dhahiri juu ya upendo na chuki na ambao hawana hisi ya haki, sembuse wale watu waovu ambao hujali tu juu ya sifa zao wenyewe na ambao wana uhasama kwa Mungu. Kama ningeendelea kuchukua kile watu wa kawaida hufikiria kuwa mtu mwema kama vigezo vya mwenendo wangu, ningehukumiwa kuwa kitu cha kuondoshwa na adhabu ya Mungu.

Ee Mungu! Ninatoa shukurani kwa uongozi na nuru Yako ambayo yameniruhusu kutambua kiasi maana ya kuwa mtu mwema kwa dhati, na ambayo aidha yaliniruhusu kuona dhana zangu mwenyewe zenye kosa na ujinga, na kutambua uasi wangu mwenyewe na upinzani. Ee Mungu! Kutoka leo, napenda kuchukua kirai “tafuta ukweli na kuwa na hisi ya haki” kama vigezo vya mwenendo wangu, kutafuta kuingia ndani zaidi katika ukweli, kutafuta mabadiliko katika tabia yangu na kujitahidi kuwa mtu mwema kwa dhati hivi karibuni ambaye yu dhahiri juu ya upendo na chuki na ambaye ana hisi ya haki.

Chanzo:  Vigezo vya Mtu Aliye Mwema Kwa Kweli

 

 

Views: 115 | Added by: hatat1946 | Tags: Ushuhuda-wa-Injili, kazi-ya-Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar