6:24 PM
Matamshi ya Kristo | Njia … (5)

Matamshi ya Kristo | Njia … (5)

Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mbele ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba karibu watu wote wanaoamini katika Mungu hawamjui Roho, lakini tu wana aina ya imani iliyochanganyikiwa. Ni wazi kutokana na hili kwamba watu hawamfahamu Mungu, na hata ingawa wanasema wanaamini katika Yeye, kuhusu kiini chake, kulingana na matendo yao wanaamini katika wao wenyewe, sio Mungu. Kutokana na uzoefu Wangu binafsi wa kweli, Naweza kuona kwamba Mungu humshuhudia Mungu katika mwili, na kutoka nje, watu wote hulazimishwa kukubali ushahidi Wake, na inaweza tu kusemwa kwa shida kuwa wanaamini kwamba Roho wa Mungu hana kosa kabisa. Hata hivyo, Nasema kwamba kile ambacho watu wanaamini si mtu huyu na hasa si Roho wa Mungu, lakini wanaamini katika hisia zao wenyewe. Je, huko si kuamini tu katika wao wenyewe? Maneno haya Nisemayo yote ni ya kweli. Huko si kupachika watu majina, lakini nahitaji kueleza wazi kitu kimoja—kwamba watu wanaweza kuletwa katika siku hii, wawe wana uwazi au wamechanganyikiwa, hii yote inafanywa na Roho Mtakatifu na si kitu ambacho wanadamu wanaweza kuamuru. Huu ni mfano wa kile ambacho Nimetaja awali kuhusu Roho Mtakatifu kulazimisha imani ya watu. Hivi ndivyo Roho Mtakatifu hufanya kazi, na ni njia moja ambayo Roho Mtakatifu hufuata. Haijalishi yule ambaye watu huamini kwa asili, Roho Mtakatifu kwa nguvu huwapa watu aina fulani ya hisia ili waamini katika Mungu ndani ya mioyo yao. Hii siyo aina ya imani uliyo nayo? Je, huhisi kwamba imani yako katika Mungu ni kitu cha ajabu? Je, hudhani kwamba ni kitu cha ajabu kwamba huwezi kuepuka kutoka kwa mkondo huu? Hujaweka juhudi yoyote kulitafakari hili? Hii siyo ishara na ajabu kuu zaidi? Hata kama umekuwa na hamu kubwa ya kutoroka mara nyingi, huwa kila mara kuna nguvu ya maisha kuu inayokuvutia na kukufanya usite kuondoka. Na kila mara unapokabiliwa na hili unasongwa roho na kuwa na kikweukweu, na hujui la kufanya. Na kuna wengine wenu ambao hujaribu kuondoka, lakini unapojaribu kwenda, ni kama kisu kwa moyo wako, na ni kama kwamba nafsi yako imetolewa ndani yako na zimwi juu ya dunia ili moyo wako uwe na wahaka na ukose amani. Baada ya hilo, huwezi kufanya lolote bali kujitayarisha kukutana na jambo gumu na kurudi kwa Mungu…. Hujawahi kuwa na tukio hili? Naamini kwamba ndugu wadogo ambao wanaweza kuifungua mioyo yao watasema: “Ndio! Nimekuwa na matukio mengi sana kama haya; Ninaona aibu sana kuyafikiria!” Katika maisha Yangu ya kila siku Mimi huwa na furaha kila mara kuwaona ndugu Zangu wadogo kama wandani Wangu kwa sababu wamejawa na umaasumu—wao ni safi na wa kupendeka. Ni kama kwamba wao ni wenzi Wangu. Hii ndio maana kila mara Mimi hutafuta nafasi ya kuwaleta wandani Wangu wote pamoja, kuzungumza juu ya maadili yetu na mipango yetu. Mapenzi ya Mungu yatekelezwe ndani yetu ili sote tuwe kama mwili na damu, bila vizuizi na bila umbali. Hebu sote tuombe kwa Mungu: “Ee Mungu! Ikiwa ni mapenzi Yako, tunakusihi utupe mazingira yanayofaa ili sote tutambue matamanio yaliyo ndani ya mioyo yetu. Utuonee huruma sisi ambao ni wadogo na wanaokosa akili, ili tutumie kila tone la nguvu ndani ya mioyo yetu!” Naamini kwamba haya lazima yawe ni mapenzi ya Mungu kwa sababu zamani sana, Nilisema ombi hili mbele ya Mungu: “Baba! Sisi tulio duniani hukuita wakati wote, na kutarajia kwamba mapenzi Yako yatatimizwa hivi karibuni duniani. Niko radhi kutafuta mapenzi Yako. Fanya Unalotaka kufanya, na timiza kile Ulichonikabidhi Mimi mapema iwezekanavyo. Maadamu mapenzi Yako yanaweza kutimizwa mapema iwezekanavyo, Niko radhi hata Wewe ufungue njia mpya miongoni mwetu. Tarajio Langu pekee ni kwamba kazi Yako iweze kutimizwa hivi punde. Naamini kwamba hakuna sheria zinazoweza kuichelewesha kazi Yako! ”Hii ni kazi ambayo Mungu anafanya sasa. Hujaona njia ambayo Roho Mtakatifu anapitia? Ninapokutana na ndugu wazee, huwa kuna hisia ya ukandamizaji ambayo Siwezi kutambua kiini chake. Ni wakati Ninapokuwa nao tu ndio Ninaweza kuona kwamba wana uvundo mbaya wa jamii, na fikira zao za kidini, uzoefu wa kushughulikia mambo, njia zao za kuzungumza, maneno wayatumiayo, n.k., yote yanaudhi. Ni kama kwamba wamejawa na hekima na Mimi kila mara hukaa mbali nao kwa sababu Kwangu binafsi, falsafa Yangu ya maisha imepungukiwa sana. Nikiwa nao kila mara Mimi huhisi kuchoshwa na kulemewa, na wakati mwingine hilo huwa baya sana, la kukandamiza sana mpaka siwezi hata kupumua. Kwa hiyo katika nyakati hizi za hatari, Mungu hunipa Mimi njia bora ya kuepuka. Labda ni kuelewa Kwangu visivyo. Ninajali tu kuhusu kinachomfaidi Mungu; kutekeleza mapenzi ya Mungu ni muhimu zaidi. Mimi hukaa mbali sana na watu hawa, na ikiwa Mungu ananihitaji Nijihusishe nao, basi Mimi hutii. Katu sio kwamba wao ni wenye makuruhu, lakini ni kwamba “hekima,” fikira, na falsafa zao za maisha zinakera sana. Niko hapa kutimiza kile ambacho Mungu amenikabidhi Mimi, sio kujifunza kutoka kwa uzoefu wao namna ya kushughulikia mambo. Nakumbuka kwamba wakati mmoja Mungu aliniambia yafuatayo: “Hapa duniani, tafuta tu kutenda mapenzi ya Baba na utimize kile Alichokukabidhi. Mengine yote ni yasiyokuhusu Wewe.” Ninapofikiria juu ya hili Mimi huhisi amani kidogo. Hii ni kwa sababu Mimi huhisi kila mara kwamba mambo ya dunia ni yenye utata sana na kwamba Siwezi kuyafahamu hayo—huwa Sijui la kufanya. Kwa hiyo sijui ni mara ngapi Nimekuwa mwenye wasiwasi sana kuhusu hili na Nimechukia wanadamu—mbona watu ni wenye utata sana? Kuna tatizo gani na kuwa wa kawaida kidogo? Kujaribu kuwa mwerevu—ya nini kujisumbua? Ninapojihusisha na watu kwa kiwango kikubwa ni kwa msingi wa agizo la Mungu Kwangu, na hata kama kumekuwa na nyakati chache ambazo hali haikuwa hiyo, nani anaweza kujua labda ni nini kimejificha katika moyo Wangu?

Kuna nyakati nyingi ambapo Nimewashauri ndugu walio nami kwamba wanapaswa kuamini katika Mungu kutoka ndani ya mioyo yao wenyewe na sio kuhifadhi mambo wayapendayo wenyewe, kwamba wanapaswa kujali mapenzi Yake. Nimelia kwa uchungu mbele ya Mungu mara nyingi—kwa nini watu hawajali mapenzi ya Mungu? Je, yawezekana kwamba kazi ya Mungu ingepotea tu bila dalili bila sababu yoyote kabisa? Sijui ni kwa nini, na inaonekana kwamba kimekuwa kitendawili katika moyo Wangu. Kwa nini watu huwa hawatambui njia ya Roho Mtakatifu, lakini kila mara wao huwa wanadumisha mahusiano yasiyofaa kati ya watu wawili? Mimi huchafuka moyo Ninapowaona watu hivi. Wao hawaoni njia ya Roho Mtakatifu, lakini huzingatia tu kile ambacho watu hufanya. Moyo wa Mungu unaweza kuridhishwa kwa njia hii? Mimi huhuzunishwa mara kwa mara na hili. Inaonekana kwamba huu umekuwa mzigo Wangu kubeba. Roho Mtakatifu pia anasikitishwa kuhusu hili—je, huhisi lawama yoyote ndani ya moyo wako? Mungu na Afungue macho yetu ya kiroho. Kama yule Anayewaongoza watu kuingia katika roho, Nimeomba mbele ya Mungu mara nyingi: “Ee Baba! Naomba Nifanye mapenzi Yako kiini na kutafuta mapenzi Yako. Niwe mwaminifu kwa kile Ulichonikabidhi Mimi ili Wewe uweze kulipata kundi hili la watu. Utulete katika ulimwengu huru ili sote tuweze kukutana na Wewe na roho zetu. Amsha hisia za kiroho ndani ya mioyo yetu! ”Natarajia kwamba mapenzi ya Mungu yatatimizwa, kwa hiyo Ninamwomba bila kukoma ili Roho wa Mungu aendelee kutupa sisi nuru na kuturuhusu sote kufuata njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Hii ni kwa sababu njia Ninayotembea ni njia ya Roho Mtakatifu. Ni nani mwingine angetembea njia hiyo kwa niaba Yangu? Ni hili ndilo hufanya mzigo Wangu kuwa mzito zaidi. Nahisi kama kwamba Ninakaribia kuanguka, lakini Naamini kwamba Mungu bila shaka hatachelewesha kazi Yake. Labda wakati ambapo kile Alichonikabidhi kitatimizwa tutawachana. Kwa hiyo labda ni kwa sababu ya athari ya Roho wa Mungu ndio Nimehisi kila mara kuwa tofauti na wengine. Ni kama kwamba Mungu anataka kufanya kazi fulani, na sasa bado Sijapata ufahamu mzuri kuihusu. Hata hivyo, Naamini kwamba hakuna yeyote duniani aliye bora kuliko wandani Wangu, na Naamini kwamba wandani Wangu wataniombea mbele ya Mungu. Ikiwa hivyo, Nitashukuru kupita kiasi kuhusu hili. Natarajia kwamba ndugu Zangu watasema Nami. “Ee Mungu! Tunaomba mapenzi Yako yafichuliwe ndani yetu sisi katika enzi ya mwisho ili tubarikiwe na maisha ya roho, ili tuone matendo ya Roho wa Mungu na uso Wake wa kweli! ”Mara tuifikiapo hatua hii tutakuwa tunaishi kweli chini ya uongozi wa Roho, na ni wakati huo tu ndipo tutaweza kuuona uso wa kweli wa Mungu. Yaani, watu wataweza kufahamu maana ya kweli ya ukweli wote. Haufahamiki au kujulikana kupitia kwa fikira za wanadamu, lakini kupata nuru hufanyika kulingana na mapenzi ya Roho wa Mungu. Katika uzima wake wote, huyu ni Mungu Mwenyewe anayefanya kazi bila hata chembe kidogo ya wazo la mwanadamu ndani yake. Huu ni mpango Wake wa kazi kwa matendo Anayotaka kufichua duniani, na ni sehemu ya mwisho ya kazi Yake duniani. Uko radhi kushiriki katika kazi hii? Unataka kushiriki katika kazi hii? Una hiari ya kukamilishwa na Roho Mtakatifu na kufurahia maisha ya roho?

Kazi muhimu sana wakati huu ni kuzama ndani zaidi kutoka kwa msingi wetu wa asili. Ni lazima tuzame ndani zaidi katika hali za ukweli, maono, na maisha yetu. Kwa hali yoyote, lazima kwanza Niwakumbushe ndugu Zangu kwamba ili kuingia katika kazi hii, ni lazima uache fikira zako za awali. Yaani, ni lazima ubadilishe mwenendo wako wa maisha wa awali, ufanye mpango mpya, na kufungua ukurasa mpya. Ukiendelea kutetea kile ambacho kimekuwa cha thamani kwako katika maisha ya nyuma, Roho Mtakatifu hataweza kufanya kazi ndani yako; Atakuwa na shida kuweza kuhimili maisha yako. Mtu asipotafuta au kuingia ndani, au kufanya mpango, Roho Mtakatifu atamwacha kabisa. Hii inaitwa yule aliyekataliwa na enzi. Natarajia kwamba ndugu Zangu wote wataweza kuufahamu moyo Wangu, na pia Natarajia kwamba “washirika wapya” wengi zaidi wataweza kuinuka na kufanya kazi na Mungu kutimiza kazi hii pamoja. Naamini kwamba Mungu atatubariki, na pia Naamini kwamba Mungu atanipa wandani wengi zaidi ili Niweze kusafiri mpaka miisho ya dunia na tuwe hata na upendo mwingi zaidi kati yetu. Nimeridhika kabisa kwamba Mungu atapanua ufalme Wake kwa ajili ya juhudi zetu, na Natarajia kwamba kazi yetu ya bidii itafikia viwango visivyo na kifani ili Mungu apate vijana wengi zaidi. Sote tuombee hili zaidi na kumsihi Mungu bila kukoma ili maisha yetu yaendelee mbele Yake, na kwamba tuwe wandani na Mungu. Kusiwe na vizuizi vyovyote miongoni mwetu, na sote tule kiapo hiki mbele ya Mungu: “Kufanya kazi kwa pamoja! Kuwa na moyo wa kuabudu mpaka mwisho! Kutotengana kamwe, kuwa pamoja kila mara!” Ndugu Zangu wekeni uamuzi huu mbele ya Mungu ili mioyo yetu isipotee na hiari yetu isiyumbeyumbe! Ili kutimiza mapenzi ya Mungu, Ningependa kusema tena: Fanya kazi kwa bidii! Ipatie kila kitu ulichonacho! Mungu atatubariki kabisa!

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Endelea Kusoma:  Je, unataka kukaribisha Bwana Yesu? Je, unataka kunyakuliwa kabla maafa? Tovuti yetu hutoa ujumbe kuhusu kuja kwa mara ya pili kwa Kristo. Tafadhali bofya kitufe hapo chini kuwasiliana nasi mtandaoni wakati wowote.

Views: 67 | Added by: flickrpinquorettfb | Tags: kazi ya Roho Mtakatifu, Matamshi ya Kristo, kumjua mungu, Umwombe Mungu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar